Sakata la Wazee EAC: Litaisha lini?

Geeque, kiwango gani cha lawama Nyerere apatiwe?

a. Jumuiya imevunjika
b. Kaanzisha mchakato wa kufuatilia mali na madeni ya EAC
c. Mchakato ukamalizika
d. Pesa zikawa tayari kabla yeye hajaondoka
e. Alipoondoka 1985 mchakato ulikwisha na fedha zilikuwa zianze kutolewa ndani ya miezi michache.
f. Wenzetu Uganda na Kenya wakaanza kuwalipa watu wao
g. Fedha zetu zikawa tayari 1987
h. Nyerere alishang'atuka na Rais alikuwa mwingine, baraza jingine na viongozi wengine waliotakiwa kutekeleza kitu kilishokwisha amuliwa.
i. Mwinyi hakutoa zile fedha ambazo Nyerere alisimamia mchakato wake toka mwanzo hadi anaondoka madarakani hakukuwa na malalamiko ya waliowahi kuwa watumishi wa EAC.
j. Ni baada ya Mwinyi kushindwa kutekeleza na kugawa fedha ilivyokuwa ndio minong'ono ilipoanza
k. akaja na Mkapa ni yale yale
l. Na sasa Kikwete ni yale yale.


Sasa Nyerere kosa lake ni kutokuwa na influence? Kama yeye mwenyewe alioneshwa kushangazwa kuwa fedha ambazo alijua tayari zipo na hazijagawiwa ilivyopaswa huoni kuwa ndio sababu ya yeye katika ile miaka ya tisini kuhoji sana mambo ya Ikulu? Aliposema kuwa "Ikulu kunanuka rushwa" yawezekana alikuwa anajua mengi kweli ambayo alijaribu kuyafuatilia (kuweka influence). Yawezekana alijaribu kufanya influence ya mambo lakini hatimaye alijua kuwa he was out of the loop?

Inawezekana alikuwa na influence lakini hakuwa Rais. Hakuwa na uwezo wa mambo mengi sana ndani ya serikali influence yake ilikuwa zaidi ndani ya chama. Na utakumbuka aliamua pia kuachia Uenyekiti wa chama kule Kizota na ninadhani ni mwaka huo huo 1987 au ilikuwa 1990 ile?

Lakini Mwinyi si bado yupo hai kwanini yeye hauulizwi kuhusu sababu zilizomfanya asiwalipe wale wazee na kama Nyerere alijaribu kumshawishi kwa namna yoyote ile.. Malecela yupo hai, na wengine waliokuwepo bado wapo kwanini hawa hatuwaulizi walihusika vipi kuhusu malipo ya wazee hawa?

Nyerere aling'atuka uenyekiti wa CCM mwaka 1987. Hata huko Kenya na Uganda wastaafu hawakuweza kulipwa mpaka baada ya mwaka 1987. Cha kujiuliza na kusikitisha ni kuwa wezi wa pesa za hawa wazee bado wapo na wanajulikana na Raisi wetu anafahamu hilo. Badala ya wanausalama kuwakamata wezi, wanawatawanya kwa virungu walioibiwa fedha zao na Kikwete anaangalia. Hili ndilo linalouma zaidi - wezi wanatanua, wazee wanarushiwa mabomu na Raisi, wabunge na mahakama wanashuhudia, kulikoni ?
 
asante,

unaweza kutupatia mwaka exact ambao waganda na wakenya walipata malipo? Pia mtulize kikongwe mwenzako, naona anaenda hovyo kama gari lilokosa rubani...



Kama Nyerere aliharibu mahala lazima watu waseme.........kwani yeye nani?
Si alikua Rais tu ..kama wengine muda wake ulipoisha akang'atuka na inawezekana blah blah zake ndio zimetufikisha hapa kama aliijua hii issue toka 87 na hakufanya kitu na yeye alipokua hai ndio kama Tanzania alafu leo mje mseme hakua na influence baada ya kuachia ngazi....?
Hamuwezi kua serious!
Hizi ni baadhi ya mambo mengi ambayo alibolongo na akawaachia mizigo walio mfatia,na kwasababu ndio system toka kwa mwenyewe then tusijiulize tumefikaje hapa!
 
