GE2025 Samia kawa wakwanza kurudisha fomu INEC

GE2025 Samia kawa wakwanza kurudisha fomu INEC

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kwa mara ya kwanza tunapata Mgombea na Mgombea mwenza wake wenye macho yabkufanana
Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amewatangulia wagombea urais wa vyama vingine kurudisha fomu ya uteuzi katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ndejengwa jijini Dodoma leo, Jumatano Agosti 27, 2025.

Hatua hiyo, inampa nafasi mkuu huyo wa nchi ya kusubiri uteuzi wa INEC, kisha kuanza mchakamchaka wa kampeni za uchaguzi, zitakazofanyika kwa kipindi cha siku 60.

Soma pia: Kurudisha fomu kwa Samia bado kitendawili

View attachment 3454690

Rais Samia ambaye ndiye mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), atazindua rasmi kampeni za uchaguzi huo, kesho Alhamisi Agosti 28, 2025, katika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, Dar es Salaam.

Mgombea huyo wa CCM, amefika katika ofisi za INEC, saa moja na dakika 50 asubuhi, akiwa wa kwanza kabla ya wagombea wengine wa nafasi hiyo, kama alivyofanya wakati wa uchukuaji fomu Agosti 9, 2025.

Rais Dk Samia ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, alisindikizwa na baadhi ya viongozi wa kitaifa wa chama hicho, huku akiambatana na mgombea mwenza, Dk Emmanuel Nchimbi.

Baadhi ya walioambatana naye katika tukio hilo ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Stephen Wasira, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt Asha Rose Migiro na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT), Mary Chatanda, sambamba na wajumbe wengine wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC).
 
UMD KUPAMBANA NA CCM ambapo wagombea warudisha fomu
1756292743841.jpeg

Bi. Mwajuma Mirambo anayegombea nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu wa 2025 kwa tiketi ya Chama cha UMD akiambatana na Mgombea Mwenza Bi. Mashavu Alawi Haji,
 
Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amewatangulia wagombea urais wa vyama vingine kurudisha fomu ya uteuzi katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ndejengwa jijini Dodoma leo, Jumatano Agosti 27, 2025.

Hatua hiyo, inampa nafasi mkuu huyo wa nchi ya kusubiri uteuzi wa INEC, kisha kuanza mchakamchaka wa kampeni za uchaguzi, zitakazofanyika kwa kipindi cha siku 60.

Soma pia: Kurudisha fomu kwa Samia bado kitendawili

View attachment 3454690

Rais Samia ambaye ndiye mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), atazindua rasmi kampeni za uchaguzi huo, kesho Alhamisi Agosti 28, 2025, katika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, Dar es Salaam.

Mgombea huyo wa CCM, amefika katika ofisi za INEC, saa moja na dakika 50 asubuhi, akiwa wa kwanza kabla ya wagombea wengine wa nafasi hiyo, kama alivyofanya wakati wa uchukuaji fomu Agosti 9, 2025.

Rais Dk Samia ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, alisindikizwa na baadhi ya viongozi wa kitaifa wa chama hicho, huku akiambatana na mgombea mwenza, Dk Emmanuel Nchimbi.

Baadhi ya walioambatana naye katika tukio hilo ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Stephen Wasira, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt Asha Rose Migiro na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT), Mary Chatanda, sambamba na wajumbe wengine wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC).
Kwani mgombea wa ccm anawapinzani? Acheni mzaa, uyu mkurugenzi anatetemeka tu
 
1756292955451.jpeg

Muasisi wa Chama cha UDP mzee John Cheyo asema kwa furaha kuwa hakijakosa kutumia fursa ya kikatiba kuwania uongozi wa nchi, hivyo kila kipindi cha uchaguzi kilisimamisha wagombea bila kukosa.

Na uchaguzi wa 2025 UPD imewapeleka Bi. Saumu Rashid, kama mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huku Bw. Juma Khamis Faki, ni mgombea mwenza.
 
SERA YA MCHAKAMCHAKA YA AAFP YAFAFANULIWA NA MGOMBEA KINJE MWIRU
Wagombea urais wa Jamhuri ya Muungano katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025 wakizungumza :

View: https://m.youtube.com/shorts/BCaqfIBsDWw
Mgombea wa Nafasi ya uRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Wakulima (AAFP), Kunje Ngombale Mwiru
 
View attachment 3454869
Muasisi wa Chama cha UDP mzee John Cheyo asema kwa furaha kuwa hakijakosa kutumia fursa ya kikatiba kuwania uongozi wa nchi, hivyo kila kipindi cha uchaguzi kilisimamisha wagombea bila kukosa.

Na uchaguzi wa 2025 UPD imewapeleka Bi. Saumu Rashid, kama mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huku Bw. Juma Khamis Faki, ni mgombea mwenza.
Uyu mzee atafia jukwaani haibu gani hii
 
Unawaona wote wanaoingia msikitini?It is too low even for your level.
Kikwete alikuwa anaingia kila ijumaa pale kinondoni Muslim hata video na picha zipo kwanini huyu Maza hatujawahi kuona hata picha Tu akiingia msikitini?
 
UMD TUPO TAYARI KUPAMBANA NA CCM KUCHUKUA DOLA KWA KUSHINDA UCHAGUZI OKTOBA 2025

Bi. Mwajuma Mirambo : UMD Tunasisitiza sera ya majimbo na maisha laini 2025 tukiingia Ikulu

View: https://m.youtube.com/watch?v=lFR_3Ud_XlQ

Bi. Mwajuma Mirambo anayegombea nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu wa 2025 kwa tiketi ya Chama cha UMD akiambatana na Mgombea Mwenza Bi. Mashavu Alawi Haji afunguka utayari wa UMD kushiriki vilivyo hadi ushindi ktk uchaguzi wa Oktoba 2025
 
Japokua hao watu wawili kwenye picha siwajui lakini body language inaonyesha huyo mama aliyekaa ni boss na huyo mwenye kidoti kwenye komwe ni chawa wake.
 
27 Agosti 2025

ACT WAZALENDO WAGONGA MWAMBA KUREJESHA FOMU

LUHAGA MPINA AAMBIWA AJE BAADAYE MAANA WAGOMBEA WA VYAMA VINGINE WANASHUGHULI YA KUREJESHA FOMU

View: https://m.youtube.com/watch?v=zI_ammzSoH4
Luhanga Mpina mgombea wa ACT WAZALENDO aliyetangazwa kuwa ni mgombea batili, leo aliishia nje ya geti kutokana na shughuli iliyokuwa inaendelea katika makao makuu ya INEC kupokea fomu za wagombea ambao wamekubaliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama Vingi.

Msajili wa vyama vingi alitangaza mapema kuwa mgombea wa ACT WAZALENDO amekosa uhalali w kugombea urais kutokana na katika ya chama chake kutozingatia vigezo vya kupatikana mgombea wao wa ACT WAZALENDO.

Hivyo mgombea huyo mwanasiasa machachari kuenguliwa kushiriki ktk mbio za kugombea nafasi ya urais Luhaga Mpina .

Geti likiwa limefungwa la INEC na kumuomba Luhaga Mpina aje siku nyingine na wakati mwingine baada ya siku ya leo tarehe 27 Agosti 2025 kuisha, ambayo ni siku pekee maalum iliyotengwa ya kurudisha fomu ya kugombea urais 2025.
 
Kikwete alikuwa anaingia kila ijumaa pale kinondoni Muslim hata video na picha zipo kwanini huyu Maza hatujawahi kuona hata picha Tu akiingia msikitini?
Unajua taratibu za kuswali kwa wanawake kwenye Uislamu.? Na ni bora zaidi waswali manyumbani.Na ibada ni jambo private baina ya mja na Mwenyezi Mungu wake.
 
Huenda tangu asubuhi kesho itakuwa ni shughuli ya kusomba Wanachama wa CCM kutoka jiji la Dar na mikoa ya Pembezoni! Kwa malori na mabasi.
Vile vile nadhani kesho hali ya Usafiri ikawa siyo nzuri.
Naona kama kampeni zinaanzia Viwanja vya TP kumpa Salamu Gwajima kwamba anapoteza muda.
 
K
Wanadai 'ujanja' ni kuwahi, leo nimethibitisha msemo huu wa wahenga

View attachment 3454775
Kwaiyo jina la kwanza likiwa la Rais Samia Suluhu Hassan kwenye form msitupigie mikelele hapa kuwa kwanini kawekwa mbele yeye ndio wa kwanza kufika 💪💪💪 ndio wa kwanza ndio kawai wapili ndio wapili imeisha iyoo ✍️
 
CCM wanacheza na hadhira kisaikolojia na kipropaganda , ili wakubali matokeo ya INEC NIDA mchezo ukiisha kuwa mgombea wao anautaka urais ili kukamilisha kazi aliyoianza.
 
Back
Top Bottom