Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Washangazwa na uteuzi wa Chenge Tume ya jengo la CCM-Vijana

Saa Mohamed na Ramadhan Semtawa
Mwananchi
Date::9/11/2008

UAMUZI wa Kamati Kuu ya CCM kuteua timu ya watu watatu kufuatilia utekelezaji wa mradi wa jengo la makao makuu ya umoja wa vijana wa chama hicho, umeungwa mkono na wengi, lakini jina la mwanasheria mkuu wa zamani wa serikali, Andrew Chenge, linawatia mashaka.

Chenge, ambaye alijizulu uwaziri wa sheria baada ya kutajwa kwenye kashfa ya ununuzi wa rada uliofanywa wakati akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, amesema: "Nitahakikisha nalinda heshima yangu na chama."

Timu hiyo ya watu watatu-Chenge, ambaye ni mbunge wa Bariadi Magharibi, Abdallah Kigoda, mbunge wa Handeni na Pindi Chana, ambaye ni mbunge wa viti maalum- waliteuliwa na Kamati Kuu Jumanne baada ya mkataba huo kuonekana una kasoro saba wakati ulipojadiliwa na kwenye kikao hicho cha watu 38 waliokutana mjini Dodoma.

Kutangazwa kwa timu hiyo kulipongezwa na watu wa kada mbalimbali waliohojiwa au kuiandikia Mwananchi, lakini wengi wao hawakupendezwa na kuwemo kwa jina la Chenge, ambaye alijizulu uwaziri wa miundombinu baada ya kutajwa kwenye kashfa ya ununuzi wa rada uliofanywa wakati akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

"Sina ubaya na mtu lakini kama huyu (Chenge) aliwahi kutuhumiwa na kama CCM wako makini, wanawezaje kumteua mtu ambaye naye bado anachunguzwa," alihoji David Gasper, mkazi wa Kilimahewa jijini Mwanza ambaye ni mmoja wa watu wengi walioongea na Mwananchi kuhusu uteuzi huo.

"Hii inatoa tafsiri kwamba CCM wanalindana katika uovu."Alisema iwapo Kamati Kuu (CC) imebaini kuwepo kwa mapungufu na kuona haja ya kuundwa kwa timu hiyo, basi wangeteuliwa watu wengine kwa vile Chenge amekuwa na mahusiano ya karibu na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, ambaye ni mmoja wa watu wanaotuhumiwa katika mkataba huo.

Naye Dk Mohamed Bakari wa Idara ya Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam, alisema hategemei kwamba kamati hiyo italeta matunda ambayo jamii inayasubiri ya kujua chanzo cha sakata hilo la mkataba wa ujenzi wa jengo la UVCCM lililoibuliwa kwa mara ya kwanza hadharani na mwanasiasa kinda wa CCM, Nape Nnauye.

"Hata jamii itashangaa kusikia kwamba mtuhumiwa wa ufisadi anachaguliwa katika kamati ya kuchunguza ufisadi uliojitokeza katika mkataba ujenzi wa jengo la UVCCM," alisema msomi huyo.

Msomaji mwingine wa gazeti la Mwananchi aliyeandika maoni yake kupitia mtandao, alisema: Watanzania hawajasahau jinsi alivyoawaingiza kwenye
mikataba tata wakati akiwa mwanasheria mkuu wa serikali na waziri.

"Wasiwasi wangu ni kuwa huyu bwana ni mtuhumiwa mkubwa wa kashfa mbalimbali za ufisadi hapa nchini na nje ya nchi (Uingereza). Hivi kwa akili za kawaida zisizohitaji kuwa angalau na digrii, huyu bwana anaweza kumtendea haki kijana huyu mzalendo."

Lakini Chenge, ambaye wakati akijibu tuhuma za kuwa na akaunti ya Sh 1bilioni nchini Uingereza alitumia neno vijisenti kuelezea mamilioni hayo, alionekana kukerwa na jinsi umma ulivyopokea taarifa hiyo kinyume na maana iliyokusudiwa.

