Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 4,953
- 4,326
1. Tangia tupate uhuru (na hata kabla yake) haijawahi kutokea mtoto wa shule (mwanafunzi) wa kike akipata mimba alipatiwa likizo ya uzazi na kurejea shuleni baada ya likizo hiyo.
2. Ni wanafunzi wa kike wa vyuo vikuu tu pekee ndiyo waliostahili na wanaendelea kustahili likizo hiyo ya uzazi. Hata wanafunzi wa vyuo vingine visivyokuwa vyuo vikuu hawastahili likizo hiyo.
3. Kama ndivyo hivyo, ni upotoshaji mkubwa kwamba ni katika awamu hii tu ya tano chini ya raisi Magufuli ndipo likizo hii ya uzazi ndipo imefutwa. Si kweli hata kidogo kwamba kabla ya awamu hii ya tano wanafunzi hawa walikuwa wanaruhusiwa kurudi shuleni baada ya kujifungua. Kama wapo waliorudi shuleni walifanya hivyo kwa wazazi wao ku forge uhamisho kwenye shule zingine ki ujanja ujanja au kwa njia za rushwa au kuwapeleka shule za binafsi (private schools). Nothing has changed. Sana sana kwa sasa mifumo mibadala ya elimu kwa watu wazima au mtu ye yeyote aliyeikoasa elimu hii ilianzishwa long time ago ambao hata hawa drop outs wanaruhusiwa kujiunga.
4. Katika awamu ya nne chini ya raisi Kikwete ili kudhibiti mimba hizi za utotoni na ongezeko la watoto wa mitaani bunge la JMT lilitunga sheria kali kwa wanaume (ikiwemo wanafunzi wa kiume) wanaowabebesha mimba watoto hawa wa kike wanafunzi na wasio wanafunzi ili mradi tu umri wao uko chini ya miaka 18. Wanaume hawa hufungwa jela kwa miaka 30 chini ya sheria hii. Hivyo adhabu kwa mwanafunzi wa kiume anayembebesha mimba mwanafunzi mwenzake wa kike ni kubwa sana inayoangamiza kabisa ndoto za mtoto huyu wa kiume ukilinganisha na ile ya mtoto wa kike. Tulitegemea hawa wanaharakati pamoja na Zitto wangalipigia kelele mtoto wa kiume (30 yrs jail) badala ya huyu wa kike ambaye aliachwa status quo na sheria hiyo.
5. Mila, maadili, desturi, tamaduni na dini zetu haziwezi hata siku moja kumfurahia mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 10 hadi 16 (wa darasa la 4 hadi kidato cha 6) kuruhusu kufanya tendo hilo la ndoa (tena bila kinga) hadi kubeba ujauzito. Hata kutoa mimba hatuwezi kuruhusu. Hata kumiliki simu haturuhusu. Kuwapata maternity leave ndiyo sahau kabisa, haturuhusu. Hata kuwapa dawa za majira (contraceptives) na kugawa condomns kwenye shule zetu haturuhusu.
6. Ni upotoshaji mkubwa Zitto anaposema kwamba ndani hakuna uhuru wa kuzungumza haya. Kila siku yuko twiter, instragram na mitandao ya jamii. Nani kamzuia kuyazungumuza hayo kwenye forum zake hizo pendwa? Zitto kila kukicha anaitisha press conferences. Nani kamzuia kuzungumza hayo kwenye hizo press conferences. Zitto ni mbunge na ni hodari sana kuongea akiwa bungeni. Na bunge ndilo lenye mamlaka ya kutunga sheria pamoja na hiyo sheria anayoitaka yeye ya maternity leave kwa watoto wa shule wa kike! Nani kamzuia kuzungumuza hoja yake hiyo bungeni au kupeleka mswaada binafsi? Anajuwa hoja yake hiyo haitaungwa mkono na walio wengi ambacho ndicho principle ya democrasy - rule of the majority, yeye anataka kulazimisha rule of the minority?
Eti anasema mkopo utabagua watoto wengi sana wa kike! Yaani anathubutu kusema uwongo kwamba watoto wengi sana wa kike walioko mashuleni wanadungwa mimba? Pathetic. Ukweli ni kuwa ni asilimia ndogo sana (less than 1%) na jitihada zinaendelea kuchukuliwa kupunguza idadi hiyo. Hata hizo pesa za WB zingesaidia pia kupunguza idadi hii ya mimba na maambukizi ya UKIMWI kwa watoto wetu hawa wa kike kwa kuwajengea mabweni and so on.