Hali ya usafi kwenye saluni unayoenda kusuka au kunyoa ikoje?

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Wakuu,

Naamini wote tunaenda saluni, iwe kusuka au kunyoa, na huduma hii sio kwa watu watu wazima pekee hata watoto pia huenda saluni kutengenezwa nywele, sasa swali ni kwamba hali ya usafi ikoje kwenye saluni unayoenda kupata huduma?

Wanaume, mataulo yanayohudumia wateja yanasafishwa baada ya muda gani? Au ni mwendo wa kukung'uta tu baada ya kumhudumia mteja halafu mwengine anatumia hilohilo? Kwenye vifaa angalau upande wa wanaume wanasafisha na spirit ama sanitaiza japo nayo sijui inaondoa wadudu/uchafu kwa kiasi gani.

Machanuo, mikasi, taulo, sindano nk, kwenye saluni za kike zinasafishwa kabla hajatumia mtu mwingine? Tukumbuke vifaa vinavyotumika vina ncha kali na ni rahisi sana kumuambukiza mtu ugonjwa.

Saluni yako vipi, usafi ni wa hali ya juu au tunamuachia Mungu?
 
Hazinaga wakaguzi wa afya hizi mabwana afya wamekuwa viumbe dhaifu sana wanahongwa hadi elfu 2 tu na kuacha watu waendeleze uchafu si salon peke yake bali na migahawa hotels bars guest houses kusema kwa uchache.

Yafaa ujisimamie unapoingia salon hizo kwa kukataa kifaa kilichotumiwa na mwingine kabla hakijafanyiwa sterilization.
 
Angalia movie hiyo uone barbershop za majuu zilivyo hatari
images.jpg
 
Kwakweli kwa hapa wahusika wanakazi ya kufanya kubwa sana, saloon, Migahawani huku/Mama Ntilie (vyakula vinavyopikwa na Joice zake ), Maguest huko hizi sehem zinatakiwa kuangaliwa kwakweli. Unakua mtu anafungua saloon na Taulo mbili to😥
 
Hazinaga wakaguzi wa afya hizi mabwana afya wamekuwa viumbe dhaifu sana wanahongwa hadi elfu 2 tu na kuacha watu waendeleze uchafu si salon peke yake bali na migahawa hotels bars guest houses kusema kwa uchache.

Yafaa ujisimamie unapoingia salon hizo kwa kukataa kifaa kilichotumiwa na mwingine kabla hakijafanyiwa sterilization.
Unachokizungumza ni sahihi lakini pia kwenye suala la usafi inategemeana na saluni gani unaenda👈 kwa mfano zipoo saluni ambazo zinakua ni za high classic ( gharama ) na za kawaida pia zipoo,,,,👐lazima vitu vitofautiane kwenye suala la usafiii kiujumla kwa mteja na kwa muhudumu ,,,,,,,,,
 
Kiukweli Jambo hili ni geni kwenye salon nyingi na watanzania wengi wanahitaji elimu kuhusu hili
 
Labda kwa salon kubwa lakini huku kwenye Buku mbili. Kitambaa kimoja kinatumika hata Wiki nzima can you imagine
 
Ukweli si saluni tu. Sisi waafrika bado tupo nyuma kuhusu usafi. Ushawahi kuona sehemu za vyakula?

Haya unatoka saluni na mifangasi yako, unaingia bar kupiga supu. Kwenye supu, malimao yamekatwa vipande, yapo kwenye sahani. Unachukua kipande unafinyia kwa bakuli lako,unarudisha kwenye sahani na mifangasi yako ya saluni. Mwenzako anakuja anaendelea ulipoachia.

Unatoka hapo, unaenda kwa mchoma mahindi. Kila mtu akija anashika hindi kwanza ndiyo ajiridhishe. Kila mtu anajua alichoshika huko alipotoka. Wewe una mifangasi ya saluni na si ajabu ushakanda ngano(umekuna pumbu ) kwa kuzibinyabinya kwa miwasho. Na wewe unashikashika kila hindi, unachagua.

Kisha unamalizia kununua mchicha kwa mama mboga. Huu umeletwa ukiwa wazi kwa baiskeli, unaburuzwa kwenye spoku. Mama mboga anauweka chini juu ya kiroba ambacho huwa hakioshwi. Anaunyunyizia maji toka kopo la uhai au afya. Hakuna anaejua kopo limeoshwa lini wala maji yaliyomo yaketoka wapi. Yeye katoboa kwenye kizibo, anabinya maji yanatoka kama mkojo wa kitoto cha kiume kirijali. Mradi mchicha usinyauke.

Siku hiyo hujapitia mijuisi ya kienyeji imejazwa kwenye mibobo ya maji ya uhai.

Ukisikia waafrika hatuugui COVID kuna mengi aisee.
 
Hazinaga wakaguzi wa afya hizi mabwana afya wamekuwa viumbe dhaifu sana wanahongwa hadi elfu 2 tu na kuacha watu waendeleze uchafu si salon peke yake bali na migahawa hotels bars guest houses kusema kwa uchache.

