Salma Kikwete: Ni nani?

NIonavyo mimi, kunahaja ya kuja na sheria ya kulinda hadhi ya raisi wa jamhuri ya Tanzania, kwani uraisi sio kampuni ya mtu ambapo hata mke wake anaweza kuwa na kauli kwa watendaji, hebu fikiria Mama Salma anapokea taarifa ya maendeleo ya mkoa, inamaana baada ya hapo yeye ndiye anambrief Raisi? je hapa tutatofautishaje mamlaka ya Raisi na Mke wa raisi.
 
Nadhani huyu mama kwao ni Singida kama sikosei!

Hapana. Huyu mama baba yake ni Mndengereko na mama yake ni mtu wa Lindi. Ila kakulia Lindi ambako baba yake likuwa akifanya kazi nadhani bandarini na baada ya kustaafu kaamua kuishi huko huko.
 
na sio tu hana mamlaka hana hata uwezo wa kufanya analysis ya issue za kisomi kama takwimu za maeneleo, yeye ni mke mkubwa kati ya wake watatu wamzee JK

Ana watatu? Kwa mila na desturi zetu wengine, huyu ni mwanaume kweli.!
 
Attachments

  • salma.JPG
    salma.JPG
    46.2 KB · Views: 71
NIonavyo mimi, kunahaja ya kuja na sheria ya kulinda hadhi ya raisi wa jamhuri ya Tanzania, kwani uraisi sio kampuni ya mtu ambapo hata mke wake anaweza kuwa na kauli kwa watendaji, hebu fikiria Mama Salma anapokea taarifa ya maendeleo ya mkoa, inamaana baada ya hapo yeye ndiye anambrief Raisi? je hapa tutatofautishaje mamlaka ya Raisi na Mke wa raisi.

Nilifuatilia kwa makini taarifa ile baada ya kusikia kuwa kanusurika na ajali. Alikuwa anafungua rasmi bweni la wasichana ambalo yeye na NGO yake ya WAMA amefadhili kulijenga na likaitwa kwa jina lakem baada ya mabinti wanafunzi katika Wilaya hiyo ya Serengeti kuathirika mno na mimba.

Taarifa aliyokuwa anapewa na Mkuu wa Mkoa ilihusu faida ya bweni hilo kwa wasichana kwa sababbu kwa mwaka jana pekee, wasichana zaidi ya 600 walipata ujauzito na hivyo kukatisha masomo yao kutokana na wao kupanga katika nyumba za wenyeji. Taarifa hiyo ilihusu shukrani zaidi na siyo taarifa ya maendeleo ya Mkoa. Hapa niko makini na sipendi upotoshaji. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Kuna wanao sema kuwa kuna harufu ya ka-ufisadi. Sasa mimi najiuliza, hivi mtu kufadhili mabinti zetu nayo imekuwa ufisadi ??? Kumbuka kuwa hata kule Rufiji nako kajenga shule ya wasichana kuwaokoa na tabia ya Wandengereko ya kuwaozesha wangali wadogo na wakiwa bado wanafunzi. Ubaya uko wapi jamani.?????

Bravo mama Salma Kikwete endelea na moyo huo huo, watu daima huangalia mabaya tu lakini mazuri hawayaoni wanakuwa na makengengeza.

Kuna mzushi mmoja kaja na hoja kwamba mama huyu anataka kugombea ubunge kwao Lindi, huo ni uongo wa mchana jamani. ACHENI UZUSHI HAPA JAMVINI.
 
Salma Kikwete ni first lady, ana haki ya kikatiba ya kupewa ulinzi kwa nafasi yake. Hata waliotangulia walikuwa wakipewa ulinzi. Ila hilo la kupewa taarifa za maendeleo ya mkoa/wilaya si sahihi, kwani yeye hana MAMLAKA ya kutoa maamuzi. Taarifa za maendeleo hazitolewi kama hadithi, lakini kwa kumsomea huyo mama ni sawa na kusoma hadithi. Anachokifanya sasa hivi ni kampeni ya kumsaidia mumewe.

unaweza ku qoute kipengele cha katiba kinachompa haki hiyo ya kupewa ulinzi kama mke wa rais??
 
Mimi napata picha kuwa familia nzima ya mkulu JK ina matatizo, kila mtu katika familia ile anajiona ni kama msaidizi wa rais kuanzia mama hadi watoto
 
Tatizo halipo kwa Salma, tatizo ni watumishi wa uma wasiojua wanamtumikia nani.

