Saluni inaweza kukuharibia pendo ati. . .

Calnde

JF-Expert Member
Oct 7, 2008
1,373
277
Huduma za saluni (wanaume na wanawake) zimekua sana Tanzania. Ila kwa kweli zinaweza

zikakuharibia pendo usipokuwa makini. Tazama

1. Huyu dada kaenda kutengeneza nywele, jilulize atakuwa anaongea nini mpaka atakapomaliza

2.Huyu dada anaoshwa na kupakwa rangi kucha na mwanaume! Jiulize matokeo yake hasa

anapokuwa na mpaka rangi permanent.

3.Huyu kaka anaoshwa kichwa na kufanyiwa facial na mrembo huyu (tena kwa mbwembwe za

ajabu usipime). Na hiyo ndo saluni yake permanent.

4. Dada huyu anapunguza nywele kwa kinyozi wa kiume, subiri sound itayopigwa hapo mpaka

anamaliza

NB. Tafiti zinaonesha matendo ya huduma (serving) huamsha mapenzi. No wonder wakinadada

wanaanguka kwa houseboy, shamba boy, muuza duka/genge, muuza chipsi, muuza matunda nk nk

Kadhalika wanaume kwa wadada wa ndani au wale wanaowahudumia mara kwa mara kama

masekretari nk nk. Tafakari. . .
 
1. Unaenda saluni kuongea ama kutengeneza unachotaka kutengeneza? Mi hua nashangaa sana watu wanavyopayuka hovyo badala ya kutulia wakimaliza kilichowapeleka warudi majumbani kwao.
Ila bado sijui hiyo inaweza ikavunja vipi mahusiano ya mtu mwenye akili zake timamu.

2. Matokeo ni kucha zinapendeza, yakiwepo mengine basi yanatokana na hulka ya mtu na sio kwasababu tu kapakwa rangi na mkaka.

3. Again, kama mtu anaongozwa na mawazo ya ngono hata anaebahatisha kukaa nae kwenye daladala anaweza akamtaka na akimpata anamchukua. Pili, kwa wanaume ambao wameoa nadhani vitu vingine ni vizuri wakawaomba wake zao wawafanyie. Itaongeza ukaribu kati yao, na akinogewa na kuoshwa kichwa anamalizia mahitaji yake kihalali.

4.Kupigwa sound kuna tatizo gani? Sound zinapigwa na vinyozi tu? Mdada ambae yuko avarage (muonekano na umbo) lazima apigwe sound sehemu na watu tofauti tofauti, hamna anaeweza kuzuia hilo. Ishu ipo kwenye mhusika kukubali ama kukataa, na kama atamkubali kinyozi jua fika angeweza akamkubali yeyote yule kati ya wanaomfuata hivyo ishu sio kuwa kinyozi bali ni mtu kuwa 'anapatikana'.

NB. Kama mtu anahitaji kuona/kuhisi mwenzake anamjali na hali ikawa tofauti na hivyo ni rahisi sana(japo sio haki) kuanguka kwa anaeonyesha kujali hata kama wewe hapo utaona hana hadhi sijui. Hivyo muhimu ni watu kutimiza majukumu yao. . . sio wanabweteka alafu wanabaki kulia lka baadae.
 
Masiku yajayo nadhani wahujumiwao wakijashtuka (chale cheja) watakuja'force watoa huduma wawe mobile kwa kwenda toa huduma majumbani mwa wateja.
 
1. Unaenda saluni kuongea ama kutengeneza unachotaka kutengeneza? Mi hua nashangaa sana watu wanavyopayuka hovyo badala ya kutulia wakimaliza kilichowapeleka warudi majumbani kwao.
Ila bado sijui hiyo inaweza ikavunja vipi mahusiano ya mtu mwenye akili zake timamu.

2. Matokeo ni kucha zinapendeza, yakiwepo mengine basi yanatokana na hulka ya mtu na sio kwasababu tu kapakwa rangi na mkaka.

