Samahani mume wangu: Halikuwa lengo langu...!

mmh hiyo hatari sana ila wanawake wanavumilia sana wakichoka madhara yake huwa makubwa sana ndio hayo sasa.hapo hamna suluhu tena.
 
Mwanamke amekosa sana, yawezekea ameweka sumu akidhani ni dawa ya penzi toka kwa mganga,
ushauri toka kwa mashoga utakuumbua. akili ya kuambiwa, changanya na yako, nyuma ya pazia huenda
hakuwa na nia kweli ya kuua, labda kuimarisha penzi au limbwata. sasa kama ni mganga katoa sumu badala ya dawa, nani mwenye kosa la kuua kama jamaa angekufa? (Ref zilipendwa: MGANGA ALIYEKUWA DAWA NI ADUI YANGU)
 
Wajemeni narudi tena jamvini...........watakaonuna au kufurahi kwa raha zao! Nimerudi toka mjini nimekutana na jambo la kusikitisha. Ile natia timu tu huku dodoma-eneo la chang'ombe, nimekuta kikao cha usuluhishi kati ya mpangaji mwenzangu na mkewe pamoja na ndugu wa mke na mume.

Kifupi ni kwamba mume amemtaliki mkewe baada ya jaribio la mke kumuua mumewe kwa kumuwekea sumu ktk chakula, wiki sita zilizopita. Baada ya mume kulazwa hospitali ya General kwa wiki 5, jana ndo katoka hospitali na kufikia kutoa talaka leo. Nami ndo nimefikia kuitwa kwa hicho kikao. Masikini bahati nzuri mume hajaathirika sana, ingawa morphology ya mdomo imeharibika kidogo. Habari ya mhusika haijafikishwa polisi kwa kuhofia watoto wao kukosa malezi ya mama-wamezaa watoto 4.

Wakati wa mjadala, mke alimuomba mume afute talaka kwani halikuwa lengo lake kumuua. Ajabu kila mume alivyokuwa akimkomalia, kutaka kujua lengo lake la kumuwekea sumu kwa chakula lilikuwa nini basi kama sio kumuua, mke alishndwa kujibu swali na kubakia kulia tu kila anapoulizwa jibu la swali hilo. Kwa kuhofia suala lisifike mahakamani, jamaa ameamua amuache mkewe kistaarabu kwa kutokwenda polisi kuwaambia 'source ya poisoning'. Kwa kuwa mume ameshikilia msimamo wa kumucha mke, sisi hatuna jinsi, mume kesha amua. Mjadala bado unaendelea jinsi ya kugawana mali, nyumba 1, daladala 2 na teksi 1.

naendelea kujiuliza, sijapata jibu-Hivi inawezekana kweli, unamuwekea mtu sumu kwa chakula halafu unadai lengo sio muathirka afe? Kama lengo halikuwa kumuua mume, alitegemea sumu imfanye nini mumewe?

Inahuzunisha sana!

mke alishindwa kusema alimtilia limbwata... ila mganga alimdanganya ni limbwata kumbe sumu.

Haya kina mama mapenzi yanalelewa kwa nia, matendo na ndimi zetu, waganga watawafanya muwe wajane.
 
Mmmmh!dunian kuna mambo,
Huyo mwanamke ashukuru mungu,mumewe mstarabu sana mpaka ana mda wa kukaa vikao!!!!
Ila huyo mmama nae kauzu bado hajaondoka tu analumbana!!!
Hii ni kali nasubiri mwisho wake maana wanaume waungwana km huyu ni wachache sana dunia miaka hii!!
 
huyo ni wa kuachwa..umeona wapi mtu uliyeolewa tayari uwe na hamu ya kunogesha mapenzi kwa kwenda kwa mganga kuchukua dawa? Hafai... Na analia tu kwa kuwa anaogopa kumtaja shoga aliyemwelekeza kwa mganga,na kuwakokota wote hadi kwa huyo mganga.. Ndo anachohofia tu..
 
Inaonekana huyu mwanamke alianza kumpa mumewe madawa ya mapenzi na kumfanya ndondocha/zezeta kwa muda mrefu na alipoona haitoshi akaamua amuue kabisa. Ndio maana pamoja na yote hayo bado mume anaona huruma kumshitaki mkewe kwa kuwa bado akili yake imevurugika kwa madawa aliyowahi kulishwa na mwanamke huyo.

Mwanamke huyu muuaji anastahili kupelekwa mahakamani ili sheria ichukuwe mkondo wake. Hata akigawiwa nusu ya mali hiyo, bado ataendelea kumsumbua mwanamume wa watu ambaye mwisho atakufa tu na kumwachia muuaji mali yote. Usimuonee huruma huyo. Akuanzaye mmalize!
 
Acording to the Laws of Tanzania; It is a falony not reporting a comited falony to the proper authorities.
 
inaonekana maybe aliweka kwa bahati mbaya,kwani walikuwa na ugomvi waoo kwa wao? yaani wana nyumba na madaladala na taxi bado mnakaa nao kwenye nyumba moja ya kupanga au imekuwaje hapo
 
inaonekana maybe aliweka kwa bahati mbaya,kwani walikuwa na ugomvi waoo kwa wao? yaani wana nyumba na madaladala na taxi bado mnakaa nao kwenye nyumba moja ya kupanga au imekuwaje hapo

madam jamaa kichwani yuko makini sana hasa kwenye business. niliwahi kumuuliza why apange wakati ana nyumba na mali za kutosha kuwa independent. Alinjibu tu kuwa kwa kupangisha nyumba zake anapata faida kubwa kwani nyumba hapa dom ni bei nzur sana kama unapangisha. Nyumba anazopangisha kwa mwezi anapata around 1.3 milioni, wakati anapokaa analipa kodi ya pango around 240,000 kwa mwezi. Unaweza ukaona ujasiriamali wake ulivyo makini.
 
Itakuwa dawa ya mapenzi alikosea tu mahali fulani. kwa taarifa wanawake kibao wanapitia haya maisha na inatokana na wanaume kupenda nyumba ndogo nakumsahau mamaa.
 
Itakuwa dawa ya mapenzi alikosea tu mahali fulani. kwa taarifa wanawake kibao wanapitia haya maisha na inatokana na wanaume kupenda nyumba ndogo nakumsahau mamaa.

we na ubeijing wako huo, shauri yako!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom