SAKATA LA UMEME ZANZIBAR: Lawama kwa Serikali, Tanesco ama ZECO?

Mtanganyika

JF-Expert Member
Jul 18, 2007
1,601
939
Salma Saidi, Zanzibar

MJI Zanzibar umefunikwa na giza zito kwa muda wa siku tano mfululizo kufuatia kukatika kwa umeme na hatimaye kusababisha biashara nyingi kusimama na nyingine kuharibika.

Akizungumza na mwandishi wa Mwananchi jana, Meneja wa Shirika la Umeme Zanzibar, Juma Isihaka Bakari alisema tatizo linatokana kuungua kwa nyanya za umeme zilizopita chini ya ardhi katika ya Mkele na Malindi hadi Mlandege.

Alisema mafundi wao wamefanya kazi tangu juzi usiku na mchana wakichimba maeneo hayo kutafuta hitilafu ilipo, lakini mpaka sasa hawafanikiwa.

Kutokana na hali hiyo maeneo mengi ya mji wa Zanzibar maduka makubwa yanayohitaji umeme kwa kiasi kikubwa yamefungwa

Katika baadhi ya maeneo yenye maduka ya samaki kama Darajani samaki wameoza na kuna harufu na kusababisha mazingira ya maeneo hayo kutokalika kutokana na harufu ya uvundo wa samaki.

Baadhi ya mahoteli ambayo hayana jenereta kama ya Bwawani ambayo ni ya serikali hakuna jenereta na hivyo baadhi ya wageni hotelini wameanza kuhamia mahali pengine kwenye unafuu.

Hospitali nyngi ya mjini hapa hazina jenereta hivyo kusababisha usumbufu mkubwa kwa wagonjwa, hususani ambao walitarajiwa kufanyiwa opasuaji.

Baadhi ya wafanyabiashara waliozungumza na mwandishi wa Mwananchi wameilalamikia hali hiyo na kulilaani Shirika la Umeme la Zanzibar kwa kuwaingiza katika hasara na kikubwa wakilalamikia kutokuwapo taarifa za uhakika.

Ibrahim Masudi ambaye ni mfanyabiashara wa duka kubwa Quality Super Market, alisema kwa sasa hapati wateja wengi kutokana joto na gizo hivyo kumfanya alifunga.

Mfanyabiashara mwingine wa samaki wa sokoni Zanzibar anayejishughulisha na uuzaji wa kamba na samaki wengine, Said Rashid alisema wamepata hasara kubwa kutokana na samaki kuoza.

"Yaani tunashangazwa sana na kitendo cha shirika la umeme kukata umeme, kwani kimetusababishia hasara kubwa," alisema Rashid.

source majira
 
Jee tutafika? Hari mpya kasi mpya. I thought tunatangaza Tanzania kwa kusema the home of Mount Kilimanjara and ireland of Zanzibar. Baada ya umeme kurudi i guess muheshimiwa Karume atatupa makisio ya hasara.

Juzi nimesoma thread mmoja inayosema Zanzibar wanatafuta njia ya kugawa mafuta yatakayochimbwa, How will they dig oil while the whole country will be dark?

Au ndio tutafungwa na mkataba mpya utakaosema umeme ukikatika mnatulipa 152Million kwa siku?
 
"Yaani tunashangazwa sana na kitendo cha shirika la umeme kukata umeme, kwani kimetusababishia hasara kubwa," alisema Rashid.

Ni kwamba hawakuwahi kupokea bil ya umeme ama ilikuaje hadi umeme ukakatwa ? Au walikuwa wanaenda kama jamaa wa JWTZ kwa kuwa wao ni zanzibar ?
 
Salma Saidi, Zanzibar

.................


Akizungumza na mwandishi wa Mwananchi jana, Meneja wa Shirika la Umeme Zanzibar, Juma Isihaka Bakari alisema tatizo linatokana kuungua kwa nyanya za umeme zilizopita chini ya ardhi katika ya Mkele na Malindi hadi Mlandege............................

source majira

lunyungu sababu sio masuali ya bili, si mbaya mzee mwenzangu ukasoma kwa uangalifu kabla ya kubofya keyboard
 
Alisema mafundi wao wamefanya kazi tangu juzi usiku na mchana wakichimba maeneo hayo kutafuta hitilafu ilipo, lakini mpaka sasa hawafanikiwa.

Kutokana na hali hiyo maeneo mengi ya mji wa Zanzibar maduka makubwa yanayohitaji umeme kwa kiasi kikubwa yamefungwa
Poleni wananchi wa Zenj, naona mlikuwa hamjazoea hii kasia ya Tanesco. Vuteni subira, subira ya vuta heri.

Poleni kwa bei ya vitu kupanda pia (expected).

Wakati ule huku kusini tunasota na shida ya umeme, ilionekana ni issue ya kawaida (miezi mitano bila umeme).
 
lunyungu sababu sio masuali ya bili, si mbaya mzee mwenzangu ukasoma kwa uangalifu kabla ya kubofya keyboard


Mtu wa Pwani ni kweli sikusoma the whole thing nilikimbia kuuliza .Lakini JF ni shule umesha nipa sababu sasa wacha watamalizana wenyewe .
 
..na hicho ndio mtaendelea kupata mkiendelea kuiweka CCM madarakani!
 
DuuuH... Yaani sasa Bia watu wanakunywaje! Joto lile na Bia ya Moto..

Kamanda,

Bia kule hazirusiwi kwa ajili ya maadili na ole wako ulale na mwananake asiye wako kama hujamwuoa basi lazima tu upate bakora!

Hayo ndoo maadili ya Visiwani!
 
Kamanda,

Bia kule hazirusiwi kwa ajili ya maadili na ole wako ulale na mwananake asiye wako kama hujamwuoa basi lazima tu upate bakora!

Hayo ndoo maadili ya Visiwani!

Kamanda hizo ni stori za Ijumaa tu... lakini bia kule ni bandika bandua..
 
Kuna tetesi Kikwete ameanza kujibu mapigo ya wahafidhina waliodai warudishiwe ASP kama CUF itajumuishwa kwenye Serikali ya Mapinduzi .Uvumi huo ambao unaonyesha kuwa maneno waliyoyatoa wahafidhina wa serikali ya mapinduzi dhidi ya wenzao wa CCM bara yamewagusa wengi ambao wanaita kuwa huo ni udhalilishaji wa hali ya juu ambao ulifanywa mbele ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano na Mwenyekiti wa CCM Mh.Kikwete ,kama alivyosikika Warioba akijibu jeuri za wahafidhina hao wa Serikali ya mapinduzi kuwa angeliwapa ruhusa hapo hapo Butiama wachukue ASP yao na wawaachie wao na CCM ili wakakumbane na dharuba za CUF huko visiwani ,akimaanisha kuwa bila ya nguvu za CCM Bara kutumika wahafidhina hao wangelikwisha kusahauliwa na kuwa wauza mbatata za urojo na pweza pale forodhani.
Inasemeka Unguja hakuna umeme leo ni siku ya tatu ,tayari maji hayapatikaniki mjini kwani shida hiyo iliondolewa kwa kuchimba visima vinavyotumia waterpump ambazo hutumia umeme ,pia mawasiliano yamekuwa duni kwani mobile simu zinahitajiwa kila baada ya matumizi.
Wahafidhina sasa wameanza kutumia toilet paper na wengine wameonekana wakijisogeza karibu ya pwanipwani ili kukidhi mahitaji yao dharura na wengine kelekea mashamba.
Nguvu za kuilazimisha na kuisemesha bara hawanazo kwani kuna kitu kimeanza kujulikana kama machafuko ya Butiama ,mbinu zilizotumika Kikwete hakuambiwa tokea mwanzo na jinsi walivyomzidi kete kwa mazungumzo Kikwete aliona ni rahisi na alidanganywa kwamba hakuna tatizo,lakini muda si mrefu aling'amua wakati maji yameshamwagika na hasira zake ndio zitakazo wakosesha raha hili genge la wahafidhina wa serikali ya mapinduzi. Wanasema ameanza kuwakatia umeme japo siku nne na mengine yatafuata baadae.
 
Guess what!!! "Waliomletea" JK jeuri wana majenereta maisha mdundo...sasa sijui nani anakomolewa mwananchi au kiongozi?
 
Mtu wa Pwani, uhafiki anachosema Mwiba au? hahahahhh, this man is comedian -- yaani JK anataka gengeni kwa wahafidhina kuwe harufu ya kinyesi tupu; teh teh teh, iko kazi!
 
siamini kabisa. wenzetu wa cuf kila kitu ni siasa tena za kipropaganda

kosa la kiufundi hugeuzwa la kisiasa.

basi Karume asiumwe katishwa maji yasikatie au umeme usizimike wanaonyeshwa jeuri.

mtabaki hivyo hivyo mafisi fupa hamling'ati ng'o na mwiba huo utawachomeni kubaya
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom