Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Mkuu usiwe na wasi wasi, Charle Kajege alikwua mbunge wa kule baada ya Nchimbi kuondoka kule, kwa hiyo usiwe na wasi wasi, utakapopatikana ukeli nitampa huyo bosi wako medali, wala isikupe taabu sana subira tu mkuu!

Record zote za bosi wako zitawekwa hapa wala usiwe na wasi wasi, JF tuncahotaka ni ukweli sio upambe.
 
Mkuu usiwe na wasi wasi, Charle Kajege alikwua mbunge wa kule baada ya Nchimbi kuondoka kule, kwa hiyo usiwe na wasi wasi, utakapopatikana ukeli nitampa huyo bosi wako medali, wala isikupe taabu sana subira tu mkuu!

Record zote za bosi wako zitawekwa hapa wala usiwe na wasi wasi, JF tuncahotaka ni ukweli sio upambe.
Kaka kama nilivyosema hapo awali ni kuwa nia yangu ni kukusaidia uache rekodi potofu za nchimbi...Kajege kwa taarifa yako pia alichangia muujiza huo wa kujenga shule bunda na zote kupata usajili na watoto kuanza kusoma ndani ya mwaka mmoja.alichangia bati mia za geji 28,wakati huo nadhani alikuwa wizara ya mambo ya nje.Namba ya Kajege ni 0773 828 782 kwa msaada zaidi
 
Naona hapa kuna mtu anakiuka kanuni,ya nini kuweka namba ya mtu bila ridhaa yake?
 
Record nzuri hufutwa na Mbaya, hatuwezi kuangalia record nzuri wakati sasa ana record mbaya. Hafai huyu nchembi na ni kijana hatari sana
 
Naona hapa kuna mtu anakiuka kanuni,ya nini kuweka namba ya mtu bila ridhaa yake?
kakwambia nani sina ridhaa yake????pili nani kakwambia namba za wabunge ni siri wakati ata kwenye website ya nbunge zipi....jenga hoja usilete kijipendekeza hapa
 
Record nzuri hufutwa na Mbaya, hatuwezi kuangalia record nzuri wakati sasa ana record mbaya. Hafai huyu nchembi na ni kijana hatari sana
hapa hatuna nafasi kwa watu wanaokurupuka kama wewe na wanaongea mambo abstract.jenga hoja mabaya ni yapi.then tukuone una akili sio kutuambia sweeping statement.
 
Nchimbi , Dr. Emmanuel J.

EDUCATION

School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level

CommonWealth Open University PhD (Management) 2001 2003 PHD

Mzumbe University MBA (Finance & Banking) 2001 2003 MASTERS DEGREE

CommonWealth Open University MSc. (Management) 1999 2001 MASTERS DEGREE

Institute of Development Management - Mzumbe Advanced Diploma in Administration 1994 1997 ADV DIPLOMA

Forest Hill Secondary School A-Level Education 1991 1993 HIGH SCHOOL

Sangu Secondary School Secondary Education 1989 1990 SECONDARY

Uru Seminary Secondary Education 1987 1989 SECONDARY

Oysterbay Primary School Primary Education 1980 1986 PRIMARY

EMPLOYMENT HISTORY

Company Name Position From Date To Date

Regional Administration and Local Governments (TAMISEMI) District Commissioner 2003 2005

Ministry of Defence and National Service Deputy Minister 2/13/2008

National Environment Management Council-NEMC Administration Officer 1998 2003

Ministry of Labour, Employment and Youth Development Deputy Minister 10/17/2006 2/8/2008

Ministry of Information, Culture and Sports Deputy Minister 1/1/2006 10/16/2006


POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/Location Position From To
Chama Cha Mapinduzi - CCM Member of District Political Committee(Bunda) 2003 2005
Chama Cha Mapinduzi - CCM Chairman of Youth (UVCCM) 1998 Todate
Chama Cha Mapinduzi - CCM Member of National Executive Council(NEC) 1997 Todate
Chama Cha Mapinduzi - CCM Member of District Council 1997 2002
 
Kaka naungoja huo ukweli wako ambao sijui umeufata sayari ya mars au jupiter.maana kama ni hapo tanzania ata ukimtuma mtu hapo wizara ya elimu tu unapewa ukweli au altenative piga namba ya mkuu wa mkoa wa Mara.wanazo taarifa zote kupitia ofisi ya mkuu wa mkoa...baada ya hapo nakuomba wewe mwenyewe utoe nishani ya uongozi uliotukuka wa nchimbi na umuombe seguyemisi amvishe kwa niaba yako.Angalizo mimi siktoki bunda na wala sikai bunda.Msaada namba ya afisa elimu mkoa wa mara ni 2622139 na std ni +25528
Kaka hapa wamekutoa kamasi kwa kweli na onyesha ukomavu kwa kukubali ukweli..nimetoka kuongea na Kajege dk tano zilizooita.kasema ni kweli na bunda wanamuheshimu sana Nchimbi kwa kazi alizowafanyia..
 
CommonWealth Open University PhD (Management) 2001 2003 PHD

Msaada tutani wakuu, exactly hii ni shule gani ambayo mkuu alipatia hii PHD yake? Je inatambulika na accademic world?

Fisadi Mtoto na wenzako naomba msaada hasa kutoka kwenu, ni kwenye kuangalia record ya your hero, maana hatutaacha any stone un-turned, na nothing personal!
 
Msaada tutani wakuu, exactly hii ni shule gani ambayo mkuu alipatia hii PHD yake? Je inatambulika na accademic world?

Fisadi Mtoto na wenzako naomba msaada hasa kutoka kwenu, ni kwenye kuangalia record ya your hero, maana hatutaacha any stone un-turned, na nothing personal!
kaka ni wazi umechemka na jasho la kwapa limekutoka,umejua huwezi kuwa fool all the ppl all the time............kabla sijatumia nguvu zako kukufuta ujinga wa jambo hili jipya ulililolianzisha kwanza tumalize na huo uchunguzi wako.nimekupa mpaka namba za Kajege...ok sasa niambie na kukiri wazi kuwa record yake ya utendaji wewe na babu yako hamjawahi kuifanya licha ya kukaa madarakani miaka kibao....hahahahaha labda record ya kuzaazaaa hovyo ya Seguyemisi ndio anyo na kutukana wagogo wenzie go to hell.
 
Nchimbi , Dr. Emmanuel J.

EDUCATION

School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level

CommonWealth Open University PhD (Management) 2001 2003 PHD

Mzumbe University MBA (Finance & Banking) 2001 2003 MASTERS DEGREE

CommonWealth Open University MSc. (Management) 1999 2001 MASTERS DEGREE

Institute of Development Management - Mzumbe Advanced Diploma in Administration 1994 1997 ADV DIPLOMA

Forest Hill Secondary School A-Level Education 1991 1993 HIGH SCHOOL

Sangu Secondary School Secondary Education 1989 1990 SECONDARY

Uru Seminary Secondary Education 1987 1989 SECONDARY

Oysterbay Primary School Primary Education 1980 1986 PRIMARY

EMPLOYMENT HISTORY

Company Name Position From Date To Date

Regional Administration and Local Governments (TAMISEMI) District Commissioner 2003 2005

Ministry of Defence and National Service Deputy Minister 2/13/2008

National Environment Management Council-NEMC Administration Officer 1998 2003

Ministry of Labour, Employment and Youth Development Deputy Minister 10/17/2006 2/8/2008

Ministry of Information, Culture and Sports Deputy Minister 1/1/2006 10/16/2006


POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/Location Position From To
Chama Cha Mapinduzi - CCM Member of District Political Committee(Bunda) 2003 2005
Chama Cha Mapinduzi - CCM Chairman of Youth (UVCCM) 1998 Todate
Chama Cha Mapinduzi - CCM Member of National Executive Council(NEC) 1997 Todate
Chama Cha Mapinduzi - CCM Member of District Council 1997 2002
haya uliojitungia hapa ndio uchunguzi uliotuahidi kutuletea kuhusu Bunda....ndio yatatoa jibu ya kama ni kweli alisimamia vema maendeleo ya bunda...nadhani sasa niache kubishana na wewe maana nilidhani nabishana na mtu mwenye akili zake kumbe huna tofauti na mama yako anne Kilango.
 
Baada ya kitimbakwila wa Seguyemisi kushindwa kukanusha record za uchapa kazi wa Nchimbi hapa na kujaribu kuchange topic....nimemdharau na kumuona ni mbabaishaji anaepaswa kusamehewa bure.nimemsamehe kwa kuwa upeo wake wa kuwaza ndio ulipoishia.......

TAARIFA ZILIZOFIKA HIVI PUNDE KUTOKA KWENYE KIKAO CHA KAMATI KUUNI KWAMBA KAMATI KUU YA CCM IMEPOKEA NA KUJADILI KWA KINA MKATABA WA JENGO LA UMOJA WA VUJANA NA KUTOA PONGEZI ZA DHATI KWA JUHUDI ZA UMOJA WA VIJANA KUJIKOMBOA KIUCHUMI,PIA KAMATI KUU IMEIPONGEZA KAMATI YA UTEKELEZAJI KWA JUHUDI HIZO NA KUSEMA MAPATO YATAKAYOTOKANA NA MRADI HUU YASAIDIE NA MIKOA MINGINE YA UVCCM ILI IWEZE KUJITEGEMEA.

INAKADIRIWA KUWA MRADI HUO UTAONGEZA PATO LA UMOJA WA VIJANA KWA TAKRIBANI SHILINGI MILIONA 107 KILA MWEZI..........nadhani hata mapato ya CHADEMA hayafiki hapo
 
1. CommonWealth Open University PhD (Management) 2001 2003 PHD

2. Mzumbe University MBA (Finance & Banking) 2001 2003 MASTERS DEGREE

3. CommonWealth Open University MSc. (Management) 1999 2001 MASTERS DEGREE

Mkuu ninapokata ishu, huwa ninaanzia kwenye shina, ya Bunda yatakuja, na sisumbuliwi na matusi yako ya nguoni maana nataka kuweka record straight hapa, na pia sheria za JF ninaamini ziko wazi na Mods wapo kwa kazi hiyo,

Now Back to the ishu: Nchimbi, katika kipindi cha kuanzia mwaka 1999 - 2003, yaani miaka minne tu, ameweza kufanya Masters mbili na PHD, ndani yake wakuu wenye elimu nzito humu JF naomba masaada kama ni kweli haya yanawezekana.
 
...au itamkubatia fisadi na kuthibitisha kwamba chama hicho ni chama cha mafisadi? Tutege sikio


Nape Vs Lowassa

na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima~Sauti ya Watu


SUALA la utata katika mradi wa ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), ni miongoni mwa ajenda zinazotarajiwa kuwasha moto mkali wa hoja wakati wa kikao cha Kamati Kuu ya CCM, kinachokutana jijini Dar es Salaam leo.

Kikao hicho kitakachokuwa chini ya Uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete, pamoja na mambo mengine kinakusudia kupitia mkataba wa mradi huo ambao katika siku za hivi karibuni, umezua maneno mengi ndani ya chama hicho tawala.

Kuibuka kwa mjadala huo kulianzishwa na kada wa chama hicho, Nape Nnauye, ambaye ni mmoja wa vijana wanaogombea nafasi nyeti ya mwenyekiti wa UVCCM, ambayo kihistoria imekuwa ikiibua ushindani mkali.

Kwa mara ya kwanza Nape alitoa hoja yake hiyo saa chache tu baada ya kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo inayompa fursa mshindi ya kuwa mjumbe wa vikao vya kimaaamuzi vyenye nguvu kubwa ndani ya chama hicho tawala, Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).

Katika madai yake, Nape alimshutumu moja kwa moja Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa umoja huo, Edward Lowassa na viongozi wengine wa juu wa UVCCM kwa kuingia katika mkataba huo ambao alisema hauna masilahi yoyote ya maana kwa umoja huo.

Tangu Nape atoe tuhuma hizo, hali ya mambo ndani ya CCM na hususan katika UVCCM imekuwa ni ya vuta nikuvute, ikiwagawa viongozi waandamizi ndani ya chama hicho tawala katika makundi mawili.

Kundi la kwanza ni lile linalomuunga mkono Nape, likijumuisha wakongwe kadhaa wa siasa za CCM (majina tunayo), ambao wanakiona kitendo cha mwanasiasa huyo kijana kuwa ni cha kijasiri na ambacho kinapaswa kuungwa mkono na kila mwanachama wa chama hicho.

Miongoni mwa watu wanaomuunga mkono Nape katika siku za hivi karibuni wanadaiwa kuwa wamekuwa wakifanya kila linalowezekana ili kuhakikisha kwamba; ‘kijana wao' huyo anashinda uteuzi wa uenyekiti wa UVCCM kwa gharama zozote.

Kundi la pili katika msigano huo ni lile linalomuunga mkono Lowassa, likiwajumuisha wanasiasa kama Makamba, ambao wamekuwa wakimtaja Nape kuwa kijana anayejaribu kujenga hoja ili kujihalalishia ushindi kwa gharama zozote zile.

Habari kutoka ndani ya CCM zinaeleza kuwa, wanasiasa wanaounda kundi hili ambalo Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Vijana, Emmanuel Nchimbi, anatajwa kuwa mmoja wao, tayari wameshaanza kupanga mikakati ya kuhakikisha wanamuengua Nape katika mchuano huyo.

Wana CCM hao ambao baadhi yao wamepata kufanya mahojiano na Tanzania Daima kwa nyakati tofauti, wamekuwa wakimuelezea Nape kuwa mwanasiasa mzushi na mtu anayetumiwa na kundi la wazee kadhaa wa ndani ya chama hicho wenye lengo la kuhakikisha wanawaengua watu wote walio karibu kisiasa na Rais Jakaya Kikwete, ambaye ndiye atakayekuwa mwenyekiti katika mchakato huu wa leo.

Habari ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka kwa watu wa kundi hili la pili zinaeleza kwamba, kikao cha leo cha Kamati Kuu kinatarajia kuridhia kupitishwa kwa mkataba huo pamoja na kuwapo kwa wana CCM wengi wanaomuunga mkono Nape katika hoja yake.

Kwa sababu hiyo basi, iwapo kweli, Kamati Kuu itaridhia kupitishwa kwa mradi huo, upo uwezekano mkubwa kwamba, nafasi ya Nape katika mchuano wa kuwania uenyekiti wa UVCCM itakuwa shakani.

Katika hoja ya Nape, mbali ya Lowassa, wanasiasa wengine anaowahusisha katika mkataba huo ni Nchimbi, na aliyekuwa Katibu Mkuu wa UVCCM, ambaye sasa ni Mweka Hazina wa CCM, Amos Makalla.

Katika hoja zake, Nape amenukuliwa akisema kwamba mkataba huo ulipitishwa kinyemela hata kabla haujafikishwa kwenye vikao vya juu vya CCM, kwa maana ya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho ili kupata baraka za mwisho.

Vipengele vingine ambavyo Nape analalamikia ni kuhusu uhai wake, kwani kimojawapo kinasema mwekezaji ataendesha mradi huo milele, huku jumuiya hiyo ikipata asilimia 25 na mwekezaji asilimia 75.

Kasoro nyingine anazozitaja Nape katika tuhuma hizo ni pamoja na ile ya kukiukwa Sheria ya Ardhi (Kiwanja), kuhamishwa kwa wabia kabla ya shughuli yoyote ya ujenzi kuanza.

Utaratibu ni kwamba, kabla hatua hiyo haijachukuliwa, sharti Kabidhi Wasihi Mkuu wa Serikali, atoe kibali kwa ajili ya uhamisho wa aina hiyo.

Mkataba wa mradi huo unaosomeka kwa kichwa kisemacho ‘Development Agreement', ulisainiwa Januari 2 mwaka 2007 kati ya UVCCM na makampuni mawili ya M. M. Integrated Steel Mills (MMISML) na Estim Construction Company Limited (ECCL).

Mkataba huo pia hauelezi kiasi cha uwekezaji kutoka kwa wabia, ambacho kinaweza kutumika kuelezea mgawo wa asilimia 25, ambayo inadaiwa UVCCM watachukua.

Aidha, mkataba huo hauna ufafanuzi wa matumizi na mapato hatua kwa hatua, jambo ambalo linaonyesha kutokuwa makini au kuashiria ghiliba katika mahusiano ya wabia.

Vilevile mkataba hauelezi iwapo ubia ni wa miliki ya pamoja au itaundwa kampuni tofauti ya kuendesha kitega uchumi.

Mbali na kujadili suala la mradi huo, kikao hicho pia kitapitia majina ya waombaji wanaowania uongozi wa jumuiya za chama hicho, ambazo mbali ya UVCCM, pia itajadili majina ya wanaoomba uteuzi wa Jumuiya ya Wanawake (UWT).

Mbali ya Nape, waombaji wengine katika uchaguzi huo wa UVCCM unaoendelea kuvuta hisa za watu kila kukicha ni Jerry Slaa, Hamad Masauni, Issa Haji Ussi, Anthony Mtaka, Said Mtanda, Haule Pangisa, Samuel Marero, Stephen Deya, Geofrey Mwankenja, David Manoti, Mussa Mnyeti, Edson Lubua, Mwamini Lusingu, Asmah Kalokola, Marco Zablon Allute, Harold Adamson, Adila Hilal Vuai, Ashura Ismail, Rashid Masalaka na Raha Ahamada.

Wanaowania uteuzi wa nafasi ya makamu mwenyekiti ni Happy Mahava, Raha Ahamada Ally, Riziki Pembe Juma, Michael Bundala, Rabia Hamid Shaka, Nuru Mohammed Ahamed na Twaha Ally Muhaji.

Taarifa iliyotolewa jana na Ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, ilisema chama hicho kitajadili masuala yanayokihusu chama, ikiwemo jumuiya zake pamoja na jamii kwa ujumla.

Katika taarifa hiyo, CCM inasema miongoni mwa ajenda hizo ni kupokea na kujadili taarifa kuhusu hali ya kisiasa nchini.

Makamba alizitaja ajenda nyingine kuwa ni ile inayohusu kupokea na kujadili taarifa ya maendeleo ya uchaguzi mkuu wa jumuiya za CCM, unaofanyika nchini kote mwaka huu, na nyingine ni kuziba nafasi za uongozi zilizo ndani ya chama hicho tawala.

"Mkutano huo pia utapokea taarifa kuhusu maandalizi ya CCM ya kushiriki uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata 34 Tanzania Bara," alisema.

Kikao hicho kitafuatiwa na kikao kingine cha Halmashauri Kuu (NEC) kinachotarajiwa kufanyika Septemba 9 hadi 10 mjini Dodoma.
 
Kaka kama nilivyosema hapo awali ni kuwa nia yangu ni kukusaidia uache rekodi potofu za nchimbi...Kajege kwa taarifa yako pia alichangia muujiza huo wa kujenga shule bunda na zote kupata usajili na watoto kuanza kusoma ndani ya mwaka mmoja.alichangia bati mia za geji 28,wakati huo nadhani alikuwa wizara ya mambo ya nje.Namba ya Kajege ni 0773 828 782 kwa msaada zaidi

FMES!

Umeshikwa pabaya, tafadhari tafuta pakutokea.
 
hakuna jipya Mkuu kwenye hili. wamezoea kutafuna serikali sasa wanahamia ndani ya chama. kesi ya mbwa kala mbwa
 
1. Quote: Mambo Jambo

FMES!

Umeshikwa pabaya, tafadhari tafuta pakutokea.


Mkuu Heshima yako, hapa tunajaribu kuangalia record ya Nchimbi, aliyempa Nape alama ya E, hatuko kwenye kushikana pabaya au pazuri, ila tunaangalia record na ndiyo hii tunaichambua bila wasi wasi, na sina mpango wa kuugeuza huu mjadala kuwa personal ila facts, jamaa wametoa facts zao na mimi niko njiani kutoa alll the facts za record ya Nchimbi, halafu wananchi kama kawaida wataamua, ukweli uko wapi, soma chini hapa more facts, na ya Bunda bado ninayafanyia uchunguzi yanakuja na hii topic ni very interesting kwa sababu kuna bwana humu anayejibadili majina huko nyuma amekuwa akimtukana sana Nchimbi, ingawa sasa yuko kambi ya Nchimbi kwa hiyo mkuu fasten your belt :-

Chiligati & Nchimbi washindwa kazi..

1. Mvutano wa ajira na serikali ya JK Ukosefu wa ajira kwa Wabongo unazidi kukua na sasa umefikia milioni 2.7 pamoja na mikakati kibao ya kujenga mazingira ya kujiajiri na kuajiriwa.

2. Serikali ya Rais JK imekuwa imehaha huku na huko nchi za nje na hadi sasa baadhi walishanza kuponda juu ya safari zake za nje kwa nia ya kusaka wawekezaji wa sekta kibao nchini.

3. Karibuni alikuwa Arusha -Ngurdoto (anapapenda) akiteta na wawekezaji kuwekezaji nchini katika sekta ya utalii, mawasiliano na kilimo.

4. Takwimu za ajira zimetolewa na Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, John Chiligati na kusema kuwa waathirika zaidi wa ujobless huo ni kwa vijana kwa asilimia 14.5.

5. Takwimu hizo ziliendelea kusema kuwa Wabongo wenye uwezo wa kufanya kazi ni milioni 21.3 lakini wenye ajira zinazoeleweka ni milioni 2.7 na kati yao zaidi ya asilimia 80 hawana shule ya kutosha.

6. Zaidi ya vijana, akina mama nao huathirika sana na ukosefu wa ajira kwa asilimia 13.7 ikifuatiwa na wanaoishi mijini ikilinganishwa na wale wanaoishi vijijini kwa asilimia 9.5.

7. Aliongeza kuwa nia ya serikali nzima ya JK ni kuongeza ajira kwa vijana kama ilivyoaidiwa wakati wa kampeni za uchaguzi 2005.
 
kakwambia nani sina ridhaa yake????pili nani kakwambia namba za wabunge ni siri wakati ata kwenye website ya nbunge zipi....jenga hoja usilete kijipendekeza hapa


Heshima kwako Mkuu,

Hilo tusi lako nimelisikia,kajipendekeza nani kati yangu na wewe kujifanya kuwabebea mafisadi wenzako Vi-note book.

Leo hii unakuja kumwaga upupu hapa kuhusu Nchimbi,unaonekana mtu wa kujipendekeza ovyo,leo unatetea nonesense za mtu aliyechonga vyeti na kuja kutuharibia system za uongozi.Hadi unajiita Fisadi mtoto sijui unafikiria kumkomoa nani hapa.


Kuanzia leo kwenye hoja zozote nikikutana na wewe LAZIMA nikulime.Ukipende rudi ukatafute Back-up kutoka kwa huyo bosi wako kilaza.Kamwambie JF tunamtumia salamu zake,Hapendwi mtu hapa.


Sisi hatutishiki na Vilaza,maanake kwasababu wewe unamsujudia unadhami kila mtu hapa ana huo muda.

Na tafadhali tunaomba utufanyie favour ya kumuomba huyo bosi wako kujiunga hapa hata kama hana huo ujasiri jaribu tu hata kufunga kwa ajili yake aje hapa na ajisajili kwa jina lake,only kama hajachonga cheti cha matumizi ya kompyuta maanake si ajabu ana vyeti vikubwa tu vya kompyuta na hawezi kutumia Comp yenyewe maanke yeye anaweza hata kufikiria Mtandao ni ule wa kwake na na yule kilaza mwezie wa Buchosha na akina Dr. Kamala, so hata Internet ni mtandao kwa hiyo aje hapa tujadili masuala ya mustakabali wa taifa letu aaache kufikiria mambo machafu machafu ya kujipatia fedha kifisadi thru mikataba.Wanasema 'an empty mind is the wokshop of a Devil' so aje hapa akiwa na part time.Ipo siku Mtaumbuka.


BTW: Huyo ni Mhunzi wa vyeti tu ,angalia hata hiyo karakana yenyewe ilivyokaa ,Eti commonwelth open university(workshop).Leo hii JK ambaye nae anapenda ujanja ujanja usio na tija kwa taifa akaamfagilia.Na unajua nini, Uwezo wake wa siasa chafu umeweza hata ku-outweigh hiyo CV yake ya Taaluma na hata yeye mwenyewe anajua
 
lOWASA ANA NGUVU SANA KWENYE nec VIPI KWENYE CC?MAANA NA YEYE ATAKUWEPO JE JK ANAWEZA KUMNYOSHEA KIDOLE EL LIVE?MAANA PALE USO KWA USO....SIO KAMA NEC.
 
Kweli sisis ni wadanganyika
Hivi bado mnafikilia kama JK anaweza kufanya swala lolote zuri katika nchi hii?
kama haliwausishi mafisadi labda naweza kushawishika kuwa anaweza kufanya, ila mambo yanayowahusisha mafisadi direct ndugu zangu, huyu jamaa anawaona kama ndio basi tena
Majibu hapo ni El 4-0 Nape

Naam, na ule usemi kwamba CCM ni chama cha mafisadi kilichojaa wahuni na mafisadi ndiyo utazidi kuthibitika
 
Back
Top Bottom