Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Vijana CCM wataka Lowassa, Chenge waachie Ubunge

*Pia wamo Karamagi na Dkt. Msabaha


Na Mashaka Mhando,Tanga

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoani Tanga umewataka viongozi wote wanaotuhumiwa kuhusika kwa namna yoyote na vitendo vya ufisadi kuachia mara moja nyadhifa zao za uongozi ndani ya chama ili kukinusuru na chuki dhidi ya umma.

Viongozi hao wametakiwa kukaa na kutafakari kama kweli bado wana uwezo wa kusimama majukwaani na kunadi sera na Ilani ya chama hicho mbele ya umma baada ya kukumbwa na kashfa hizo.

Akitoa tamko la Kamati ya Utekelezaji ya Umoja huo Mkoa wa Tanga kwa waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa UVCCM mkoani hapa, Bw. Emanuel Kiondo, alisema viongozi walioachia nyadhifa zao serikalini hivi karibuni kutokana na kashfa za ufisadi, wameendelea kubaki na madaraka makubwa ndani ya chama hicho jambo ambalo ni hatari katika kujenga imani ya umma.

Bw. Kiondo ambaye pia ni Katibu wa Idara ya Uenezi na Siasa Mkoa wa Tanga, alisema viongozi hao hawana budi kutafakari upya na kupime kama bado wanaheshima ya kusimama mbele ya jamii na kunadi sera bora na Ilani ya CCM na kama hawataaminiwa, wajiondoe haraka.

"Kuachia ofisi za serikali hakutoshi, bado wengine ni wajumbe wa Kamati Kuu, Halmashauri Kuu, wabunge na hata Kamati ya Madili na hizo zote ni ofisi za umma...Kwa kuwa CCM ndicho chama kikongwe na wananchi wengi wanakitegemea kutoa mwongozo na mwelekeo wa Tanzania ya leo na ijayo, tunawaomba wote waliojiuzulu nafasi zao serikalini wafanye hivyo kwenye chama ili kukinusuru kusemwa vibaya," alisema Bw. Kiondo.

Mwenyekiti huyo huku akinukuu mifano mingi kutoka katika vitabu mbalimbali vya marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Dkt. Ibrahim Kaduma, alisema viongozi hao kwa kuziachia nafasi zao za uongozi ndani ya chama kutasaidia kupunguza kilio cha wanachama, wapenzi na mashabiki wa chama hicho.

Alisema wakijiondoa watakuwa wamekubali kujisafisha na kukinusuru chama chao na wakati huo huo kumuenzi Mwalimu Nyerere katika kutoa maamuzi mazito likimwemo la kukubali kukosolewa na kujikosoa.

Miongoni mwa viongozi waliowajibika hivi karibuni kutokana na kashfa mbalimbali ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa aliyeachia wadhifa huo kwa kashfa ya Richmond sambamba na mawaziri wengine wawili, Bw. Mustafa Karamagi aliyekuwa Waziri wa Madini na Nishati na Dkt. Ibrahim Msabaha aliyekuwa Waziri wa Afrika Masharki.

Waziri wa Miundombinu, Bw. Andrew Chenge pia alijizulu kutokana na kashfa ya ununuzi wa rada iliyomhusisha na kutunza mabilioni ya fedha kwenye akaunti yake nje ya nchi.

Katika hatua nyingine, UVCCM Tanga imekitaka Chama cha Wananchi (CUF) kukubali kwenda kwa wananchi kupata maoni yao juu ya kumaliza mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar na kukaa meza moja na CCM kupata ufumbuzi wa tatizo hilo.

"Kitendo cha CUF kukataa kwenda kwa wananchi ili watoe maoni yao si cha kiungwana hata kidogo, wanapingana na jina la chama chenyewe, 'Chama cha Wananchi' halafu wanaogopa kwenda kwa wananchi hao hao," alisema Bw. Kiondo.

Bw. Kiondo alisema UVCCM inapinga kauli ya CUF kutaka Rais Jakaya Kikwete naye ajiuzulu kwa tuhuma za ufisadi na kukariri maneno ya Mwalimu Nyerere kuwa "Kuwajibika kuna ngazi zake, hatuwezi kusema mtendaji akifanya kosa Rais ajiuzulu, hapana aliyetenda kosa likathibitika awajibike mwenyewe."

Aliwataka Watanzania kutambua kwamba CCM ni kama familia kubwa wanamozaliwa watu wenye hekima , waadilifu, vilema, mataahira, majambazi, vichaa na wengine hivyo si busara watu kuisakama familia hiyo kwa kuwepo jambazi moja wakati kuna wengi wenye hekima zao.

