SAKATA LA UMEME ZANZIBAR: Lawama kwa Serikali, Tanesco ama ZECO?

Hao mabulls wenyewe wanasemaje kuusiana na kutokuwa na umeme siku zote hizo, wanamkakati gani wakati hicho kifaa kinasubiriwa, ina maana hawakuwa hata na spare walisubiri kife ndowaagize?

weee kuwa na heshima tafadhali,unaweza ukaja kutukana BABA ZAKO na WAJOMBA zako humu.
 
Duh,
Yaani suala la kiufundi linageuka kuwa la kisiasa? Kweli JF hapana dogo!
 
Duh,
Yaani suala la kiufundi linageuka kuwa la kisiasa? Kweli JF hapana dogo!
Sio linageuka kuwa la kisiasa bali hapa kuna jeuri inajibiwa ,angalia leo ni siku ya saba kama sikosei maana masiku yameanza kuongezeka kwa kasi,sasa hili jambo linaelekea kwenye mambo ya Muungano ,wakati Tanganyika wameungana na Zanzibar na kumetokea tatizo linalohusu nchi nzima lazima kuwepo na hali ya imajensi ,je umesikia lolote kutoka katika serikali ya Muungano au serikali ya Kikwete au serikali ya CCM ,haya ni mambo ya ndani Waziri wa mambo ya ndani wa Muungano anajua au anayo habari kuwa wananchi wa sehemu ya pili ya Muungano wako katika hatari ya kukumbwa na janga la maradhi kwa kukosekana umeme na maji katika mji mkuu hapo Unguja,hakuna umeme inamaana hata mafuta yatakuwa hayapo ,sidhani kama katika vituo vya umeme na hata kwenye bohari kuu ya kuhifadhia mafuta kuna generators ,hivyo kutakuwa hakuna nguvu za kusukuma mafuta na kama kuna watu au hospitali zinatumia generator zitapoteza utoaji wa nishati hiyo kwa kukosa mafuta,hata magari ya zimamoto ambayo yanasemekana yatatumika katika kutoa huduma za maji nayo yamechakaa na pia yanahitaji mafuta ya kwenda na kurudi kuchukua maji na kuyasambaza kwenye vituo walivyoanzisha au vitakavyoanzishwa---------leo ni ya saba------- Nini waziri wa Muungano amefanya kulishughulikia suala hili ambalo ni nyeti na linagusa jamii ya upande wa pili wa Muungano----------- Je wanayo haki ya kudai na kusema Muungano hauna faida ? Mimi nitajibu kama ni waziri au ni Muungwana hawa wahafidhina waliwahi kusema mambo yao waachiwe wenyewe am I right ? na nitakuwa nimemaliza kazi ,lakini tukumbuke hapa kuna suala la ubinadamu tumekwenda Comoro kwa vishindo na kurudi baada ya kumaliza kazi tuliokwendea nini tulichokiendea huko ?
Sasa isiwe kupeleka vyombo vya dola siku za uchaguzi kutisha na kupiga watu lakini na hili la sasa kunatakikana huduma zisimamiwe na za kutolewa na vyombo hivyo haswa jeshi la wananchi na polisi kuzidisha doria ili kulinda wananchi na mali zao ,jeshi linaweza kuchimba visima vya dharura ,mbinu na njia wanazo ambazo ni maarufu kwa vikosi vya jeshi katika fani ya kutayarisha temporary camp , hapa ndipo imani na udugu wa Muungano unapopata mrija na kuteka mawazo ya wananchi ,mimi naamini kabisa ikiwa leo hii upinzani utajikusanya na kutaka kutoa huduma muhimu kwa wakati walio nao wananchi wa Unguja basi serikali ya wahafidhina itapinga kwa nguvu zake zote na pengine kuwakama na kuwaita wahaini.
Upinzani sijui unasubiri kitu gani wahafidhina nchi imewashinda na Muungwana nae kabana kimya ,nimesikia watu wakisema Karume amewaambia watu wasidanganyane shida ya umeme haifiki mwezi wa Ramadhan.i
 
mwiba
sasahawa wahafidhina hawana uwezo hata wa kureples fuse?
sasa wao si wana nguvu za mapinduzi?
mtu wa pwani vipi au bado munasherehekea ushindi wa tsunami?
 
Umeme umerudishwa au bado wanaendelea kusubiri kifaa kutoka nje. Spare je haikuwapo?
 
hahaha mwiba unafurahisha hasa! umeme hadi jana bado haujarudi!
 
hahaha mwiba unafurahisha hasa! umeme hadi jana bado haujarudi!
Anaefurahisha ni Karume maana alihojiwa na watu wa habari na utangazaji aliwambia wasitie hofu wananchi watazoea ,huyo ndie Raisi wa Unguja aliepewa Shahada ya udaktari huko amerika ya Utawala bora na uongozi mahili.
Ila Muungwana na e kaweka gear kubwa anataka kusikia tena kauli ya wahafidhina ya kama hawakusaidiwa watadai warudishiwe ASP.

Ila kiza kinaendelea na sasa wezi wa waya za Umeme kutoka Dar wamewasili na weshafyeka mita kama mia nne times 4 na sijui wale wa mafuta ya Transformer pengine hawajapata habari kama zenji kuna dezo..
 
nawaonea huruma sana wananchi wanaotawaliwa na Karume.......aa yalaiti wangeliweza, hata hao ccm wasingemuunga mkono.
 
Its now 8 days since the power went off in Zanzibar. This is not "mgao" style but total blackout!

Initial news: Faulty on Zanzibar side.
Developing story: The sea cable has been severed AND Norwegians have been contacted to investigate. This kind of work may take up to Three Months!

There is no backup generator for Zanzibar in case power from Mainland is lost. People are suffering. Is there anyone with the inside information? As it seems this no big deal in Tanzania...
 
Watajua maana ya Muungano, hivi hakuna mafundi umeme huko bara hadi mafundi watoke Norway? Au ndio tanzania haithamini wahandisi umeme wake hadi ije kampuni kutoka nje ndio waamini kazi imefanyika?
 
Hapa ndipo tunaonekana kuwa bado tuko mbali sana na maendeleo. Zanzibar imekaa kwenye bahari, siku hizi kuna Renewable Energy/Generators soln kibao zinazotumia maji ya bahari.

Bado tangu miaka hiyo tunawekeza kweye siasa zisizokuwa na maendeleo tunasahau vitu vya maana sana ambavyo vingeweza kuleta maendeleo. Nina wasi wasi infrastructure zetu zilivyokaa hata hakuna aliyekuwa anaangalia life span ya underwater cable( General monitoring) inayotoa umeme bara kwenda zanzibar.Anyway nafikiri wakihitaji soln ya haraka usikute ka-Richmond kengine hapa.

Hapa sasa ndo tutaona umuhimu wa kuwa na wataalamu wetu miezi mitatu? Zanzibar itabidi waamie tuwawekee sehemu za kukaa Dar kama wakimbizi.

Je hao waNorway wameisha fika Zanzibar?
 
Ingekuwa nchi nyingine wananchi wangeandamana na kushinikiza waambiwe kinachoendelea...in Tanzania...jamaa wameuchuna na Wanzanzibari nao wameuchuna. They need to pressurize their president to act!
 
Ingekuwa nchi nyingine wananchi wangeandamana na kushinikiza waambiwe kinachoendelea...in Tanzania...jamaa wameuchuna na Wanzanzibari nao wameuchuna. They need to pressurize their president to act!

Kabla ya kuandamana wataambiwa wapige kura ya maoni kama wanataka umeme au la!
 
Ingekuwa nchi nyingine wananchi wangeandamana na kushinikiza waambiwe kinachoendelea...in Tanzania...jamaa wameuchuna na Wanzanzibari nao wameuchuna. They need to pressurize their president to act!

Wa-mpressurize kwani walimchagua? Anyway nashangaa kuona wamekaa kimya au kuna underground ambazo hatuzijui?
 
unajua NYUMBU wakishagundua mwenzake mmoja ameshakamatwa na simba na kuliwa wanajiona ni salama wala hawastuki.....
 
Kabla ya kuandamana wataambiwa wapige kura ya maoni kama wanataka umeme au la!

kwi kwi kwi, langu jicho jamani, inawezekana muungano umeshavunjika si unajua tena mambo ni kwa siri-kali. Maana huyo waziri wazanzibar alisema hilo swala serikali ya mapinduzi haijafikia kuomba msaada, mtu kufa na tai shingoni.
 
Back
Top Bottom