Sakata la Wazee EAC: Litaisha lini?

pesa imetoka toka 1984, Mchonga akiwa rais...lakini lawama zote kwa Kikwete!! Ndio Tanzania hiyo, kaaaazi kweli....

hawa wazee ilibidi wapewe fweza zao mwaka 1984. Vinginevyo hapa tuje na mawazo ya kupata ufumbuzi badala ya kunyoosheana vidole...kwani aliewanyima pesa zao hawa ndugu ni Nyerere!! Pesa ilitoka 1984, ilikuwaje watu wasipewe mafao yao?? sielewi hii blame Kikwete kabisa, kama Nyerere alikula pesa, yeye akazitoe wapi? Mkapa na Mwinyi walifanya nini? hivi hamwoni kama mnamwonea huyu jamaa...?

Unasahau babu, hapa haonewi mtu. Anaedaiwa siyo kikwete, ila ni serikali, na serikali ndiyo inayoongozwa na kikwete. Serikali daima ipo ila viongozi ndio wanaobadilika. Kama ingekuwa hivyo basi kusingekuwa na sababu ya Tanzania kuendelea kulipa madeni ambayo ilikopa wakati Nyerere au Mwinyi wakiwa Marais.
 
..thats the reason ..siku hizi kikwete hapendi kukaa dar es salaam..ahamie kwenye ikulu mpya inayojengwa dodoma haraka ...maana kila anapopita dar ni kero....next step watamziba kutoka kwenye mageti yote ya ikulu na hata akiruka na helicopter message sent.....

rais failure kabisa huyu....ahh!! shame ..shame !!..tumetokana naye wapi huyu!!...anavuna laana tu kwa vizee vya watu....pesa ya kuwalipa haifiki hata bilioni 3...kweli tunakosa....na infact tukiwalipa zinabaki hapa hapa na kuboresha maisha...,infact kama kulipana hadi ugomvi hata heshima hakuna....

taifa limeingia aibu leo ...THEN TUNASEMA TUNA KITENGO CHA USALAMA WA TAIFA...ambao intelligence yao imefail ku reveal ..hili...aibu aibu !!!...tatizo la ushikaji kwenye nafasi nyeti!
 
Mwalimu gani? kama ni marehemu Julius, huyu babu mwacheni tu apumzike, kwani inaboa sasa hii tabia ya kila kitu mwalimu, mwalimu.....ukweli ni kwamba EAC ilivunjika mwaka 1977, yeye Mwalimu ibn Mtukufu, a.k.a messiah, a.k.a the saint akiwa rais, wakti anang'atuka ilikuwa ni takribani miaka nane toka hii kitu i-collapse!! swali, alikuwa wapi kuwalipa hawa waungwana mafao yao? Leo hii ni miaka 31 toka kuanguka kwa EAC...awamu zote nne za serikali nchini Tanzania zimepitia hili tatizo, lakini all of a sudden lawama zooooooooote kwa huyu kikwete na serikali yake ya kifisadi, wakti tunajua kuwa tatizo hili kalirithi toka kwa Mkapa, Mkapa toka kwa Mwinyi na Mwinyi toka kwa Nyerere.......

Badala ya kutoa lawama kwa serikali kwa staili hii ya chuki na kutafuta visababu, tuanze kutoa mawazo sahihi ya jinsi gani ya kutatua matatizo ya namna hii badala ya finger pointing wakti fwacts zipo wazi....pesa za hawa wazee zilishatoka na kuliwa kabla Kikwete hajawa POTURT!!!.

Hili tatizo si jipya, mnyonge mnyongeni lakini kuweni wa kweli.......njooni na mawazo na jinsi mbadala za kupata fweza za kuwalipa hawa wazee, badala ya makelele na ku-politik huu "mshipa" ulioachwa na Nyerere!

asubuhi njema....

Mkuu, huko si ndio kupokezana vijiti????!!!!
 
Wazee wawatu wamechoka ile mbaya nawaona hapa ndio wanapita barabara ya bibi titi karibu na maktaba kuu ya taifa.sijui hata wanakwenda wapi wakongwe wawatu.Kweli hii serikali ya kikwete sijui baada ya miaka miwili itakuaje

...watu wanafikiri kila anayeweza kuongea anaweza kuwa rais...urais ni kazi ya wenye akili,ustaarab,ucha mungu...na majasiri,....sio wasanii wa ku pretend!!!

..hapa kama si kuvuna laana kikwete anavuna nini.........hawa wazee wengi kabla kikwete hajaingia walilipwa ile 2004/5....kwa nini hawa waliobakiwa anashindwa kuwamalizia malipo yao..
 
..thats the reason ..siku hizi kikwete hapendi kukaa dar es salaam..ahamie kwenye ikulu mpya inayojengwa dodoma haraka ...maana kila anapopita dar ni kero....next step watamziba kutoka kwenye mageti yote ya ikulu na hata akiruka na helicopter message sent.....

rais failure kabisa huyu....ahh!! shame ..shame !!..tumetokana naye wapi huyu!!...anavuna laana tu kwa vizee vya watu....pesa ya kuwalipa haifiki hata bilioni 3...kweli tunakosa....na infact tukiwalipa zinabaki hapa hapa na kuboresha maisha...,infact kama kulipana hadi ugomvi hata heshima hakuna....

taifa limeingia aibu leo ...THEN TUNASEMA TUNA KITENGO CHA USALAMA WA TAIFA...ambao intelligence yao imefail ku reveal ..hili...aibu aibu !!!...tatizo la ushikaji kwenye nafasi nyeti!

Sina kumbu kumbu sahihi, serikali jamani iliwapa wale wahindi waliowekeza kwenye shirika la reli Shs Billion nne!! Wanashindwa nini kulipa hawa babu zetu...sielewi kabisa na Mzee aliyepinda anadai anachukia waoisema serikali yake....JK anakazi na wasanii wenzake mwaka huu. Tusiwe wepesi wa kukwepa ukweli, wachangiaji hapo juu wanaposema hili ni tatizo la mwalimu JK amelikuta ni kutaka mtetea pasipo stahili, tuangalie majukumu ya raisi kwenye katiba nini? Waalimu nao ni tatizo aloacha mwalimu?

Ushi
 
Uhuru siku hizi umekuwa mpana sana.
Kumbe hawa wazee wameanza kupigwa dana dana toka miaka ya 1988 wametumia kila aina ya njia kudai haki yao lakini viongozi wa serikali ndo hivyo tena wana jali matumbo yao walalahoi na amini katika nchi hii hawana haki kabisa.
Kwa nini msiwalipe?Au bado mnazungushia kwenye biashara zenu K/KOO?
 
Zipo pia namna nyingine za kudai haki kuliko kusababisha usumbufu kwa watu wasiohusika na mzozo huo. Kuna jamaa wamechelewa flight na wengine tunafanya kazi za kubangaiza na binafsi nimechelewa kutuma bid. Manake nimekosa dili na nina bifu na wazee na serikali vile vile.

Mnapodai haki zenu watazameni na wengine kama kila mtu anajijali mwenyewe hatutafika. Huu ni uchoyo wa watu weusi kutazama kila mtu maslahi yake hatutafika na tutaendelea kuchapa miguu na kubuluzwa miaka yote. Politike kuweka mbele pia sio poa maisha ni zaidi ya siasa.

..kaka falsafa ya wanamapinduzi inasema kwenye mapambano lazima wachache wataumia ..kwa ajili ya wengi...impact waliyoleta wale wazee pale ni funzo kubwa,,.....kwa namna yeyote business could not just be as usual....hata sisi tupo hapa leo hii ..there are people who sacrificed for us....thats a revolution circle..ukijua hilo muda wowote utakuwa tayari kujitoa kwa ajili ya vizazi vya kesho kama wazee wetu wa kale walivyojitoa kwa ajili yetu....mfano kama nchi inatekwa kifisadi ni vita ambayo kila mmoja anatakiwa aone fahari kupigana....
 
Mwacheni Nyerere wangu apumzike.

Fedha za wastaafu hawa zilikuja baadaye zikaliwa na serikali katika matumizi mengine kwa visingizio mbalimbali. Serikali irudishe sasa!

Ujinga wa serikali umefanya hawa wazee waje na madai mapya ya kudai riba ya fedha zao zilizokaa serikalini na kulipwa kwa viwango vya thamani ya sasa ya sarafu.

Madai mapya na ongezeko la wadai ndio mambo yanayofanya serikali iwapige danadana hawa wazee wetu.

Hivi kuna wazanzibar wenzetu katika hawa wazee?

