Samahani mume wangu: Halikuwa lengo langu...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Samahani mume wangu: Halikuwa lengo langu...!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by ndyoko, Jan 23, 2012.

 1. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Wajemeni narudi tena jamvini...........watakaonuna au kufurahi kwa raha zao! Nimerudi toka mjini nimekutana na jambo la kusikitisha. Ile natia timu tu huku dodoma-eneo la chang'ombe, nimekuta kikao cha usuluhishi kati ya mpangaji mwenzangu na mkewe pamoja na ndugu wa mke na mume.

  Kifupi ni kwamba mume amemtaliki mkewe baada ya jaribio la mke kumuua mumewe kwa kumuwekea sumu ktk chakula, wiki sita zilizopita. Baada ya mume kulazwa hospitali ya General kwa wiki 5, jana ndo katoka hospitali na kufikia kutoa talaka leo. Nami ndo nimefikia kuitwa kwa hicho kikao. Masikini bahati nzuri mume hajaathirika sana, ingawa morphology ya mdomo imeharibika kidogo. Habari ya mhusika haijafikishwa polisi kwa kuhofia watoto wao kukosa malezi ya mama-wamezaa watoto 4.

  Wakati wa mjadala, mke alimuomba mume afute talaka kwani halikuwa lengo lake kumuua. Ajabu kila mume alivyokuwa akimkomalia, kutaka kujua lengo lake la kumuwekea sumu kwa chakula lilikuwa nini basi kama sio kumuua, mke alishndwa kujibu swali na kubakia kulia tu kila anapoulizwa jibu la swali hilo. Kwa kuhofia suala lisifike mahakamani, jamaa ameamua amuache mkewe kistaarabu kwa kutokwenda polisi kuwaambia 'source ya poisoning'. Kwa kuwa mume ameshikilia msimamo wa kumucha mke, sisi hatuna jinsi, mume kesha amua. Mjadala bado unaendelea jinsi ya kugawana mali, nyumba 1, daladala 2 na teksi 1.

  naendelea kujiuliza, sijapata jibu-Hivi inawezekana kweli, unamuwekea mtu sumu kwa chakula halafu unadai lengo sio muathirka afe? Kama lengo halikuwa kumuua mume, alitegemea sumu imfanye nini mumewe?

  Inahuzunisha sana!
   
 2. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Inawezekana kakosea step badala ya kuweka chumvi katia sumu.
   
 3. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #3
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Ndyoko ! Habari yako mbona imenistua hadi vinyweleo vimenisimama !.
  Ama kweli MKE SIO NDUGUYO !
   
 4. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Huyo ni talaka na kifungo juu!
   
 5. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #5
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Sasa lengo lilikuwa ni ili iweje? Au labda siku hizi kuna sumu ambazo haziui? Ikishaitwa 'SUMU' itaachaje kuua! Amwache tu manake ni muuaji!
   
 6. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #6
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Duh!! Hii Kali mwanamke anakuwaje na roho mbaya Kama hiyo ...
   
 7. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #7
  Jan 23, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mh kwa kweli hata mi naona talaka ni sahihi kabisa,tena wala asimpe chochote,
   
 8. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #8
  Jan 23, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  endelea kutujuza mkuu..
  Please wait while loading...
   
 9. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #9
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Hilo la kifungo wameamua kulificha kwa polisi, ili watoto wasijisikie vibaya kuishi na baba pekee! wameamua kulimalizia 'kiushikaji'-kindugu na kifamilia zaidi
   
 10. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #10
  Jan 23, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,174
  Trophy Points: 280
  Limbwata gone bad?
   
 11. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #11
  Jan 23, 2012
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mwe mie tutengane tu lakini siwezifikiria kukuua aisee!!
   
 12. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #12
  Jan 23, 2012
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160
  Niliwaambia wanaume ni wakatili but ukikuta mwanamke katili ujue ni katili kweli tena usimsogelee
   
 13. m

  mhondo JF-Expert Member

  #13
  Jan 23, 2012
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Labda alıtaka azıpate yeye hızo malı za ndoa baada ya mume wake kufa lakını Mungu amekataa.
   
 14. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #14
  Jan 23, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  ntasoma kesho, leo naah!
   
 15. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #15
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  watu tunawaza na kuamua tofauti sana madam!
   
 16. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #16
  Jan 23, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,710
  Trophy Points: 280
  alikwenda kutafuta limbwata kumbe kapewa sumu daaah pole zake
   
 17. t

  tatanca New Member

  #17
  Jan 23, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hayo ni mambo makubwa sana, lakini me naona kunajambo ambalo mdada kalipata ao kutoka kwa marafiki zake ao kalifikiria tu mwenyewe, pengine wazo kuu ni lile la kumwondoa mmewe ili arithi mali zote.
  swala la adhabu huyo baba kafanya uamuzi wa busara sana tena ni wa kibinadam zaidi, haja taka kumrudishia ubaya kwa kumshtaki polisi afungwe na ataabike, kwa wototo isingalikua ni picha nzuri na pia wangekua na mazingira magumu sana katika maisha yao.

  Kuhusu kugawana mali hizo mi naona mwanamke hakustahili tena kupata sehemu yake kwa kitendo alicho kifanya angalienda mahakamani angalipoteza vilevile kila kitu, hivyo basi naona ni vema sehemu yake ibakie kwa watoto kwa maisha ya baadae,
   
 18. roby2006

  roby2006 JF-Expert Member

  #18
  Jan 23, 2012
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 399
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hakuna mtu katili duniani kama mwanamke
   
 19. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #19
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Ukatili wanafunzwa na wanaume.
   
 20. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #20
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Abaki na watoto wake, huyo mama aondoke tu mwenyewe....asije kosea sumu akawawekea wao.....inauma aisee!
   
Loading...