Djumbe
Member
- Apr 8, 2011
- 39
- 62
Salamu rasmi IRAMBA MAGHARIBI, Timu ya kazi inaingia na kupiga kambi kuanzia Jumamosi hii kutoa elimu ya URAIA na UKOMBOZI wa Jimbo Hili kutoka kwenye ulaghai wa ccm uliowafumba macho wananchi kwa miaka mingi na maisha yao yakizidi kuwa magumu siku hadi siku, eti MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA!!!! huku wale waliopewa nafasi ya kuwatumikia wananchi wakiishia kuleta propaganda za kukandamiza harakati za mageuzi nchini na kujifanya MIUNGU WATU, kwamba hawataki kuona IRAMBA ikifanyiwa kazi za kisiasa na vyama vya upinzani kwa kuwazushia kesi za uongo na vitisho wanaharakati wanaoingia jimboni hapo, tumejiandaa sio tu kupokea vitisho, bali kwa lolote lile watakalokuja nalo ili mradi wananchi wa IRAMBA Magharibi wakombolewe,,,,, tutakuwepo hapo mimi David Djumbe, Jesca Kishoa (Iron Lady) pamoja kamanda wa upepo Ally Bananga, huku tukiwakaribisha wale wote wanajisikia kushiriki kazi hii katika jimbo hili, kwa namna yeyote ile ,wanaweza kuwasiliana nasi mapema kwa ajili ya utaratibu mzima.>>>