Salim Asas tambua kuwa wengi wa UVCCM hawafurahii mnavyouza nchi. Wanaofaidi ni wachache, hawawezi kutetea ufisadi

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
1,126
4,169
Usilazimishe watetee uovu.

----

MNEC SALIM ASAS ATAKA VIJANA KUVUNJA UKIMYA KUJIBU HOJA ZA WAPOTOSHAJI

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Salim Asas ameushangaa ukimya wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Iringa katika kutetea viongozi na mipango mbalimbali ya maendeleo inayofanywa na serikali ya chama chao likiwemo suala la uendeshaji wa bandari lililoibua mjadala mkubwa hivi karibuni.

Akifungua Baraza la UVCCM la mkoa huu leo Asas amesema; “Kuwa wanachama wa UVCCM sio kuwa watu wa hamasa na kuimba tu, ni pamoja na kutimiza wajibu kusema mazuri ya chama na serikali yake, na kuwatetea viongozi wake dhidi ya kejeli na hujuma zinazofanywa na wapinzani.”

Akizungumzia makubaliano ya ushirikiano wa uendeshaji wa bandari baina ya serikali ya Tanzania na Dubai, Asas alisema wapo baadhi ya watu kwa makusudi kabisa wamekuwa wakipotosha dhamira njema ya serikali katika mpango huo wakisema nchi inauzwa.

“Kuna vita ya kiuchumi na mnasikia kuna watu wanapotosha umma wakisema nchi inauzwa na ninyi vijana wetu mpo kimya tu. Hivi wanaosema nchi inauzwa wanajua thamani ya nchi hii kama sio lugha za kipuuzi tu?”alisema.

Akiwashangaa vijana kwa kushindwa kujibu hoja kama hizo alisema wakiendelea kufanya hivyo katika masuala nyeti na ya msingi inaweza kutoa tafsiri kwamba ukimya wao ni kwasababu wao pia wanaunga mkono upotoshaji unaoendelea.

“Lazima vijana wetu mjue kila unapofanya mema na mazuri ndipo unapozidi kupingwa. Jibuni hoja zao kwasababu hoja walizonazo zinajibika,” alisema na kuongeza kwamba ukiona hupingwi na badala yake unasifiwa tu ujue kuna mahali hufanyi vizuri.

Katika kujibu hoja za wapinzani hao wa maendeleo, Asas aliwataka vijana hao kutumia lugha za kistaarabu bila kutukana na watumie mitandao ya kijamii inayofikisha ujumbe kwa haraka badala ya kusubiri mikutano ya hadhara ambayo haiwezi kufanyika kila siku.

“Huko kwenye mitandao ya kujamii hatusikii kama kuna UVCCM, Rais na baadhi ya viongozi wanatukanwa na vijana wetu mliopa kulinda chama na viongozi wake mpo kimya, hatusikihi mkijibu hoja. Tambueni kazi yenu ni pamoja na kutetea chama ,viongozi wake na serikali yake,” alisema.

Aliwataka pia kupima uadilifu wao na kama haupo sawa wajirekebishe ili wasiwe na dosari pale itakapojitokeza watahitajika kwa majukumu mengine.

Awali Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Iringa, Aggrey Tonga alisema katika kipindi cha uongozi wao wamejipanga kutekeleza majukumu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuimarisha uhai wa jumuiya hiyo, kujijenga kiuchumi na kuweka mikakati ya kushinda chaguzi zote za serikali.

Mengine ni kuamsha hali ya vijana kushiriki michezo, kujenga mahusiano na makundi mbalimbali ya vijana, kukamilisha ujenzi wa nyumba za watumishi wake na kuwa na mawazo chanya katika kushugulikia changamoto mbalimbali za kijamii ukiwemo ukatili wa kijinsia.

Naye Katibu wa UVCCM Mkoa Hassan Makoba alisema watahakikisha wanaimarisha dhana ya jumuiya hiyo kuwa walinzi wa chama na viongozi wake na akaomba ushirikiano toka kwa wadau wao wote.

Katika kuimarisha jumuiya hiyo Makoba aliomba pia wadau mbalimbali kuwawezesha kupata gari kwa ajili ya kurahisisha kazi za jumuiya hiyo.

Chanzo: Matukio Daima
 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa mh Salim ASAS ameshangaa ukimya wa UVCCM mkoani kwake

ASAS ameshangaa ukimya wa UVCCM katika kutetea Viongozi na miradi mbalimbali ya Maendeleo inayofanywa na Serikali ya Chama chao ikiwemo suala la Uendeshaji wa Bandari ambalo limezua Mjadala mkubwa

Source: Kitenge media
 
Tunatetea viongozi ama tunatetea katiba,kanuni ya Chama. Ikiwemo na kulinda viongozi na mali nyingine za Chama.

Kuna tofauti kati ya kulinda na kutetea!
 
Uvccm hayo maji siyo size Yao wanajua mawe watakayorushiwa na vijana wa upinzani uenda wasiwe na nguo au kuwavua wakubwa zao. Waacheni waendelee kupiga pesa Kwa kukagua miradi ya BBT kisha kuvizia teuzi za UDAS , DC Kwa migongo ya fitina na majungu. Nyie waNEC mliokomaa ndiyo mumsaidie SSH kujibu hoja za kuhusu kuuzwa au kubinafsishwa bandari Kwa DP WORLD Kwa ushahidi na hekima ili wananchi wapate elewa mustakabli wa chama juu ya kusimamia serikali .
 
Mkiti CCM ni mzanzibari mkiti UVCCM ni mzanzibari anaogopa akijitokeza wanasema wazanzibari wameungana kuiuza nchi
 
Usilazimishe watetee uovu.

----

MNEC SALIM ASAS ATAKA VIJANA KUVUNJA UKIMYA KUJIBU HOJA ZA WAPOTOSHAJI

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Salim Asas ameushangaa ukimya wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Iringa katika kutetea viongozi na mipango mbalimbali ya maendeleo inayofanywa na serikali ya chama chao likiwemo suala la uendeshaji wa bandari lililoibua mjadala mkubwa hivi karibuni.

Akifungua Baraza la UVCCM la mkoa huu leo Asas amesema; “Kuwa wanachama wa UVCCM sio kuwa watu wa hamasa na kuimba tu, ni pamoja na kutimiza wajibu kusema mazuri ya chama na serikali yake, na kuwatetea viongozi wake dhidi ya kejeli na hujuma zinazofanywa na wapinzani.”

Akizungumzia makubaliano ya ushirikiano wa uendeshaji wa bandari baina ya serikali ya Tanzania na Dubai, Asas alisema wapo baadhi ya watu kwa makusudi kabisa wamekuwa wakipotosha dhamira njema ya serikali katika mpango huo wakisema nchi inauzwa.

“Kuna vita ya kiuchumi na mnasikia kuna watu wanapotosha umma wakisema nchi inauzwa na ninyi vijana wetu mpo kimya tu. Hivi wanaosema nchi inauzwa wanajua thamani ya nchi hii kama sio lugha za kipuuzi tu?”alisema.

Akiwashangaa vijana kwa kushindwa kujibu hoja kama hizo alisema wakiendelea kufanya hivyo katika masuala nyeti na ya msingi inaweza kutoa tafsiri kwamba ukimya wao ni kwasababu wao pia wanaunga mkono upotoshaji unaoendelea.

“Lazima vijana wetu mjue kila unapofanya mema na mazuri ndipo unapozidi kupingwa. Jibuni hoja zao kwasababu hoja walizonazo zinajibika,” alisema na kuongeza kwamba ukiona hupingwi na badala yake unasifiwa tu ujue kuna mahali hufanyi vizuri.

Katika kujibu hoja za wapinzani hao wa maendeleo, Asas aliwataka vijana hao kutumia lugha za kistaarabu bila kutukana na watumie mitandao ya kijamii inayofikisha ujumbe kwa haraka badala ya kusubiri mikutano ya hadhara ambayo haiwezi kufanyika kila siku.

“Huko kwenye mitandao ya kujamii hatusikii kama kuna UVCCM, Rais na baadhi ya viongozi wanatukanwa na vijana wetu mliopa kulinda chama na viongozi wake mpo kimya, hatusikihi mkijibu hoja. Tambueni kazi yenu ni pamoja na kutetea chama ,viongozi wake na serikali yake,” alisema.

Aliwataka pia kupima uadilifu wao na kama haupo sawa wajirekebishe ili wasiwe na dosari pale itakapojitokeza watahitajika kwa majukumu mengine.

Awali Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Iringa, Aggrey Tonga alisema katika kipindi cha uongozi wao wamejipanga kutekeleza majukumu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuimarisha uhai wa jumuiya hiyo, kujijenga kiuchumi na kuweka mikakati ya kushinda chaguzi zote za serikali.

Mengine ni kuamsha hali ya vijana kushiriki michezo, kujenga mahusiano na makundi mbalimbali ya vijana, kukamilisha ujenzi wa nyumba za watumishi wake na kuwa na mawazo chanya katika kushugulikia changamoto mbalimbali za kijamii ukiwemo ukatili wa kijinsia.

Naye Katibu wa UVCCM Mkoa Hassan Makoba alisema watahakikisha wanaimarisha dhana ya jumuiya hiyo kuwa walinzi wa chama na viongozi wake na akaomba ushirikiano toka kwa wadau wao wote.

Katika kuimarisha jumuiya hiyo Makoba aliomba pia wadau mbalimbali kuwawezesha kupata gari kwa ajili ya kurahisisha kazi za jumuiya hiyo.

Chanzo: Matukio Daima
Mzee utaratib ni kwamba... Wanaccm wanatakiwa kwanza kutetea maslahi ya chama Taifa baadae kbs!! So ukiona wapo kimya ni sawa tu ila gusa maslahi ya chama utajua ujui!!
 
Back
Top Bottom