SAKATA LA UMEME ZANZIBAR: Lawama kwa Serikali, Tanesco ama ZECO?

Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), limesema kukatika kwa umeme katika miji ya Dar es Salaam na Zanzibar juzi usiku kumesababishwa na njia ya umeme kati ya Morogoro na Ubungo kuzidiwa na mzigo.

source Nipashe

......
Dk. Rashid alifafanua kuwa kwa upande wa Zanzibar njia inayopeleka umeme visiwani ilipata hitilafu kufuatia vikombe kupasuka baada ya kuzidiwa na mzigo mkubwa wa umeme.

...... Umeme huo ulirejea jana alfajiri kwa upande wa Dar es Salaam na kwamba Zanzibar tatizo limeendelea kutokana na hitilafu zilizoko kwenye mitambo ilioko Ras Fumba visiwani hapo, kwa mujibu wa taarifa ya Tanesco. Kifaa kibovu kilichosababisha tatizo kati ya Dar es Salaam na Morogoro kiliondolewa jana saa 5:30 asubuhi baada ya kugundua eneo lenye hitilafu.

source nipashe

haya mwiba lete mengine, mwaka huu hamna maneno ya kutuwambia gogo tushalichanja
 
Mtu wa Pwani, uhafiki anachosema Mwiba au? hahahahhh, this man is comedian -- yaani JK anataka gengeni kwa wahafidhina kuwe harufu ya kinyesi tupu; teh teh teh, iko kazi!

Jamani hii si kweli. Kikwete hawezi kufanya mambo kama haya. Hata yeye ni binadamu na anajua machungu ya wananchi wake.
 
the president ( JK) has a lot of means at his disposal which enables him to exercise his authority. sasa huyu jamaa JK yeye kwanza ni muoga. yaliyotokea butiama yalionyesha kabisa kwamba he has no influence whatsover over CCMs policy making and implementation. He has not been able to initiate anything but has been reduced to react to events.It is now evident that Karume is a small time politician who is obsessed with self preservation at the cost of peace and development in zanzibar. lakini penye ukweli uongo hujitenga: bila CCM bara, karume na wenzake zanzibar wamekwisha! and that is a fact. sasa hicho kiburi anachoonyesha sijui kinatoka wapi.
JK aliingia madarakani akiwa amedhamiria kutatua mgogoro wa zanzibar. so far he has abdicated that responsibility and has not shown any leadership at all on this issue. badala yake kawaachia akina makamba na kingunge waendeshe mambo. the shelf life of partucularly these two guys has long since expired. sasa sijui nini kimempofua JK mpaka halioni hilo!
 
: bila CCM bara, karume na wenzake zanzibar wamekwisha! and that is a fact. sasa hicho kiburi anachoonyesha sijui kinatoka wapi.
!
SI KIBURI KABISA HUYU BWANA NAYO ELIMU NI NDOGO HANA REASONING CAPASITY YA KUTOSHA KAMA YA ALI KARUME,WEWE ANASHINDA NA AKIN SHAMUHUNA, KIDOGO ZAMANI ALIKUWA ANSHINDA N AKINA MWAKANJUKI AKAWA ANANUKIA UA RIDI
 
Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), limesema kukatika kwa umeme katika miji ya Dar es Salaam na Zanzibar juzi usiku kumesababishwa na njia ya umeme kati ya Morogoro na Ubungo kuzidiwa na mzigo.

source Nipashe

......
Dk. Rashid alifafanua kuwa kwa upande wa Zanzibar njia inayopeleka umeme visiwani ilipata hitilafu kufuatia vikombe kupasuka baada ya kuzidiwa na mzigo mkubwa wa umeme.

...... Umeme huo ulirejea jana alfajiri kwa upande wa Dar es Salaam na kwamba Zanzibar tatizo limeendelea kutokana na hitilafu zilizoko kwenye mitambo ilioko Ras Fumba visiwani hapo, kwa mujibu wa taarifa ya Tanesco. Kifaa kibovu kilichosababisha tatizo kati ya Dar es Salaam na Morogoro kiliondolewa jana saa 5:30 asubuhi baada ya kugundua eneo lenye hitilafu.

source nipashe

haya mwiba lete mengine, mwaka huu hamna maneno ya kutuwambia gogo tushalichanja

Ndugu mambo kidogo kidogo sasa ulitegemea nipashe waandike nini ? Embu itazame hiyo habari yenyewe Morogoro na Dar ,halafu kuna vikombe halafu kuna Fumba halafu kuna njia inayopeleka umeme halafu kuna kuna kifaa ,leo ni ya nne Zanzibar haina umeme , tatizo si watumiaji wa toilet paper sasa kama huamini magazeti na mifuko ya rambo ni mali ,wala usijie ukapita mitaani ukaona kifuko cha rambo kimefunga fungwa ukakifungua.
Ujue hawa CCM Zanzibar wanaogopewa na CCM bara ,tafu la kutunisha msuli halikuanza huko Butiama ni mara nyingi wamekuwa wakitishia ikiwa hamkufanya hivi tutavunja Muungano nafikiri Muungwana ameamua nae kutunisha na wahafidhina hawa huenda wakawa nao wanam-blackmail.Ila kuna siku mmoja wao zitamfyetuka awatolee uvivu.

Sasa kama hujasikia Kikwete ( haya shirika la umeme) ka(lime)sema kifaa au hivyo vikombe vinapatikana Sweden. Baadhi ya ya wahafidhina wanafikiria kuvunja Muungano kama kesho umeme haukurudishwa. Kisa alizomewa alipoonekana mmoja wao akiranda na ndoo kutafuta maji.
 
mwiba nafasi yako nii ktk chama cha CUF ?

unafaa uwe katibu mwenezi katika kitengo cha Propaganda mkuu nimekukubali.

ila hili halina ubishi si la kisiasa.

kimuungano kikao tulichokaa hivi karibuni baina ya Waziri Pinda Shein Seif Khatib Makamo wa Rais na wenzao wa zanzibar wamezungumzia mengi ya kuimarisha muungano likiwemo la umeme Pemba na Unguja.

wamo wakifikiria uwezekano wa kutumia umeme wa upepo

na wewe balahau endelea kuwadanganya wenzio nchana
 
.

wamo wakifikiria uwezekano wa kutumia umeme wa upepo

na wewe balahau endelea kuwadanganya wenzio nchana
Umeme wa upepo ni mojawapo energy mbadala, na kwa maeneo ya Kaskazini na Mashariki ya unguja yapo maeneo mengi ambayo yanaweza kutumiwa kuvuna upepo. Ni wazo zuri na iwapo litatekelezwa basi itakuwa jambo la msingi sana.
 
Sikio la kufa halina dawa ,kwa ufupi CCM hata wajenge Pepo huko Zanzibar basi wakati wao umekwisha ,hilo halina mjadala ,Lowasa na wenzake wameonekana mafisadi japo sio kweli kama wanavyodai lakini hawana la kuwafanya WaTz kuwaamini hata wafanye kitu gani na ndio wamekwisha kataliwa si rahisi kurudi au kurudishwa tena katika ngazi walizokuwepo,sio kwamba mimi ni CUF au mhafidhina wa Chama fulani ,hapana wandugu ,kuna wakati unakataliwa na huna utakalolifanya ukakubalika ,CCM imeshakataliwa Zanzibar hawaitaki hata kuiona , huo ndio ukweli uliopo na ndio ukweli ambao CCM wanapigana nao ,ni ukweli usiofichika kuwa CCM haina nafasi ya uhalali kuitawala au kuendeleza madaraka yake huko Zanzibar wanachokifanya ni kutumia nguvu za ziada ili ibaki madarakani na wenyewe hilo wanalitambua.
Hii kasumba ndio iliyowafanya Wahafidhina wampe ukweli Kikwete achague kama yupo na sisi au na wao > If you are with us or with them < by Joji Kichaka wakati akitayarisha mkakati wa kuivamia Iraq ,hivyo kuidai ASP ni kuivamia Zanzibar upya na kufanya Mapinduzi ya kuiondoa mabaki ya CCM na CUF au mfumo wa vyama vingi kwa ujumla.
Kwa maana ile CCM na CUF zingelibakia Tanganyika na Pemba.

Kama umeangalia gazeti la jana utaona kuna mvutano kati ya Chama cha Michezi cha Zanzibar na Tanganyika(Tanzania Bara) suala ambalo lina mtazamo wa kisiasa wazenji wamesema wanapunjwa na hawatazamwi wala hawasaidiwi kuna zaidi ya dola za kimarekani kutoka FIFA na CAF.
Hili unaliona ni kuhusiana na michezo lakini kuna siasa hapo kuwa wazenji wanabaguliwa na hawapewi haki zao au share kwa misaada inayotolewa katika mambo ya Muungano.

Embu tazama hapa.
Mbali na hayo Tamim aliongeza kuwa TFF imekuwa ikikaa kimya na dola 250,000 zinazogawiwa na FIFA, lakini hakuna hata senti inayopelekwa huko pia uteuzi wa makocha wasaidizi kwenye timu za Taifa, hauzingatii ushirikiano na makubaliano yaliyofikiwa kwenye vikao, ambapo TFF imekuwa ikifanya inavyotaka.
Aidha, aliongeza kuwa TFF, imekuwa ikiyafuta majina ya waamuzi wa Zanzibar kwenye orodha ya majina ya waamuzi wanaohitajika kupewa beji za FIFA, ambapo pia TFF imepokea mradi wa Gold, kutoka FIFA, mara mbili mmoja ukiwa wa kujenga hosteli na mwingine wa kuweka nyasi bandia katika viwanja viwili.
Cha kushangaza miradi yote imeelekezwa bara badala ya angalau kuutupia mmoja Zanzibar.
ZFA, pia imelalamikia suala la kusafiri kwa timu ya taifa, Taifa Stars, ambapo kimsingi kunatakiwa kuwe na mwakilishi mmoja kutoka Zanzibar lakini hilo halifanyiki pamoja na kutumia fedha zote zinazotumwa na CAF ambazo ni dola 100,000.
 
Nyie si mnabisha subirini muone yatakayo jiri huko visiwani kwa wahafidhina
 
Hilo la TFF na ZFA lina husika vipi na Umeme wa Upepo?

Hili ni jukwaa la siasa hivyo siasa ina ncha nyingi sana Ndugu Kibunango ,Mwalimu Nyerere alikuwa ni mwanasiasa ila aliposema anafuata Siasa ya Ujamaa na kujitegemea ulitumai kitu gani ?
Hivyo ukichanganyisha yote ya Umeme na Michezo utapata kitu mvutano wa kisiasa ambao unapenyeshwa katika sehemu mbali mbali na wahafidhina wa CCM ,Ndugu Kibunango elewa tu hata siasa inaingia katika kundi la michezo wenyewe wanaita mchezo mchafu.
Wahafidhina wanatafuta kila upenyo ili wairudishe ASP na kuwa na Utawala wao ambao hautashirikisha Bara ,wahafidhina hawa wameunda vikundi vingi vya majeshi kuna KMKM ,kuna JKU ,kuna Mafunzo ,kuna Zimamoto hawana hata gari moja la kuzimia moto wakati wanafika zaidi ya elfu ,kuna janjaweeds sasa hata hawa au vikundi hivi havimo katika muungano wala havisimamiwi na mkuu wa Majeshi ni vyao wenyewe wanajitayarisha ikiwa mabo yao yatafanikiwa basi watakuwa wamekwisha kujitayarisha ,kama lile ombi lao lingekubaliwa kule Butiama la kurudishiwa ASP tayari wangekwisha mtangaza mkuu wao wa majeshi,kama unakumbuka karibuni tu karibuni ya kijomba ,gari la KMKM lilipita kwenye kituo kimoja cha polisi kufika hapo polisi wakataka kulipekua jamaa waliokuwemo humo ambao ni askari wa KMKM wakashuka wote na kuwashushia kisago askari hao wa polisi ambao ni wa Muungano walipigwa vibaya sana ,hadi hii leo hujasikia kelele na polisi hao kelele zao zilizimwa na wahafidhina kwa kuambiwa kama wanataka kuendelea na kazi wanyamaze la wanataka kurudishwa kwao Tanganyika waendeleze madai ,walikaa kimya wakiambiwa mambo yanafuatiliwa ,kuna kikosi kimoja ambacho ni cha jeshi ambacho walikuwa ndio kwanza wapo depo sehemu za uwanja wa ndege Zanzibar ,hawa waliwashukia vijana waishio karibu na nyumba za wakubwa na kutembeza buti kinoma kisa mmoja wao alishushwa na kufokewa kutoka kwenye daladala ,jamaa akaenda zake kambini na kurudi na kikosi cha maangamizi hapo nje ya airport walitembeza mkong'oto wa nguvu bahati mbaya au nzuri watoto wa vigogo walikuwepo wakipiga gumzo nao walichanganywa kilicho fuata jamaa waote walioshiriki walifukuzwa depo na kurudishwa Tanganyika ,walikuwa bado mwezi tu kumaliza depo(mafunzo ya Kijeshi) ,serikali imetumia gharama za kuwalisa na kuwafundisha kwa miezi mingi ,nionavyo walikuwa wanastahili kupewa adhabu ndani ya jeshi na si kufukuzwa ila ubabe ndio uliotumika kuwaondoa watu hao kwa kuwa tu walikuwa Watanganyika na kwa vile watoto wa wahafidhina ndio walioguswa walitumia nguvu walizonazo dhidi ya Serikali ya Muungano.
 
