Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Hoja hujibiwa kwa hoja:-

1.
Quote: Mtanzania

Ben,

Nakubaliana na baadhi uliyoandika hapo juu ila ni muhimu mno kufuata sheria/taratibu na pia hakuna sababu ya kubadili sheria kwa ajili ya mtu mmoja. Nape alikuwa na miaka zaidi ya mitano ya kuipinga hiyo kanuni mbovu na hakufanya hivyo. Kama ni kweli ana umri zaidi ya unaotakiwa ningelikuwa mimi Mwenyekiti wa CCM ningelimpiga stop!

Sheria ni sheria wakuu hata kama inakukaba mwenyewe bado ni sheria na inabidi ifuatwe. Ila kwa jinsi CCM walivyo wanaweza kubadili na kumwacha Nape agombee. Nape mwenyewe kama anang'ang'ania kuwa Mwenyekiti pamoja na kujua hana sifa, inaonyesha tuna aina gani za wanasiasa Tanzania. Ma opportunists ambao wako tayari kusema lolote ili wachaguliwe. Binafsi siwataki wanasiasa wa namna hiyo.

Maneno ya kale ka mama ka McCain yamenigusa sana hata kama siwapendi Republicans. Aliongea kitu karibu na haya maneno "some use change to further their careers while others use their careers to bring change"

Siasa za slogans zimepitwa na wakati, vijana mnaotaka kuingia kwenye siasa lazima muamini na kutenda mnayohubiri. Yale ya slogan nzito kama JK huku matendo sifuri hayatufai kabisa. Nape kama umri umepita basi asubiri 2010 na awe cheche kwenye ubunge.

Quote: Sober

Wakuu,

1. Kuhusu suala la umri kwenye uchaguzi wa UVCCM, utakuta kanuni zenyewe za UVCCM zinajichanganya. Na, hii ni kwa sababu kipengele cha umri kiliingizwa kimizengwe.

2.[*]Kanuni zinaainisha umri ambao mwanachama wa UVCCM atakua ni kijana wa miaka 15 mpaka 35.

3.[*]Kanuni hizohizo zinasema wakati wa uchaguzi, kila mwanachama atakua na haki ya kuchagua au kugombea nafasi ya uongozi wa UVCCM kama atakua na sifa.

4.[*]Halafu kanuni hizohizo tena zinakuja kusema, ili kugombea nafasi ya uongozi mwanachama unatakiwa usiwe umezidi umri wa miaka 30. Tayari haki mojawapo iliyoyajwa na kanuni za hapo juu imekiukwa.

5. Sasa hapa unaona kuna kundi kubwa sana(30-35yrs) ambao lina sifa za kupiga kura lakini haliwezi kugombea uongozi.

6. Kwa akili ya kawaida tu utaona hizi kanuni zina walakini. Hii ndio mifano ya kanuni zinazochomekwa kwa maslahi ya mtu mmojammoja badala ya kutizama maslahi ya chama kwa ujumla.

Kiko wapi chama cha Mwalimu???....
 
Hoja hujibiwa kwa hoja, sio viroja na kubadili majina, hizi hoja chini ni kwa manufaa ya taifa sio fadhila za Mnauye (RIP), aliyekuwa kiongozi muadilifu na kuishia kutokuwa hata na nyumba yake binafsi ya kuishi, kwamba hata alipofariki ilibidi msiba ukafanyike kwa ndugu ye Mzee Makamba,
hoja kama hizi chini zijibiwe kwa hoja, kwa sababu hazina uhusiano wowote na hizo fadhila ambazo sijui alizitoaje akiwa hana kitu wala sio mfisadi, au ndio malipo ya fadhila za Nchimbi, kutuingiza bungeni wakati wa kikao?:-

1. Katika hoja ya Nape, mbali ya Lowassa, wanasiasa wengine anaowahusisha katika mkataba huo ni Nchimbi, na aliyekuwa Katibu Mkuu wa UVCCM, ambaye sasa ni Mweka Hazina wa CCM, Amos Makalla.

2. Katika hoja zake, Nape amenukuliwa akisema kwamba mkataba huo ulipitishwa kinyemela hata kabla haujafikishwa kwenye vikao vya juu vya CCM, kwa maana ya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho ili kupata baraka za mwisho.

