Majs
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 232
- 497
Ifahamike kuwa mnamo tarehe 02/05/2017 TANROADS kupitia Serikali waliwakilisha Notisi ya kuwataka wakazi wa kuanzia Kimara Bekary kuhama maeneo yao kwa kuwa wako kwenye hifadhi ya barabara kwa kuwapa siku 30 wawe wamevunja nyumba wenyewe ama Tanroads wakija kuvunja watalipia gharama za kuvunja wananchi wenyewe.
Eneo la TANROADS wanalodai ni la kwao kutoka katikati mwa barabara kuna upana wa mita 121.5 kwa kila upande kwahiyo jumla la eneo labarabara ni mita 243 kwenye eneo la Morogoro Road eneo hili lilipitishwa na sheria ya barabara mwaka 2007 Bungeni.
Hoja ya wakazi wa maeneo husika ni kuwa hawakatai maendeleo lakini wapo kwenye maeneo husika kwa uhalali wengine wana hati halali za serikali, wana vibali vya ujenzi wa majengo, wana hati za serikali za vijiji za miaka ya 1970 ambazo ziliwasogeza pembezoni mwa barabara.
Kama Serikali hii inajenga hoja kwamba wakazi hawa ni wavamizi wa maeneo kwa sheria iliyopitishwa na mkoloni mwaka 1932 kwanini serikali hii hii ilitoa hati kwa wakazi wa kimara kwa miaka tofauti kuna mkazi ana hati halali ya mwaka 1964 huyu mzee ametangulia mbele za haki ndio alitoa eneo barabara mpya ya Morogoro ikajengwa kuachwa ile ya OLD MOROGORO ROAD.
Lakini kuna wakazi walio hamishwa kwenda maeneo husika kwenye operation ya vijiji ya mwaka 1970 iliyo fanywa na Hayati Mwl Nyerere kuwasogeza karibu na barabara kupata huduma za kimsingi za maendeleo kama barabara nk
Lakini kwanini kipindi chote hiko kama eneo lilikua la TANROADs kwanini walishindwa kulilinda watu wasijenge, kwanini serikali hii hii ilitoa vibali vya ujenzi na hati za ardhi kwa wakazi wa eneo hili kuendelea na ujenzi wa makazi yao kwa zaidi ya miaka 50.
Kwanini kama sehemu hii sio halali na wananchi wamevamia kwanini serikali imeendelea kupokea kodi za majengo na ardhi kwa nyakati tofauti basi serikali isingepokea kodi hizi kwanini sasa tuwe haramu na wakati tumelipia kodi za ardhi, majengo hapo mwanzo hadi hivi sasa.
Lengo letu kubwa sisi wakazi wa maeneo haya hatukatai kuondoka lakini tunahitaji serikali itufikirie inatuhamishaje kwa sababu tunazo haki zote za kulipwa fidia kama makosa yalifanyika huko mwanzo kwanini watuaadhibu sisi wakati hadi Serikali ina makosa kwenye hili suala.
Kwa mara kadhaa tumejaribu kuomba kuongea na Mkuu wa wilaya wa Ubungo bila mafanikio huku akienda East Africa Radio akisema namnukuu "wakazi wa maeneo ya kimara hadi kiluvya wamekubali kuhamisha mali zao kupisha bomoa bomoa" kauli hizi ni za uongo ni lini Mkuu wa wilaya alikaa na sisi.
Tulijaribu kukutana na mkuu wa Mkoa naye akaturudisha kwa TANROADS ambao majibu yao daima wanasema yametoka juu kwa Mh Mtukufu sana Rais John Pombe Magufuli.Baada ya juhudi zote kugonga mwamba tukaomba kwa kuandika barua kuonana na Raisi wa Jamhuri ya Muungano,Barua yetu mpaka sasa haijapata majibu ya uhakika kwamba Raisi amekubali kuonana na sisi Raia wake anaotuongoza.
Baada ya kuona juhudi zote hizi wakazi wa maeneo haya ambayo kwahesabu za haraka kuna zaidi ya nyumba 5000,kuna sheli 5,hospital3,makanisa 6,misikiti 3, ambazo zote zitavunjwa waliamua kwenda kudaihaki yao mahakamani kuomba Stop Order ifahamike kuna wakazi ambaomwanzo walipeleka Ombi lao mahakamani.Kwahiyo kuna wahusika kwenye hiibomoa bomoa wale wenye nyumba zaidi ya 1000,kwenye hili eneo linawakazi zaidi ya 50000 ambao wengine ni wapangaji,wafanyabiashara.hivyo zoezi hili linagusa umati wa watu wengi sana kwaniniSerikali haitaki kukaa na Raia wake kujadiliana.
Kwa kuwa kuanzia tarehe 02/6/2017 Tanroads wanaweza kuja kuvunja hivyotunamuomba Mh Raisi John Magufuli asitishe zoezi hili kwanza tukutanenaye tuongee naye Raisi wetu,Tumueleze shida zetu haswa ukizangatiwawengi wahusika ni wazee,yatima,wajane wataenda wapi.
Lakini serikali ililipa watu waliobomolewa kwenye mradi wa BRT kwaninisisi kuanzia stop over tusilipwe fidia tumemkosea nini Mungu kwaninituishi kama wakimbizi nchini kwetu mnataka tuende wapi,tukaewapi.Tunaziomba haki za Binadamu ziangalie hili suala kwa jicho laziada wananchi tupate haki zetu.
Mheshimiwa Raisi Tunaomba usikie hiki kilio chetu
Tunaenda wapi tutendee haki sisi wapiga kura wako...
Attachments
-
Ikangula.Tula_2017-05-29_12-03-17(1).pdf216 KB · Views: 68
-
Ikangula.Tula_2017-05-29_12-03-17.pdf216 KB · Views: 224
-
Ikangula.Tula_2017-05-29_12-04-01(1).pdf141.9 KB · Views: 51
-
Ikangula.Tula_2017-05-29_12-04-01.pdf141.9 KB · Views: 55
-
Ikangula.Tula_2017-05-29_12-04-39(1).pdf6.8 MB · Views: 67
-
Ikangula.Tula_2017-05-29_12-04-39.pdf6.8 MB · Views: 66
-
Ikangula.Tula_2017-05-29_12-04-52(1).pdf1.6 MB · Views: 95
-
Ikangula.Tula_2017-05-29_12-04-52.pdf1.6 MB · Views: 75