Sala ya kuwaombea wanawake

Sala ya kuwaombea wanawake

MorTimer

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2013
Posts
1,195
Reaction score
968
1. Atakua na simu yake mpo nyumbani dakika hiyo anakwambia umbip hajui kaiweka wapi.
- Tuhurumie Baba

2. Ana Nguo zimejaa makabati mawili lakini hajui avae nini ukimwambia mtoke!
- Baba, ni magumu kwetu mambo haya.

3. Anakasirika ukikosa kumtumia text ya good night lakini yeye akikosa wewe inabidi uwe muelewa!
- Tuwaeleweje, Baba?

4. Ana viatu zaidi ya pea 50 lakini hana viatu vya kuvaa vya kwenda ibadani.
- Mungu uwasamehe

5. Akianza kuvaa saa moja atamaliza saa tano muda wote inabidi umsubiri tu.
- Si kupenda kwao Baba ila nasi yanatushinda Bwana

6. Akienda saloon anakaa kuanzia asubuhi mpaka jioni na huna budi kumsubiri na usilalamike.
- Mungu wetu, tupe moyo wa kuyahimili haya

7. Ana mafuta tofauti ya kujipaka mikono, shingo, kisogo, miguu, mpaka kisigino! Hata Mdomoni
- Ee Mungu ni Wewe uyajuaye mateso tuyapitiayo Baba

8. Mnaachana asubuhi akiwa na furaha, na ukirudi jioni amenuna hataki hata kukusalamia na ukiuliza tu balaa.
- Tupe uvumilivu ee Bwana!

9. Anajaribu ku match nguo na hereni na akiona hazifanani abadili nguo sababu tu ya hereni.
- Teremka uwashike mikono yao baba..

10. Mkitembea barabarani inabidi ukae upande wa barabara eti wewe ni mwanaume ukigongwa na gari haina noma.
- Eeh baba tuepushe na Hiki kikombe ulisema hawa ni wasaidizi wetu lakini tumekuja kuwa wafanyakazi wao.
 
Huwa wananunua Hand bag Kwa bei kubwa Lakini Sisi wanaume Huwa hatuna hata stori na handbag zao, wanazobeba,
.
huwa wanachana nywele na kujiangalia kwenye kioo kabla ya kwenda kulala,
Eeh Mungu Uwaokoe
 
waporadhi watembee umbali mrefu lakini sio kupita shortcut kwa kuhofia kupotea,
.
wanawake hata wakisafiri safari ya kukaa siku tatu, Lakini watabeba nguo za kuvaa siku saba, kwaajili ya kuchagua kipi cha kuvaa wakati wakiwa ugenini...

EWE MUNGU UWAOKOE
 
Eh baba wambinguni, ninakuomba uzipokee na kuzibariki sala zilizoletwa kwako na wanaume wote. Ninakuomba baba hawa viumbe wenye ukubwa wa miili, misuri mikubwa lakini wadhaivu na wanyonge wa nafsi uwainulie mkono wako wa nguvu ili waimarike ktk kuchunguza udhaifu wetu unaoonekana. Amina[emoji120]
 
Back
Top Bottom