Sambwee Shitambara aachwa solemba na wananchi

Sambwee Shitambara aachwa solemba na wananchi

Hawa ndio viongozi uchwara. Uchoyo (selfishness) tu! Watu wote walio CDM, na wanaoiunga mkono, bado anatokea mtu anadiriki kusema yeye ndio aliyoijenga CDM, kwa mikono yake mwenyewe! What a selfish attitude! Halafu kibaya zaidi waandishi wa habari wanaandika tu bila kumuuliza afafanue aliijenga je CDM kwa mikono yake. Wnagemuuliza, au wangetafuta wenyewe, aliingia lini CDM - 1992? au kabla? Au lini?
 
Mnafiki bwana utamjua tu................

Maneno haya angeyasema alipokuwa angali kwenye cdm,

but as for now chochote anachosema inakuwa kama mwanamke anayemdanganya mwanaume ili afanikiwe kumchuna.

kifupi ashawafanya chama cha magamba ni BUZI, anawawekea mazingira tu, aonekane anampenda sana huyo bwanake ccm ili akishaingia line aanze kumchuna
 
Huyu ndugu Shitambala anafanya mambo tunayoyaita ya mbwa kurudia matapishi yake au nguruwe ambaye amekwishaogeshwa kurudi kwenye matope kwa sababu zifuatazo:
1.Kama aliibomoa CCM na kuijenga CDM na kutaka kurudi CCM ili aibomoe CDM kwa mawazo yangu namuona kama mtu wa ajabu sana; ni nyumba gani itakayomfaa? maana zote kaziboa.
2. Akumbuke kwamba aliibomoa CCM kwa sababu imejengwa ktk msingi dhaifu kwani miaka hamsini ya uhuru umeme shida, maji n.k ni shida na hadi leo wanafikiri watu wananchi wana shida na sura (gamba uongo).
3. Aliweza kujenga CDM kwa viwango (CDM standard) vilivyotolewa na chama na hakutumia tofari bali aliijenga kwenye mioyo ya watu sasa ataitoa kwa viwango vipi? au vya magamba sura ya ccm?

Namshauri ajiandae kufanya yafuatayo ndani ya gofu lake la zamani - ccm
1. Atoe ushauri wa kisheria kwa Makamba jinsi ya kuandaa makao ya magamba mengine yatakayomfuata.
2. Aanze kuandaa utetezi kwa waliopewa siku 90 ili wajipeleleze ili wa kifukuzwa awatetee mbele ya mkuu wao..
3. Awasaidie ccm kwamba huko nilikokowa nilipopajenga ni kazi ngumu kupabomoa kwani hawadanganyiki na sura hata nikirudi mwenyewe.
4. Waambie hao wa gofu lako ulilolibomoa kuwa wananchi wanashukuru maandamano ya CDM (hata wewe mwenyewe kwa sababu bei ya sukari imeshuka, bei ya vyakula itashuka (kuamliwa chakula kiingizwe sokoni kutoka maghala ya serikali), Dowans haikulipwa na wala mkataba wa kidharula haukufanikiwa n.k.
If your ship doesn't come in swim out to it.

 
Huyo ni sawa na mtu aliacha mwenzi ilhali bado anampenda , atajitahidi kusema yasiyofaa na kujifanya mwema kuwaepusha wengine ilhali lengo lake kuu ni kujifariji kwa kosa lake mwenyewe.
yeye hajui hata Slaa akirudi ccm CHADEMA itabaki iendelee.
 
tunakupa mwaka mmoja hutakaa usikike kwenye medani ya kisiasa unazo ml 600 ulizouza ubunge unafikiria tumesahau ndio mana unajeuri
 
na ndo maana ameshindwa kuhold wota!
anachofanya ni makosa sana kuanza kupakaza. anasahau kwamba usitukane mamba kabla hujavuka mto na kwamba, "dont burn bridges on your way cause they may help you on your way back"
yatamshinda huyu shitambala
 
Ngoja wamtumie kwanza!! Lakini muungwana hafanyi hivyo! kuna haja ya kuanzisha sheria kali kwa watu kama hawa wanaopenda kuvujisha siri za chama (Confidential Information) ili next time mtu akiamua kuhama ahame yeye na aheshimu aliko toka.
 
Kumbe haya ni ya kweli? Alisema kuwa CHADEMA ni chama chenye watu wasioweza kufikiri kwa haraka kutokana na ukweli kuwa Watanzania wanazo akili za kutosha kujitambua na kutoyumbishwa wala kuamuliwa juu ya amani ya nchi yao.
 
Hii habari imeandikwa na gazeti gani? Lingesema pia kuwa alikuwa anahutubia watu wangapi...
 
Hii habari imeandikwa na gazeti gani? Lingesema pia kuwa alikuwa anahutubia watu wangapi...

Nashukuru umeliona hilo mkuu - mwandishi wa habari hii hakuwa balanced. Zomea zomea hakuiona yeye. Huyu ni shemeji ya Shitambala na ni muumini mkuu wa CCM na hasa pale viongozi wa CCM wanapokuwepo. Hilo ni Majira mkuu.
 
Shitambala acha kujitia aibu, eti unasimama kwenye mkutano na unadiriki kusema muswada wa katiba hauna tatizo lolote? Kelele zote toka bara hadi visiwani wote hao ni wendawazimu? Hata kama umeondoka CDM nakushauri simamia ukweli na acha njaa maana unaumbuka.😛anda:


Hapo kwenye red!! Kisha anasema yeye ni msomi wa sheria! On the contrary watu wanatoka nje ya bunge na kuandamana kwa sababu wanajua sheria. Honesty Shitambala ansumbuliwa na njaa zaidi, siamini kama kweli ana uelewa mdogo kiasi hiki. Come to think of it, CCM wanajipanga kuandamana kuunga mkono kijivua gamba je atasemaje hapo? Please give us a break.
 
Ukisoma waraka mzima kwa kweli hana tuhuma za kuwatuhumu Chadema ameshikwa na kigugumizi amerudia maneno yanayosemwa na wana CCM anajua hasira ya wana Mbeya juu yake ,akapumzike kwa amani milele amina
 
mbwa koko huyo.paka shume,fisi maji huyo.tulimjua mapemaaaa!!! aende aka wa bong'olee watoa magamba!!!!
 
Shinyambala ni mfa maji................................
 
Sasa angesema nini jamani mbele ya mkulu (ccm) wake mpya? Inabidi ajitutumue kidogo hata kwa maneno!
 
amefulia huyo....... alishajua kwamba anakaribia kufukuzwa cdm so kaamua kujifukuzsha mwenyewe
 
Back
Top Bottom