Alitetea kuwa CCM imekuwa na viongozi wengi wenye busara na uadilifu mkubwa na kuongeza kuwa chama hicho ni kikubwa ndio maana Rais Kikwete hivi karibuni alikaririwa akisema umefika wakati wa kutenganisha siasa na biashara.


majira

As if they are serious vile! Hawa si ndio waliotoa kauli za kebehi baada ya ufisadi kuibuliwa wakisema kuwa ni uwongo mtupu na hila za upinzani kujitafutia umaarufu? Wakamwambie kwanza boss wao Amos Makala aombe radhi kwa Dr Slaa kwa maneno yake ya dhihaka baada ya list of shame kumwaga hadharani. Na hawa CCM Tanga si ndio waliandamana kabisa? hebu mwenye kumbukumbu azimwage hapa.

Yangu macho, labda wamrudia Allah

Asha
 
Nawaunga mkono hawa mafisadi sio waachie uanachama. Wafukuzwe kabisa, na wakamatwe na kufunguliwa mshitaka. Lakini kituko ni kuwa sasa hivi utasikia wanaanza kunyoosheana vidole vya aliyewatuma vijana hawa
 
Jamani nasi tumepachikwan jina la "wanasema tu hawana lolote,waoga wa kufuatilia mambo...wao ni maneno matupu...nani wa kumvalisha paka kengele...nawaambieni wadau wote JF ...labda shinikizoo litoke kwa wahisani na wachangia bajeti ndio mtaona angalau changes...au hata kubanwa kidogoo......kwa mafisadi wetu hawa..la sivyo.......no way...maneno matupu tuuu
 
CCM youth now call on 'tainted' member to go

By Tom Mosoba, Dar and Burhani Yakub, Tanga
THE CITIZEN

The ruling Chama Cha Mapinduzi's youth, UVCCM, wing wants all top party officials implicated in corruption scandals to relinquish their leadership positions both within and outside the party.

In a new twist to the corruption allegations in which a number of influential CCM members have featured prominently, UVCCM officials in Tanga Region yesterday became the first to publicly demand the resignation of such members.

The call by the CCM youth came as the Opposition Chadema also issued a statement castigating Prime Minister Mizengo Pinda, whom it accused of allegedly attempting to shield CCM and its leaders from corruption accusations.

Chadema said CCM and its government could not separate the overlapping roles of their officials implicated in corrupt deals as they were the same.

In Tanga, UVCCM regional chairman Emmanuel Kiondo said it was time that all CCM members linked to corruption stepped down immediately for the sake of redeeming the image of the ruling party.

These leaders still hold powerful positions in the party even though they have relinquished their posts in the Government. Many of them still sit in the National Executive Committee and Central Committee and are members of parliament and the party's ethics committee, he said.

He was addressing reporters in Tanga after chairing the region's UVCCM executive committee meeting that issued the resignation call.

Without mentioning names, Mr Kiondo said apart from giving up their party positions, the suspects should also consider resigning as MPs.

We have decided to make this call because we realise that those who have been forced out of government still continue to enjoy privileges as top leaders in CCM he said while flanked by UVCCM regional secretary Mwita Waitara.

Mr Kiondo said people mentioned in corruption scandals should reconsider whether clinging to their posts in the party would help to build the party or destroy it

We ask them to think hard with a view to establishing whether they still command the respect of the society. They should see if they can defend and sell the party's manifesto and if they still retain the respect of the nation, he said..


Mr Kiondo added that they were not forcing the corruption suspects out of office, but were merely appealing for them to make sensible decisions so that CCM and its government are not scorned in public.

Even though the Tanga officials avoided mentioning names, several influential CCM members have resigned from the Government in recent months after being implicated in corruption.

They are Mr Edward Lowassa, who resigned as Prime Minister in February, and Mr Nazir Karamagi and Dr Ibrahim Msabaha, who quit the Cabinet after all were adversely mention in a report that detailed the irregular awarding of a multibillion-shilling tender to generate emergency electricity to Richmond Development Company in 2006.

Mr Andrew Chenge resigned as Infrastructure Development minister last month after it was reported that he operates an offshore account with more than a million dollars (Sh1.2 billion).

The account was reportedly discovered by the UK's Serious Fraud Office, which is investigating the sale of an overpriced radar top Tanzania in 2002. Tanzanian officials are said to have pocketed $12 million in kickbacks in the $70 million deal.

Messrs Lowassa, Karamagi and Chenge all sit in CCM's national executive committee. Mr Chenge also doubles as a member of the party's ethics committee.