Yafaa ujisimamie unapoingia salon hizo kwa kukataa kifaa kilichotumiwa na mwingine kabla hakijafanyiwa sterilization.
Hili ni kweli kabisa, saluni za wanawake ndio kabisa balaa
 
Kwakweli kwa hapa wahusika wanakazi ya kufanya kubwa sana, saloon, Migahawani huku/Mama Ntilie (vyakula vinavyopikwa na Joice zake ), Maguest huko hizi sehem zinatakiwa kuangaliwa kwakweli. Unakua mtu anafungua saloon na Taulo mbili to😥
Taulo mbili daaah😅😅 unaenda kukusanya magonjwa ya mtaa mzima
 
Unachokizungumza ni sahihi lakini pia kwenye suala la usafi inategemeana na saluni gani unaenda👈 kwa mfano zipoo saluni ambazo zinakua ni za high classic ( gharama ) na za kawaida pia zipoo,,,,👐lazima vitu vitofautiane kwenye suala la usafiii kiujumla kwa mteja na kwa muhudumu ,,,,,,,,,
Haijalishi saluni yako ipo wapi kwakweli, labda useme kwenye utofauti wa vifaa na huduma, ila linapokuja suala la usafi wote mwenye ako na saluni high class ama hali ya chini wanatakiwa kuhakikisha kuna usafi wa hali ya juu.
 
Labda kwa salon kubwa lakini huku kwenye Buku mbili. Kitambaa kimoja kinatumika hata Wiki nzima can you imagine
Hili linatakiwa kubadilika, na nyinyi pie muwaelimishe ambao hawajui na kuwakazia wanaokaza shingo, maana mwisho wa siku wewe unayefuata huduma ndio inakula kwako
 
Wakuu,

Naamini wote tunaenda saluni, iwe kusuka au kunyoa, na huduma hii sio kwa watu watu wazima pekee hata watoto pia huenda saluni kutengenezwa nywele, sasa swali ni kwamba hali ya usafi ikoje kwenye saluni unayoenda kupata huduma?

Wanaume, mataulo yanayohudumia wateja yanasafishwa baada ya muda gani? Au ni mwendo wa kukung'uta tu baada ya kumhudumia mteja halafu mwengine anatumia hilohilo? Kwenye vifaa angalau upande wa wanaume wanasafisha na spirit ama sanitaiza japo nayo sijui inaondoa wadudu/uchafu kwa kiasi gani.

Machanuo, mikasi, taulo, sindano nk, kwenye saluni za kike zinasafishwa kabla hajatumia mtu mwingine? Tukumbuke vifaa vinavyotumika vina ncha kali na ni rahisi sana kumuambukiza mtu ugonjwa.

Saluni yako vipi, usafi ni wa hali ya juu au tunamuachia Mungu?
Dah usafi ndio jambo lilifanya nitafute mtu anaejua kunyoa na kitana basi muda wowote nakua huru kunyoa mataulo hata kwenye saloon kubwa yanakung'utwa tu kufua ni baada ya kuona limechafuka sio kila baada ya mtu kutumia. Na kule walipo na usafi mzuri bai zao zimechangamka sana unakuta kunyoa ni 10k alooo hio bei noma kwangu kwahyo kuliko kuvagaa mataulo machafu bora mwanangu bondeni aninyoe nimpe ganji mambo iishe
 
Ukweli si saluni tu. Sisi waafrika bado tupo nyuma kuhusu usafi. Ushawahi kuona sehemu za vyakula?

Haya unatoka saluni na mifangasi yako, unaingia bar kupiga supu. Kwenye supu, malimao yamekatwa vipande, yapo kwenye sahani. Unachukua kipande unafinyia kwa bakuli lako,unarudisha kwenye sahani na mifangasi yako ya saluni. Mwenzako anakuja anaendelea ulipoachia.

Unatoka hapo, unaenda kwa mchoma mahindi. Kila mtu akija anashika hindi kwanza ndiyo ajiridhishe. Kila mtu anajua alichoshika huko alipotoka. Wewe una mifangasi ya saluni na si ajabu ushakanda ngano(umekuna pumbu ) kwa kuzibinyabinya kwa miwasho. Na wewe unashikashika kila hindi, unachagua.

Kisha unamalizia kununua mchicha kwa mama mboga. Huu umeletwa ukiwa wazi kwa baiskeli, unaburuzwa kwenye spoku. Mama mboga anauweka chini juu ya kiroba ambacho huwa hakioshwi. Anaunyunyizia maji toka kopo la uhai au afya. Hakuna anaejua kopo limeoshwa lini wala maji yaliyomo yaketoka wapi. Yeye katoboa kwenye kizibo, anabinya maji yanatoka kama mkojo wa kitoto cha kiume kirijali. Mradi mchicha usinyauke.

Siku hiyo hujapitia mijuisi ya kienyeji imejazwa kwenye mibobo ya maji ya uhai.

Ukisikia waafrika hatuugui COVID kuna mengi aisee.
Ni balaa, hii cheni si ya kitoto!
 
Back
Top Bottom