Gharama za misafara yake siyo tu fedha bali pia muda wa watumishi wa idara mbalimbali za serikali (wanaoacha shughuli zao na kushughulikia ujio wake), zinaweza kuwa mara kumi zaidi ya anachokifanya!

Urais anapata mtu mmoja, wanafamilia wanatakiwa wabaki kuwa wanafamilia ya rais na wasihusike katika uendeshaji wa siku kwa siku wa shughuli za kiserikali wala chama, wakiwa na NGO au miradi yao waiendeshe kama wananchi wengine!

Jamii nzima inatakiwa iache kujikomba kwa familia za wakubwa.

hao watumishi wnachokifanya ni kujipendekeza wawe kwenye good books za Mkuu. Lakini hebu tujiulize, kwani mumewe haoni? Si anaona. Mbona hajamwambia mama unavuka mipaka yako. Shughuli za kiserikali zina kanui zake.wewe huhusiki!
 
unaweza ku qoute kipengele cha katiba kinachompa haki hiyo ya kupewa ulinzi kama mke wa rais??
sasa kali zaidi Juzi nimekutana na mama Mkapa kwenye duka linalouza Pombe kule jirani na mtaa wa Jamuhuri , akiwa na Mlinzi wake Pembeni, nikaambiwa ni mlinzi wa serikali.
Ila huyu mama ni ni mpenda sifa, nae anajiona ni sehemu ya utawala wa nnchi hii......
 
huwa nafurahi sana

yaani huyu mama basi tu, yaani yuko bezie kweli na siasa,

anafaa sana kwa kipindi cha watoto ( cheichei shangazi)
 
Watumishi chini ya JK hawajui cha kufanya.
Salma inatakiwa anapokuwa na ziara mikoani kivyake bila kuwa na JK anakwenda kwa jina la NGO-yake ya WAMA, na si vingenevyo. Zaidi ya kuwa FL, cheo alicjonacho ni kuwa mkuu wa WAMA. Na nigedhani anatumia fedha za WAMA kutembea huko na huko. Tatizo ni kwamba hata anapotembea tunasikia machache kuhusu WAMA sana sana tunamsikia yeye tu. Kama anatumia fedha zetu kwa kuzururia huko na huko basi JK inabidi ajibu hizo embezzlement na akitoka urais achunguzwe kama alitumia mamlaka vibaya kupitia kwa familia yake!
 
Ana watatu? Kwa mila na desturi zetu wengine, huyu ni mwanaume kweli.!
Wilcard lakini utawala wa nnchi ni zaidi ya ulijali na mapenzi, inawezekana yuko Busy na mahaba kuliko kazi za Uraisi na mambo mengine ya kazi.
na hii ndio maana Mkuu hana muda hata wakujisomea nyaraka na machapisho muhimu.
 
sasa kali zaidi Juzi nimekutana na mama Mkapa kwenye duka linalouza Pombe kule jirani na mtaa wa Jamuhuri , akiwa na Mlinzi wake Pembeni, nikaambiwa ni mlinzi wa serikali.
Ila huyu mama ni ni mpenda sifa, nae anajiona ni sehemu ya utawala wa nnchi hii......
Hiyo ni haki yake!!! Na huyu mama wala hapendi sifa labda wewe mwenyewe ndiyo mpenda sifa. Tangu zamani wala hajawahi kuwa wa namna hiyo wa kupenda sifa!!!!
 
Watumishi chini ya JK hawajui cha kufanya.
Salma inatakiwa anapokuwa na ziara mikoani kivyake bila kuwa na JK anakwenda kwa jina la NGO-yake ya WAMA, na si vingenevyo. Zaidi ya kuwa FL, cheo alicjonacho ni kuwa mkuu wa WAMA. Na nigedhani anatumia fedha za WAMA kutembea huko na huko. Tatizo ni kwamba hata anapotembea tunasikia machache kuhusu WAMA sana sana tunamsikia yeye tu. Kama anatumia fedha zetu kwa kuzururia huko na huko basi JK inabidi ajibu hizo embezzlement na akitoka urais achunguzwe kama alitumia mamlaka vibaya kupitia kwa familia yake!
ni kwamba anatumia fedha za Umma, kwasababu anatumia gari za serikali, ana ulinzi wa serikali, anaongozwa na misafara mirefu ya serikali, analala wakati mwingine katika rest house za serikali....huyu mama anatumia sana pesa za wavuja jasho wa Tanzania.
 
tatizo langu hata kama alienda kwaajili ya WAMA,lakini anaongea kama waziri fulani na si kama mwenyekiti wa NGO ya WAMA. Ipo haja ya kumpiga msasa upya mama wa kwanza ili ajue nafasi yake katika nchi hii na namna ya kuongea kwa nafasi yake.
 