3. Vipengele vingine ambavyo Nape analalamikia ni kuhusu uhai wake, kwani kimojawapo kinasema mwekezaji ataendesha mradi huo milele, huku jumuiya hiyo ikipata asilimia 25 na mwekezaji asilimia 75.

4. Kasoro nyingine anazozitaja Nape katika tuhuma hizo ni pamoja na ile ya kukiukwa Sheria ya Ardhi (Kiwanja), kuhamishwa kwa wabia kabla ya shughuli yoyote ya ujenzi kuanza.

5. Utaratibu ni kwamba, kabla hatua hiyo haijachukuliwa, sharti Kabidhi Wasihi Mkuu wa Serikali, atoe kibali kwa ajili ya uhamisho wa aina hiyo.

6. Mkataba wa mradi huo unaosomeka kwa kichwa kisemacho ‘Development Agreement', ulisainiwa Januari 2 mwaka 2007 kati ya UVCCM na makampuni mawili ya M. M. Integrated Steel Mills (MMISML) na Estim Construction Company Limited (ECCL).

7. Mkataba huo pia hauelezi kiasi cha uwekezaji kutoka kwa wabia, ambacho kinaweza kutumika kuelezea mgawo wa asilimia 25, ambayo inadaiwa UVCCM watachukua.

8. Aidha, mkataba huo hauna ufafanuzi wa matumizi na mapato hatua kwa hatua, jambo ambalo linaonyesha kutokuwa makini au kuashiria ghiliba katika mahusiano ya wabia.

9. Vilevile mkataba hauelezi iwapo ubia ni wa miliki ya pamoja au itaundwa kampuni tofauti ya kuendesha kitega uchumi.
 
FMES
Sijakupata sawasawa ,ina maana Mzee Mnauye(RIP)/Nape wanauhusiano wa kindugu na Katibu wa CCM Mzee Makamba?
 
Ben,

Nakubaliana na baadhi uliyoandika hapo juu ila ni muhimu mno kufuata sheria/taratibu na pia hakuna sababu ya kubadili sheria kwa ajili ya mtu mmoja.

Sheria ni sheria wakuu hata kama inakukaba mwenyewe bado ni sheria na inabidi ifuatwe.

Mtanzania nakubaliana na wewe kuhusu umuhimu wa kufuata na kuzingatia sheria, with a caveat. Caveat yangu hapa ni kwamba hiyo sheria inabidi izingatia haki. Kwa sababu ukisema sheria tu, kuna sheria zingine zimetungwa ili kupokonya haki za msingi za kundi la watu fulani na kupendelea kundi lingine.

Sasa hii kanuni waliyojiwekea wana UVCCM ni wazi kwamba inapokonya haki za baadhi ya wanachama wa UVCCM kama Nape. Sifa ya msingi ya kugombea uongozi ni mtu awe na sifa za kuwa mwanachama wa taasisi husika. Madamu Nape ana sifa zote za uanachama wa UVCCM ana wajibu wa kutekeleza malengo ya UVCCM na ana haki ya kufaidi matunda yake, ikiwemo kugombea uongozi. Kwa hiyo utaona kwamba ile kanuni waliojitungia ya kusema mtu akivuka miaka 30 asigombee inanyang'anya haki za msingi za mwanachama, na hivyo inapaswa sio tu kukataliwa lakini pia kudharauliwa.

Hata hivyo tatizo langu katika jambo hili lipo kwa Nape mwenyewe. Mambo ambayo anayasimamia Nape yanakwenda kinyume na maadili ya msingi ya CCM, na kwa hivyo yanamtenga moja kwa moja na chama hicho na ndio maana anapata taabu sana. Yeye, kwa mfano, anazomea uingiaji wa ovyo au tusema deal la mkataba wa jengo la UVCCM. Lakini sote tunafahamu kwamba ujanjaujanja, short cut, kupindisha mambo, ubabaishaji ndio hasa sifa za msingi za CCM ya leo, na yeyote anayepingana nazo anakuwa anaipinga CCM moja kwa moja. Nape ana mambo mawili ya kuchagua: Ama atoke CCM ili aungane na wapiganaji wengine katika mapambano ambayo yanaendelea au aendelee kubaki CCM lakini akubali yaishe na afuate kanuni za chama hicho. Nape hawezi kuuma na kupuliza. Ni lazima aamue ama kuuma au kupuliza. Kwa kifupi ni kwamba Nape aache unafiki katika hili maana hautamsaidia.

Kama Nape ataendelea kubali CCM na huku akiendelea kubwabwaja kuhusu madhira ya chama chake hiki, tutajua kuwa anayoyasema hayatokeni moyoni bali anaongea kama mtaji wa kujipatia sifa ili afanikishe azima yake ya kuwa mwenyekiti wa UVCCM.
 
Kitila,

Ni kweli kabisa lazima hiyo kanuni iwe na haki. Lakini kama kanuni ina miaka zaidi ya mitano, naona Nape angeipinga kwanza kabla hata ya kugombea hiyo nafasi ya kuwa Mwenyekiti.

Suala la kwamba ana sifa zote nafikiri tutakuwa tunakosea maana kuna sheria nyingi za namna hiyo. Kwa mfano ukiwa chini ya miaka 40 huwezi kugombea kuwa rais wa Tanzania wakati watu kama hao wana haki zingine zote. Hivyo hivyo kwenye ubunge kuna sheria kama hiyo (siijui vizuri) nadhani unatakiwa uwe na miaka kuanzia 21.

Pia suala la kwamba kwasababu viongozi wa CCM ni wabovu basi watu safi hawawezi kufanya kazi ndani ya CCM nafikiri sio sahihi. Tukiamini hivyo tutaishia kuwafanya watu safi wasishiriki kwenye siasa za Tanzania. Wakati wengi tunaamini viongozi wa CCM sio safi lakini
pia viongozi wa vyama na jumuia zingine ambazo tunajiunga nazo nao sio safi. Labda dawa kwa Tanzania ni kuruhusu wagombea huru. Vinginevyo kila mtu atabeba msalaba wake. Ni makosa kumlaani mtu kwasababu tu yuko CCM au CHADEMA na viongozi wao ni mafisadi.

Kama huyo mwanachama/kiongozi anaunga mkono viongozi kama hao, hapo tuna haki ya kumlaumu, vinginevyo tutakuwa tunawaonea bure watu ambao wanataka kufanya mambo ya maana kwenye jamii na njia pekee ni kuwa kwenye hivyo vyama/jumuia.

Mimi nitamhukumu mtu kwa matendo yake na wala sio by association.
 
sasa wameamua kumgeuzia kibao bwana mdogo, wanaenda kumjadili kwenye kamati ya Chenge
 
Habari kutoka ndani ya CCM zinaeleza kuwa, wanasiasa wanaounda kundi hili ambalo Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Vijana, Emmanuel Nchimbi, anatajwa kuwa mmoja wao, tayari wameshaanza kupanga mikakati ya kuhakikisha wanamuengua Nape katika mchuano huyo.

Hawatafanikiwa na hata wakifanikiwa, wajue itakuwa ni kitanzi kingine kwa CCM
Wana CCM hao ambao baadhi yao wamepata kufanya mahojiano na Tanzania Daima kwa nyakati tofauti, wamekuwa wakimuelezea Nape kuwa mwanasiasa mzushi na mtu anayetumiwa na kundi la wazee kadhaa wa ndani ya chama hicho wenye lengo la kuhakikisha wanawaengua watu wote walio karibu kisiasa na Rais Jakaya Kikwete, ambaye ndiye atakayekuwa mwenyekiti katika mchakato huu wa leo.

Hii ina malengo ya kumchonganisha Nape na Kikwete.

Habari ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka kwa watu wa kundi hili la pili zinaeleza kwamba, kikao cha leo cha Kamati Kuu kinatarajia kuridhia kupitishwa kwa mkataba huo pamoja na kuwapo kwa wana CCM wengi wanaomuunga mkono Nape katika hoja yake.

Na hii ndio mkakati wao na kwa bahati mbaya sana wameutangaza kabla ya utekelezaji ni sawa na wale waliotangaza Zitto amekufa kabla ya hata utekelezaji wake na hapo ndipo mambo yalipoharibika. Wametangaza Mkataba umepitishwa, wametangaza Nape anapelekwa Kamati ya Maadili ya Chama wakati ajenda ya mkataba na Nape hata haijajadiliwa. Kati ya Ajenda 19 zilijadiliwa tatu tu na ajenda ya UVCCM ni ya 19. Jina la Nape wala halikutajwa na mjumbe yeyote kwani ajenda kubwa iliyochukua muda hadi usiku ni ya Hali ya Kisiasa na ilimezwa na hoja ya Zanzibara.

Kwa sababu hiyo basi, iwapo kweli, Kamati Kuu itaridhia kupitishwa kwa mradi huo, upo uwezekano mkubwa kwamba, nafasi ya Nape katika mchuano wa kuwania uenyekiti wa UVCCM itakuwa shakani.

Huo ndio mkakati halisi wa Nchimbi na kundi lake. Wamepata muda wa kujiandaa tena na sasa wamekikoroka kikao cha UVCCM cha Jumapili kwa wajumbe kudanganywa kwamba Kamati Kuu ya CCM imekwishakuhukumu Nape.

Bila aibu Nchimbi anatoa habari ambazo hazijatokea. Hii ni hatari
 
sasa wameamua kumgeuzia kibao bwana mdogo, wanaenda kumjadili kwenye kamati ya Chenge
mwenyekiti wa hiyo kamati mwenyewe hana maadili, mnategemea nini? mwenyekiti wa tume ya maadili ya CCM ni chenge kwa wale ambao hawajui
 
mwenyekiti wa hiyo kamati mwenyewe hana maadili, mnategemea nini? mwenyekiti wa tume ya maadili ya CCM ni chenge kwa wale ambao hawajui

Hii inaonyesha 'wao' ni akina nani
 
Ukitaka kuingia msikitini lazima ukubali kuchukua udhu kabla na kutoingia na viatu au makubadhi msikitini kama huwezi jua huuwezi uislam!
 
Jamani mimi namtabiria mambo mabaya sana huyu mtoto! Alikurupuka, na mshauri wake inonekana ni mgeni kwenye siasa za nchi hii. Kamati yenyewe mwenyekiti Chenge! Aliye rafiki mkubwa wa Lowasa? Haya tutaona.....
 
Ni kweli kabisa lazima hiyo kanuni iwe na haki. Lakini kama kanuni ina miaka zaidi ya mitano, naona Nape angeipinga kwanza kabla hata ya kugombea hiyo nafasi ya kuwa Mwenyekiti.

Mkuu Mtanzania,

Hapa ndipo unapokosea sana, unaongea siasa za bongo kama vile majuu, wakati hapa ukweli wa UV-CCM uko wazi kuwa ni chama ambacho hakina kanuni wala sheria, isipokuiwa huwa zinapangwa na kubadilishwa as Nchimbi anavyotaka,

Wewe umeona tumeuweka mpaka mkataba wa jengo la vijana, jisni Nchimbi alivyikiuka mpaka sheria za jamhuri kuhusu mikataba kama aliyoifanya, ukiangalia record yake kuhusu ukweli ni suspect, sasa ni vipi tunaweza kumuamini sasa kwenye hili la sheria za UV-CCM, ambazo nazo zimekwua suspect kwa sababu yake?

I mean, Nape anawezaje kuwa mjinga kiasi hicho unachojaribu kuonyesha kwamba anajua sheria za UV-CCM, lakini anataka kuzipindisha kwa makusudi, yeye ni nani hasa mpaka afanikiwe hilo? Imefika wakati unahitaji kukubali kuwa UV-CCM, haina mpangilio wala muelekeo,

kwa sababu just imagine, kwamba kiongozi amechukua fomu kugombea nafasi ambayo ni very celar kuwa anazidi au hatimizi umri unaotakiwa, hivi hiyo form anairudisha wapi? Halafu kikao cha UV-CCM kilichompa E, mbona hakikugusa hilo la umri, lakini badala yake tumelisikia likiibuka mitaaani na wapambe wa Nchimbi?

Binafsi silielewi vizuri hili la umri, lakini as the Nchimbi's leadership record goes, sioni cha ajabu hapa, mkuu tunatakiwa kukemea uovu na uhuni uonendeshwa huko UV-CCM kwanza, ambacho ndio hasa chanzo cha haya matatizo ya umri na mikataba mibovu ya jengo, the ishu hapa ni bigger than umri na you should know better na hizi siasa za uenyekiti wa UV-CCM toka zilipoanzia mpaka zilipofikia leo! Kosa la Nape hapa ni lipi? Kama amechukua fomu na sheria za UV-CCM ziko clear hatuwezi kuwa hata na debate on this, lakini kuna some fo things huko haviko sawa na hii confusion inakwenda moja kwa moja mikononi mwa Nchimbi,

Mimi ninaifahamu hii kitu toka ikiwa TANU Youth League, magwanda ya kijani na nyeusi, nilikuwa mdogo sana enzi hizo vijana wa TANU wanawazuia kina dada kutovaa nguo fupi, chini ya viongozi wa vijana kina Marehemu Rajabu Diwani, RC Mustafa Songambele, na Rashid Kawawa, sijawahi kusikia UV-CCM imekumbw ana matatizo na mpaka kushuka thamani kwa jamii yetu as now, WHY? haya huyaoni ya hiki chama kutokuwa hata na thamani mbele ya jamii, lakini umeshikia bango Nape tu, WHY? Nape hawezi kuwa bigger than UV-CCM mpaka kufikia kuamini kuwa anaweza kubadili sheria zake, lakini pia hawezi kuwa that small kwamba asisimame na kuomba nafasi kama anatimiza masharti, kwa sababu kama hatimizi tusingekuwa hata na debate hapa!

What is the agenda mkuu?
 
Ukitaka kuingia msikitini lazima ukubali kuchukua udhu kabla na kutoingia na viatu au makubadhi msikitini kama huwezi jua huuwezi uislam!

Haya ni matusi mkuu kwa dini za watu, huwezi linganisha uhuni wa Nchimbi na sheria za Mungu wa Wa-Isilamu, think kabla ya kuandika mkuu jaribu kuheshimu dini zisizokuwa zako!

Mtetee Nchimbi kwa hoja, nimekuambia mara nyingi sana sio kwa viroja!
 
Kweli hii au ni usanii wa CCM tu?

CCM yagundua uchafu

na Kulwa Karedia
Tanzania Daima~Sauti ya Wa
tu

VIONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wamewatuma wanasheria kuchunguza utata wa kisheria uliojitokeza katika mkataba wa mradi wa ujenzi wa jengo la Makao Makuu la Umoja wa Vijana (UVCCM), lililopo jijini Dar es Salaam.

Taarifa za kufanyika kwa uchunguzi huo ambao matokeo yake yalitarajiwa kujadiliwa jana katika kikao cha Kamati Kuu ya CCM iliyokuwa ikikutana jijini Dar es Salaam, yalitangazwa mbele ya waandishi wa habari na Naibu Katibu Mkuu (Bara) wa chama hicho tawala, Kapteni George Mkuchika.

"Ni kweli tulipokea malalamiko kuhusiana na ujenzi wa jengo la UVCCM na sisi kama chama, tuliamua kuwatuma wanasheria wetu, wakachunguze upungufu uliopo na kazi hiyo wameifanya vizuri na majibu yake yatatolewa," alisema Mkuchika wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari.

Kwa mara ya kwanza taarifa za kuwapo kwa utata katika mkataba huo ziliibuliwa na kada wa chama hicho, Nape Nnauye, ambaye ni mmoja wa vijana wanaogombea nafasi nyeti ya mwenyekiti wa UVCCM, ambayo kihistoria imekuwa ikiibua ushindani mkali.

Kwa mara ya kwanza, Nape alitoa hoja yake hiyo saa chache tu baada ya kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo inayompa fursa mshindi kuwa mjumbe wa vikao vya kimaaamuzi vyenye nguvu kubwa ndani ya chama hicho tawala, Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).

Katika madai yake, Nape alimshutumu moja kwa moja Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa umoja huo, Edward Lowassa na viongozi wengine wa juu wa UVCCM kwa kuingia katika mkataba huo ambao alisema hauna masilahi yoyote kwa umoja huo.

Hadi tunakwenda mitamboni jana usiku, kulikuwa hakujapatikana taarifa rasmi kutoka ndani ya Kamati Kuu (CC), kuhusu suala hilo.

Mbali ya kuzungumzia suala la mradi huo, Mkuchika pia alizungumzia uchaguzi wa jumuiya za chama hicho, ambapo alisema kuanzia sasa, chama hicho kimepiga marufuku wagombea wake wa nafasi mbalimbali za uongozi katika jumuiya hizo kutoa takrima au bahasha kwa wajumbe wake.

"
Katika hali isiyotarajiwa, CCM makao makuu imeanza kupokea taarifa kwamba kuna baadhi ya wagombea wameanza kujishirikisha na mambo yanayoashiria rushwa, sasa tumesema ni marufuku kwa mgombea kuzunguka mikoani kabla ya kuteuliwa kuwania nafasi wanazotaka," alisema Mkuchika.

Alisema wapo wagombea wanaozunguka wilayani na mikoani na kujitangaza wakati hata majina yao hayajateuliwa na vikao husika vya chama.

Kapteni Mkuchika alisema watu hao wamekuwa wakikutana na baadhi ya wajumbe na kufanya mikutano na matukio mbalimbali yakiwemo kula chakula, kunywa na kutoa takrima.

"Wengine wameanza kutuma wapambe na kuwagharimia kwa kila kitu kuzunguka nchini kote kwa niaba yao kwenda kuwanadi na kugawa bahasha au takrima, tunasema suala hili tunalikataa na atakayebainika, hata kama aliteuliwa, uteuzi wake utatenguliwa," alisema Mkuchika akionyesha kuwalenga baadhi ya makada wa chama hicho, akiwamo mtoto mmoja wa kigogo wa CCM na serikali ambaye amekuwa akimpigia debe mgombea mmoja wa uenyekiti wa UVCCM.

Alisema mbali ya matukio hayo, pia CCM imegundua baadhi yao wameanza kupakana matope, mambo ambayo ni kinyume cha maadili ya chama hicho.

"Sisi ndani ya CCM tunaamini kwamba, viongozi wazuri na wakataoweza kukisaidia chama ni wale tu wanaochaguliwa bila kutoa rushwa, lakini viongozi wanaochaguliwa kwa rushwa hawawezi kukisaidia chama kamwe na hawawezi kukemea uovu huo na baadaye wanaweza kuwa sehemu ya tatizo ndani ya chama chetu," alisema Mkuchuki.

Alisema kutokana na hali hiyo, kuanzia sasa ni marufuku kwa wagombea au wapambe wao kwenda mikoani na wilayani kujinadi au kumnadi mgombea yeyote.

"Tunasema kwamba kuanzia sasa ni marufuku kwa wagombea au wapambe kwenda mikoani, kwani tunaamini watapata nafasi ya kujieleza na kujinadi katika vikao vya uchaguzi kabla ya kupigiwa kura," alisema Mkuchika.

Mkuchika alisema wagombea wanajulishwa kwamba wote watakaobahatika kuchaguliwa, wanapaswa kuheshimu watakayopewa na si vinginevyo.

"Kama kutakuwa na mgombea ambaye atashindwa kutekeleza hayo na kama akibainika kwa kujihusisha na vitendo hivi, uteuzi wake utatenguliwa wakati wowote," alisema Mkuchika.

Kutokana na hatua hiyo, Kapteni Mkuchika amewaagiza viongozi wa ngazi zote nchini na kamati za maadili kuchukua hatua mara moja kwa watakaobainika.

Alisema tayari CCM imekwisha kuwasiliana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa ajili ya kufuatilia uchaguzi huo ili kuwanasa watoa na wapokea rushwa kama ilivyofanya mwaka jana wakati wa uchaguzi wa ndani ya chama hicho.