Asha
Nasikia zilitumika kwenye vita ya Uganda!!! ehe mlishangilia kumng'oa Nduli Iddi Amini lakini haya ndiyo maumivu yake. Mlipe sasa!!!
 
unawatumia karandinga na maji ya upupu wazee!!!!!!!
Unapanga kumwgia baba yako upupu!!!!!!!!!!!!! HII LAANA UTAISAFISHIA WAPI.
HALAFU TUENDELEE KUITA KISIWA CHA AMANI??????? kWELI NATATOKWA NA MACHOZI.
 
what is 2 to 3 billion out of 133 Billion and those of dubious contracted made by the same Fisadis.

Alama za nyakati zinasomwa. ambapo awamu ya pili ya uraisi kuwepo katika hali ya utata.
 
Hivi Usalama wa Taifa (UwT) wako wapi? Inawezekana vipi kwa kikundi hiki cha zaidi ya watu 80 na wenye umri wa zaidi ya 50+ kupanga mpango kama huu na kufanikisha kwa asilimia 100 bila ya kugunduliwa na Usalama wa Taifa!!! Hivi kweli tuna usalama wa taifa? au Mwl. Nyerere aliondoka nao?

Originally Posted by Songambele;
Zipo pia namna nyingine za kudai haki kuliko kusababisha usumbufu kwa watu wasiohusika na mzozo huo. Kuna jamaa wamechelewa flight na wengine tunafanya kazi za kubangaiza na binafsi nimechelewa kutuma bid. Manake nimekosa dili na nina bifu na wazee na serikali vile vile.

Mnapodai haki zenu watazameni na wengine kama kila mtu anajijali mwenyewe hatutafika. Huu ni uchoyo wa watu weusi kutazama kila mtu maslahi yake hatutafika na tutaendelea kuchapa miguu na kubuluzwa miaka yote. Politike kuweka mbele pia sio poa maisha ni zaidi ya siasa.

Songambele;
- Mara ngapi umesikia mgomo wa "waongoza ndege", je hao waliokuwa wasafiri unafikiri ilikuwaje?

- Mara ngapi tumekuwa na mgomo wa "wafanyakazi wa benki", je hao waliokuwa na mahitaji wa fedha ilikuwaje?

- Mara ngapi umesikia mgomo wa "madaktari", je umeshawahi kujiuliza waliopoteza ndugu zao kutokana na mgomo huo!

- Mara ngapi tumekuwa na mgomo wa "vyombo vya usafirishaji", "waalimu", nk!

Hao wote hapo juu hugoma kutokana na kazi zao, lakini wazee hawa wa EAC hawana kazi, na namna pekee ya kusikilizwa na serikali pamoja na jamii ndio hiyo!

Nina wapongeza hawa wazee kwa 100%, kwanza wameonyesha nchi hii haina Usalama wa Taifa, pili nchi hii sasa porojo nyingi, utekelezaji sifuri!
 
Sina kumbu kumbu sahihi, serikali jamani iliwapa wale wahindi waliowekeza kwenye shirika la reli Shs Billion nne!! Wanashindwa nini kulipa hawa babu zetu...sielewi kabisa na Mzee aliyepinda anadai anachukia waoisema serikali yake....JK anakazi na wasanii wenzake mwaka huu. Tusiwe wepesi wa kukwepa ukweli, wachangiaji hapo juu wanaposema hili ni tatizo la mwalimu JK amelikuta ni kutaka mtetea pasipo stahili, tuangalie majukumu ya raisi kwenye katiba nini? Waalimu nao ni tatizo aloacha mwalimu?

Ushi

Wewe unasema bilioni nne!!! Pole sana! Serikali imetoa tena bilioni 83 wiki hii ili kuinusuru TRL kwa kuwa hawana pesa ya kuwalipa mishahara wafanyakazi.

Lazima kuna pesa nyingine inaliwa na wakubwa kwa kupitia mgongo wa TRL. Hii ya wastaafu wa EAC haina dili kwao ndio maana hawaitilii maanani!
 
kwahiyo ni sahihi kwa Nyerere kuto walipa hawa wazee pesa zao? pia ni sahihi kwa Mwinyi na Mkapa kukopa kisha hatuoni maendeleo yoyote?? na wasiwasi kuwa hatuelewani hapa.....mie nataka tatizo likome na lawama ziende kule panapo faa, wewe unakimbilia kuweka band aid na unaangalia right now,right here!!

kwanini imekuwa hivi ilivyo at first place? why? hilo ndio tatizo langu kubwa zaidi ktk hili saga......lakini ninyi mmepania Kikwete, haya, goodluck na hiyo regime change.

..siku hizi kumtetea KIKWETE lazima uwe KICHAA.....kama yeye aliyosema akiwa marekani akihojiwa na jarida moja kuwa ..siku hizi kuongelea ujamaa na KUJITEGEMEA...lazima uonekane chizi....

akasahau aliapa kulinda katiba inayosema TANZANIA ITAFUATA SIASA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA....alisahau kuwa kabla ya kuukosoa ujamaa na kujitegemea hadharani alitakiwa KUONDOA KIPENGELE CHA SIASA YA UJAMAAA NA KUJITEGEMEA KWENYE KATIBA YA NCHI.....
 
Itafika pahala hii itabadilika tu, wazee wameonyesha njia kwa vijana kwamba haki inatafutwa kwa njia nyingi.Ujumbe umefika pahala pote duniani leo wanajua serikali hii imedhulumu haki ya wazee hawa, du aibu kweli sijui Mkulo atapita wapi na bakuli lake la kuombaomba.kweli hawa wazee jeiri na ndio maana henzi zao waliweza kumtoa mkoloni sisi tusinge weza, si mnaona sasa hivi tunavyo muita na kumrudisha mkoloni kwa nguvu zote,Hawa wazee walimkataa, ama kweli aibiwi mtu hapa mpaka kieleweke lisi hivyo tume iundwe na ukweli ujulikane.
 
Inaonaka nchi yetu siku hizi huwezi kupata haki yako kama huwezi kuonyesha ujeuri; hii ni hatari kwa mustakabali wa Taifa na kizazi kijacho maana style ya kudai haki itakuwa lazima utunishe msuli kwanza.
 
kwani usalama wa Taifa wanalipwa vizuri hadi kumtetea jamaa...? Si ajabu nao wanasema ni poa tu. kwani nchi hii ni yetu sote, usalama wa taifa, wanajeshi, walimu, wazee wa EAC n.k. Wote wamechoka!! hakuna nuru mbeleni. Nani asiyependa maisha bora?
 
Inaonaka nchi yetu siku hizi huwezi kupata haki yako kama huwezi kuonyesha ujeuri; hii ni hatari kwa mustakabali wa Taifa na kizazi kijacho maana style ya kudai haki itakuwa lazima utunishe msuli kwanza.

Ndugu yangu Ibrah unajua leo siri hii!!!!? Ndugu zetu wasomi pale mlimani [sasahivi karibu vyuo vyote] walishavumbua hii kitu siku nyingi tu!!! Ndio maan kale kamchezo kao hakaishi. Na kwa kiasi fulani inawasaidia. Wenyewe wanaita SERIKALI YA MAKELE. Raia Mwema moja sikumbuki ni toleo gani, ilishawahi kudokeza hili. YAANI KAMA HAUNESHI KWAMBA UNADAI HATA KAMA WANAJUA KWAMBA UNADAI LAZIMA UTOKE TATU BILAAA!

LAKINI, THANK GOD KWAMBA SIKU HAZIGANDI!!!!!!!???
 
Taarifa zilizofika hivi punde ni kuwa wale wazee wetu wa iliyokua Jumuiya ya Afrika Mashariki wamekuja na style mpya ya kushinikiza madai yao baada ya kuamua kufunga barabara ya Ali Hasan Mwinyi karibia na Salender ili kuonyesha ni jinsi gani wamechoshwa na usanii na uonevu huu wa serikali yetu.
Hii ni hatua mpya binafsi nimependa style yao LAKINI JE SERIKALI YETU ITAWASIKILIZA au ndo yale yale ya kuziba masikio?

Taarifa zinasema kuwa kikosi cha askari kimetumwa kikiambatana na gari la maji ya kuwasha kwenda kuwaondoa bara barani.
Habari ndio hiyo,
KWELI TUMECHOKA NA MFUMO HUU WA LICHAMA HILI LA JEMBE NA NYUNDO huku kiukweli NI UFISADI NA UBINAFSI

Rafiki yangu mmoja huwa anasema hizi alama za hiki chama ni balaa, ati tafsiri yake ni kuwa nyundo ni ya kumtwanga mhanga kichwani, na jembe la kumchimbia kaburi kumzika! Mambo kama haya yatasababisha watu waamini hivyo.
 
""WATANZANIA SI MABWEGE TENA", Dk. H. Mwakyembe (MB) Kyela

Naam, Mwakyembe aliongea point kubwa sana ambayo hadi leo hii inaelekea serikali bado haijaielewa na hivyo bado wanaendeleza usanii wao.
 
Back
Top Bottom