Salma Kikwete: Ni nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Salma Kikwete: Ni nani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by miner, Mar 30, 2010.

 1. m

  miner Member

  #1
  Mar 30, 2010
  Joined: Dec 14, 2009
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Najua kwamba Salma Kikwete ni mke wa Rais J.M.Kikwete kinachonisumbua ni nafasi yake katika utumishi wa Umma maana mama huyu amekua akifanya ziara nyingi nchini sijui ni za kiserekali, binafsi au za chama na kila alipoenda amepokelewa kwa hadhi ha kupewa ulinzi na kupewa taarifa za utendaji wa serekali na wakuu wa mikoa na wilaya.

  Hilo linanisumbua anapewa taarifa hizo kama nani ? Uraisi ana ubia nani anajua tuliangalie pia gharama za ziara zinatokana na kodi zetu ? Mimi sijui maana waliomtangulia hawakua na vituko kama salma jana alikua anahutubia mkutano wa hadhara Tarime chini ya ulinzi mkali wa askari wa FFU
   
 2. M

  Mzawa Halisi JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 500
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Salma Kikwete ni first lady, ana haki ya kikatiba ya kupewa ulinzi kwa nafasi yake. Hata waliotangulia walikuwa wakipewa ulinzi. Ila hilo la kupewa taarifa za maendeleo ya mkoa/wilaya si sahihi, kwani yeye hana MAMLAKA ya kutoa maamuzi. Taarifa za maendeleo hazitolewi kama hadithi, lakini kwa kumsomea huyo mama ni sawa na kusoma hadithi. Anachokifanya sasa hivi ni kampeni ya kumsaidia mumewe.
   
 3. Zemu

  Zemu JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkuu hata mimi nashangaa mno, jana pia kafungua shule kabla ya kuhutubia, kweli sioni mantiki ya yeye kufanya yote haya, ziara kibao kama waziri fulani hivi.Hebu tukumbuke Mama Maria Nyerere, Mama Sitti Mwinyi na Mama Anna Mkapa, mbona wao hawakuwa kama yeye? Ndo haki za mwanamke labda.Tuyaacheni jamani tutafuter ugali wetu.
   
 4. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hapo kwenye suala la kuhutubia mikutano ya hadhara tena akiwa kama kiongozi wa dola (na ulinzi mkali mkali) pananiacha hoi. Pia kauli zake zina utata. Labda sisi ndo hatujui mambo ya itifaki. Ngoja tusubiri wenye uelewa wao watusaidie. Ila napata wasi wasi sana kwamba haka pia ni ka-uchochoro ka-kifisadi!
   
 5. B

  Bunsen Burner Member

  #5
  Mar 30, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 95
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Eeh bwanae hebu fikiria first ladies wa President Zuma decides to make visits to inspect development activities all around RSA, itakuwa kaaazi kwelikweli, manake kazi zisimame kupisha misafara na barabara zote ziwe nyeupe!!! hahahaaaaa.....
   
 6. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Mara nyingi FLs wanakuwa na wajibu kwa jamii. Kwa wote walopita hapa Tz isipokuwa mama Maria Nyerere ambaye sijui kama alikuwa na NGO yake nilikuwa mdogo bado, wengine wote wamekuwa nazo kwa ajili ya kusaidia watu wa hali ya chini. Nakumbuka Mama Siti Mwinyi, Mama Mkapa alikuja na Fursa Sawa, na huyu amekuja na WAMA. Sizungumzii ni kwa jinsi gani walifanikiwa kumkomboa mtu wa hali ya chini ila nazungumzia malengo yake. Hizi zote ndo zinawafanya wawe na ziara nyingi mikoani na nje ya nchi. That's the First Lady!
   
 7. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #7
  Mar 30, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Mimi huwa namwita mama kihelehele.

  Yeye ni first lady sawa. Lakini hawajawahi kuapa kikatiba kama kiongozi sasa kupewa taarifa au kufanya kazi za kiserikali si ndio hayo hayo? anavunja katiba na sheria zetu. Ni sawa na wale matapeli niliowahi kusikia wakijiita madaktari na kuingia theatre kufanya operation! unategemea nini kitatokea? Any way tuko katika nchi ya majaribio ya kinyozi. Kila anayejfunza kunyoa anajaribu kwetu. Wadhani tutafanyaje?

  Hawa mafirst lady wetu wa awamu kuanzia kwa mzee Mwinyi wamekuwa wakifanya mambo ya ajabu ajabu. Wamekuwa wakigiribu watu kuwaonyesha kuwa waume wao wanafanya mambo mazuri kumbe ni wizi mtupu! Ngoja mwisho wa awamu usikie!
   
 8. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Hii biashara iko Tz tu au ni nchi zote?

  Binfasi niliuona utawala wa mwalimu kwa karibia miaka 8 hivi nikiwa na akili nzuri (toka enzi za operesheni vijiji) ila sikuwahi kumsikia Mama Maria Nyerere akifanya ziara yoyote au kuhutubia mikutano hadhara (naomba kusahihishwa kama nimekosea). Hii kitu nadhani ilianza kwa sababu ya ujasirimali wa akina Mama Sitti Mwinyi na Anna Mkapa.
   