3. Again, kama mtu anaongozwa na mawazo ya ngono hata anaebahatisha kukaa nae kwenye daladala anaweza akamtaka na akimpata anamchukua. Pili, kwa wanaume ambao wameoa nadhani vitu vingine ni vizuri wakawaomba wake zao wawafanyie. Itaongeza ukaribu kati yao, na akinogewa na kuoshwa kichwa anamalizia mahitaji yake kihalali.

4.Kupigwa sound kuna tatizo gani? Sound zinapigwa na vinyozi tu? Mdada ambae yuko avarage (muonekano na umbo) lazima apigwe sound sehemu na watu tofauti tofauti, hamna anaeweza kuzuia hilo. Ishu ipo kwenye mhusika kukubali ama kukataa, na kama atamkubali kinyozi jua fika angeweza akamkubali yeyote yule kati ya wanaomfuata hivyo ishu sio kuwa kinyozi bali ni mtu kuwa 'anapatikana'.

NB. Kama mtu anahitaji kuona/kuhisi mwenzake anamjali na hali ikawa tofauti na hivyo ni rahisi sana(japo sio haki) kuanguka kwa anaeonyesha kujali hata kama wewe hapo utaona hana hadhi sijui. Hivyo muhimu ni watu kutimiza majukumu yao. . . sio wanabweteka alafu wanabaki kulia lka baadae.

Kinachotokea hapo ni effects za continuous service. Huyo wa daladala ni one time and may not have

any effect. lakini wewe fikiri kwamba mumeo kila siku ankwenda saluni flani na anaoshwa na

mwanadada flani! Uwezekano wakutegwa kutokana na ukaribu unaojengwa kwa huduma

inayotolewa ni mkubwa sana. Hulka ya mtu inachangia lakini mazingira pia yanahusika kubadilisha

mtizamo wa mtu. . . .
 
Kwanza sipendelei kwenda saluni hizo, Pili, sijui kwenu wanaume, for me as woman. Mwanaume wa anyefanya kazi saluni ya wanawake yaani hanitii tamaa hata siku moja, namwona kama ******/hanisi au mwanamke mwenzangu vile.

Yaani nahisi walost their masculine part....sorry thats me.
 
kujitambua na kujua nafasi yako, kujua unachotaka ni muhimu.

Ukijua pale unatengeneza kucha na kuondoka. Ukijua unanyia nywele na kundoka. Huna haja ya kupayuka saluni, na hata vinyozi au wale wadada wanaotega waume za watu saluni hawatokupata.

Hata majumbani mwanaume/mwanamke anayejitambua na anayejiheshimu, anayeheshimu na kuthamini ndoa yake, anayemuheshimu na kumpenda mwenzie kwa dhati na kui-value familia yake hawezi kutembea na housegirl/boy
 
Kazi kweli! Sasa watoa huduma woote ukawapa si utafungua kabiashara ka hiyo biashara? Manake mie hata butcher, groceries, saluni, u name it nina permanent suppliers!
 
Kwanza sipendelei kwenda saluni hizo, Pili, sijui kwenu wanaume, for me as woman. Mwanaume wa anyefanya kazi saluni ya wanawake yaani hanitii tamaa hata siku moja, namwona kama ******/hanisi au mwanamke mwenzangu vile.

Yaani nahisi walost their masculine part....sorry thats me.

Dah, mimi siwezi kufanya kazi saluni za kike. Lakini sidhani kama ni vyema kuwageneralize wote

wanaofanya kazi huko. Ingawa wengi kwa judgement ya macho unaweza kudhani kuna walakini fulani hivi
 
Kinachotokea hapo ni effects za continuous service. Huyo wa daladala ni one time and may not have

any effect. lakini wewe fikiri kwamba mumeo kila siku ankwenda saluni flani na anaoshwa na

mwanadada flani! Uwezekano wakutegwa kutokana na ukaribu unaojengwa kwa huduma

inayotolewa ni mkubwa sana. Hulka ya mtu inachangia lakini mazingira pia yanahusika kubadilisha

mtizamo wa mtu. . . .