Siamini kabisa kuwa JK anaendekeza wahafidhina wa Unguja.Suala la maridhiano ya kisiasa lipo moyoni mwake na ni imani yangu kuwa JK atamaliza matatizo ya Zenj soon.

Jk ana uwezo mkubwwa wa kutatua mambo mazito.Nia yake ameionesha waziwazi kwamba atafanya juu chini kutafuta muafaka.

Ni tu anayepima mambo,si wa kukurupuka,JK Nyerere mwenyewe yalimshinda kaishia kumfukuza Aboud Jumbe wakati wa kuchafuka kwa hali ya hewa ya Zanzibar.Hapo hakukuwepo CUF.

Mkapa aliishia kuwamwagia mabomu na risasi hadi kuwafanya wakimbizi.Hakuwa na suluhu ila kuwashikisha adabu na kuua watu zaidi ya 20.

Kikwete anatumia maarifa zaidi kuliko hawa watangulizi wake na mtaona matokeo yake.Kura ya maoni ni proposal ambayo CUF walikuwa wanaipigia debe miaka ya nyuma.Demokrasia sasa ni pana zaidi kuliko wakati wowote sidhani kama kutapelekwa tena majeshi ya ulinzi na usalama kuwanyanyasa wapiga kura na kuwatesa kama enzi zile za giza.
Subirini mtaona ,wakati utafika kila kura itahesabiwa bila mtutu wa bunduki kutumika wala wizi wa massanduku ya kura kuibiwa na uchaguzi wa baadhi ya majimbom kuahirishwa.
Subiri mtahakikisha kuwa Madiba wa Tanzania ni JK.
 
Hili ni jukwaa la siasa hivyo siasa ina ncha nyingi sana Ndugu Kibunango ,Mwalimu Nyerere alikuwa ni mwanasiasa ila aliposema anafuata Siasa ya Ujamaa na kujitegemea ulitumai kitu gani ?
Hivyo ukichanganyisha yote ya Umeme na Michezo utapata kitu mvutano wa kisiasa ambao unapenyeshwa katika sehemu mbali mbali na wahafidhina wa CCM ,Ndugu Kibunango elewa tu hata siasa inaingia katika kundi la michezo wenyewe wanaita mchezo mchafu.
Hilo la mchezo mchafu kwenye vyama vya michezo sio mwake...
ZFA kushiriki na kupata mgao wa FIFA & CAF hawana budi kujiendesha pasipo kutegemea SMZ, Tatizo linakuja kwa hawa BMZ kupenda sana kuingilia uendeshaji wa ZFA, mpaka sasa imekuwa ni vurugu kabisa..TFF kwa kutumia loop hole hiyo ndio wanafanya hivyo wafanyavyo. Kipindi kile ZFA inaongozwa na yule jamaa wa Masomo Bookshop ilikuwa imefika katika hatua nzuri sana ya kuweza hata kutambuliwa na FIFA, hadi sasa CAF inaitambua ZFA kupitia mwanamichezo huyo...