 9. W

  WildCard JF-Expert Member

  #9
  Mar 30, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  JK angempa nafasi kwenye Cabinet yake kama alivyofanya Museveni wa Uganda. Huyu mama anaonekana anayamudu majukwaa ya siasa. Nasikia atagombea ubunge huko kwao Lindi. Acheni tupate "Hillary Clinton" wetu hapa.
   
 10. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #10
  Mar 30, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  Mie nataka kujua pia hapa jana nimeona Mkuu wa Mkoa wa Mara akisoma Risala mbele ya mama Salma nikajiuliza maswali mengi kichwani bila majibu
  Kwani anakazi gani katika nchi mpaka asomewe hiyo Risala ?
   
 11. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #11
  Mar 30, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35

  Wake wa marais ni wajasiriamali sana, NGO wanazianzisha kama first ladies,wanapata fursa za misaada kama first ladies lakini wakitoka madarakani wanaondoka nazo.

  Hii siyo sawa kabisa.
   
 12. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #12
  Mar 30, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Nadhani huyu mama kwao ni Singida kama sikosei!
   
 13. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #13
  Mar 30, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ndo maana rais Museven kuondoa utata katika hili akaamua kumpa Mkewe uwaziri....kwa hiyo sometimes huwezi jua yupo pale kama waziri au FL...!!
   
 14. Mwananzuoni

  Mwananzuoni JF-Expert Member

  #14
  Mar 30, 2010
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 288
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Mkumbuke "Mama wa Kiswahili" akipewa nafasi ndio yanayotokea.
   
 15. J

  Jafar JF-Expert Member

  #15
  Mar 30, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hilo la kupewa taarifa za maendeleo ni kosa - taarifa anapewa mtu mwenye dhamana, na aliyeapa kufanya kazi kwa niaba ya aidha wananchi au serikali.

  Lakini kutembelea mikoani sioni kama ni tatizo, pia huenda wakuu wa mikoa wanajipendekeza mpaka kupitiliza. Nakumba mama Laura Bush alitembelea Bongo, lakini kwenye msafara wake mwenyeji wake alikuwa Anna na alitembelea miradi ya mama Anna (fulsa sawa) ambayo Laura alikuwa akiipa mchongo. Yes, alikuwa na walinzi kibao, gari nyingi na abulance ya kwao. Kwa hiyo sioni tatizo Salma akizurura ila naona tatizo ITIFAKI KUTANIWA.
   
 16. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #16
  Mar 30, 2010
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 518
  Trophy Points: 280
  Tatizo halipo kwa Salma, tatizo ni watumishi wa uma wasiojua wanamtumikia nani.

  Gharama za misafara yake siyo tu fedha bali pia muda wa watumishi wa idara mbalimbali za serikali (wanaoacha shughuli zao na kushughulikia ujio wake), zinaweza kuwa mara kumi zaidi ya anachokifanya!

  Urais anapata mtu mmoja, wanafamilia wanatakiwa wabaki kuwa wanafamilia ya rais na wasihusike katika uendeshaji wa siku kwa siku wa shughuli za kiserikali wala chama, wakiwa na NGO au miradi yao waiendeshe kama wananchi wengine!

  Jamii nzima inatakiwa iache kujikomba kwa familia za wakubwa.
   
 17. W

  WildCard JF-Expert Member

  #17
  Mar 30, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Na uswahili wote ule alionao? Hawezi kuwa ametoka bara! Wanaomfahamu zaidi wamo humu. Watatujuza. Shida yetu nyingine TZ ni kwamba mtu anafikia hatua ya kula na kulala IKULU yetu huku wengi wetu tukiwa hatumfahamu kabisa zaidi ya kumwona kwenye luninga na magazetini!
   
 18. mtuwatu

  mtuwatu Member

  #18
  Mar 30, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 95
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Haya wasoma risala ndo akili zao hazina pingili vichwani mwao!!
  Afu jamaani mkoa wa mara sio mkoa - nadhani ule mkoa ni nchi nyingine kabisaaaaa!
  Maana hata - sheria hawazijui,utaratibu hwajui so hata viongozi waliopo huko wanapelekwa wale wasojua itfaki na utaratibu ss tangu lini mkuu wa mkoa anasoma risala!!??
  Huyo mama alitakiwa kuwapa pole wanawake wanaopigwa na waume zao - basi! na hiyo ndo kazi kubwa - kukemea tabia hizo huko tarime sio vinginevyo
  Wanabore hawa!!!!
   
 19. T

  Tata JF-Expert Member

  #19
  Mar 30, 2010
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,737
  Likes Received: 657
  Trophy Points: 280
  Salma Kikwete ni mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Twawala. Mkuu wa Mkoa ni mteuliwa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Kada wa Chama Twawala. Hivyo ili uwe karibu na Rais lazima umkirimu mke wake na jamaa zake wa karibu. Hivyo usijeshangaa na mtoto wa Rais naye akisomewa risala na mkuu wa mkoa.

  Labda tujiulize hivi hawa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wana kazi gani zinazowashughulisha kila siku? Mimi nadhani hizi post zote hazina shughuli yoyote ya maana zaidi ya kuwa vibaraka wa Rais na Chama Tawala.
   
 20. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #20
  Mar 30, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  na sio tu hana mamlaka hana hata uwezo wa kufanya analysis ya issue za kisomi kama takwimu za maenDeleo, yeye ni mke mkubwa kati ya wake watatu wamzee JK
   
Loading...