"Vyombo vya dola viko imara, vimejiandaa kufuatilia uchaguzi wote na kuwashughulikia kwa mujibu wa sheria watakaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa na wakati huo chama kikichukua hatua za kichama kwa upande wake," alisema Mkuchika.

Katika hatua nyingine, Mkuchika alishindwa kueleza hatua zitakazochukuliwa na chama hicho dhidi ya mawaziri wanaliojiuzulu kutokana na kashfa ya ufisadi.

"Napenda kuwaambia kwamba wale waliojiuzulu, Waziri Mkuu Mizengo Pinda amekwisha sema wameandikiwa barua za kujieleza, sasa sisi ndani ya chama hatuwezi kusema lolote wakati tayari wamepewa maagizo ya kujieleza," alisema Mkuchika.
 
Sijakupata sawasawa ,ina maana Mzee Mnauye(RIP)/Nape wanauhusiano wa kindugu na Katibu wa CCM Mzee Makamba?

Ndio mkuu, hawa wakuu wawili walikuwa na undugu, either kupitia kwa wake zao, au wao wenyewe.
 
Jamani mimi namtabiria mambo mabaya sana huyu mtoto! Alikurupuka, na mshauri wake inonekana ni mgeni kwenye siasa za nchi hii. Kamati yenyewe mwenyekiti Chenge! Aliye rafiki mkubwa wa Lowasa? Haya tutaona.....

JF mkuu huwa hatutishiki hata kidogo, Nape ni mjumbe wa NEC tayari sasa hao walikuwa wapi kumzuia asiwe? Wakimzuia UV-CCM sio tatizo, kwa wale tunaoabudu mabadiliko ya taifa kisiasa na kikatiba huwa hatujali kupata nafasi tunachojali ni kufikisha ujumbe kwanza, mengine baadaye,

Ni washauri wa Nchimbi, ndio wasiojua vizuri sana siasa wangejua basi wasingepoteza muda kujaribu kumzuia Nape, wakati tupo wa-Tanzania chungu nzima ambao tumeamuka na tunataka mabadiliko kwa taiffa letu, leo ukimzuia Nape, kesho hutaweza kutuzuia wote wengine,

Chenge na Lowassa, wanaozijua siasa za bongo, ilikuwaje wakatoka kwenye uwaziri? Acheni kututisha na hao mafisadi! Hawana lolote wako njiani kwenda chini, maana hawawezi kutushinda wananchi wote!
 
Mkuu Mtanzania,

Hapa ndipo unapokosea sana, unaongea siasa za bongo kama vile majuu, wakati hapa ukweli wa UV-CCM uko wazi kuwa ni chama ambacho hakina kanuni wala sheria, isipokuiwa huwa zinapangwa na kubadilishwa as Nchimbi anavyotaka,

Wewe umeona tumeuweka mpaka mkataba wa jengo la vijana, jisni Nchimbi alivyikiuka mpaka sheria za jamhuri kuhusu mikataba kama aliyoifanya, ukiangalia record yake kuhusu ukweli ni suspect, sasa ni vipi tunaweza kumuamini sasa kwenye hili la sheria za UV-CCM, ambazo nazo zimekwua suspect kwa sababu yake?

I mean, Nape anawezaje kuwa mjinga kiasi hicho unachojaribu kuonyesha kwamba anajua sheria za UV-CCM, lakini anataka kuzipindisha kwa makusudi, yeye ni nani hasa mpaka afanikiwe hilo? Imefika wakati unahitaji kukubali kuwa UV-CCM, haina mpangilio wala muelekeo,

kwa sababu just imagine, kwamba kiongozi amechukua fomu kugombea nafasi ambayo ni very celar kuwa anazidi au hatimizi umri unaotakiwa, hivi hiyo form anairudisha wapi? Halafu kikao cha UV-CCM kilichompa E, mbona hakikugusa hilo la umri, lakini badala yake tumelisikia likiibuka mitaaani na wapambe wa Nchimbi?

