Sambwee Shitambara aachwa solemba na wananchi

Sambwee Shitambara aachwa solemba na wananchi

Imeonekana misululu ya magari na matipa ya CCM yakizomewa kwa nguvu zote wakati yakitoka "mkutanoni" . Watembea kwa miguu wenye sale wanazomewa. Jumamosi iko kazi. Wananchi wanasikitika huyu jamaa kawasaliti mchana kweupe!!

Siasa kitu cha ajabu aliowatukana akiwa CDM ndo hao anakokotana nao kwenye msululu.

Amakweli hakuna adui wa kudumu kwenye siasa!
 
Mbona kulikuwa na watu wengi sana? Pia wajumbe wa CCM kutoka wilaya mbalimbali walihudhuria.

Ujumbe wako hauko sahihi kabisa.
pamoja na kuwaleta watu toka sehemu mbalimbali za wilaya nane za mkoa wa Mbeya na nchi jirani Malawi bado idadi haikuwazidi wana uyole waliotaka kusikia shitambala atasema nini na sababu zilizomtoa Chadema ukweli walienda kumsuta ,ndio maana walitulia kusikiliza hata mzee Tinga tinga alivyokuwa anauza sera hawakumbughudhi,Shitambala alivyoanza kuwambia wananchi waachane na chadema eti ni chama kisichokuwa na sera,eti wao badala ya kufanya maendeleo wanaandamana,eti wanataka kuhatayarisha usalama kwa kudai katiba wananchi wakaanza kupiga miluzi,kelele wakawa wanamzomea ,huku vidole viwili vikitawala, kukawa vurugu hakuna kusikilizana ,miluzi kwa wingi tuuu , makofi ile mbaya yake, Mwandosya akawa very uncomfortable alikuwa anajigeuza kushoto kulia haamini macho yake manake alijidai ni raisi wa Mbeya,wananchi kwa kweli wamewapa dozi yao, mashuhuda waliopigwa na juumizwa wakilinda kura zake walikuwepo pia wakimkumbusha ilivyokuwa mbaya kwa usalama wao ,wakamuuliza kipi heri maandamano ya amani ya chadema au mateso waliyopata kupigwa virungu na polisi walivyotoka pale wakajipanga barabarani kuwazomea wa kwenye magari na yeyote aliyekuwa amevaa sare ya CCM,kama wanauwezo wakae mpaka jumamosi waone maandamano yatakavyotisha
ya wananchi
 
Muda wake umekwisha.. Sasa atakuwa mpambe nadhani wa nape nauye na wenzie...
 
Jamani sasa sisi wanachadema tulio na kesi na huyo jamaa alikuwa anatutetea bure,tufanyaje?...mwe....mwe....mwe... nitafungwa jamani
 
Jamani sasa sisi wanachadema tulio na kesi na huyo jamaa alikuwa anatutetea bure,tufanyaje?...mwe....mwe....mwe... nitafungwa jamani
Poel ulikuwa unatetewa wakili kilaza, ndio maana aliamua kujiapisha mwenyewe wakati anagombea Ubunge kinyume na sheria. Kabla hajahamia Chadema ulikuwa unatetewa na nani? Kama vipi na wewe kasomee sheria au hamia CCM aendelee kukutetetea
 
uzuri wa mshiko nikwamba ukiwa nazo utaona ulifanya jambo la msingi ngoja siishe utajuta mara mia yake ,TANZANIA BILA UFISADI NA CCM INAWEZEKANA TIMIZA WAJIBU WAKO JITAMBUE ILI UWE HURU
 
Na Charles Mwakipesile, Mbeya

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) mkaoni Mbeya ambaye sasa amejiunga na CCM, Bw. Sambwee Shitambala ametangaza kuibomoa ngome ya chama chake za zamani mkoani Mbeya Mbele ya Mjumbe wa Kudumu wa Kamati Kuu, Dkt. John Malecela huku akitamba kuwa kwa kadri alivyokijenga chama hicho ndivyo atavyokibomoa kwa mikono yake mwenyewe.

Alisema kuwa anathamini kwa sehemu kubwa heshima aliyopewa na uongozi wa chama ukiongozwa na Rais Kikwete, baada ya kuamua mwenyewe kujiunga na chama hicho kutokana na usaliti anaodai alifanyiwa na uongozi wa CHEDEMA.

