Waziri wa Nishati, Doto Mashaka Biteko, Mkurugenzi wa Tanesco - Wananchi wa Goba tunaomba tusikilizwe

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Jan 3, 2013
2,161
1,493
Waziri wa Nishati, tunatambua kazi nzuri unayofanya wewe pamoja na Serikali ya Awamu ya sita kwa ujumla.

Waziri, Wakazi wa Goba tunajua shida ya umeme iliyopo na tunatambua jitihada ambazo Serikali inazifanya.

Licha ya kazi hiyo nzuri, Wakazi wa Goba hasa mtaa wa Cha Simba tunasikitishwa na mtumishi wa Tanesco anayefanya kazi ya kukataa umeme mitaa hii ya Goba, Eneo hili lina line mbili tofauti za umeme, kea bahati mbaya mtu huyu anayehusika na kukataa umeme hukata line moja tu kila siku, tena usiku. TUNAHISI MTU HUYU NI MKAZI WA GOBA HIVYO LINE AMBAYO HUWA HAIKATWI NI LINE ANAYOISHI YEYE.

TUNAOMBA MTUMISHI HUYO AKAHUDUMIE ENEO LINGINE.

HAIWEZEKANI KILA UMEME UKIKATIKA ENEO HILI BASI LINE B NDIYO INAKATWA , HATA ZIKIKATWA LINE ZOTE UTAKAPORUDISHWA LINE B HAURUDI.

Tumetoa taarifa mara nyingi sanaa juu ya jambo hili kupitia number ya Kutoa taarifa ya Tanesco lakini bado ufumbuzi haujapatikana.

MWENYEZI MUNGU IBARIKI TANZANIA

MWENYEZI MUNGU MBARIKI RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
 
Nutashangaa sana kama Tanesco hawatachukua hatua keshi asubuhi ya kumhoju na kufukuza huyi afisa wao
 
Back
Top Bottom