Binafsi silielewi vizuri hili la umri, lakini as the Nchimbi's leadership record goes, sioni cha ajabu hapa, mkuu tunatakiwa kukemea uovu na uhuni uonendeshwa huko UV-CCM kwanza, ambacho ndio hasa chanzo cha haya matatizo ya umri na mikataba mibovu ya jengo, the ishu hapa ni bigger than umri na you should know better na hizi siasa za uenyekiti wa UV-CCM toka zilipoanzia mpaka zilipofikia leo! Kosa la Nape hapa ni lipi? Kama amechukua fomu na sheria za UV-CCM ziko clear hatuwezi kuwa hata na debate on this, lakini kuna some fo things huko haviko sawa na hii confusion inakwenda moja kwa moja mikononi mwa Nchimbi,

Mimi ninaifahamu hii kitu toka ikiwa TANU Youth League, magwanda ya kijani na nyeusi, nilikuwa mdogo sana enzi hizo vijana wa TANU wanawazuia kina dada kutovaa nguo fupi, chini ya viongozi wa vijana kina Marehemu Rajabu Diwani, RC Mustafa Songambele, na Rashid Kawawa, sijawahi kusikia UV-CCM imekumbw ana matatizo na mpaka kushuka thamani kwa jamii yetu as now, WHY? haya huyaoni ya hiki chama kutokuwa hata na thamani mbele ya jamii, lakini umeshikia bango Nape tu, WHY? Nape hawezi kuwa bigger than UV-CCM mpaka kufikia kuamini kuwa anaweza kubadili sheria zake, lakini pia hawezi kuwa that small kwamba asisimame na kuomba nafasi kama anatimiza masharti, kwa sababu kama hatimizi tusingekuwa hata na debate hapa!

What is the agenda mkuu?

Mkuu FMES,

Hapo ndipo tunapotofautiana. Siko hapa kuhubiri siasa za Bongo au za wapi, niko kuelezea kilicho haki na kisicho haki.

Kama tunataka kuleta mabadiliko Bongo, dawa ni moja tu, kuwa waumi wa haki na sheria zetu.

Vinginevyo mimi hayo ya siasa za Bongo simo. Nitaendelea kufanya mambo kwa kufuata yale ninayoyaamini bila kujali niko Bongo au Ulaya. Siko tayari kubadilika kama Kinyonga, that is not for me. Ndio msimamo wangu na ndivyo ninavyoishi. Kama wengine mnachagua tofauti, ndio binadamu tulivyo kila mtu ana akili zake.
 
Kama wengine mnachagua tofauti, ndio binadamu tulivyo kila mtu ana akili zake.

Hapana tunachotafuta hapa ni haki na ukweli, kwangu ukweli ni kwamba Nape atakuwa mwenda wazimu kwenda kuchukua fomu ya uongozi wa chama cha taifa, ambacho anajua kabisa kuwa hatimizi masharti yake, au akiamini kuwa eti ana nguvu ya kumsukuma kuweza kubadili sheria hai za UV-CCM, ili aweze kugombea that is insane na ninaamini kuwa that is not the ishu here,

The ishu haiko clear, kwa sababu ingekuwa clear wala hakutakiwi kuwa na even mjadala, the fact kwamba hata kuna mjadala tena wa pembeni lakini sio official ndani ya UV-CCM as it should, maana yake ni kwamba kuna mtu huko UV-CCM, anataka kufanya uhuni,

We have had Enough of it, sheria ni msumeno Nape amepitisha umri wa kugombea then why even discuss him mpaka kumpa E? Wewe Mtanzania ni mwenyekiti wa UV-CCM, leo unaletewa fomu ya mtu aliepitisha umri wa sheria za chama chako, eti unamjadili mpaka kumpa E ya uongozi? Is that so?

Mimi nilifikiri kuwa fomu yake inatupwa kwenye garbage bin, ndio iliyokuwa tabia ya Mwalimu, kuna wapuuuzi waliokuwa wakijaribu kugombea uongozi, alikuwa akichukua fomu zao na kutupa kwenye uchafu, bila kelele wala kuwajadili kwenye vikao, sasa hapa UV-CCM kilichoshindikana ni nini hasa kama sio kuna uhuni na not even worthy kuujadili hapa JF!

Tunazungumza haki na sio kwamba tunajali jina la mtu au kiongozi kuliko sheria, tunasema haki itendeke, that is all!
 
Back
Top Bottom