"Watanzania wanapaswa kufikiri mambo yenye tija na si ya vijiweni na majungu," alisema 'Bilionea' Chenge alipoongea na Mwananchi akiwa mjini Dodoma.

"Wakati mwingine, sitaki kujibizana na watu hao ambao wanapenda kutumia nguvu nyingi na akili kujadili mambo ambayo hayana tija, hebu ninyi watu wa vyombo vya habari jaribuni kuwaelimisha waelewe."

"Kamati inapitia na kurekebisha mkataba huo kwa manufaa ya pande zote mbili."

Chenge alifafanua kwamba ni vema watu kabla ya kuzungumza wakafahamu kwanza adidu za rejea walizopewa si kuchunguza mkataba bali kuupitia na kuangalia marekebisho ili uwe na faida kwa pande zote mbili.

"Sisi hatuchunguzi, tunapitia na kuangalia namna ya kufanya marekebisho ili pande zote mbili zinufaike" alisema.

"Hebu watu wawe wanafikiri mambo ya maendeleo. Kuna baadhi ya Watanzania wanatumia akili na nguvu nyingi kujadili mambo ya mitaani na taarifa za vijiweni."

Lakini baadaye aligeuka na kusema:
"Nitahakikisha nalinda heshima yangu na chama; tutahakikisha mkataba unakuwa na manufaa kwa pande zote mbili."

Mjumbe mwingine kwenye timu hiyo, Dk. Abdallah Kigoda alisema wanatarajia kutoa majibu mazuri yatakayomridhisha kila mmoja ndani ya umoja huo.

"Tunatarajia kuufanyia kazi na kufanya vema kwa maslahi ya vijana wa umoja huo," alisema Dk. kigoda.

Dk. Kigoda alifafanua kuwa wataufanyia kazi mkataba huo mapema iwezekanavyo na kutoa majibu kwa haraka zaidi, na kwamba hilo linatokana na suala hilo kuzungumzwa nchi zima.

Miongoni mwa kasoro ambazo CC iliziona kwenye mkataba huo ni mkataba huo kushindwa kubainisha madaraka ya bodi za wakurugenzi wa pande zote mbili, kutobainisha njia za kutatua migogoro iwapo itaibuka na kutoweka wazi uendeshaji wa jengo hilo.

Nape, ambaye anawania uenyekiti wa UV-CCM, alivuliwa uanachama wa jumuiya hiyo baada ya kuukosoa mkataba huo akisema kuwa haukupitishwa na vikao halali, hauna maslahi kwa jumuiya hiyo na kwamba unanuka rushwa, maneno yalitafsiriwa na Baraza Kuu la umoja kuwa ni uongo na ukosefu wa nidhamu.

Baraza hilo liliamua kumvua uanachama na kupendekeza kwa CC kuwa avuliwe nyadhifa zake zote alizonazo ndani ya CCM. Nape, mtoto wa mwanasiasa maarufu wa zamani, Moses Nnauye, ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na afisa kwenye kurugenzi ya mambo ya nje katika ofisi ndogo ya chama hicho iliyo jijini Dar es Salaam.

Lakini mapendekezo hayo pamoja na kigingi cha kumzuia asikate rufaa sehemu yoyote, ziligonga mwamba baada ya Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete kumpa ruhusa ya kukata rufaa na CC kukataa kuupitisha mkataba huo na kuurudisha ili ufanyiwe kazi zaidi.

Halmashauri Kuu ya CCM, pia ilikataa pendekezo la kumvua nyadhifa zake na kutangaza kuendelea kumtambua kama mwanachama na mjumbe wa NRC.

Maamuzi hayo ya NEC kuendelea kutambua Nnauye na kumpa nafasi ya kukata rufaa, pia imemuweka katika nafasi nzuri ya kuweza kupigania kiti cha uenyekiti wa UV-CCM, ambacho alikikosa katika uchaguzi uliopita aliposhindwa na mwenyekiti wa sasa, Emmanuel Nchimbi.
 
