Saluni za kike ni shule hatari kuliko zote

Mbona Nyiee wanaume mna vijiwe vyenu vya kuzungumza

Saloon ni Kama kijiwe,

Ukiwa kijiwen kila story itazungumzwa ya ukweli na Uongo mradi masaa yapite Kikubwa Akili ya kuambiwa changanya na yako
 
Kwenye Saluni nyingi za wanawake, mazungumzo mengi yanahusu maisha ya watu na hasa kuhusu mapenzi na kipato, kashfa na saikolojia zisizo rasmi kuhusu ndoa na uhusiano. Kuna mazungumzao ya kukatishana tamaa na kuumizana zaidi, kwa sababu kila mmoja anajaribu kuonyesha kwamba ana nafuu fulani.

Lakini mbaya zaidi ni kwamba, saluni za wanawake hutumiwa na wanawake hao kama maeneo ya kusemea hisia zao chungu na kutoa jumuisho kuhusu wanaume na uhusiano. Huko saluni hakuna wataalamu, bali kuna wazungumzaji ambao wanaamini wao ni wataalamu, na wengine kwa sababu ya kuzidiwa na mzigo wa matatizo hasa ya uhusiano na pengine ya kipato, huwaaamini hao wataalamu wasio rasmi.

Huko saluni ndiko ambako wanawake wanaambiana`kwamba, mwanaume akiacha kufanya tendo la ndoa kwa wiki moja na mpenzi wake, ni lazima mwanaume huyo atakuwa na ‘nyumba ndogo.’ Ndiko ambako wanafundishana kwamba, ukipata Mganga wa nguvu unaweza kumshika mwanaume. Ndiko huko ambako hutajwa orodha ya wanawake ambao wamewashika waume zao kupitia kwa waganga. Ndiko huko ambako majina ya waganga maarufu hutajwa.

Lakini ndiko huko saluni ambako, wanawake hutaja orodha ya wanawake wenzao waliopata mali kupitia ‘mabuzi,’ ambao huwapa mitaji ya biashara inayowawezesha kusafiri hadi Uchina. Pia hutajwa majina ya wanaume wanaohonga sana. Ni saluni ambako wataalamu wasio rasmi hutoa suluhu ya matatizo ya ndoa. Ndiko ambako wataalamu hao huwaambia wanawake wenzao kwamba, ukimuonyesha mwanaume kwamba unampenda sana, atakudharau na kukuacha.

Kwa hiyo mwanamke akitoka saluni anakuwa ametoka shule anayoiamini . ambapo huacha kumwonesha mumewe kwamba, anampenda. Ni wazi shule hii ya saluni haijui kwamba, unapoonesha kutokupenda, nawe utaoneshwa kutokupendwa. Kwani unachopanda ndicho unachovuna. Wakati mwingine shule hii inajua jambo hilo, isipokuwa inataka waliopotea na kuharibikiwa wawe wengi.

[emoji653][emoji653][emoji653][emoji653][emoji653]
Ni huko saluni ambako utasikia wanawake wakifundishana namna ya kuwadanganya wanaume zao. Hufundishana namna ya kujenga nyumba bila kunaswa na mume, kwani wanaume hawaaminiki, huwezi kuacha kujiandaa. Lakini shule hii haijui kuwa, hiyo ni sumu kubwa kuliko sumu nyingine kwenye ndoa, kutafuta mali na kujenga msingi wa kipato kwa siri.

[emoji844][emoji844][emoji844][emoji844][emoji844][emoji844]
Ni hukohuko saluni ambako wanawake huambiana uongo kuhusu wakwe, watoto wa kambo, na mawifi. Hufundishana kwamba, kumpenda mama mkwe au wifi ama mtoto wa kambo ni kutafuta muhali. Haiishia hapo huendelea kufundishana hata namna ya kuwachukia watu hao.

Mwanaume, kama ukiona mwenzi wako anakwenda saluni na akitoka huko amekuwa mtu mwingine kabisa, unapaswa kujua kwamba, huenda amepata ‘dozi’ ya wataalamu hao.

Wanawake, nawashauri jihadharini sana na maneno ya saluni. Kwani katika kila maneno mia moja, ni moja tu linalokaribia ukweli. Kumbuka, linalokaribia ukweli . siyo kuwa ni la kweli……
Uliyoyaorodhesha yanaweza kuwa na ukweli, kwa sababu nilishawahi kuyasikia kabla ya leo(na lisemwalo LIPO-wahenga)! Lakini, kwa sehemu kubwa sana sisi wanaume tunachangia hayo kutokea. Unaruhusuje mkeo aende saluni KUPOTEZA MUDA? Jobless WOMAN is a workshop of devil. Kuruhusu mkeo aende saluni ni sawa na kumruhusu akacheze BAO au KARATA! Serious?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unafahamu maana ya kutafiti..?
Usijali, GT! Great Thinkers tumekuelewa. Hayo niliyasikia siku nyingi mno, KABLA sijaoa. Nilipotaka kuoa, nilimwambia mchumba wangu(ambaye sasa ni mke wangu) MAPEMA KABISA: Mama, mimi nimekupenda, nimekuchagua mwenyewe, nataka uwe mke wangu. SIKUSHAWISHIWA NA MTU YEYOTE, kwa sababu wazazi wangu huwajui, ndugu zangu huwajui wala marafiki zangu huwajui! Na SITAKI kukuonesha kwa sababu wanaweza kufanya kitu au kusema kitu ambacho kikakukwaza ukaghairi tusifike tunakoelekea. WATAKUFAHAMU/UTAWAFAHAMU SIKU YA ARUSI(na nikienda kulipa mahali nitatafuta wazee wa hekima, wenye mvi-ambao SI ndugu zangu, waniwakilishe). Na sasa, nataka kwenda kwa wazazi wako kujitambulisha, nitalipa mahali yoyote watakayonipangia! Na katika maisha yangu YOTE, SIYO siku 2, 3; nasisitiza, YOTE, nitakupenda; LAKINI, sitaki moja, mbili, tatu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye Saluni nyingi za wanawake, mazungumzo mengi yanahusu maisha ya watu na hasa kuhusu mapenzi na kipato, kashfa na saikolojia zisizo rasmi kuhusu ndoa na uhusiano. Kuna mazungumzao ya kukatishana tamaa na kuumizana zaidi, kwa sababu kila mmoja anajaribu kuonyesha kwamba ana nafuu fulani.

