Sambwee Shitambara aachwa solemba na wananchi

Yaelekea tuhuma za kupokea fweza ili kuuza jimbo zina ukweli fulani. Huyu bwana anaonekana atakuwa new Tambwe Hiza huko SiSieM.
 
Uelewe kwanza basi kabla huja-post bana! Prof Safari ulimsikia akisema maneno kama haya:

"ametangaza kuibomoa ngome ya chama chake za zamani mkoani Mbeya Mbele ya Mjumbe wa Kudumu wa Kamati Kuu, Dkt. John Malecela huku akitamba kuwa kwa kadri alivyokijenga chama hicho ndivyo atavyokibomoa kwa mikono yake mwenyewe."

"Alisema kuwa CHADEMA ni chama chenye watu wasioweza kufikiri kwa haraka"


Hakuna mtu anaekerwa na kuondoka kwake chadema hapa, suala ni maneno anayoyasema hayaendani kabisa na elimu yake,kitu kinachoeleza kuwa tatizo la CCM halipo kwenye magamba tuu,limeingia damuni kabisa. Yaani "my learned brother" kabisa ameshakua na akili za kitambwe-tambwe (Hiza)mara hii? Kumbe mission yake ni "kubomoa" chama fulani tu? yaani kweli kuna watu wamepunguza thamani ya siku zao za kuishi duniani to this low!!!Hilo tu ndo linalosikitisha. As for him moving on, CDM is as happier, because he would have been given the sack anyway.....loong time!

Wazee mbona muna hasira? Mbona hatukusikia haya mlipo mpokea Prof. Safari? Akihamia poa, akihama noma? Acheni hizo!
 




Na Tumaini Makene

MMOJA wa mabingwa wa sheria, ambaye pia ni Profesa wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere cha Chuo Kikuu Dar es Salaam, Issa Sivji, amesema wananchi, hasa vijana, ndiyo
wanatakiwa kuwa cheche ya kudai mabadiliko na kuikomboa nchi, hasa katika zama hizi ambapo viongozi wanatumia madaraka yao kujitajirisha.

Akizungumza na waandishi wa habari jana wakati wa mapumziko ya Kongamano la Wiki ya Mwalimu Nyerere lililoanza juzi katika Ukumbi wa Nkrumah, Prof. Shivji alisema kuwa baada ya 'kuuawa' kwa Azimio la Arusha, viongozi nchini sasa wanatumia nafasi zao kujitajirisha, huku wananchi ambao walipigania uhuru wa nchi, wakiachwa kando.

Prof. Shivji aliyasema hayo alipozungumzia uamuzi wa Kigoda cha Mwalimu kuchapisha Kitabu cha Azimio la Arusha na kuendelea kukigawa bure kwa wananchi licha ya azimio hilo kuuawa miaka ya tisini, baada ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kukutana Visiwani Zanzibar.

Alisema kuwa wakati wa kuadhimisha miaka 30 ya CCM, chama ambacho kimekuwa madarakani tangu uhuru, wananchi walisikika wakikumbuka azimio hilo wakisema kuwa liliwajali watu wanyonge, kwa kuwa lilizungumzia utu wa binadamu, miiko ya uongozi na maendeleo ya watu kwa ujumla, hivyo linastahili kurudishwa.

"Kimsingi sisi tunachapisha tu hili azimio na kulisambaza kwa watu, lakini ni wananchi wenyewe, tena ninyi (waandishi wa habari) ndiyo mliwauliza na wakasema kuwa Azimio la Arusha liliwajali wanyonge, lilizungumzia misingi ya utu wa binadamu na maendeleo, lakini sasa viongozi wameliacha na wananchi wamewekwa pembeni.

"Mimi kwa kweli wakati mwingine nasita hata kuwaita hawa ni viongozi...maana kiongozi ni yule anayeona majukumu ya kuwatumikia watu. Hawa wanatumia madaraka ya kisiasa, wanatumia vyeo vyao kujitajirisha, wanapenda madaraka...kiongozi wa kweli ni yule asiyependa kuongoza, asiyekimbilia madaraka, maana anauona uongozi ni majukumu. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema hili, kiongozi ni yule asiyeona utamu katika madaraka, anaona majukumu, kiongozi ni yule anayekataa madaraka.

"Wanatumia madaraka kujitajirisha na kuwasahau wananchi. Sasa ni wakati mwafaka kwa wananchi, hasa vijana kuichambua jamii yao, kutafakari, historia ya nchi yao, wapi tulikotoka, tunakwenda wapi, vijana ndiyo wanapaswa kuwa cheche ya kuikomboa nchi yao wenyewe," alisema Prof. Shivji.
 
Jina la Zitto linavuma kwenye mitaa, jina lake lina hadhi ya Kisupastaa, jina lake linaongeza idadi ya maadui wengine wako CDM na wengine ni CCM!
 
.....am amazed by his words! watanzania njaa zinafanya tunasahau hata tunasimamia upande upi, shitambala njaa imemzidi acheni atetee tumbo lake, tatizo ni kwamba amechagua sehemu mbaya kutetea njaa yake, Tz ya sasa sio ile ya zidumu fikra za mwenyekiti and yada yada yada.. Anyway this is another cheap and stupid politics
 
Ipo siku mtamuacha Zitto na kuendesha maisha yenu. Siku hiyo ikifika ndio mtaanza kujiuliza kilichokuwa kinawasukumu kumjadili kwa mistari isiyo na vina kilikuwa kipi? Jina la Zitto limewakosea nini? Limewasikitisha nini? Nijibuni!
 
jAMANI hayo ni maoni yake yupo huru kutoa maoni,hakuna wa kumzuia Mh Zito ktk kutoa maoni,lakini pia hatuwezi kumjaji mtu ama kumsemea mtu kwa jambo fulamu tusilikuwa na uhakika nalo,tumwache Kijana Mh Zito afanye kaze zake na pia aendelee kutoa maoni kadri afikiliavyo na aonavyo tusitake kumziba mdomo

Criticism to a politician,whether distructive or constructive,is in his/her job description.
An engineer might not understand this.
 
Na Charles Mwakipesile, Mbeya

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) mkaoni Mbeya ambaye sasa amejiunga na CCM, Bw. Sambwee Shitambala ametangaza kuibomoa ngome ya chama chake za zamani mkoani Mbeya Mbele ya Mjumbe wa Kudumu wa Kamati Kuu, Dkt. John Malecela huku akitamba kuwa kwa kadri alivyokijenga chama hicho ndivyo atavyokibomoa kwa mikono yake mwenyewe.

Alisema kuwa anathamini kwa sehemu kubwa heshima aliyopewa na uongozi wa chama ukiongozwa na Rais Kikwete, baada ya kuamua mwenyewe kujiunga na chama hicho kutokana na usaliti anaodai alifanyiwa na uongozi wa CHEDEMA.


Alisema kuwa viongozi hao badala ya kufanya kazi kwa maslahi yao wamekuwa wakifanya kazi kwa ajili ya kutafuta umaarufu wao wenyewe.


Alisema wakati akiwa katika chama hicho walikuwa wakifanya kampeni kwa kutangaza wazi kuwa wakiingia madarakani watahakikisha kuwa wanaendesha nchi katika hali ya amani na utulivu, lengo likiwa ni kuwaunganisha Watanzania na kujipatia maendeleo yao wenyewe pasipo kufanya vurugu hali ambayo alisema kuwa imekuwa tofauti na makubaliano hayo.


Bw. Shitambala alisema kuwa kutokana na kuwa mpiganaji na msomi wa sheria alishangaa kuona viongozi hao ambao wengi wao ameshiriki kuwapa ubunge wakigeuza ajenda na kuamua kuanzisha maandamano nchi nzima na kutoka nje bungeni wakati Rais Kikwete akihutubia hali ambayo alisema ni utovu mkubwa wa nidhamu.


"Hatukukubaliana kufanya maandamano ya kuvunja amani wala hatukuwatuma waende wakatoke bungeni na kisha kurudi ukumbini kwa kujadili hotuba ya rais, nawaambia ndugu zangu hii ni sababu kubwa iliyonifanya nikaamua kuondoka katika chama hicho.


Alisema kuwa CHADEMA ni chama chenye watu wasioweza kufikiri kwa haraka kutokana na ukweli kuwa Watanzania wanazo akili za kutosha kujitambua na kutoyumbishwa wala kuamuliwa juu ya amani ya nchi yao.

Kama hizi ndiyo hoja zake basi hajui anachofanya. Kwa kifupi amepotea njia. CCM yenyewe imekiri kuwa imekosa mvuto kwa wananchi halafu wewe ndiyo unajiunga nayo. Hiki ni kituko cha mwaka. Elimu anayosema anayo haimsadii. Halafu siasa na sheria ni taaluma mbili tofauti.

Eti anasema yeye ni mpiganaji, Wewe ni mpiganaji gani ambaye unajiunga na adui wakati vita inaendelea?
 
Wazee mbona muna hasira? Mbona hatukusikia haya mlipo mpokea Prof. Safari? Akihamia poa, akihama noma? Acheni hizo!

Jesuit, hapa sio swala la kuongea mtu akihama....kuhama kila mtu anahaki yake na ni vema lakini kuna maswali ya kujiuliza mtu anaposema anabomoa alipojenga...je alimjengea nani, ni wananchi au tumbo lake?

Waliokomaa kama Safari hawawezi hata siku moja kuzungumzia kubomoa walikotoka...watasema kwa nini wamejiunga na sikumbuki kama alisema "kama nilivyojenga CUF nitabomoa CUF"...huu ni upuuzi....we eneza itikadi zako na mwengineyo lakini sio matisho ya kubomoa na majigambo kuwa ndie uliejenga kana kwamba wananchi wafuasi wa vyama husika vya upinzani ni matofal unayoweza yapanga na kuyapangua
 
Sijui kama huyu anajua kuwa fomu yake ya ubunge ilikosewa kimakusudi ili viongozi wake wachukue fedha kutoka CCM? Kama hawa CCM wangekuwa wanampenda wasingemhujumu kupitia viongozi wa CDM. Lakini kwa kuwa kaungana nao huenda akatoa ile ripoti ya kwa nini fomu yake ilikosemwa wakati yeye ni wakili anafahamu sheria vema.
 
zitto ni reasonable mind,he got all sign of extraordinar future that why kivuli chake kinatesa wengi. .
Ila unatia aibu kusema zito ndo amepeleka watu chadema,nadhan yeye anafahamu kua kinachomfanya messi awe bora ni wachezaji wenzake,namba anayocheza,club,kocha,timu pinzani. .tht why he did nt make it kwenye timu ya taifa agentina. .
 

Zitto: Shitambala ajimaliza

Asema amejiunga kwenye chama kinachokufa

na Christopher Nyenyembe, Mbeya


NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe, amesema aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mbeya, Sambwee Shitambala, amejimaliza kisiasa kwa hatua yake ya kuhamia kwenye Chama cha Mapinduzi (CCM).

Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alisema Shitambala ameshindwa kusoma vema alama za nyakati na matokeo yake amejiunga na CCM inayokufa.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka mjini Dodoma anakohudhuria vikao vya Mkutano wa 10 wa Bunge alisema Shitambala hawezi tena kung'ara akiwa CCM kwani amekikimbia chama ambacho sasa hivi ndicho kinachopendwa na kuwavutia mamilioni ya Watanzania.

"Nimeshtushwa sana na uamuzi wa Shitambala kuhamia CCM najua ametumia haki yake ya kidemokrasia lakini hakuweza kusoma alama za nyakati …CCM aliyoikimbilia inaelekea kufa, amejimaliza na atakuja kujutia uamuzi aliochukua wakati CHADEMA sasa ndiyo chama kinachozidi kupanda chati," alisema Zitto.

Alisema kuondoka kwa Shitambala hakuwezi kuteteresha jitihada za CHADEMA mkoani humo za kuzidi kuchota majimbo mengine, kwani wana wanachama na wafuasi wengi ambao wameonyesha dhahiri kuchoshwa na ahadi zisizotekelezeka za CCM.

Source: Tanzania Daima
 
Msimlaumu jamani anaanza kuzifanyia kazi zile M 600 alizolamba mwaka jana.Shitambala alikuwa zigo la mavi halibebeki
 
Wana jf naomba kuwauliza kwanini zitto?kila napoona thread ya mtu aki comment postive kuhusu zitto watu wanakashifu na kumkosea heshima?

Naamini na nitaendelea kuamini hivi - heshima kubwa iliyo nayo cdm mbele ya watanzania kwa mchango mkubwa ni kwa ajili ya zitto, wangapi mlikuwa wanachama au mashabiki wa cdm kabla ya zitto kuwasha moto katika bunge la tisa?wangapi mlikuwa mnaikubali cdm kabla ya zitto kuonyesha msimamo thabiti mpaka kufukuzwa bungeni katika kashafa ya buzwagi? Hebu kuweni waungwana na mpeni heshima yake jamani

wengi mnamuona zitto mbaya toka alipotaka kugombea uenyekiti wa cdm , ila si ametumia haki yake ya kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa?mnamuona mbaya pale anapotofautiana mitazamo na baadhi yetu- ila mitazamo tofauti daima ni manufaa ya chama kama daima mnakubaliana hamuwezi kuwa na jipya

Ni kweli akisemwa vibaya hata mimi sifurahii, anamchango mkubwa kwenye upinzani ndani ya nchi yetu lakini si kwamba yeye ndiye aliyechangia peke yake chadema imechangiwa na wengi na zaidi sana SLAA.

Mimi na mpongeza sana ZITO ni buldoza ya upinzani bungeni, nafikiri mmeona jana kwenye mjadala bungeni jinsi alivyokuwa na ujasiri wa kumtetea Wenje katikati ya zomea zomea ya wabunge wa ccm
 
Back
Top Bottom