Former President Benjamin Mkapa, who retired in 2005, is also facing accusations of abuse of office. He still sits in the party's Central Committee.

Chadema said in a statement signed by information secretary David Kafulila that people who had been directly linked to corruption were still in charge in CCM.

Mr Kafulila said it was unacceptable that Mr Pinda was trying to stop the public from demanding a corrupt-free country by separating CCM officials and their roles as policymakers in the Government.

Mr Kafulila said the current situation where influential CCM members had been implicated in corruption reflected the nature of its government, adding that all those involved should be forced out of public posts they were still holding.

The party said it was saddened by remarks attributed to Mr Pinda last Friday when he reportedly appealed to the public not to blame CCM or its government for corrupt deals entered into by individual members.

Similar sentiments have in the past been expressed by CCM secretary general Yusuf Makamba who said people in the party's ranks implicated in corruption should be treated as individuals and not be used to tarnish the party's image.

However, Chadema reiterated yesterday that it was agitating for the removal of CCM from power because its officials are driving the country into the ground through corruption.

The ruling party could not boast of clean leadership if the Prime Minister had confessed the Government was facing an uphill task fighting unnamed individuals who are said to have been behind the EPA scandal in which Sh133 billion was looted from public coffers, the party added.
 
Hawa watoto wa Tanga ujasiri wa kusema mafisadi waachie ubunge wameupata wapi?
Waziri mkuu ameshakiri hao ni watu hatari sana tena wana mapesa mengi kwa hiyo si rahisi kuwakamata.

Siku chache tu mtasikia wanafuta kauli hiyo kauli hadharani.

Kama wanayo nia ya dhati waandae hayo maandamano nchi nzima kushinikiza mafisadi wajiuzulu
 
Moto CCM!

2008-05-06 16:12:27
Na Sharon Sauwa, Mikocheni

Moto wa chini kwa chini unazidi kufukuta ndani ya Chama cha Mapinduzi, CCM kufuatia kuibuka kwa makundi yenye misimamo tofauti juu ya nini kifanyike baada ya baadhi ya wanachama wake kuhusishwa na kashfa ya ufisadi.

Taarifa ndani ya chama hicho zinadai kuwa sakata hilo limeleta mgawanyiko mkubwa.

Alipoulizwa juu ya msimamo wa chama kuhusiana na tuhuma za ufisadi zinazowakabili baadhi ya wanachama wake vigogo, Katibu Mwenezi wa CCM, Kapteni Mstaafu John Chiligati, amesema wao hufanya kazi zao kwa mujibu wa kanuni na taratibu za chama.

Akasema kwa sababu hiyo, watashughulikia mambo hayo kwa kufuata kanuni hizo za chama, ambazo zimeainisha maadili yanayopaswa kufuatwa na hatua za kuchukua pale inapobidi kufanya hivyo.

``Hawa wanaotuhumiwa si wanachunguzwa? Tusubiri, kama ikithibitika... chama kina maadili yake. Kitachukua hatua kulingana na taarifa za uchunguzi,`` akasema Katibu huyo.

Aidha Kapteni Chiligati ametoa ufafanuzi kuhusiana na tamko lililotolewa na Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) mkoani Tanga, ambalo liliwataka vigogo wote waliokumbwa na kashfa na kujiuzulu nafasi zao serikalini, kuachia pia nafasi nyingine za uongozi ndani ya chama ili kukinusuru na chuki zinazoweza kujengeka kwa umma.

Amesema kwa vile watu hao bado wanachunguzwa, ni vema wanachama wakasubiri matokeo ya uchunguzi.

Tamko la UVCCM Tanga lilitolewa na Mwenyekiti wao, ambaye pia ni Katibu wa Idara ya Uenezi na Siasa mkoani humo, Bw. Emmanuel Kiondo.

Nafasi ambazo UVCCM Tanga walitaka ziachiwe na watuhumiwa ni pamoja na zile za ujumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya chama, ubunge na uongozi ndani ya kamati mbalimbali za chama ikiwemo ya maadili.


SOURCE: Alasiri
 
Huyu kijana naona kafirisika kisiasa hana hata chakuongea, mimi nilifikiri ujinga wao wanauleta hapa JF tu ambako wanaficha ID zao kumbe wanaweza kuupeleka hata ambako ID zao zinaonekana, huyu hana tofauti na dogo mmoja aliyekuwa anatukana watu matusi ya nguoni hapa JF.

Wezako wamekuja na evidance badala ya kupayuka lete zako pia watu waamue nani ansema ukweli au nani anapotosha watu, anatangaza vita yeye kama nani, au anfikiri kuwa CCM ndo ngao ya yeye kutopata kibano kama vita inatokea. Huyu unaweza kukuta hata vijisenti vya mafisadi hapati hata kidogo lakini kwa kuwa kanyweshwa maji ya bendera hata kama anaona CCM imekosea anapayuka.
 
dush ....." kama noma na iwe noma"! ccm inajishushia hadhi vibaya sana, mpaka inasikitisha.

hizi siasa za mabavu za dhahiri ndani ya ccm ndio sera mpya ya chama au?
 
Huyu bwana mdogo ni wa Singida namfahamu ufahamu wake mdogo sana na amekuwa na vile vikundi vya chipukizi wa ccm kwa muda mrefu sana! Amekuwa hapo na baadaye UVCCM akitegemea madaraka kupitia hapo alitegemea sana angepata something baada ya JK kuchukua madaraka kwa vile anafahamiana na baba yake alipokuwa katibu wa mkoa enzi hizo lakini ikaw hola... Capacity yake ya kuchanganua mambo ni ndogo na sijui hapo SUA alikuwaje hebu mwnye data amwage hapa JF
 
Another Vanity and empty talkings on UVCCM!

Kule TANGA mlikuwa na tone nyingine na DAR napo mmetoka na tone nyingine.Which is which?Nani msemaji wa ako ka umoja wenu mpaka mnaropoka na kutukana?Usalama wa Taifa hautawalinda hadi chooni!Kuna msalama mwingine Kafa kule Tarime.Semeni mambo ya msingi ya kuwaletea watu maendeleo siyo kutisha kwa kuwa sisiem ina dola.Waliowatuma wamebugi step.Wananchi tunaelewa pumba na mchele.
Hamna Dira yeyote kaeni pembeni mmeshindwa kuongoz nchi hii.

Jifunzeni propaganda ya MzeeTHABIT KOMBO,Mzee P.Sozigwa n.k.


Huu si wakati wa noma na iwe noma.Washaurini baba zenu hao wakamilishe mwafaka waache vitisho.Ujinga na upuuzi huu hauvumiliki.
 
Tunaomba JESHI la PILISI limkamate huyu kiongozi wa vijana UVCCM na umfungulie kesi mala moja kwa kosa la uchochozi na matusi vinginenevyo serikali hatuielewi...Hivi kwa nn mnachagua viongozi wavuta bangi ??kwa mtazamo huu CCM hakuna kitu kabisa.Lazima tujiulize mala kadhaa labda huyu kijana katumwa na uongozi wake wajuu kuwatisha CUF.
Tunamashaka vinginevyo huyu jamaa anaupungufu wa akili watu kila kukicha tunatafuta amani yeye anatangaza vita hii ni aibu kwa UVCCM na CCM kwa ujumla.
 
Isaack kasema wakati wamesha tenda .S tayari wameanza kamatakamata huu ni ujumbe fika so watanzania kaeni macho sana .
 
“CUF ni mufilisi wa mawazo na wamejawa na madikteta wasiopenda kuona maendeleo ya Zanzibar,” alisema Isack

Znz kuna maendeleo gani ya ajabu sana yaliyoletwa na CCM, aje kifua mbele na kuyasema hapa
 
“Nguvu tunazo, uwezo upo, na kuanzia sasa kama ‘noma na iwe noma’, tutapamabana na wale wote wenye nia ya kuwachafua viongozi wetu,” alisema Isack.

Hii ni reflection ya uongozi wa juu wa CCM, hichi ndicho kiburi cha CCM kinacho wafanya waibe, wawanyanyase wanainchi an kuwafanyia kila aina ya uinovu

Huu ni ulevi wa hali ya juu, kwa maneno haya hiyu hajui kabisa nani ni dicteta kati ya CCM na CUF
 
kwani msemaji mkuu wa CCM ni nani maana nao kila mtu CCM anaongelea swala la znz na anakuja na tamko lake
 
"Lipumba inaonekana ni Profesa wa mitishamba kwani amekuwa akiendeshwa na Seif ambaye ana nia ya madaraka," alisema Isack.

Chama kimekosa watu wa kuzungumza kwa sasa,siamini haya maneno ya naweza kutoka kwa mtu ambaye anaitwa kiongozi.Busara iko wapi kwa sasa.

Mie nahisi kuna haja ya kuwapa semina elekezi jinsi ya uongozi,kuna mtu ana profile ya huyu kijana??amenikitisha sana kwa maneno yake.Na hata kama ametumwa na mtu basi yeye ni Mjinga,sababu katumwa jambo la kijinga na yeye kalisema
 
Back
Top Bottom