Hiyo ni haki yake!!! Na huyu mama wala hapendi sifa labda wewe mwenyewe ndiyo mpenda sifa. Tangu zamani wala hajawahi kuwa wa namna hiyo wa kupenda sifa!!!!
kama si mpenda sifa kwanini akiwa kwenye ziara anatoa maagizo kama mtu mwenye mamlaka..
mama Kikwete ni kama mama mwingine yoyote mwimba taarabu.
 
Nilifuatilia kwa makini taarifa ile baada ya kusikia kuwa kanusurika na ajali. Alikuwa anafungua rasmi bweni la wasichana ambalo yeye na NGO yake ya WAMA amefadhili kulijenga na likaitwa kwa jina lakem baada ya mabinti wanafunzi katika Wilaya hiyo ya Serengeti kuathirika mno na mimba.

Taarifa aliyokuwa anapewa na Mkuu wa Mkoa ilihusu faida ya bweni hilo kwa wasichana kwa sababbu kwa mwaka jana pekee, wasichana zaidi ya 600 walipata ujauzito na hivyo kukatisha masomo yao kutokana na wao kupanga katika nyumba za wenyeji. Taarifa hiyo ilihusu shukrani zaidi na siyo taarifa ya maendeleo ya Mkoa. Hapa niko makini na sipendi upotoshaji. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Kuna wanao sema kuwa kuna harufu ya ka-ufisadi. Sasa mimi najiuliza, hivi mtu kufadhili mabinti zetu nayo imekuwa ufisadi ??? Kumbuka kuwa hata kule Rufiji nako kajenga shule ya wasichana kuwaokoa na tabia ya Wandengereko ya kuwaozesha wangali wadogo na wakiwa bado wanafunzi. Ubaya uko wapi jamani.?????

Bravo mama Salma Kikwete endelea na moyo huo huo, watu daima huangalia mabaya tu lakini mazuri hawayaoni wanakuwa na makengengeza.

Kuna mzushi mmoja kaja na hoja kwamba mama huyu anataka kugombea ubunge kwao Lindi, huo ni uongo wa mchana jamani. ACHENI UZUSHI HAPA JAMVINI.

Naona wewe hujui unachokiongea!! Maswali yetu ni haya;
1. Je mkuu wa mkoa alipaswa asome ile risala? Kwa nini isisomwe na mkuu wa shele ama mwenyekiti wa bodi ya shule? (iko wapi itifaki hapo kama si kujipendekeza?)
2. Anavyohutubia wananchi anahutubia kama nani na kwa minajiri ipi?
3. Je mke wa Rais ana mamlaka yoyote kikatiba hapa kwetu?
4. Je WAMA ni taasisi ya serikali? Kwa nini inatumia resources za serikali kama magari n.k.
5. Kwa nafasi yake kama mke wa Rais, je tutapimaje kama misaada inayotolewa kwa WAMA (based on her influence as the first lady) haitumiki kwa maslahi binafsi ya kwake na familia yake?
6. Kwa nini wakimaliza muda wao wa uongozi wanaondoka na taasisi zao?
7. Je huoni kwamba WAMA inatakiwa iwe responsible kwetu wananchi kwa sababu inatumia resources zetu kuanzia magari mpaka ofisi, sina uhakika na payroll, inawezekana pengine inatoka ikulu!!

Binafsi naona nchi hii inaendeshwa bila kufuata taratibu na best practice, mke wa rais ni mke kama walivyo wake zetu. Naamini anastahili ulinzi, mshahara na posho akisafiri basi. Haya mengine tunayoyaona ni mbwembwe tu za kikwere na yote yanatokana na watanzania kufubaa kiakili!

Vinginevyo tunatakiwa kuhoji haya mambo, kinyume na hapo siku Mama atakuja kumfukuza kazi waziri ama ofisa yoyote wa serikali kwa sababu naamini yeye na Mr. hawajui kama anavyofanya sasa si sahihi!! Wasaidizi wa rais pale ikulu wanajua haya si sahihi lakini hakuna mwenye ujasiri wa kumwambia Mama Salma wala Mkuu mwenyewe!
 
jamani hii ni tanzania zaidi ya uijuavyo akuna mwenye kujua itifaki zaidi jamani maana hili swala ni kubwa zaidi ya tunavyoliona au ni kujikomba kwa wahusika kwa mkuu wa nchi mana watz kwa kujikomba atujambo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom