Sakata la ubomoaji kuanzia Kimara mpaka Kiluvya, Rais Magufuli tunaomba usikie kilio chetu

Cha msingi...Serikali isiache kufanya mradi kwa sababu ya kuogopa kubomoa...mhimu serikali ione udhaifu wa sheria iliyotumika, 1932, na kuwafidia hawa ndg zetu pesa yenye thamani ili wakatafute maeneo wajenge...na wananchi tuache kujenga kwa mazoea kisa kukaa karibu na barabara.
 
kwahiyo kodi inakusanywa na serikali mbili sio

Inakusanywa na Serikali Kuu inayojitambua sasa ya Jemedari Rais Dkt. Magufuli na zile Serikali za Rushwa na Umagumashi zilizopita hasa hasa ya awamu ya Nne ( 4 )

Ninachowashaurini tu ni kwamba toeni tu ushirikiano wenu kwa hao Wabomoaji kwani si lazima sana muishi Dar es Salaam wakati hata huko Dodoma sasa Viwanja ni vya kumwaga tu. Na kama mkiamua kuishi tena Dar es Salaam basi tafadhalini sana fuateni Sheria za Ardhi na acheni kuishi kwa kupenda Umagumashi kwani tumechoka na hii Janja Janja lifestyle yenu.
 
Hatuwezi kuhukumu Tanroads na idara ya Ardhi mpaka tuwasikie wao wanasemaje ili tujue ukweli.
 
Kabisa lazima tujali utu kuna wengine wanafanya kebehi sana humu
Nimeona baadhi ya watu wanaona kana kwamba hawa wahanga wa tatizo hili wanaigiza kumbe mambo ambayo yanataka sisi tuwatie moyo na kuwapa ushauri wa jinsi ya kupata haki zao cha ajabu ktk mambo kama haya mtu analeta mzaha na koment za kejeli uko wapi utu wetu ktk matatizo ya hawa Watanzania wenzetu!!!
 
Poleni...wakati mbaya tupo katika harakati za kuishi kama mashetani....hivyo shukuruni tu na kunyweni maji.
Ila 2020 msijisahau
 

Ifahamike kuwa mnamo tarehe 02/05/2017 TANROADS kupitia Serikali waliwakilisha Notisi ya kuwataka wakazi wa kuanzia Kimara Bekary kuhama maeneo yao kwa kuwa wako kwenye hifadhi ya barabara kwa kuwapa siku 30 wawe wamevunja nyumba wenyewe ama Tanroads wakija kuvunja watalipia gharama za kuvunja wananchi wenyewe.

Eneo la TANROADS wanalodai ni la kwao kutoka katikati mwa barabara kuna upana wa mita 121.5 kwa kila upande kwahiyo jumla la eneo labarabara ni mita 243 kwenye eneo la Morogoro Road eneo hili lilipitishwa na sheria ya barabara mwaka 2007 Bungeni.

Hoja ya wakazi wa maeneo husika ni kuwa hawakatai maendeleo lakini wapo kwenye maeneo husika kwa uhalali wengine wana hati halali za serikali, wana vibali vya ujenzi wa majengo, wana hati za serikali za vijiji za miaka ya 1970 ambazo ziliwasogeza pembezoni mwa barabara.

Kama Serikali hii inajenga hoja kwamba wakazi hawa ni wavamizi wa maeneo kwa sheria iliyopitishwa na mkoloni mwaka 1932 kwanini serikali hii hii ilitoa hati kwa wakazi wa kimara kwa miaka tofauti kuna mkazi ana hati halali ya mwaka 1964 huyu mzee ametangulia mbele za haki ndio alitoa eneo barabara mpya ya Morogoro ikajengwa kuachwa ile ya OLD MOROGORO ROAD.

Lakini kuna wakazi walio hamishwa kwenda maeneo husika kwenye operation ya vijiji ya mwaka 1970 iliyo fanywa na Hayati Mwl Nyerere kuwasogeza karibu na barabara kupata huduma za kimsingi za maendeleo kama barabara nk

Lakini kwanini kipindi chote hiko kama eneo lilikua la TANROADs kwanini walishindwa kulilinda watu wasijenge, kwanini serikali hii hii ilitoa vibali vya ujenzi na hati za ardhi kwa wakazi wa eneo hili kuendelea na ujenzi wa makazi yao kwa zaidi ya miaka 50.

Kwanini kama sehemu hii sio halali na wananchi wamevamia kwanini serikali imeendelea kupokea kodi za majengo na ardhi kwa nyakati tofauti basi serikali isingepokea kodi hizi kwanini sasa tuwe haramu na wakati tumelipia kodi za ardhi, majengo hapo mwanzo hadi hivi sasa.


Lengo letu kubwa sisi wakazi wa maeneo haya hatukatai kuondoka lakini tunahitaji serikali itufikirie inatuhamishaje kwa sababu tunazo haki zote za kulipwa fidia kama makosa yalifanyika huko mwanzo kwanini watuaadhibu sisi wakati hadi Serikali ina makosa kwenye hili suala.

Kwa mara kadhaa tumejaribu kuomba kuongea na Mkuu wa wilaya wa Ubungo bila mafanikio huku akienda East Africa Radio akisema namnukuu "wakazi wa maeneo ya kimara hadi kiluvya wamekubali kuhamisha mali zao kupisha bomoa bomoa" kauli hizi ni za uongo ni lini Mkuu wa wilaya alikaa na sisi.

Tulijaribu kukutana na mkuu wa Mkoa naye akaturudisha kwa TANROADS ambao majibu yao daima wanasema yametoka juu kwa Mh Mtukufu sana Rais John Pombe Magufuli.Baada ya juhudi zote kugonga mwamba tukaomba kwa kuandika barua kuonana na Raisi wa Jamhuri ya Muungano,Barua yetu mpaka sasa haijapata majibu ya uhakika kwamba Raisi amekubali kuonana na sisi Raia wake anaotuongoza.


Baada ya kuona juhudi zote hizi wakazi wa maeneo haya ambayo kwahesabu za haraka kuna zaidi ya nyumba 5000,kuna sheli 5,hospital3,makanisa 6,misikiti 3, ambazo zote zitavunjwa waliamua kwenda kudaihaki yao mahakamani kuomba Stop Order ifahamike kuna wakazi ambaomwanzo walipeleka Ombi lao mahakamani.Kwahiyo kuna wahusika kwenye hiibomoa bomoa wale wenye nyumba zaidi ya 1000,kwenye hili eneo linawakazi zaidi ya 50000 ambao wengine ni wapangaji,wafanyabiashara.hivyo zoezi hili linagusa umati wa watu wengi sana kwaniniSerikali haitaki kukaa na Raia wake kujadiliana.

Kwa kuwa kuanzia tarehe 02/6/2017 Tanroads wanaweza kuja kuvunja hivyotunamuomba Mh Raisi John Magufuli asitishe zoezi hili kwanza tukutanenaye tuongee naye Raisi wetu,Tumueleze shida zetu haswa ukizangatiwawengi wahusika ni wazee,yatima,wajane wataenda wapi.

Lakini serikali ililipa watu waliobomolewa kwenye mradi wa BRT kwaninisisi kuanzia stop over tusilipwe fidia tumemkosea nini Mungu kwaninituishi kama wakimbizi nchini kwetu mnataka tuende wapi,tukaewapi.Tunaziomba haki za Binadamu ziangalie hili suala kwa jicho laziada wananchi tupate haki zetu.

Mheshimiwa Raisi Tunaomba usikie hiki kilio chetu
Tunaenda wapi tutendee haki sisi wapiga kura wako...





Mwimbaji mmoja kutoka Afrika kusini aliwahi kuimba kuwa " kulia hakusaidiii kitu" na akaongeza kuwa alipokuwa mtoto mdogo mwalimu wake alimwambia "elimu ndio ufunguo wa maisha"

Ni kwa bahati mbaya sisi tunakosa maarifa ya kujitambua, kwa maana ya kutambua wewe kama mwananchi wajibu wako ni nini? na wewe kama mwananchi haki yako nini?

kama tungekuwa na maarifa ya kutosha tungetambua ni nani anayesababisha watu wajenge holela kwa maana ya watu kujenga mahali wasipostahili kujenga.

nani anasababisha makazi yakae, huduma, viwanda vijengwe mahali pasipo pake na unapotaka kufanya kitu cha maendeleo ndio tunagundua kuwa tunapotaka kuweka miradi ya maendeleo watu wamejenga.

Je ni kosa la nani? watu wenyewe ndio hawataki kufuata mipango iliyowekwa au mipango haipo na watu wanajenga wakati waliotakiwa kupanga hawapangi na wanakuja kupanga wakati maeneo watu walikwisha jenga.

Je mji unapangwa kwa kuwaacha watu wajenge holela alafu serikali inakuja ikitaka kujenga barabara inatazama eneo wanakotaka kuweka barabara na kuwabomolea waliojenga holela kama wao ndio waliokosea kwa maana hiyo ndiyo staili yao ya kupanga au mji unapangwa kwa wenye wajibu wa kupanga kuwaonyesha wananachi kabla hawajenga kuwa makazi yanaa hapa, shule zitakaa hapa, hospitali, nyumba za ibara, barabara, viwanda na kila tayari wamepanga na kila anayetaka kufanya jambo lolote anafuata mpango. na hapo anayekiuka mpango huo anakuwa mkaidi ambaye akianza tu kujenga anaaambiwa bomoa haraka.

tatizo kwetu liko wapi?

kama jamii tunahitaji kumbebesha dhamana anayewajibika, kama ni serikali ni kuwabebesha mzigo huu na sio kumbebesha mwananchi ambaye ni muhanga na kama serikali imetimiza wajibu na wananchi walikaidi basi hasara ni yao.

Acheni kulialia kudhani mtahurumiwa na wale wale bali undeni hata umoja wa wananchi wanaokaa katika makazi holela na nendeni mahakamani kudai haki yenu kwa maana hamkupenda wala kuchagua kukaa katika makazi holela bali mmekaa huko kwa uzembe wa serikali wa kutopanga mji. Na muidai serikali ipange maeneo yenu na kutoa fidia kwa wale wote wataoonekana kuathiriwa na mpango. yaani watabainika kuwa sehemu za huduma na kutakiwa kuhama
 
sasa wazee wa miaka 65 unawapeleka wapi angalia hiyo video inasikitisha sana
Inatisha wapi?
Wakati apa morogoro wafugaji wanapouana kwa maswala ya aridhi. Uku mjini masikio tuliweka pamba, sasa majanga yamekuja apo mnaona kama tatizo la Tanzania nzima
 
Nyie wananchi wa kimara mpk kibamba si ndo huwa mnamzomea mh rais akipita kwenu sasa mkome
 
tatizo wengi waliojenga maeneo hayo wametoka kanda ya ........ hivyo imekula kwao ingawa kwenye msafara wa mamba na kenge wamo
 
hujamaliza soma uzi wote ndio maana unakurupuka angali hapo juu kama baadhi ya wakazi hawana hati halali za makazi na wanazilipia kodi
Kwa sheria ya nchi yetu, Rais ana uwezo wa kutengua umiliki wako wa aridhi kwa ajili ya kupisha miradi ambayo yatakuwa na mafanikio mapana kwa jamii.
Alafu kuwa na Hati ya nyumba sio ishu sana, hata unapokuwa na umeme wa Tanesco au mita ya maji tayari ni utambulisho mkubwa wa kumiliki aridhi.
 
wengine wamesha tii amri wamehama, ila baadhi huwa hawakubali hadi wasuguane!

maendeleo Hauser I kuzuiwa kwa kuwaonea huruma watu wachache!! hilo kamwe haliwezekani!

raisi JPM wakati fulani akiwa waziri wa ujenzi aliwahi kusema " kuishi karibu na barabara ni sawa na kuufuata/ kujitakia umasikini"

wananchi wenzangu tuwe na utamaduni wa kujenga mbali na barabara ili nyumba zetu ziwe salama hata kwa kipindi cha miaka 100!!
Nilichojifunza aya maisha, ukikaaa karibu na barabara, unatakiwa ujue pesa unayopata kama unapangisha unaiwekeza sehemu ingine pia. Maana karibu na barabara sio sehemu salama, inabidi tujiulize pale, kuanzia Akiba kwenda Posta ya zamani, wakati wanajenga mwendokasi wameenda wapi wale wenye majengo ya ghorofa. Maendeleo yana changamoto sana
 
Kwani mkuu serikali haikuwapa taarifa mapema na kipimo wanachotumia???!!!!
 
Achana na hiyo, kwanini raia wakiona tu kaeneo kako wazi basi hukurupuka na kwenda jenga?! Kwanini hawapendi kuanzia ardhi, kujuwa hilo aneo wanalotaka jenga kwamba kuna miundoi mbinu au lah? Hawa ni wale wafanyabiashara wa kariakoo, kupenda kujenga karibu na barabara, kutumia njia za mkato na baadaye matokeo yake ndio haya, mie siwahurumiii kabisa, hata waende kortini wanapoteza tu muda na fedha zao, wao wafungashe waende, itakula kwao tena vibaya mno..
binadamu ukikosa huruma kwa wenzako unabidi ujitafakari, hata kama wana makosa. swala la kuona huruma ni ubinadamu.
 
Waache ujinga , barabara gani hiyo upana 243m , wajenge barabara itakapoishia hapohapo wenye nyumba ziendelee kubaki .. kama ajali zipo tuu
 
Achana na hiyo, kwanini raia wakiona tu kaeneo kako wazi basi hukurupuka na kwenda jenga?! Kwanini hawapendi kuanzia ardhi, kujuwa hilo aneo wanalotaka jenga kwamba kuna miundoi mbinu au lah? Hawa ni wale wafanyabiashara wa kariakoo, kupenda kujenga karibu na barabara, kutumia njia za mkato na baadaye matokeo yake ndio haya, mie siwahurumiii kabisa, hata waende kortini wanapoteza tu muda na fedha zao, wao wafungashe waende, itakula kwao tena vibaya mno..
shetani mkubwa wewe
 
Back
Top Bottom