Wadau nimekuwa mtazamaji wa Habari za Kimataifa wa TV za Tanzania kwa kipindi kifupi tu ila huyu jamaa/mzee nampigia saluti.
Anaandaa vizuri mpaka 99% anapozisoma sasa 100%
Anaitwa Samadu Hassan na siyo Samadu Hassan Maduhu. Maduhu alikuwa kama si mwandaaji basi mhariri wa vipindi RFA.
Umenena, hata mimi Samadu Hassan namkubali sana, nadhani kwa habari za kimataifa anashikilia usukani kwa tz kwa mujibu wa maoni yangu.
jamaa yuko poa sana,ni mtangazaji wa kimataifa yule mzee,kati ya vichwa vinavyotangaza habari hapa bongo,yule ni nambari oneakifuatiwa na djaro warungu,oooh,no nimekosea sio djaro warungu,anafuatiwa na hemedi kivuyo.
Alifanya kazi Kenya kisha akaenda London,baba yake alikuwa katibu wa tawi wa TANU (nasikia baba yake alikosana na mwalimu,so akakamatwa na kuwekwa ndani wakati huo Samadu ni mwanaharakati za kweli,ndo Samadu akakimbilia nje)
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.