GE2025 Samia kawa wakwanza kurudisha fomu INEC

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amewatangulia wagombea urais wa vyama vingine kurudisha fomu ya uteuzi katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ndejengwa jijini Dodoma leo, Jumatano Agosti 27, 2025.

Hatua hiyo, inampa nafasi mkuu huyo wa nchi ya kusubiri uteuzi wa INEC, kisha kuanza mchakamchaka wa kampeni za uchaguzi, zitakazofanyika kwa kipindi cha siku 60.

Soma pia: Kurudisha fomu kwa Samia bado kitendawili

Screenshot 2025-08-27 021821.png

Rais Samia ambaye ndiye mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), atazindua rasmi kampeni za uchaguzi huo, kesho Alhamisi Agosti 28, 2025, katika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, Dar es Salaam.

Mgombea huyo wa CCM, amefika katika ofisi za INEC, saa moja na dakika 50 asubuhi, akiwa wa kwanza kabla ya wagombea wengine wa nafasi hiyo, kama alivyofanya wakati wa uchukuaji fomu Agosti 9, 2025.

Rais Dk Samia ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, alisindikizwa na baadhi ya viongozi wa kitaifa wa chama hicho, huku akiambatana na mgombea mwenza, Dk Emmanuel Nchimbi.

Baadhi ya walioambatana naye katika tukio hilo ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Stephen Wasira, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt Asha Rose Migiro na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT), Mary Chatanda, sambamba na wajumbe wengine wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC).
 
Sijawahi kuomuona anaingia msikitini sijui ana shida gani na MUNGU.
Hajawahi kuingia msikitini Toka amekuwa raisi
 
Mimi nadhani kale ka hoja ka pole pole Viongozi washtakiwe na wafungwe.

Hivi Kuna haja gani Kuingia kwenye Uchaguzi kuteketeza mabilioni ya walipa Kodi wakati Ushindi umesha upata?

Kwenda kwenye Uchaguzi wakati una Matokeo mfukoni Uo ni uhaini kabisa.

Sisi Watanzania hatuna shida hata mjitangaze mmeshinda lakini kuchezea mabilioni ya walipa Kodi wakati Ushindi umesha upata ni uhaini.
 
Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amewatangulia wagombea urais wa vyama vingine kurudisha fomu ya uteuzi katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ndejengwa jijini Dodoma leo, Jumatano Agosti 27, 2025.

Hatua hiyo, inampa nafasi mkuu huyo wa nchi ya kusubiri uteuzi wa INEC, kisha kuanza mchakamchaka wa kampeni za uchaguzi, zitakazofanyika kwa kipindi cha siku 60.

Soma pia: Kurudisha fomu kwa Samia bado kitendawili

View attachment 3454690

Rais Samia ambaye ndiye mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), atazindua rasmi kampeni za uchaguzi huo, kesho Alhamisi Agosti 28, 2025, katika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, Dar es Salaam.

Mgombea huyo wa CCM, amefika katika ofisi za INEC, saa moja na dakika 50 asubuhi, akiwa wa kwanza kabla ya wagombea wengine wa nafasi hiyo, kama alivyofanya wakati wa uchukuaji fomu Agosti 9, 2025.

Rais Dk Samia ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, alisindikizwa na baadhi ya viongozi wa kitaifa wa chama hicho, huku akiambatana na mgombea mwenza, Dk Emmanuel Nchimbi.

Baadhi ya walioambatana naye katika tukio hilo ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Stephen Wasira, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt Asha Rose Migiro na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT), Mary Chatanda, sambamba na wajumbe wengine wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC).
Huyo mwenyekiti wa tume aliyeteuliwa na CCM unategemea atamwambiaje SAMIA? Wakati mwingine tutumie akili zetu badala ya utumbo.....Atapendelewa siku zote.....aseme ngwe' tuone kama ajira yake itabaki?
 
TOKA MAKTABA :
Mzee John Cheyo - "Hili la vyama vinavyojiita Chama Tawala na Chama Kikubwa kuteka agenda za nchi halikubaliki"

27 Agosti 2025
Dodoma, Tanzania

NLD WARWJESHA FOMU YA URAIS

1756290938145.jpeg

Mhe. Doyo Hassan Doyo wa NLD mgombea urais akiwa ameambatana na mgombea mwenza NLD, Mhe. Chausiku Khatib Mohamed,

AAFP WAREJESHA FOMU YA URAIS

1756291027977.jpeg

Mgombea wa Nafasi ya uRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Wakulima (AAFP), Kunje Ngombale Mwiru akiwa na Mgombea Mwenza Chumu Abdallah Juma.

UDP NACHO CHAREJESHA FOMU

1756291078072.jpeg

Bi. Saumu Rashid, Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Juma Khamis Faki, Mgombea Mwenza

1756292120578.jpeg
 
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya chama cha ADA -TADEA, Bw. Georges Bussungu, akiambatana na Mgombea Mwenza Bw. Ally Issa Makame, wamerudisha fomu
1756292278953.jpeg
 
Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amewatangulia wagombea urais wa vyama vingine kurudisha fomu ya uteuzi katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ndejengwa jijini Dodoma leo, Jumatano Agosti 27, 2025.

Hatua hiyo, inampa nafasi mkuu huyo wa nchi ya kusubiri uteuzi wa INEC, kisha kuanza mchakamchaka wa kampeni za uchaguzi, zitakazofanyika kwa kipindi cha siku 60.

Soma pia: Kurudisha fomu kwa Samia bado kitendawili

View attachment 3454690

Rais Samia ambaye ndiye mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), atazindua rasmi kampeni za uchaguzi huo, kesho Alhamisi Agosti 28, 2025, katika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, Dar es Salaam.

Mgombea huyo wa CCM, amefika katika ofisi za INEC, saa moja na dakika 50 asubuhi, akiwa wa kwanza kabla ya wagombea wengine wa nafasi hiyo, kama alivyofanya wakati wa uchukuaji fomu Agosti 9, 2025.

Rais Dk Samia ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, alisindikizwa na baadhi ya viongozi wa kitaifa wa chama hicho, huku akiambatana na mgombea mwenza, Dk Emmanuel Nchimbi.

Baadhi ya walioambatana naye katika tukio hilo ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Stephen Wasira, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt Asha Rose Migiro na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT), Mary Chatanda, sambamba na wajumbe wengine wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC).

Ila ucheo anautaka kwa kweli. Looh!
 
Hivi huyu Nchimbi ana undugu na yule Pimbi aka Dr. Love wa magazeti ya Sani maana ni kopiraiti kabisa.
 
😂
Hii imenikumbusha Ile ya JPM 2020

Alirudisha wa kwanza akawa wa kwanza kwenye karatasi la kupigiwa kura na chadema walikuwa wa mwisho hvy wakawa wa mwisho kwenye karatasi 😂

2025 chadema watakuwepo kwenye karatasi la kura ila watakuwa wa mwisho.

🔥
 
Back
Top Bottom