Lakini mbaya zaidi ni kwamba, saluni za wanawake hutumiwa na wanawake hao kama maeneo ya kusemea hisia zao chungu na kutoa jumuisho kuhusu wanaume na uhusiano. Huko saluni hakuna wataalamu, bali kuna wazungumzaji ambao wanaamini wao ni wataalamu, na wengine kwa sababu ya kuzidiwa na mzigo wa matatizo hasa ya uhusiano na pengine ya kipato, huwaaamini hao wataalamu wasio rasmi.

Huko saluni ndiko ambako wanawake wanaambiana`kwamba, mwanaume akiacha kufanya tendo la ndoa kwa wiki moja na mpenzi wake, ni lazima mwanaume huyo atakuwa na ‘nyumba ndogo.’ Ndiko ambako wanafundishana kwamba, ukipata Mganga wa nguvu unaweza kumshika mwanaume. Ndiko huko ambako hutajwa orodha ya wanawake ambao wamewashika waume zao kupitia kwa waganga. Ndiko huko ambako majina ya waganga maarufu hutajwa.

Lakini ndiko huko saluni ambako, wanawake hutaja orodha ya wanawake wenzao waliopata mali kupitia ‘mabuzi,’ ambao huwapa mitaji ya biashara inayowawezesha kusafiri hadi Uchina. Pia hutajwa majina ya wanaume wanaohonga sana. Ni saluni ambako wataalamu wasio rasmi hutoa suluhu ya matatizo ya ndoa. Ndiko ambako wataalamu hao huwaambia wanawake wenzao kwamba, ukimuonyesha mwanaume kwamba unampenda sana, atakudharau na kukuacha.

Kwa hiyo mwanamke akitoka saluni anakuwa ametoka shule anayoiamini . ambapo huacha kumwonesha mumewe kwamba, anampenda. Ni wazi shule hii ya saluni haijui kwamba, unapoonesha kutokupenda, nawe utaoneshwa kutokupendwa. Kwani unachopanda ndicho unachovuna. Wakati mwingine shule hii inajua jambo hilo, isipokuwa inataka waliopotea na kuharibikiwa wawe wengi.

[emoji653][emoji653][emoji653][emoji653][emoji653]
Ni huko saluni ambako utasikia wanawake wakifundishana namna ya kuwadanganya wanaume zao. Hufundishana namna ya kujenga nyumba bila kunaswa na mume, kwani wanaume hawaaminiki, huwezi kuacha kujiandaa. Lakini shule hii haijui kuwa, hiyo ni sumu kubwa kuliko sumu nyingine kwenye ndoa, kutafuta mali na kujenga msingi wa kipato kwa siri.

[emoji844][emoji844][emoji844][emoji844][emoji844][emoji844]
Ni hukohuko saluni ambako wanawake huambiana uongo kuhusu wakwe, watoto wa kambo, na mawifi. Hufundishana kwamba, kumpenda mama mkwe au wifi ama mtoto wa kambo ni kutafuta muhali. Haiishia hapo huendelea kufundishana hata namna ya kuwachukia watu hao.

Mwanaume, kama ukiona mwenzi wako anakwenda saluni na akitoka huko amekuwa mtu mwingine kabisa, unapaswa kujua kwamba, huenda amepata ‘dozi’ ya wataalamu hao.

Wanawake, nawashauri jihadharini sana na maneno ya saluni. Kwani katika kila maneno mia moja, ni moja tu linalokaribia ukweli. Kumbuka, linalokaribia ukweli . siyo kuwa ni la kweli……
Ahsante sana ,somo limeeleweka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mwanamke anakuaga na akili akiwa mwenyewe wakishakuwa wawili watatu akili hupotea yani kufundishana ujinga ndo kunaanziaga hapo. Ukweli mtupu umeongea. Lkn kumkataza mwanamke kutengeneza nywele ni sawa na kumnyima kitu cha thamani sana kwenye maisha yake mwache aende ila mpe angalizo na mambo ya saluni kama ni mwelewa ataelewa na kama ulioa matembele ataendelea kua tembele tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmh. Sio kweli kwamba saloon nyingi ziko hivyo.

Na pia kama zipo na hayo yanafanyika inategemea na akili ya huyo aliyeenda huko saluni kama akili yake ni ya kushikiwa yote yatayosemwa atayabeba kama yalivyo na kama akili yake iko sawa atachukulia ni story tu kama story nyingine ambazo huwa zinapigwa pindi watu wanapokusanyika sehemu moja.
 
Hata M/mke Anaangalia Mtu Wa Kumbadilikia Tabia Kuna Type Ya Wanaume Hasubutu Hata Nusu Labda Wale W/ume Waosha Vyombo Nyumban
 
Back
Top Bottom