Inaonekana hata Kenya nako kulikuwa na tatizo kama hili tunaloliongelea .....see below, inawezekana kama anavyosema Nyani ..."Ndivyo Tulivyo", lakini mimi siamini hivyo.

More Queries on Sh70b Dues for EAC Retirees
The East African Standard (Nairobi)
March 12, 2007
News Article By Omwa Ombara
More than 50,000 Kenyan retirees and former employees of East Africa Community want the Government to pay them Sh70 billion in benefits.
The amount demanded by those who worked with the community between 1967 and 1977, includes interest for the last 23 years.
The workers also demand that the Government provides evidence that it has paid them as alleged by some officers from the Ministry of Finance.
Documents in our possession indicate that Crown Agency, on behalf of the UK Government, paid cheques worth Sh2.5 billion ($20,592,450 dollars) to former presidents Milton Obote (Uganda), Julius Nyerere (Tanzania) and Daniel arap Moi.
Kenya was to get 42 per cent of the amount, Tanzania 32 and Uganda 26.

Cheque lying at Central Bank of Kenya
The retirees claim that their East Africa Community "Workers of Kenya Cheque" paid by the UK Government, has been lying at the Central Bank of Kenya in the custody of Central Bank of Kenya Governor since 1984 awaiting payments and instructions from the Finance Minister or most probably a Presidential Decree.
They say payment of retirees who worked from 1978 should not be confused with their mediation payment.
The payment they are demanding is in conformity with Article 17 of the EAC mediation agreement of 1984 duly signed by the three East African Heads of States -Daniel Moi, the late Milton Obote and the late Julius Nyerere. Kibaki was then a Finance Minister.

Uganda and Tanzania have paid
They further claim that their colleagues in Uganda and Tanzania were paid through a presidential decree ordered and signed by Uganda's President Yoweri Museveni and Tanzania's Jakaya Kikwete in 2005 and 2006.
The payment and list of beneficiaries for their Tanzanian colleagues were published in Tanzania's newspapers - Tanzania Daima of Sunday October 23, 2005 and Nipashe of Sunday, December 3, 2006.
The notices are signed by the Permanent Secretary, Ministry of Finance, Tanzania, Gray S Mgoja and has a Government seal and letterhead.
Speaking in Mombasa on Sunday, more than 3,000 Kenyans representing 50,000 ex-workers countrywide narrated to The Standard their sufferings for the last 20 years.

Ignorant on rights
They said they believed that since most of them were not well educated and were poorly versed on their legal rights, the Government had taken advantage of their ignorance to deny them their dues.
The defunct EAC state corporations include EA Post and Telecommunication, EA Railways, EA Cargo Handling Services, EA harbours, EA Extelecommunications and EA Custom and Excise.
Among former employees affected are some current ministers in the Government like Heritage minister, Mr Suleiman Shakombo and Changamwe MP, Mr Seif Kajembe. Shakombo worked with Customs while Kajembe was with Cargo.
Secretary General of Ex East Africa Community Association, Mr Omar Kombo said their efforts to reach President Kibaki during his recent visits to Mombasa to table the documents, had been frustrated by the local Provincial administration.
He said the office of the AG had also frustrated their effort to register their organisation and pursue their payments as a team, since October 31, last year.
Kombo informed The Standard of the organisation's frequent trips to Nairobi.
"We were told to pick our certificates after two weeks in October. On November 16, we sent a reminder but were told to go back in January. On February 21, we went to Sheria House and followed the file for four days. We went to the deputy registrar who told us that organisation looked like a Trade Union.
The deputy registrar told us to hold on as they awaited information from National Security Intelligence services," says Khadija Mohamed, committee member and EEACWA co-ordinator.
Impeccable sources told The Standard that, Finance minister, Mr Amos Kimunya, had sent the deputy director for pensions to Arusha late last year for one month.
Sources said he was studying how others were paid and questioned those who had been paid.
The matter then died, until February 25, when EEACWA officials appeared in Mandhari ya Wiki on KTN to publicise their plight.
None of the officials from the ministry of Finance invited for the show, showed up.