Hulka ya mtu ndio kila kitu. . .hata kuwe na continuity sijui kitu gani kama mtu hulka yake sio kuruka ruka kila kona hatofanya hivyo. Wanaofanya hivyo hata wasingekuwa na hao wanaowapa huduma wangechukuana na watu wengine huko mitaani bila kujali hayo uliyoongelea mwanzo.
 
Kuaminiana ni vyema! Sasa hutakiwi uamini tuu blindly hata pale ambapo kuna factors zinazoweza

kukushawishi otherwise.
 
Kama kakubali kuchukuliwa aende akirdihia,sababu kama ndio tabia yake hata akibadilisha saloon 101 kazi itakua ndio ile ile.
 
Hulka ya mtu ndio kila kitu. . .hata kuwe na continuity sijui kitu gani kama mtu hulka yake sio kuruka ruka kila kona hatofanya hivyo. Wanaofanya hivyo hata wasingekuwa na hao wanaowapa huduma wangechukuana na watu wengine huko mitaani bila kujali hayo uliyoongelea mwanzo.

Unaamini hulka ya mtu yaweza kubadilishwa na mazingira anayopitia?
 
Kuaminiana ni vyema! Sasa hutakiwi uamini tuu blindly hata pale ambapo kuna factors zinazoweza

kukushawishi otherwise.

seriously speaking, kama mtu amedhamiria kutoka nje ya mahusiano, there is nothing you can do about it... mtu hachungwi kama mbuzi, anajichunga mwenyewe
 
duh, na maofisini je?
Kuna clients ambao kila siku waongea nao
kuna msekretaru ambao kila siku wanakuandalia chai, cha mchana, kupanga ratiba, kuhakikisha uko proper kimwonekano

utakuwa na wa ngapi?

Hiyo ni hulka tu, hata ufungiwe ndani utaangua hata tango kwenye friji.
 
Napenda kuamini kwamba mambo ya kukosa uaminifu na tabia ya uzininzi haikuanza leo wala jana, ni jambo la zamani sana.Haina haja kupoteza muda mwingi kujadili kwamba watu wanafanya uzinzi.Ninavyofahamu nchi nyingi hata Tanzania umalaya ni jambo la kawaida sema tunajaribu kufanya siri, leo hii ikatokea kila uliyewahi kuzini naye akajitokeza;yatakuwa mastaajabu.

Jambo la msingi kama mtu mwnye akili la kutillia maanani ni AFYA YAKO hapa namaanisha ukimwi.Kama una uhakika kwamba afya yako itakuwa salama 100% baada ya uzinzi huo, endelea wala usikate tamaa; kama ndiyo starehe yako kuu.Ila siku ukapata hiyo ngoma, hadithi yote itakuwa imeishia hapo.Kila mtu anayo nafasi ya kuchagua njia aipendayo, yaweza kuwa giza au mwanga.
 
duh, na maofisini je?
Kuna clients ambao kila siku waongea nao
kuna msekretaru ambao kila siku wanakuandalia chai, cha mchana, kupanga ratiba, kuhakikisha uko proper kimwonekano

utakuwa na wa ngapi?

Hiyo ni hulka tu, hata ufungiwe ndani utaangua hata tango kwenye friji.

Nikuulize, utamruhusu mmeo/mkeo kufanya kazi saloon majukumu yake yakiwa ni kuwapatia massage

wateja?
 
ungeniuliza, napenda patina wangu awe klasi gani ningekuelewa zaidi.

Sasa mimi sina hoja ya mapatina. Swali umelielewa lakini umeamua kutoelewa zaidi. Sasa jibu kama

ambavyo ungetaka nikuulize
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom