Sakata la ununuzi wa S-400: Marekani yaiwekea vikwazo Uturuki

Sawa mbona ata ujerumani ni member wa NATO, lakini ananunua mafuta na Gesi Urusi? wa muache Uturuki anunue atakacho, Uturuki wamejiridhisha S-400 ni bora katika kujilinda, asie Mturuki anabisha.
Ujerumani pia kaeKewa vikwazo na USA. Fuatilia ishu ya NORD STREAM 2.
 
Hivi uturuki unaisikia ama unahadithiwa?,,uturuki ishawahi kuinyuka karibu ulaya nzima na ilizipiga Russia na kuteka maeneo kibao,kama crimea,bosnia,turkeministan etc,uturuki ni nchi yenye jeshi la kueleweka,usiichukulie poa
Ottoman empire imepigwa Sana na russia empire. Karibia kila vita Russia alikua anamchapa ottoman empire.
 
Kwa nje, ni vikwazo sababu ya S-400, ila kwa ndani vita baridi kati ya USA against Turkey.
Hii ishu imeanzia kwenye failed coupe d'etat, ikaja ishu ya wakurd na pia kucounter influence ya turkey middle east ambayo inatishia interest za marekani

Hii issue ya mapinduzi ya 2016 imesheheni conspiracy theories kedekede huku kila upande ukitoa madai tofauti-tofauti!

Hoja kuwa Marekani imehusika katika jaribio la mapinduzi nchini Uturuki ni hoja isiyo na uthibitisho unaojitosheleza hivyo sioni kama ni sababu ya hii issue ya sasa.

Hoja nyingine kuwa Marekani ilikataa kuipatia Uturuki mfumo wa kujihami kwa sababu iwe rahisi kwa Marekani kuishambulia Uturuki siku watakapokosana, pia si hoja yenye mashiko.

Kuna jambo lisilofahamika na wengi:
Hii mifumo ya ulinzi iko katika udhibiti wa kimfumo unaojitosheleza wa NATO sambamba na Marekani ambaye ndiye mzalishaji mkuu wa mifumo iliyopo na itumikayo na Jumuiya. Hivyo, kama ni suala la Uturuki kushambuliwa na Marekani, mifumo ya Patriot kwa Uturuki si suluhisho la mashambulizi.

Mifumo ya ulinzi wa anga ya NATO iko katika ushirika wa kimfumo na mifumo mingineyo ya kivita ndani ya Jumuiya hiyo.

Mfano mmojawapo ni ndege za F-35 ambazo zimeundwa kupitia mpango maalumu wa pamoja ujulikanao kama, Joint Strike Fighter (JSF). Mifumo ya ulinzi wa anga ya NATO imewezeshwa ama imedhibitiwa kutambua mifumo mingineyo rafiki zikiwemo ndege hizo, hivyo kutozishambulia. Hili linafanyika hasa kupitia mifumo ijulikanayo kama, Identification Friend or Foe.

Ukiachana na hilo, kuna mengineyo na ya ndani zaidi ambayo hata kampuni nyinginezo huwa zinayafanya pale zinapohitaji kuweka udhibiti zaidi wa bidhaa hususani masuala ya kiusalama endapo bidhaa husika itatumika vibaya ama kuangukia katika mahali pasipo salama ama kwa mtu asiyefaa. Kuna mechanisms mbalimbali za kiusalama ikiwemo moja maarufu sana, kwa kiingereza tunaiita, Kill Switch!

Complexity iliyopo katika mifumo hii ya kujihami haitoi fursa kwa mtumiaji wa mwisho kuwa na udhibiti wa asilimia 100 sawa na yule aliye-design ama aliyeiunda kiwandani. Hata linapokuja suala la kuanza kuitumia, 'semina elekezi' lazima ihusike kwa muda wa kutosha ndiposa mnunuzi ama mtumiaji aweze kuitumia mifumo ipasavyo.

Hivyo, hoja ya Uturuki kutopewa mfumo wa ulinzi ili ashambuliwe automatically inakosa mashiko sababu hata ikipewa ama kuuziwa mfumo huo ambao uko integrated na mifumo mingine ya NATO, hautoweza kuwa na ufanisi dhidi ya mifumo ya udhibiti ya NATO na Marekani.
 
Suala la marekani kushiriki kutaka kumpindua endorgan mbona liko wazi sana,wala sio consipracy theory,,kwa tuliiojuwa tunafuatilia tukio live wala haihitaji kujiuliza mara mbili,au hujui hadi jeshi la uturuki liliizunguka kambi ya askari wa marekani na wakazuiwa kutoka au kuingia kwa wiki nzima na walikatiwa hadi huduma za maji,,fuatilia nyuzi za wiki ile..
Kuhusu mifumo ya kuulinzi ya anga ya NATO kuwa ya pamoja,,mbona ujerumani,UK,ufaransa,ugiriki etc wana mifumo yao individually?
 
Hayo ni madai (allegations). Hayana uthibitisho unaojitosheleza.

Wapo pia wasemao kuwa mapinduzi yalikuwa staged aidha na Erdogan mwenyewe ama watu wake kwa sababu zao kadha wa kadha.

Zote hizo ni conspiracy theories. Hazina uthibitisho na yanabaki kuwa madai tu.

Ujerumani, UK, Ufaransa, Ugiriki n.k. ziko katika mtandao wa NATO unaofahamika kama NATINADS. Mifumo mbalimbali ya ulinzi inayotumika katika nchi hizo iko integrated na NATO (NATO Integrated Air Defense System), mtandao ambao upo tangu miaka ya 60.
 
Unajua kwamba ujerumani ilikuwa na air defence yake uturuki?,ntakupa evidence kuonyesha hizi nchi zina individuals air defence pia na hazitegemei sana defence shield ya NATO ambayo kiuhalisia ipo katika ardhi ya uturuki,,sasa jiulize kwanini licha ya defence shield kuwa uturuki,kwanini waturuki bado walihisi wanajitaji air defence yao,tena ya mrusi?.
Kwanini marekani alikuwa anajivuta vuta kumuuzia uturuki air defence ya patriot-3 richa ya uturuki kutaka kulipia?.
Kwanini siku moja baada ya tukio la kutaka kupinduliwa Endorgan,majeshi ya uturuki yaliizingira kambi ya marekani na kuwaweka askari wa marekani hostage kwa wiki nzima?.
 
Turkey: U.S. Airmen & Their Families Locked Down at Air Base

Some 1,500 US airmen and their families have been locked in the southern Turkish air base of Incirlik together with a stock of tactical nuclear bombs since President Reccep Erdogan crushed an attempted coup on Saturday, July 16. In the four days up until Wednesday, July 20, therefore, no air strikes against ISIS in Syria and Iraq have been staged from that Turkish base.

This extraordinary situation, reported here by Debkafile s military sources, whereby a large group of American military personnel are held virtual captive by an allied government, was almost certainly raised in the phone call that took place Tuesday between President Barack Obama and Erdogan. But the most outlandish aspect of this affair is that no American official has raised it in public - nor even by the administrations most vocal critics at the Republican convention which nominated Donald Trump as presidential candidate.

The situation only rated a brief mention in some Russian publications under the heading: Turkish investigators enter & search Incirlik air base where US nukes are housed.

Our military sources report that deep bunkers located near the base s running strips house B61 tactical nuclear gravity bombs.

In the course of the massive sweep-cum-purge Erdogan is conducting in every corner of the country, hundreds of police officers accompanied by Ministry of Justice and Attorney General Office investigators are the only people permitted to enter the strategic air base, and only emergency cases may leave, after coordinating with the Turkish authorities.

The base is under virtual siege by large police contingents, cut off from electric power for several days except for local generators which will soon run out of fuel. This pressure appears to be Erdogan
 
Defense shield ya NATO ndiyo hiyo NATINADS niliyoitaja hapo awali.

Nchi wanachama zinaweza kuwa na local defense systems lakini zikawa integrated na mifumo ya NATO.

Isitoshe, hiyo mifumo maalumu "individual" hata uzalishwaji wake ni kupitia joint programs na kampuni za Kimarekani na ushirika wa nchi nyingine ndani ya NATO. Ukifanya research ndogo, Ujerumani, Italy, Uingereza, Spain, Marekani n.k. hufanya miradi mbalimbali ya pamoja ya utengenezaji silaha na mifumo ya kijeshi kama Jumuiya.

Chukulia mfano mradi wa MEADS ambao ume-replace Patriot nchini Ujerumani, ni mradi ulio chini ya NATO unaoijumuisha Marekani na nchi washirika.

Tukirudi katika sakata la Uturuki:
Ni kweli kuwa Uturuki inahitaji air defense system. Waturuki hawakuanzia kwenye S-400 bali walikwisha fanya mazungumzo hadi na mataifa mengine kama China kuhusu alternative.

Pia, hii si biashara tu ya kawaida bali ni mpango maalumu wa Uturuki kujiimarisha kiuchumi hasa kiviwanda. Hili tumekwisha lizungumzia humu mahali fulani.

Waturuki si kwamba wanataka kulipia tu bali wanataka na kitu kingine kihusike katika mkataba wa mauziano, nacho ni technology transfer.

Hawataki mfumo tu bali pia na teknolojia ya uzalishaji wa mfumo mzima ili iwawezeshe kujitegemea kwa kuzalisha mifumo yao wenyewe yenye kushabihiana na ya Kimarekani, kitu ambacho kampuni za Kimarekani hazikuwa tayari ku-offer teknolojia zao kwa upcoming competitor kwenye soko. Ndio maana ya huko kusua sua.

Hili ni tofauti kwa upande wa Urusi maana kampuni kuu za uzalishaji wa silaha zinamilikiwa na serikali (state owned). Hili lilirahisisha dili la S-400 kukamilika na kuendana na matakwa ya Uturuki ya kupewa teknolojia ya uzalishaji wa S-400, pia kizazi kijacho cha S-500.

Unasema, askari wa Marekani waliwekwa hostage? Hostage kwa kosa gani na makubaliano yapi?
 
Ujerumani pia kaeKewa vikwazo na USA. Fuatilia ishu ya NORD STREAM 2.

Bado kilometer 160 bomba likamilike
Hivyo vikwazo kwa nord stream 2 havita saidia na germany watakua wajinga sana kuacha ile project na kamwe hawata fanya hivyo
 
Ha..!!,kuwekwa hostage hakunaga makubaliano,,waliwekwa lock down na wakakatiwa umeme,,hujasoma hiyo article hapo juu?..
Vilevile ujerumani walinunua patriot air defence kutoka marekani na wala haikuwa joint production,,
Issue ya Jointstrike program,yaani F-35 ,ilikuwa ni program ya nchi za ulaya kutengeza jetfighter kwa pamoja,marekani hakuhusika mwanzo,,Turkey alihusika,baadae ufaransa wakajitoa,,mradi ukakumbwa na uhaba wa pesa ndo marekani nae akaingia na kuhodhi program lakini mwanzo marekani haikuhusika,,ndo maana hata hiyo fighter sikuhizi haiitwi jointstriker
 
Hostage situation na Lockdown ni vitu viwili tofauti kabisa!

Umedai, askari wa Marekani waliwekwa hostage? Hostage situation ni utekaji unaohusisha madai ambayo yatahitaji kutekelezwa ili aliyetekwa aachiliwe. Ndio makubaliano hayo ambayo lazima yafikiwe!

Taarifa inahusu kuwekwa lockdown kwa airbase. Hii base ina majeshi ya nchi mbalimbali zikiwemo Saudi Arabia, Ujerumani n.k. na si majeshi ya Marekani pekee. Kuwekwa lockdown kwa hii base kuna uhusiano gani na kile kinachotajwa kama kuhusika kwa Marekani katika mapinduzi?

Issue ya Ujerumani kununua Patriot SAM system si hoja yangu. Hoja yangu ni kuwepo kwa joint programs za uzalishaji silaha zinazofanywa na nchi wanachama wa Jumuiya ya NATO. Nimekupa mfano wa MEADS program ambayo imehusisha mataifa mbalimbali. MEADS ni mfumo wa ulinzi wa anga unaotumiwa na Ujerumani, mfumo ambao ni NATO-managed.

Hilo la Joint Strike Fighter kuwa program ya nchi za Ulaya ni jipya!

Ulaya haikuwahi na wala haijawahi kuwa na Joint Strike Fighter program inayoitwa F-35. Joint Strike Fighter (JSF) ni initiative ya Wizara ya Ulinzi ya Marekani miaka ya 90 kwa ajili ya uundwaji wa ndege ya mashambulizi ya kizazi cha tano itakayotumiwa na Marekani pamoja na nchi washirika (NATO). Get your facts straight maana JSF haikuwahi kuwa program ya nchi za Ulaya!
 
Ujerumani pia kaeKewa vikwazo na USA. Fuatilia ishu ya NORD STREAM 2.
Vikwazo vimeekwa ila ile project ilishakamilika kwa 90% us anapiga kelele tu hana lakuwafanya vikwazo vishazoeleka mpaka kenya na uganda wanaekewa ila havina maana yyte zaidi yakuumiza raia sio mifumo husika(serikali) kuhusiana na vikwazo US alishafel mda sanaaaaa
 
Nitajie hivyo vikwazo mkuu, mimi nijuavyo alitishia lakini hakuweka vikwazo, labda unaweza kuwa na taarifa kamili karibu
Nikweli mkuu wameekewa ila havina athari yeyote ile kwaile project maana ushakamilika kwa 90%
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…