Samia anasema Ajira si jukumu la Serikali. So msitegemee kitu

Samia anasema Ajira si jukumu la Serikali. So msitegemee kitu

Jukumu la serikali ni kuweka Mazingira yanayochochea Ajira. Ni jukumu la sekta binafsi kutengeneza Ajira.
Jukumu la Sekta Binafsi kutengeneza faida kubwa iwezekanavyo kwao na kwa wana HISA wao employment ni by the way kwahio kwenye karne tunayoelekea ya kutumia cameras, tractors na machinery badala ya binadamu kufanya kazi usitegemee wataajiri watu na hakuna mtu wa kuweza kuwalaumu sababu watakuwa wamekidhi Primary Objective yao (Making Money)

Now sababu tunafahamu hilo na tupo kwenye crossroads watu hawana ujira wala buying power hata sekta binafsi ikifanya production huenda ikakosa soko..., kwa nchi ambayo ina vivutio na natural resources za kumwaga, nchi ambayo watu wanakosa huduma za afya na kukosa wakufunzi wakati wamezagaa kitaa, nchi ambayo ina vyanzo vya umeme lakini unatumia kodi ya mlalahoi kununu gesi ughaibuni...., Niambie ni nani hapo mwenye Kosa ? Sekta Binafsi ambaye akiweka biashara yake huenda akaunguza mtaji kutokana na kukosekana kwa soko au serikali ambayo ipo busy kujisafisha kwamba hili au like sio jukumu letu ? Bila kuhakikisha ujira wa watu hao wao watapata vipi mahitaji yao Muhimu.... Okay bora waache kila kitu ila mbona Kodi / Tozo zinazidi ?!!!



 
Back
Top Bottom