Kama kawaida yake BMZ na Wizara yao ya michezo wakaingilia kati juhudi za ZFA, mpaka leo sijui lengo lao lilikuwa ni nini, matokeo yake juhudi zote za kuweza kutambuliwa na FIFA zikarudi nyuma..
 
Leo ni ya tano Kikwete anawaendesha gwaride wahafidhina wa Mapinduzi na mandoo ya maji ,amewafanya wawepo kama jangwani wakisikia mtaa fulani kuna pump inatoa maji utaona mkururu mbio unaelekea huko mara unarejea mbio unaelekea kwengine sijui hii sasa inageuka kuwa laana .
Muungwana kamata uzi huo huo na hawa wahafihina wa Serikali ya Mapinduzi wakitishia kuvunja Muungano safari hii tutawashitaki kama wahaini.
Hapa ndipo panaponifanya nibaki na kadi ya CCM hadi leo maana wanapoamua kujibu mapigo kwa mwenzao basi hawana sumile.
 
Umeme wa upepo ni mojawapo energy mbadala, na kwa maeneo ya Kaskazini na Mashariki ya unguja yapo maeneo mengi ambayo yanaweza kutumiwa kuvuna upepo. Ni wazo zuri na iwapo litatekelezwa basi itakuwa jambo la msingi sana.

Kibunango,

Hili la Umeme wa Upepo lisiishie Zanzibar tuu, hata Bara kunahitajika kanza mikakati ya kutengeneza umeme wa upepo na jua.
 
kosa kubwa la jk ..ni kuwa mnyonge pale butiama ..aliwapa kichwa mahafiodhina ...kwa ni hata angewakubalia asilimia kubwa ya wananchi wa leo wamezaliwa baada ya 1977..na kwa ASP ni historia tu!!kama alivyosema warioba....tena yenye kumbukumbu mbaya za mauwaji
 
...kamwe kikwete hawezi kuwakatia umeme zanzibar kwa makusudi...kwani hiyo ni sehemu ya jamhuri yetu..ni mkoa kama singida ,moro ets ..rais hawezi kufurahia wakitaabika ...na mtoto mdogo akikunyea mkono ..huukati!.......wahafidhina dawa yao ni kuwanyima kura tu!...sasa yeye kikwete anachoweza kufanya ni kukataa kuwasaidia kuiba kura....na kuwakatalia kuwajazia meli iliyojaa vijana mamluki wa kupiga kura basi.....
 
Kibunango,

Hili la Umeme wa Upepo lisiishie Zanzibar tuu, hata Bara kunahitajika kanza mikakati ya kutengeneza umeme wa upepo na jua.
Kwa Bara mikoa ya Dodoma, Singida na Shinyanga inafaa sana kwa kuwa umeme wa upepo. Nimewahi kupita katika mikoa hiyo na kukutana na windmill kwa ajili ya kusukuma maji, na inafanya kazi karibu mwaka mzima. Tatizo la wind power ni gharama kubwa katika ujenzi wake(aidha katika kutafuta sehemu muafaka kwa kuweka hizo wind power), aidha ukiondoa kelele ni nzuri kwa mazingira yetu.
 
Leo ni ya tano Kikwete anawaendesha gwaride wahafidhina wa Mapinduzi na mandoo ya maji ,amewafanya wawepo kama jangwani wakisikia mtaa fulani kuna pump inatoa maji utaona mkururu mbio unaelekea huko mara unarejea mbio unaelekea kwengine sijui hii sasa inageuka kuwa laana .
Muungwana kamata uzi huo huo na hawa wahafihina wa Serikali ya Mapinduzi wakitishia kuvunja Muungano safari hii tutawashitaki kama wahaini.
Hapa ndipo panaponifanya nibaki na kadi ya CCM hadi leo maana wanapoamua kujibu mapigo kwa mwenzao basi hawana sumile.

kwa hio una kadi mbili ya CUF na hio? au hii yetu hujarejesha tu lakini imani yako yote iko kwa hao wenzako?
 
Back
Top Bottom