source : More Queries on Sh70b Dues for EAC Retirees ~ Kenya's Ultimate Real Estate Guide, Comprehensive listings, prime properties for sale and to let, in-depth realtor information, extensive real estate directory
 
Sasa hapa tukubali kitu kimoja: Tusizungumze kana kwamba hakuna mfanyakazi hata mmoja wailiyokuwa jumuiya ya Afrika ya Mashariki ambaye amelipwa mafao yake. Ushahidi wote uonesha kuwa malipo yameshafanyika kwa kiasi kikubwa.

Nadhani suala kubwa ambalo bila ya shaka vyombo vya habari haviripoti kwa usahihi ni kuwa hawa wengine wanaodai ni kina nani, na kwanini hawakujumuishwa katika malipo mengine na ni kwa jinsi gani serikali inaweza kuwahakiki (najua imeshafanya tena) ili kuhakikisha kuwa wanapatiwa kiinua mgongo cha aina yeyote ile.

. Je wote hawa walikuwa waajiriwa rasmi wa idara au shirika lolote la EAC?
. Je wote walipoteza kazi zao baada ya jumuiya kuvunjika?
. Je wana ushahidi wowote wa kuonesha kuwa wamewahi kufanya kazi kwenye EAC kwa muda wowote ule.

Kwa sababu jambo jingine ni hatutaki wajanja wachache ambao maisha yamekuwa magumu wanaamua kujiingiza kwenye kundi la watumishi wa EAC ili na wao wapate chochote mbele ya safari? Je kuna jinsi yoyote ya serikali kuweza kupitia kesi ya kila mmoja wao?

Ningekuwa mimi ningefanya hivi:

a. Ningewaandikisha wale wote wanaodai mafao yao.
b. Ningehakikisha natengeneza jalada lao (ndani kukiwa na picha, taarifa za maisha yao n.k) Hapa ni lazima kuoanisha vitu kama umri n.k ili kuhakikisha "wazee vijana" wasijichomeke kiujanja.
c. Ningekusanya ushahidi wa utumishi wao na kuupanga kwa kufuata uzito wake (kama mtu ana mkataba wa ajira, kama mtu ana kitambulisho cha kazi, kama mtu ana hati ya malipo n.k wakati wa utumishi wake)
d. Ningewagawa kwa makundi makubwa matatu:

a. Kundi la kwanza la wenye ushahidi wa ajira ya muda mrefu/kibarua cha muda mrefu. Ushahidi huu lazima uwe wa maandishi na siyo maneno.

b. Kundi la pili la wenye ushahidi wa wa muda mrefu wa kitambulisho na taarifa nyingine ambazo zinaoona na rekodi sahihi. Kwa mfano, mtu akisema nilikuwa nafanya kazi chini ya idara ya Posta, bosi wangu alikuwa x, meneja alikuwa a wakati naanza kazi mwaka 1987 nilikuwa mji huu na pale bosi alikuwa m. Rekodi hizo zinapolinganishwa na taarisa rasmi zinazoona na ushahidi mwingine wa nje unaokubaliana na madai yake. (huyu anakuwa na hadhi kama ya kundi la a)

c. Kundi la tatu lenye kutoa madai ya kuwahi kuwa wajane wa watumishi wa iliyokuwa EAC na wenyewe walete taarifa za ushahidi wa waliokuwa watumishi na kupima ushahidi huo na ukiwa na nguvu wanawekwa kwenye kundi la a au b.

d. Kundi la nne la wale ambao wanadai kuwa waliwahi kuwa watumishi lakini hawana nyaraka yoyote au kumbukumbu yoyote yenye kukubaliana na rekodi yoyote rasmi. (hawa watashughulikiwa tofauti).

