Salma Kikwete: Sikubaliani na suala la mtoto aliyepata ujauzito kurudi shule

Hizo ni nadharia zako mzee,ushungi haumsuti popote kwa sababu hata dini yake haikatazi mjamzito au mtoto wa kike akijifungua aendelee kusoma,huo ushungi wake wala haujakataza jambo hilo.

Kwa maana hiyo hata kiushungiushungi(kidini yake)bado yuko sahihi sana.

Kuwaruhusu wasome hakuna maana ya kwamba anakubali mimba mashuleni.
Achana nae huyo,huyo na wenzie chuki yao kubwa kwa Samia sababu ni muislamu tu!!
 
Ni mawazo yake,Mimi Kama mwallimu mzoefu kwa miaka 20 sasa nashauri serikali izingatie pia katika utoaji wa elimu ya uzazi wa mpango,na mabinti wahimizwe katika kutumia njia za uzazi wa mpango ili angalau kupunguza idadi ya mabinti kupata mimba katika umri mdogo.

Nimewahi kuishia mikoa ya mtwara na Lindi Kama mwalimu kwa miaka 10 ,Ni nadra Sana kushuhudia mtoto akibeba mimba angali masomoni,hii ni tofauti na mikoa ya mwanza ,shinyanga na kagera,kwani Hawa wakaazi wa mikoa hii Wana mawazo hasi juu ya matumizi ya njia za uzazi ,lakini kwa mikoa ya Lindi na mtwara mwamko ni mkubwa Sana juu ya matumizi ya njia za uzazi wa mpango.

Tatizo la watanzania tunapenda kupambana na asili na uhalisia,tutafika lakini tukiwa tumechoka Sana!!!

..asante sana kwa mchango wako.

..je, njia za uzazi wa mpango za ndugu zetu wa kusini na hizi za kisasa, au za kijadi?

..Ni vizuri uka-share taarifa hizo kwani hili ni tatizo kubwa ktk maeneo mengi hapa nchini.

..kuna umuhimu wa kuhakikisha mtoto wa kike anajielewa na anakuwa na malengo ktk maisha yake.
 
"Mimi sikubaliani na suala la mtoto aliyepata ujauzito kurudi shule hata kidogo,hii ni kwa sababu ya Mira,desturi,utamaduni na mazingira pamoja na dini, hakuna dini yoyote inaruhusu mtoto wa kike kupata mimba kabla ya wakati"

Mhe.Salma Kikwete,mbunge wa Mchinga

Akisema hivyo anamaanisha anaporwa wateja wake wa ile taasis ya Mama Salma Foundation? Au alikuwa anataka kuanziasha taasis nyingine ya kulea hao watoto Sasa ameona wakirudi shuleni atakosa wateja?
Hiyo ndio sababu lakini hakuna dini inayomzuiya kijana aliyepata mimba kurudi shule
 
"Mimi sikubaliani na suala la mtoto aliyepata ujauzito kurudi shule hata kidogo,hii ni kwa sababu ya Mira,desturi,utamaduni na mazingira pamoja na dini, hakuna dini yoyote inaruhusu mtoto wa kike kupata mimba kabla ya wakati"

Mhe.Salma Kikwete,mbunge wa Mchinga

Akisema hivyo anamaanisha anaporwa wateja wake wa ile taasis ya Mama Salma Foundation? Au alikuwa anataka kuanziasha taasis nyingine ya kulea hao watoto Sasa ameona wakirudi shuleni atakosa wateja?
Huyu ana ugomvi na mama
 
Maelezo ya kwa Nini warudi shule na au wasirudi, bado hakuna mwenye logic!

Kurudi shule Ni kuhamasisha mapenzi shuleni

Kutorudi shule, Ni kuwanyima haki yao ya msingi,

Lipi Bora!
 
Huyu hana uwezo wa ku reason,kwanza hajasoma. Vipi wanaopata ngoma, mira zinaruhusu uzinzi? mbona wanatafutiwa ARV
 
Ila tuwe waangalifu, wengi si mimba za bahati mbaya, bali utukutu, yaani wengine wataongeza wakiwa huko shuleni, kwani hao uwezi kuwazuia tena kutofanya ngono, na wengi upenda starehe zaidi ya masomo, sita shangaa f4 watoto 3!
 
Mimi kitu ambacho mpaka leo hakijaniingiaga akilini ni suala la mama kuendelea na shule wakati baba amefungwa gerezani miaka 30! Yaani mama amlee mtoto peke yake miaka yote ya maisha yake, na mtoto akose malezi ya baba. . Wajinga wanashangilia kuwa wamemkomoa mwanaume kumbe ni mateso kwa huyo mzazi wa kike na maisha yaliyojaa msongo kwa mtoto.

Na sijui mtoto anakua anaambiwa baba yako yuko wapi? Na kama ni gerezani alifungwa kwa kosa gani? Kama kosa la baba yake lililomfanya akafungwa miaka 30 ni kumzaa yeye, sijui huyo mtoto kama atajiona ana thamani!!! Yaani baba kunizaa mimi ilikuwa makosa?? Kwa hiyo sikutakiwa kuzaliwa??? Inafikirisha sana.

