Mwakalinga Bujo
JF-Expert Member
- Oct 22, 2008
- 2,719
- 1,440
Moja ya mambo yaliyonisukuma nianike jambo hili ni mwanzo wa story hii ya miamba hawa wawili . Story ilianzia FB kwa mkuu Zitto kuweweka bandiko hili:
Wakiweza kujibu hoja kutokana na mambo hayo manne kweli naamini utakuwa mwanzo mzuri wa kumaliza tofauti za manguli hawa wawili
Majibu ya Zitto kwa hili
Kama ulivyoona hapo juu alitajwa ndugu yetu Albert Msando, sasa leo kamanda Albert Msando amevunja ukimya na kuweka haya kwenywe wall yake ya FB kama Salamu kwa Godbless J Lema na Zitto.Zitto juu ya Posho;
"Enyi Watanzania, wabunge wenu wanataka posho ziongezwe na mishahara. Mbunge mmoja wa upinzani kanisemea mbovu huko Dodoma kwenye kikao cha wabunge eti mimi ni kikwazo kwa wao kuongezewa posho. Kasema nikiwa Arusha nakaa chumba cha dola 600 kwa siku. Hivi Hoteli gani Arusha ina chumba dola 600 kwa siku? Albert Msando naomba msaada nikija Arusha unionyeshe hiyo hotel japo nione chumba cha dola 600 kinafafanaje...."
by Msando Alberto
Salaam Zitto na Lema...
Tatizo lenu sio posho. Si vyema kuwadanganya watu au kuwaaminisha kwamba tofauti iliyopo kati yenu ni mawazo au misimamo tofauti kuhusu Posho.
Kama ingekuwa hivyo basi isingekuwa tatizo. Kuwa na mawazo au misimamo tofauti sio tatizo hata siku moja.
Mtu hauhitaji rocket science kuona kwamba kuna zaidi nyuma ya pazia.
Ila kabla sijasema sana niweke mambo machache wazi.
1. Zitto na Lema ni marafiki zangu. Nawafahamu wote kiasi cha kuweza kusema kwamba najua uwezo wa kila mmoja wenu.
2. Sioni tatizo kutumia socia media kugombana au kukosoana. Najua wapo ambao wanasema vikao vitumike. Lakini vikao hivyo wengi wetu hatuhudhurii kwa sababu sio wajumbe. Yatokanayo na vikao hivyo hubaki siri na tunayoletewa ni muhtasari wa vikao. Hatupati nafasi ya kujua nani kasema nini na kwa nini na amesemaje.
3. Chama lazima kikue. Na kukua lazima mambo fulani fulani yatokee. Najua yanaweza yakapitiliza na kuathiri chama ila ni bora yatokee na kuathiri chama kuliko yaje yatokee na kuathiri NCHI. Kama tutavurugana na kugombana chama kikasambaratika basi ni kheri kuliko tuje kufarakana, kuvurugana na kugombana wakati tumepewa madaraka kuongoza watanzania.
Baada ya kuweka hayo mambo matatu wazi niseme kwamba suala la kupokea au kutopokea posho ni suala binafsi sana. Ni suala la NAFSI.
Kama nafsi yako inakutuma upokee posho basi ndio ulivyo. Nafsi hiyo hiyo itakutuma upokee rushwa, useme uongo, ukose maadili nk.
Kama nafsi yako inakutuma ukatae posho basi ndio ulivyo. Nafsi hiyo hiyo itakutuma usipokee rushwa, usiseme uongo, uwe na maadili nk.
Lakini, nafsi pia inaweza kukutuma kuchanganya mazuri na mabaya. Ukapokea posho ukakataa rushwa. Au ukakataa posho ukapokea rushwa. Ni nafsi yako.
Zitto na Lema mjipime kwa kile kilicho ndani ya nafsi zenu. Uzuri ni kwamba mwanadamu huwezi kuidanganya nafsi yako.
Ila kumbukeni yafuatayo;
1. Nyinyi ni vijana ambao mmepewa nafasi za kuongoza wananchi ambao wanawaamini.
2. Nchi yetu inahitaji viongozi ambao ni WAKWELI na WASIO NA TAMAA.
3. Lazima mtofautishe KUJULIKANA na KUWA MAARUFU. Nyie wote mnajulikana. Hamna umaarufu wowote. Sidhani kama mmekuwa viongozi ili muwe maarufu.
4. Mna nafasi kubwa sana kwa vijana kwa sababu ya kujulikana kwenu. Nchi hii itasonga mbele tu kama vijana wataamua kushiriki kikamilifu kwenye siasa. Lakini vijana hawatashiriki ipasavyo kama tutawavuruga na kuwachanganya.
5. Wananchi watapima uongozi wenu sio kwa idadi ya mabandiko FB, tweets au articles. Wananchi hawakuchagua bloggers au waandishi wa articles. Walichagua viongozi wa kuwawakilisha.
Jiulizeni ni watanzania wangapi wako FB na Jamii Forum? Kwa nini idadi yao ni hiyo!? Ukweli wenu au uongo wenu unawafikia?!
Nimesoma andiko la Lema. Limejaa hasira, jazba na kiasi fulani chuki. Nimesoma majibu ya Zitto. Yamejaa kujiamini, kupuuzia na kiasi fulani dharau. Nawajua jinsi mlivyo kwa hiyo sishangai na wala hainikeri.
Lakini mwisho wa siku najua itakavyokuwa. Ukweli utajulikana. Kuna mmoja atabaki mwingine atatwaliwa. Kuna mmoja historia yake itakuwa ni kufundishia mwingine itakuwa kwa ajili ya kukemea. Kwa mlipofikia sasa lazima tujue nani Muongo nani Mkweli.
Kwa sababu mmeamua kufulia nguo kisimani basi zianikeni tuone madoa na usafi wake. Hatutarajii mrudishe kwenye tenga mkaanikie nyumbani.
NB:
Kila mmoja wenu kwa nafasi yake awajulishe watanzania amefanya nini kama Mbunge na Kiongozi wa chama. Kwenye mambo haya;
1. Elimu
2. Afya
3. Ajira
4. Uwajibikaji.
Hayo tu manne. Sitegemei mtatuangusha katika hili. Mkishatoa taarifa zenu basi tutaamua kama mpokee au msipokee posho. Tutatoa msimamo wetu pia.
Wakiweza kujibu hoja kutokana na mambo hayo manne kweli naamini utakuwa mwanzo mzuri wa kumaliza tofauti za manguli hawa wawili
Majibu ya Zitto kwa hili
By Zitto Kabwe
Siku zote najitajidi kutowaangusha. Kila nikifanya jambo najiuliza naweza kujitetea mbele ya ndugu na rafiki zangu? Naweza kujitetea mbele ya umma? Ni suala la misingi tu maana ukiwa muumini wa misingi hutetereshwi. Mimi mjamaa, maisha yangu yanaakisi hivyo tofauti kabisa na watu wanavyotaka kuaminishwa. Lakini silazimishi kila mtu awe kama Mimi ndio maana nina marafiki wakubwa mabepari na wengine Marxists haswa. Tunapishana kimawazo lakini tunaheshimiana mawazo ya kila mmoja wetu.
Wasiwasi wangu huu mjadala wa posho sio mjadala wenyewe, labda ni kianzio tu