Nikishayapata makundi hayo na kujiridhisha kuwa ndio wote (baada ya kutoa muda maalum wa kumaliza mchakato huo) basi tunaangalia ni kiasi gani kinadaiwa na lile kundi la kwanza na la pili.

kundi la kwanza na la pili lazima walipwe mafao yao kwa kiwango na kanuni zilizotumika kuwalipa wale watumishi wengine. Kundi la tatu nalo litalipwa kwa misingi ile ile iliyowalipa waliokuwa wajane wa watumishi.

Kundi la nne kufuatana na wingi wake, tutalipatia jina la "Kundi la Waunga Mkono". Hawa ingawa wamejaribu kutapeli lakini kutokana na umri wao tutaamua kuwapa tufweza kidogo twa miradi baada ya kuoneakana wamewaunga mkono wazee wenzao lakini fedha hiyo itatolewa kwa masharti fulani fulani ikiwemo kufanya kazi ya jamii (community service) kulipia jaribio lao la kutapeli serikali (this is just an idea).

Tukimaliza yote tutakuwa tumelimaliza suala hili ndani ya miezi michache tu.
 
...kama umechoka kusikia si uzibe masikio? kwani kuna mtu kakulazimisha uingie huku? halafu mambo ya kuongea vitu usivyojua utaumbuka, hivi unajua DSM-IV TR criterias zinazotumika ili ku-Rx zoloft?? au ndio mambo ya TV tu!!? hovyo sana wewe manyani nyani....you're todayz worst in the world.

Wewe ndio unatakiwa kufunga mdomo wako na kuacha kung'ang'ania kumlaumu Nyerere. Dizaini hata ukiibiwa demu wako utamlaumu Nyerere.

Here is a newsflash for ya....Nyerere died nine years ago and he will never come back. So get over your fixation of him and move on.

Kuendelea kumlaumu Nyerere kwa kila kitu hakutarudisha ng'ombe aliopoteza babu yako (kama unavyodai) na wala hakutatui tatizo lolote. Nakusihi ulenge nguvu na juhudi zako katika kufikiri namna ya kutatua matatizo yaliyopo sasa kuliko kulenga, kulalamika, na kunung'unikia mambo yaliyokosewa miaka 30 iliyopita.....
 
Unashindwa kuelewa kuwa check zilizoandikwa kwanza na Umbricht zilikuwa ni za hawa wazee? Na hii ni baada ya Umbicht kuhakiki mali na madeni ya EAC. Kenya na Uganda ziliwalipa watu wao bila matatizo. Ni serikari ya Mzee Ruksa na zilizofuata zinaendeleza mzozo huu.
 
Geeque, kiwango gani cha lawama Nyerere apatiwe?

a. Jumuiya imevunjika
b. Kaanzisha mchakato wa kufuatilia mali na madeni ya EAC
c. Mchakato ukamalizika
d. Pesa zikawa tayari kabla yeye hajaondoka
e. Alipoondoka 1985 mchakato ulikwisha na fedha zilikuwa zianze kutolewa ndani ya miezi michache.
f. Wenzetu Uganda na Kenya wakaanza kuwalipa watu wao
g. Fedha zetu zikawa tayari 1987
h. Nyerere alishang'atuka na Rais alikuwa mwingine, baraza jingine na viongozi wengine waliotakiwa kutekeleza kitu kilishokwisha amuliwa.
i. Mwinyi hakutoa zile fedha ambazo Nyerere alisimamia mchakato wake toka mwanzo hadi anaondoka madarakani hakukuwa na malalamiko ya waliowahi kuwa watumishi wa EAC.
j. Ni baada ya Mwinyi kushindwa kutekeleza na kugawa fedha ilivyokuwa ndio minong'ono ilipoanza
k. akaja na Mkapa ni yale yale
l. Na sasa Kikwete ni yale yale.


Sasa Nyerere kosa lake ni kutokuwa na influence? Kama yeye mwenyewe alioneshwa kushangazwa kuwa fedha ambazo alijua tayari zipo na hazijagawiwa ilivyopaswa huoni kuwa ndio sababu ya yeye katika ile miaka ya tisini kuhoji sana mambo ya Ikulu? Aliposema kuwa "Ikulu kunanuka rushwa" yawezekana alikuwa anajua mengi kweli ambayo alijaribu kuyafuatilia (kuweka influence). Yawezekana alijaribu kufanya influence ya mambo lakini hatimaye alijua kuwa he was out of the loop?

Inawezekana alikuwa na influence lakini hakuwa Rais. Hakuwa na uwezo wa mambo mengi sana ndani ya serikali influence yake ilikuwa zaidi ndani ya chama. Na utakumbuka aliamua pia kuachia Uenyekiti wa chama kule Kizota na ninadhani ni mwaka huo huo 1987 au ilikuwa 1990 ile?

Lakini Mwinyi si bado yupo hai kwanini yeye hauulizwi kuhusu sababu zilizomfanya asiwalipe wale wazee na kama Nyerere alijaribu kumshawishi kwa namna yoyote ile.. Malecela yupo hai, na wengine waliokuwepo bado wapo kwanini hawa hatuwaulizi walihusika vipi kuhusu malipo ya wazee hawa?

Mwanakijiji,
Ahsante sana kwa maelezo yako mazuri, nadhani kama ulinipata vizuri mimi nalaumu marais wote waliotawala Tanzania kuanzia Mwalimu Nyerere, Mwinyi, Mkapa na sasa Kikwete. Na zaidi nailaumu CCM ambayo kwa miaka hiyo yote iko kwenye madaraka ya kuongoza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ukichukulia hawa wazee wengi wao ni makada au wapenzi wakubwa wa hiki chama. Nadhani hiki chama kimeshindwa kabisa kutetea maslahi ya wananchama wake na wananchi kwa ujumla.

Issue yangu kuhusiana na Nyerere ilitokana na baadhi ya watu kudai kuwa yeye ahusiki kabisa na wala asilaumiwe katika hili jambo.

Nadhani Mwinyi ni mshiriki mkubwa katika kuwanyima haki hawa wazee kama ilivyo kwa Mkapa na sasa Kikwete.

Ninachokisema tuwe fair kwa sababu kumekuwa na tabia ya watu kutetea kila kibaya cha Mwalimu na wakati mwingine kufikia hata kuwazima watoa hoja wote wanaojaribu kuonyesha mabaya ya uongozi wa mwalimu Nyerere. Kama vile tunavyopenda kunukuu mazuri mengi ya Mwalimu Nyerere basi pia tuwe tayari kukubali na kuyaepuka mabaya yake machache.
 
Wewe ndio unatakiwa kufunga mdomo wako na kuacha kung'ang'ania kumlaumu Nyerere. Dizaini hata ukiibiwa demu wako utamlaumu Nyerere.

Here is a newsflash for ya....Nyerere died nine years ago and he will never come back. So get over your fixation of him and move on.

Kuendelea kumlaumu Nyerere kwa kila kitu hakutarudisha ng'ombe aliopoteza babu yako (kama unavyodai) na wala hakutatui tatizo lolote. Nakusihi ulenge nguvu na juhudi zako katika kufikiri namna ya kutatua matatizo yaliyopo sasa kuliko kulenga, kulalamika, na kunung'unikia mambo yaliyokosewa miaka 30 iliyopita.....

