Salma Kikwete: Ni nani?

GO MAMA SALMA GO......! Usikatishwe tamaa na watu waangaliao karibu.....fanya uonalo vyema.....WAKUBWA TUACHANE KUCHONGA TUMPE HESHIMA YAKE...!
 
Salma Kikwete ni mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Twawala. Mkuu wa Mkoa ni mteuliwa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Kada wa Chama Twawala. Hivyo ili uwe karibu na Rais lazima umkirimu mke wake na jamaa zake wa karibu. Hivyo usijeshangaa na mtoto wa Rais naye akisomewa risala na mkuu wa mkoa.

Labda tujiulize hivi hawa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wana kazi gani zinazowashughulisha kila siku? Mimi nadhani hizi post zote hazina shughuli yoyote ya maana zaidi ya kuwa vibaraka wa Rais na Chama Tawala.

Hiyo red, Kwa hiyo relation ya wateuliwa wa raisi wa Jamhuri kwa first lady ni sawa na relation ya shamba boy wako kwa mkeo?

Hiyo blue nakubaliana na wewe kabisa mkuu, post za RC na DC ni kuongeza garama za uendeshaji. Wakurugenzi na makatibu wa mikoa wanatosha.
 
Huu ni aina ya ufisadi pia. Kutumia rasilimali za walalahoi wa Tz kufanya promosheni ya urais wa JK. Huyu mama hana title ya kumruhusu kupewa taarifa na ma RC. Halafu kinachokera RC mwenyewe unakuta kavaa shati la kijani wakati yeye ni kiongozi wa serikali.
 
Mkuu hata mimi nashangaa mno, jana pia kafungua shule kabla ya kuhutubia, kweli sioni mantiki ya yeye kufanya yote haya, ziara kibao kama waziri fulani hivi.Hebu tukumbuke Mama Maria Nyerere, Mama Sitti Mwinyi na Mama Anna Mkapa, mbona wao hawakuwa kama yeye? Ndo haki za mwanamke labda.Tuyaacheni jamani tutafuter ugali wetu.
Walikuwamo wafanyabiashara humo ndani ha ha ha ha kila enzi na tamaduni zek tehetehetehe ni sawa na mama Obama kwenda kufundisha shule , kualikwa katika mazoezi na kufanya kicheni pati za kimarekani kwani si tamaduni tu mnasahau kwamba taasisi yake inamwaga mafedha katika miradi mbalimbali ya wamama na watoto tehe tehe tehe watu bwana wanacha kuulizia chumvi wanaweka taa kwenye mvungu ha ha ha ha
 
GO MAMA SALMA GO......! Usikatishwe tamaa na watu waangaliao karibu.....fanya uonalo vyema.....WAKUBWA TUACHANE KUCHONGA TUMPE HESHIMA YAKE...!
Hii imekaa safi na salama kama salma mwenyewe go big girl go!!!!! hata mke wa chifu uluguruni alikuwa na heshima kubwa na alilindwa kama anavyolindwa chifu anayesema wanawake zenu si wabadala wenu waanze kuzungumza hadharani ha ha ha ha ha ha ha ha nyi nyie jadilini maendeleo na namna ya kuwezesha nchi hii kujamp si kutembea kigoigoi machifu wakifika mahali watu huneemeka kwani hawajui mkono mtupu na hata nyie mlipitishia maombi yenu kwa mama zenu wacheni kudharau ukweli tehe tehe tehe
 
yeye na JK mwili mmoja nadhani umenipata!bado kupigiwa mizinga na kukagua gwaride, escort yake zaid ya spika na jaji mkuu
 
Huwa hawachinji watu baki....ni wao kwa wao

Mura !!! Unareta utani kwenye kasi yetu, arrryyyaaaaaaaa nengotema mura tamaha mona akwing'eina umuchabani ono (maana yake: ohooooo, nitakupiga aisee, angalia huyu jamaa anavyojidanganya) Wewe jidanganye tu kuwa ni wao kwa wao, naona siku zako zinahesabika. Akishasema arrryyyyaaaaaa basi kaa mbali naye maana chochote kilicho karibu naye atakitumia kama silaha na itakula kwako. Ogopa kukorofishana na MURA, utakufa siku si zako.

Mura, chihasari kabisa gwa sababhu umegwisa niretea maneno ya gitoto, singo yako nitaigata na soka sasa hibhi.
 
Jamani kwani amewaomba wamsomee hizo risala au ameomba apewe taarifa?? ni sisi wa TZ kujipendekeza - yaani viongozi wa kitanzania kwa ajili ya kulinda maslahi yao wanatetemeka tetemeka hadi wanafanya na kusema mambo wasiyopaswa. Hata ingekuwa mimi Salma, ningewasikiliza tu na mradi nitimize malengo yangu.
Viongozi wengi hawajiamini - wakisikia tu "mke wa Rais" basi - wanaona kama ndio wamemwona Rais mwenyewe - kumbe ni mkewe tu!!!!!
SALMA HANA MAKOSA - WENYE MAKOSA NI HAO WANAOJIPENDEKEZA - AU WAMEPEWA AGIZO WAFANYE HIVYO???? HATUJUI ...... ngoja wengine tuendelee kumngojea Yesu arudi.....
 
Kwa vile First Lady, anaishi nyumba moja moja na mkuu wa kaya, anafikiri kuwa First Lady ni sahihi kupokea taarifa na ataifikisha kwa mkuu wa kaya..... haa haaa. Hii inanikumbusha Lucy Kibaki , anavyowaingilia na hata kuwapiga vibao watendaji wasiojitambua kule Kenya. Huyu mkuu wa mkoa ni aina ya viongozi ambao mke wa kiongozi anaweza akawafanya lolote, kwani ni watupu! tupu! tupu!

Hebu sikiliza alichosema huyu First Lady, anawambia watu wa Tarime waache kuoa wake wengi!!! Ndiyo maana alihitaji ulinzi wa FFU, kwani alikuwa anasema mambo ambayo si kipaumbele kabisa cha watu wa Tarime.
Inamaanisha,

Kama Salma anapinga kuoa wake wengi je anaupinga uislam? Je mbona na yeye yupo katika ndoa ya wake wengi????

angeanzia nyumbani..charity begins a home.
 
Back
Top Bottom