Na kama lengo ni kuzuia mimba kwa nini isiwekwe sheria hata ya mtoto wa kike kufungwa au kupewa adhabu yoyote? Baba afungwe miaka 30 lakini mtoto wa kike waweke hata miaka mi3 tu inatosha. Uje uone kama mtoto wa kike mwanafunzi atakubali kukuvulia kizembe. Hawa watoto wa sasa ni watu wazima kabisa kiakili na kimatendo. Hakuna anaebakwa, asilimia kubwa wapo kwenye mahusiano kama watu wazima tu. Na nani ana justify kuwa wa kiume ndo chanzo all the time? Kuna mazingira mengi ambayo wa kike anakuwa chanzo. Hawa wa siku hizi hadi kutongoza mwanaume kwenye simu wanatongoza. Kumuadhibu wa kiume tu ni kuonea jinsia ya kiume na sijajua lengo hasa huwa ni nini.

Wanafunzi wa kike hata hiki kidogo walichokuwa wanajilinda ni kwa kuogopa kuwa akipewa mimba ataachishwa shule na kukatiza ndoto zake. Hii ilikuwa adhabu inayomuogopesha. Sasa hivi unaiondoa alafu unategemea kuzuia mimba mashuleni au unapanga kufungua clinic shuleni? Maana itafika hatua itakuwa ni fashion kwa wanafunzi, kiasi kwamba itaonekana ndio ujanja na ambae hajazaa ni mshamba na wanamcheka.

Tujifunze kufikiria kwa kina kuokoa kizazi chetu. Tusipokee kila kitu tunacholetewa, na sisi tuna akili zetu, tuzitumie. Na namna nzuri ya kumuinua mtoto wa kike ni kumpandisha amfikie wa kiume, na wala sio kumshusha wa kiume alingane na wa kike.

Nawasilisha.

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
..asante sana kwa mchango wako.

..je, njia za uzazi wa mpango za ndugu zetu wa kusini na hizi za kisasa, au za kijadi?

..Ni vizuri uka-share taarifa hizo kwani hili ni tatizo kubwa ktk maeneo mengi hapa nchini.

..kuna umuhimu wa kuhakikisha mtoto wa kike anajielewa na anakuwa na malengo ktk maisha yake.
Mkuu Kama sikosei mwaka 2017 mkoa wa Lindi uliongoza kwa utumiaji wa njia za uzazi wa mpango,hivyo kwa kifupi tu wakazi wa mkoa wa Lindi ikiwemo na mkoa wa mtwara wanatumia Sana njia za kisasa katika kuzuia mimba .

Kuna shule moja niliwahi fundisha huko mtwara kwa miaka mitano,huwezi amini ndani ya miaka yote hiyo ni mimba nne tu ndo zilizolipotiwa kwa shule hiyo.

Baada ya kuhama mazingira na kuja Mwanza ,Kuna shule nilipangiwa ,nilibahatika kuwa mwalimu wa darasa kwa kidato Cha Cha kwanza ,ambao walikuwa mikondo mitatu,Mimi nilipewa mkondo mmoja ,ndani ya nusu mhula kulikuwa na lipoti sita za watoto kupewa mimba katika mkondo wangu,nilipofanya analysis kwa shule nzima kwa mwaka huo kulikuwa na mimba zaidi ya 15 ,na hapo hakuna hata mimba moja iliyopata mhusika,au hata wahusika wa mimba kutiwa nguvuni,

Nilichogundua Ni kuwa watu wa Kanda ya ziwa hasa Hawa jamii ya wasukuma Wana taarifa hasi Sana juu ya njia za uzazi wa mpango,hivyo bado nasisitiza kuwa serikali licha kusisitiza watoto waliojifungua kurudi mashuleni bado wanayo nafasi pia ya kutoa elimu ya uzazi wa mpango huku ikisisitiza watoto kutumia njia za uzazi wa mpango.Hii itasaidia Sana kuwaokoa vijana wetu kupata watoto wasiotarajiwa.

Huku usukumani watu bado wako gizani Sana juu ya elimu ya uzazi wa mpango,hapa nilipo nina jirani yangu ambaye maisha yake Ni duni Sana,Cha kushangaza ana watoto wengi kuniliko Mimi mwenye unafuu wa maisha,kula shida ,kulala shida ,inafikia kipindi unatamani kumuuliza huu uzaaji wake Ni kwa faida ya Nani,but unakaa kimya tu!!!!


Elimu kwa watoto wetu ni muhimu Sana.
 
"Mimi sikubaliani na suala la mtoto aliyepata ujauzito kurudi shule hata kidogo,hii ni kwa sababu ya Mira,desturi,utamaduni na mazingira pamoja na dini, hakuna dini yoyote inaruhusu mtoto wa kike kupata mimba kabla ya wakati"

Mhe.Salma Kikwete,mbunge wa Mchinga

Akisema hivyo anamaanisha anaporwa wateja wake wa ile taasis ya Mama Salma Foundation? Au alikuwa anataka kuanziasha taasis nyingine ya kulea hao watoto Sasa ameona wakirudi shuleni atakosa wateja?
Lete ushahidi
 
Na kuwa na mtazamo tofauti sidhani kama ni kosa

Mimi kwangu swala la msingi sio kurudi shule, ila ni wale watoto waliowazaa.

Wao pia ni watoto, hata kama ni wadogo sijaona mahali popote wakisemewa au kujadiliwa haki zao. Au ndio mnyonge mnyongeni???

Wanaweza kurudi shule baada ya muda gani baada ya kuzaa?

Nyingi ya familia wanamotoka hazina uwezo hata wa kuwalea wao, itakuaje kwa watoto wao?

Watabaki nyumbani au ustawi wa jamii wameandaa mfumo gani kuhakikisha wanakua salama kimalezi?

Nani atawalea watoto na kuwapatia upendo wa mama?


MIMI NAONA BORA KINGA KULIKO TIBA
 
Back
Top Bottom