Kwamba mambo yaliyokosewa miaka 30 iliyopita ni mwiko kuyaongelea, kuyalalamikia,na kuyanung'unikia???? Tutawezaje kuongea mfumo wa uongozi uliopo sasa bila kugeuka na kuangalia mfumo wa jana????Tutawezaje kuongelea maendeleo bila kujua jana ulikuwaje?? Tutawezaje kuongelea madai ya wazee wetu ya miaka hiyo 30 iliyopita bila kuongelea hiyo miaka 30 iliyopita????
Kaaazi kwelikweli
 
Eti Nyerere hakuwa na influence mwaka 1987 ur kidding me? Hiki sio kile kibabu kilichozunguka nchi nzima mwaka 1995 kumnadi Mkapa?

Nani asiejua BWM ni zao la Kifimbo?

Mpakeni rangi apendeze lakini kama ni kesi mchonga ni mshtakiwa namba moja!

Kalabagho!
 
nadhani wote tunakubaliana jambo moja la msingi..UMUHIMU WA KUWALIPA WAZEE WETU ....KUENDELEA kungangania walikuwa vibarua haitasaidia sana ..kwani wameikamata pabaya serikali yetu....madhara tutakayopata ni makubwa kwani bado bajeti yetu ni tegemezi...nchi za jumuia ya ulaya ,uingereza ikiwemo ni wafadhili wakuu wa bajeti yetu...leo hi kwa kitendo cha hawa wazee wanaweza kuamua ku hold michamgo yao kwenye bajeti ya maendeleo ..we l feel the pinch all of us...mabalozi wao walikuwa sehemu ya umati uliokwama kutokana na demo ya hawa wazee leo hii.....

kwa kuwa basi lengo letu ni moja...si vema watu wazima hapa kuanza kuambiana lugha za "huwa sisahau ..and you will pay...bla bla bla.."...achana na hizo HALLUCCINATIONS bro.......tukate ishu ..kwa maendeleo ya TAIFA...you dont know what i am able to ..either..so ukichukia unakunywa kahawa au whisky fundo moja unashusha hasira..tunaendelea....,otherwise wahenga wanasema .."ukirusha jiwe gizani atakayelia mh!...limempata!!"
 
Eti Nyerere hakuwa na influence mwaka 1987 ur kidding me? Hiki sio kile kibabu kilichozunguka nchi nzima mwaka 1995 kumnadi Mkapa?

Nani asiejua BWM ni zao la Kifimbo?

Mpakeni rangi apendeze lakini kama ni kesi mchonga ni mshtakiwa namba moja!

Kalabagho!



acheni kumuonea mkapa sometimes inabidi kusoma records utaona kwa hili la wastaafu wa east africa mkapa ndio mwanzo kabisa aliyeamua kuanza kuwalipa kabla hajaondoka ......hili kundi lilkikuwa kubwa sana na wengi alifanikiwa kuwalipa[waliokuwa na records zao zipo sawa..]...angalia magazeti ya mwishoni mwa 2004/2005......wakati huo hazina bado wapo mama blandina nyoni ,mgonja na msaidizi wake akiwa peniel....

what happened ni kuwa baada ya lile kundi la kwanza kubwa kulipwa na hadi 2006 alipoingia kikwete walimaliziwa kullipa wachache waliokuwa na document waliosalia........HAWA WANAODAI SASA NI WALI AMBAO NYARAKA ZAO HAZIKUWA SAWA ....HASA KAMA MAFAO YAO YALIKUWA HAYAPELEKWI ..KUTOKANA NA SERIKALI KUSEMA KUWA WALIKUWA VIBARUA........NDIO MAANA SERIKALI NA WATAALAMU WAKE WA HAZINA INASEMA KUWA KIMAHESABU...WASTAAFU AMBAO WAPO KWENYE KUNDI LA 2004/5 NA HAWAJALIPWA NI 22......INA MAANA HAWA HAIWATAMBUI.......

SO KIMSINGI SERIKALI .....IKISHAWALIPA HAWA 22..HAWA WANAODAIWA KUWA VIBARUA WANAJUWA WATAKUWA HAWANA CHAO..THATS WHY WANAONGEZA UKALI.....HAPA BUSARA ITABIDI ITUMIKE.....KWA KU EXTEND MAJINA YA VIBARUA WOTE WALIOTUMIKA HIYO EAST AFRICA...SERIKALI WA COMPROMISE TU ...WAKIWEZA HATA KUWALIPA KILA MMOJA MILIONI 5 HADI 10....HAIFIKI BILIONI 3....ILI WAMALIZE HII KADHIA..NA AIBU....

TUNAJUWA KUWA PESA WAANAYODAI HAIFIKI HATA MAKUSANYO YA SIKU NZIMA PALE LONG ROOM - TRA..LETS PAY THEM!!!
 
Mwanakijiji,

Kinachogomba hasa ni makubaliano yaliyokuwa kwenye mkataba kuwa wastaafu, walipwe kulingana na thamani halisi ya dola na riba ya 7% kwa mwaka. Wakati jumuiya inavunjika dola moja ya kimarekani ilikuwa shilingi nane ya Tanzania. Sasa tuchukue mfano wa aliyetakiwa kulipwa mathalani Tshs.500,000.00 (laki tano) sawa sawa na US$ 60,000.00 mwaka 1977. Serikali ilichotakiwa kufanya ni kumlipa huyu mdai fedha zake mara moja na hakungekuwapo na ugomvi. Lakini serikali kwa sababu zisizoeleweka ikatumia hizo fedha na sasa miaka 30 baadaye inataka kulipa hizo hizo laki tano ambazo kwa sasa ni sawa sawa na US$ 420.00 tena bila riba. Kwa hesabu za haraka ni kuwa serikali ilikopa US$ 60,000.00 mwaka 1977 na sasa mwaka 2007 serikali inalipa US$ 420.00 !!!! na kusema haidaiwi tena. Hapa ina maana mstaafu anaibiwa mchana mchana na bila aibu fedha zake kiasi cha US$ 59,580.00..

Lakini kibaya zaidi ilikuwa ni kwa wafanyakazi serikalini kushindwa kutofautisha hizi fedha na za wastaafu wa kawaida wa serikali. Wivu na chuki zilitawala sana na kuna waliosikika wakisema ahh, kwa nini walipwe fedha zote hizo wakisahau zilitoka wapi. Baada ya kuvunjika kwa EAC kuna secretariat ilibaki Arusha kutayarisha mahesabu ya malipo na kutoa mchanganuo wake. Majina yote yaliorodhesha na mchanganuo wa malipo kufanywa na hatimaye kukabidhiwa serikalini. Wizara ya fedha bila shaka kwa lengo la kutaka kuiba eti na lenyewe badala ya kuandika cheki kwa wahusika, wakaanza mchanganuo wa kwao. Wizi una mkono mrefu.
 
..sawa kaka na asante sana kwa juhudi zako! umetulia kuliko MKJJ anayetaka confrotations za kukandiana na kuingiza babu za watu ktk mjadala ambao hawahusiki! asante sana.....

tatizo langu lipo palepale kwamba, "waajiliwa wa EAC walipaswa kulipwa kwanza incase jumuia inavunjika." Hayo ni maneno yako msee, sasa kama ndivyo hivyo kwanini hilo lisiwe la kwanza na badala yake limekuwa la mwisho? Kama Nyerere alikuwa muadilifu, mpenda maslahi ya watu wake na kumweka nje ya hii mess (kilawama) ilitakiwa asimamie utekelezaji wa waajiliwa kulipwa kwanza kabla ya hayo mengine.

tatizo la TZ, viongozi wanapokezana vijiti, wananchi wengi ni myopic na wavivu wa kufikiria...watu wanataka short term fixes bila kuangalia mzizi wa tatizo kiasi kwamba liking'olewa ndio iwe mwanzo na mwisho! na hiyo ndio tofauti kati yangu/yetu na nyie mliobaki.

Naona hukunielewa labda ni mimi sikueleza vizuri. Shughuli za Idara na mashirika ya iliyokuwa EAC ilkuwa ni lazima ziendelee baada ya kufa kwake na hazingeweza kusimama. Hivyo mkataba wowote ambao serikali ingeingia na wastaafu wa EAC ili huduma ziendelee kuwapo hazikutakiwa kuhusishwa na ajira zao za zamani na malipo yao yangebaki palepale. Hata hivyo malipo hayangeweza kufanyika kabla ya mgawanyo wa mali kwa sababu ulihusisha kuorodhesha assets na liabilities zote. Malipo niliyoongelea ni baada ya kupokea cheki kutoka crown agents kwa serikali ya Tanzania kupitia Benki Kuu. Kumbuka hela hazikuwa za serikali wala hazikuwa zinatoka kwenye mfuko wa serikali.
 
Maswali ya kujiuliza ni kama haya ;

1. Baada ya cheki kutolewa na Crown Agents hizo fedha ziliingizwa kwenye account gani Benki Kuu ?

2. Wakati serikali inakabidhiwa fedha hizo iwafikishie walengwa, je juhudi gani zilifanyika kutekeleza hilo kuanzia mwaka 1985 mpaka 1990 wadai walipoanza kupiga kelele ?

3. Nani aliagiza hizo fedha zianze kutumika kinyume na malengo yaliyokusudiwa na kwa sababu gani hasa ?

4. Je kulikuwa na nia yoyote ya kuwalipa wahusika baadaye au huu ulikuwa ni mpango wa kuwaibia na kusubiri wafe moja baada ya mwingine ?

5. Usumbufu mkubwa walioupata hawa wazee - kufikia wengine kufa kwa kukosa fedha za matibabu, wengine kushindwa kuwapeleka watoto wao shuleni kwa kukosa ada, wengine kulemaa kwa kupigwa virungu na polisi wakidai haki zao na wengine wengi kufa njaa kwa kukosa chakula - nani atawafidia ?

Bahati nzuri wahusika wote katika sakata hili lililohusisha taasisi tatu nyeti - ikulu, wizara ya fedha na benki kuu - wote wapo na ingekuwa vizuri wakajitokeza kujibu haya maswali. Mwingine ambaye lazima aunganishwe ni ofisi ya Mwanasheria Mkuu ambayo bila shaka lolote ndiyo mshauri na mtetezi wa serikali. Waliokuwa wakishikilia ofisi zote hizo bado wako hai na kukaa kwao kimya wakati wazee wanarushiwa mabomu ya machozi kunaonyesha jeuri na dharau walilo nalo kwa wananchi. Kwa upande mwingine mpira pia uko uwanjani kwa wabunge ambao wameamua kuziba masikio na macho lakini hawasiti kushupalia maslahi yao kama ya posho na pensheni. Ikiwezekana tume liundwe ndani ya bunge kufuatilia hizo fedha zilivyoyeyuka Benki Kuu.
 
Wengi wa mliowaona barabarani jana SIO wafanyakazi wa iliokuwa EAC. Kuna UTAPELI mwingi pia umeingizwa kwenye madai haya. Katika MKANGANYIKO kama huu, Serikali ingefikia makubaliano ya jumla nini kilipwe kwa Wazee wetu hawa kama ilivyofanya kwa waliobomolewa nyumba zao pale TABATA DAMPO.
Najua Wazee wetu hawa hawataridhika lakini nadhani tunahitaji kusonga mbele kama TAIFA.
 
Back
Top Bottom