Alisema kuwa viongozi hao badala ya kufanya kazi kwa maslahi yao wamekuwa wakifanya kazi kwa ajili ya kutafuta umaarufu wao wenyewe.

Alisema wakati akiwa katika chama hicho walikuwa wakifanya kampeni kwa kutangaza wazi kuwa wakiingia madarakani watahakikisha kuwa wanaendesha nchi katika hali ya amani na utulivu, lengo likiwa ni kuwaunganisha Watanzania na kujipatia maendeleo yao wenyewe pasipo kufanya vurugu hali ambayo alisema kuwa imekuwa tofauti na makubaliano hayo.

Bw. Shitambala alisema kuwa kutokana na kuwa mpiganaji na msomi wa sheria alishangaa kuona viongozi hao ambao wengi wao ameshiriki kuwapa ubunge wakigeuza ajenda na kuamua kuanzisha maandamano nchi nzima na kutoka nje bungeni wakati Rais Kikwete akihutubia hali ambayo alisema ni utovu mkubwa wa nidhamu.

"Hatukukubaliana kufanya maandamano ya kuvunja amani wala hatukuwatuma waende wakatoke bungeni na kisha kurudi ukumbini kwa kujadili hotuba ya rais, nawaambia ndugu zangu hii ni sababu kubwa iliyonifanya nikaamua kuondoka katika chama hicho.

Alisema kuwa CHADEMA ni chama chenye watu wasioweza kufikiri kwa haraka kutokana na ukweli kuwa Watanzania wanazo akili za kutosha kujitambua na kutoyumbishwa wala kuamuliwa juu ya amani ya nchi yao.
 
Sitaweza ku post link kwasababu na-post via mobile. Atakayeweza kuweka na aweke.

Tanzania Daima leo imemnukuu Zitto akisema Shitambala kajiua kisiasa kwa kujiunga kwenye chama (CCM) kinachokufa!
I can confidently claim this is his boldest statement in a loooong time. Why now Zitto?

Inanifanya nifikiri kua kweli ulianza uswahiba na mafisadi sasa umeona wanaporomoka ndio warudi nyumbani kama mwana mpotevu?

Sikushutumu maana sina ushahidi, ila i'm tryin to put 1 and 1 together.
 
Hii sio hoja ya msingi.Zitto ametakiwa kutoa maoni yake na akayatoa .kwa uhalisia wake maoni ya zitto dhidi ya Shitambala ni ya kweli .Unasema unaushahidi so post yako siyo ya kujadili bali ni ya kuipuuza
 
anapoteza muda wake kwa ccm ilivyo vipande vipande sidhani kama bado wanamkumbuka kwamba siku chache zilizopita alirudi ccm.pamoja na usomi wake haelewi wananchi wanachodai hali ngumu ya maisha ccm kukumbatia mafisadi na mengine ni vizuri akawashauri huko alikorudi watatue hayo matatizo vinginevyo kwa uelewa wa watz sasa hivi huyo bwana ni kituko kingine cha mwaka
 
Huyo kweli shitambala wasukuma mnajuwa maana ya shitambala, kama hiYo sababu aliyotoa ndio imesababisha aondoke CDM basi atakuwa aliingia kimakosa toka mwanzo,MTU ANAYEOGOPA GHARAMA HAWEZI KUSIMAMIA HAKI, anaogopa gharama ndogo tu kutoka bungeni,kuandamana.HUTUFAI

Narudia alikuwa mwenyekiti wa CDM Mkoa KIMAKOSA
 
Sikushutumu maana sina ushahidi, ila i'm tryin to put 1 and 1 together.

We sema2 unataka ka umaarufu humu JF. Hoja Zitto hapa 2shazichoka na hatuzitaki. Naomba atakayesoma reply yangu ampuuze mleta hoja na asicomment chochote, ili mwisho kapost kake kawe mbali kwenye page na kukaweka front page niku2potezea muda wa kukasoma haka kapost. Mods hubu ka2pien kwenye dustbin.
 
Anatafuta umaarufu ili apewe kauongozi CCM. Awaulize kina Ngawaiya naTambwe Hiza. Anajidai yeye ni mwanasheria, yuko wapi Masumbuko Lamwai, mwanasheria aliyeitingisha serikali ya CCM mwaka wa 1995+?
 
Teeh teeh nadhani anatafuta umaarufu ndani ya CCM na anataka amalize njaa zake ndogondogo kwa kupewa fungu la kwenda kuibomoa CDM mbeya, ila namsikitikia kuwa its wrong timing anaye entertain huo ujinga wa kuchukua mamluki ameshavuliwa gamba
 
Shitambala anataka kuokota magamba yaliyovuliwa na wenzie. Anadhani ni rahisi sana kwa watu kudanganyika sana. "You can cheat some people all the time but you can not cheat all the people all the time". Shitambala sema tu wazee wa kujivua gamba wamekupa nini?:disapointed:
 
Hana lolote.Chama hakijengwi na mtu,chama kinajengwa na fikra pevuko za watu.Msomi mwenzangu Shitambala ameshapoteza dira.....hafai hata kuwa Katibu Kata.Huruma kweli!
 
Shitambala aanza kuwananga CHADEMA

Na Charles Mwakipesile, Mbeya

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) mkaoni Mbeya ambaye sasa amejiunga na CCM, Bw. Sambwee Shitambala
ametangaza kuibomoa ngome ya chama chake za zamani mkoani Mbeya Mbele ya Mjumbe wa Kudumu wa Kamati Kuu, Dkt. John Malecela huku akitamba kuwa kwa kadri alivyokijenga chama hicho ndivyo atavyokibomoa kwa mikono yake mwenyewe.

Alisema kuwa anathamini kwa sehemu kubwa heshima aliyopewa na uongozi wa chama ukiongozwa na Rais Kikwete, baada ya kuamua mwenyewe kujiunga na chama hicho kutokana na usaliti anaodai alifanyiwa na uongozi wa CHEDEMA.

Alisema kuwa viongozi hao badala ya kufanya kazi kwa maslahi yao wamekuwa wakifanya kazi kwa ajili ya kutafuta umaarufu wao wenyewe.

Alisema wakati akiwa katika chama hicho walikuwa wakifanya kampeni kwa kutangaza wazi kuwa wakiingia madarakani watahakikisha kuwa wanaendesha nchi katika hali ya amani na utulivu, lengo likiwa ni kuwaunganisha Watanzania na kujipatia maendeleo yao wenyewe pasipo kufanya vurugu hali ambayo alisema kuwa imekuwa tofauti na makubaliano hayo.

Bw. Shitambala alisema kuwa kutokana na kuwa mpiganaji na msomi wa sheria alishangaa kuona viongozi hao ambao wengi wao ameshiriki kuwapa ubunge wakigeuza ajenda na kuamua kuanzisha maandamano nchi nzima na kutoka nje bungeni wakati Rais Kikwete akihutubia hali ambayo alisema ni utovu mkubwa wa nidhamu.

"Hatukukubaliana kufanya maandamano ya kuvunja amani wala hatukuwatuma waende wakatoke bungeni na kisha kurudi ukumbini kwa kujadili hotuba ya rais, nawaambia ndugu zangu hii ni sababu kubwa iliyonifanya nikaamua kuondoka katika chama hicho.

Alisema kuwa CHADEMA ni chama chenye watu wasioweza kufikiri kwa haraka kutokana na ukweli kuwa Watanzania wanazo akili za kutosha kujitambua na kutoyumbishwa wala kuamuliwa juu ya amani ya nchi yao.

  1. kwa hiyo Shitambala atakuwa akijenga na kubomoa ambayo anaweza kujikuta mwisho wa maisha yake ame score zero (yaani "0")
  2. kama ni 'mpiganaji' na aliona busara ku fight against CCM kwa nini arudi huko huko, NCCR, CUF, TLP, TADEA hawaoni?
  3. Ina maana (mfano) suala la mswada wa katiba angeli handle vipi maana waliouleta walikusudia na kupitia hao anaowaita "waandamanaji" na "wavunja amani" sasa wamesaidia nchi kwa kuusimamisha?
  4. Inampasa kuwa makini maana anaweza kuwa amefanya baadhi ya mambo mazuri CDM na akayabomoa kama anayotaka kufanya na huko anakoelekea akafeli below negative, CCM 'imejivua' magamba ambapo hawahitaji "wakina Tambwe Hizza" wengine kama hapo awali.
 
Kweli nimeamini kuwa Shitambala aliuza Jimbo kwa CCM katika Uchaguzi wa 2010.....msaliti mkubwa huyu,aende zake kule!
 
Back
Top Bottom