Chanzo muhimu kiko Mlimani City kwa lengo la kujiburudisha. Mbele ya chanzo chetu hicho amekaa Nape Mnauye akiwa na watu wengine wawili katika meza moja. Watu hawa wanasherehekea kwa dhahiri kabisa. Kila tukio libaonyesha kumpongeza Nape. Ni imani yangu kuwa Nape ameshinda Zengwe kubwa alilokuwa amewekewa CCM. Tutawapa habari zaidi hasa tutakapofanikiwa kupata majina ya drinking mates wa Nape hapa.
 
Mmoja kati ya wanaokunywa naye hadi sasa ni Constantine Mwaligo.
 
Unajua Obama bwana kiboko sana, eti majuzi umesikia alivyosema kuwa a pig ni a pig tu hata ukimpaka lipstick bado ni a pig tu, bwha! ha! ha! ha! ha! ha!,

Obama bwana, noma tupu! a piiiiig bwana ! Naona ishakuwa noma, oooh ishakuwa soo na uchaguzi!maana Makeni sasa anakuja na lipstick kama a pig!
 
Unajua Obama bwana kiboko sana, eti majuzi umesikia alivyosema kuwa a pig ni a pig tu hata ukimpaka lipstick bado ni a pig tu, bwha! ha! ha! ha! ha! ha!,

Obama bwana, noma tupu! a piiiiig!
Hahahah!! Lakini alikuwa anaongelea Uchumi wa Bush na McCain kwamba ni sawaa, ila vyombo vya habari haviweki maneno kabla ya hilo neno na McCain kaweeka tangazo tayarii.
 
Mkuu FMES,

mhh naona kama hii ya obama inatoa message tofauti na aliyoifikiria mkuu Lusajo. Nahisi niko ukurasa mmoja na wewe! sijui lakini mtazamo wangu labda!
 
mhh naona kama hii ya obama inatoa message tofauti na aliyoifikiria mkuu Lusajo. Nahisi niko ukurasa mmoja na wewe! sijui lakini mtazamo wangu labda!

Hapana mkuu, tupo ukurasa mmoja unajua sometimes ni kazi na dawa na blogging ni burudani pia.
 
Labda ni washikaji zake wa miaka nenda miaka rudi wanapata moja baridi moja moto na nyama choma wala hasherehekei maana anajua bado ana safari ndefu katika kupambana na mafisadi ndani ya CCM
 
Hongera sana bwana mdogo nape, lakini kumbuka safari bado ni ndefu angalia usije ukabweteka.
 
Kwa maoni yangu safari bado, ndio kwanza kafanya booking, tiketi hana wala safari bado. Hakuna cha kurehekea ila 'a single battle' won. Bado kazi iko mbele na mwambieni kuwa katika kunyoosha CCM, wapo wengi tu nyuma yake. Aanze tu safari.
 
kwa CCM sikutegemea lingine out of hilo.Corrupt leaders,Corrupt ideas,corrupt minds,Corrupt decisions.WE NEED ANOTHER CCM NOT OF KINGUNGE,NCHIMBI,MAKAMBA AND OTHER OLD KAMANDAS
 
kuna nini cha kusherekea? he is just a fisadi in the making like others
 
Cha muhimu ni kwamba amesema akasikika, na nyuma yake tuko wananchi wengi sana wenye uchungu na taifa letu,

Now let all of us be mafisadis in the making kwa kulilia taifa letu, kutoka mikononi mwa mafisadi!

Bravo Nape!
 
Maisha yangu yote ya uanachama wa CCM, sikujua kuwa Chenge ni mwenyekiti wa kamati ya maadili ya CCM, maana sijawahi kuwasikia CCM wakilisema hilo hadharani,

Mungu amlinde Nape maana bila kasheshe lake wengine tusingelijua hayo! What an eye opener!
 
Yaleyale ya Mbowe kusherehekea kifo cha Wangwe! Yaani mtu akikaa anajibarizi basi anasherehekea!
 
Habari ndio hiyo...


1-1.jpg
 
Back
Top Bottom