Sakata la maslahi ya Wabunge na hekaya ya Hilda Newton

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,734
6,292
Habari wanabodi,

Kumekuwa na trend ya muda kuhusu sakata lililoibuliwa na Mh Nicodemas Henry Maganga mbunge wa Mbongwe kuwa maslahi yao ni madogo kuliko inavyodhaniwa. Katika kuutanabaisha huu mjadala ulioleta hasira toka kwa wapiga kura.

Nimekutana na kasimulizi toka kwa Hilda Newton juu ya bwana Fulani hivi ambaye alikuwa MP na sasa ni muuza chips hapo msamvu.

Je, ni nani huyo Mheshimiwa?

Je, ni kweli maslahi yao ni madogo au matumizi yao ni makubwa?

Namnukuu Bi Hilda Newton:

"Kuna jamaa alikuwaga Mbunge 2010-2015 ila kwakuwa ilikuwa first time kushika pesa mingi kila kitu ambacho aliwahi wish kuwa nacho enzi za Ukata alihakikisha anakipata, alikuwa anaenda kula bata na Babe's nchi mbalimbali, 2015 alikosa Ubunge now yupo Moro anauza Chips pale Msamvu."
 
Baada ya Magufuli tutasikia mengi sana kadri siku zinavyokwenda, hasa kuhusu mishahara na maslahi ya wafanyakazi wa serikali! Itabidi nitunze vidola vyangu kwa muda kidogo kabla ya kuvipeleka Tanzania kwa vile muda siyo mrefu huenda dola moja ikwa Sh. 3200 kutokana na wingi wa shilingi mitaani wakati huo.
 
Mheshimiwa Kichuguu,

Nafahamu wewe ni mtu mwenye michango mizuri sana huku kwa siku nyingi. I have nothing but respect for you. Ila hili la shilingi kushuka kwa kasi sasa nadhani umekosea. Ni sahihi kwamba miradi ya SGR, madaraja, ujenzi wa meli na kadhalika itachukua forex nyingi, lakini miradi ya LNG na bomba la mafuta italeta nchini forex nyingi pia. Miaka michache ijayo shilingi itapanda, na sio kushuka. Wekeza tu dola zako Bongo sasa. I am in the same boat.
 
Kitakachoshusha thamani ya shilingi siyo hiyo miradi bali wingi wa shilingi zatakazokuwa kwenye mzunguko bila kuwa proportional na mwenendo wa uchumi. Wabunge akishaanza kujipangia kuwa wapewe pesa nyingi, viongozi wa serikali nao wakaanza hizo zinazoitwa semina endekezi zenye per diem kubwa kubwa ambazo zinaishia kwenye mzunguko, ndipo hapo thamani ya shilingi itakapoanza kuporomoka.
 
Sio kweli. Huu uchumi umesomea wapi? Magufuli hakupandisha mshahara hata mia mbona dola haikupanda?
Hela ya semina haiwezi leta inflation kwa sababu ni hela halali sio ya madawa ya kulevya!
 
Ni kweli mnachosema kukiwa na hela nyingi mtaani italeta hiyo hali, lakini serikali ikiwa makini na monetary and fiscal policies zake hiyo hali haitatokea. Kwani ukimwongeza mtu mshahara ndiyo lazima hela ziwe nyingi mtaani?

Serikali tu icheze vizuri na policies zake. Ila huyo mbunge mpuuzi sana. Watumishi wa umma tumenyimwa increment miaka sita sasa yeye anasema mishahara na posho ni midogo! Si aache ubunge aingie mtaani!
 
Sio kweli. Huu uchumi umesomea wapi? Magufuli hakupandisha mshahara hata mia mbona dola haikupanda?
Hela ya semina haiwezi leta inflation kwa sababu ni hela halali sio ya madawa ya kulevya!
Wakati anaingia ilikuwa shilingi ngapi na kaiacha shilingi ngapi? Toa siku 130 kabla ya 17,March,2021.
 
Sio kweli. Huu uchumi umesomea wapi? Magufuli hakupandisha mshahara hata mia mbona dola haikupanda?
Hela ya semina haiwezi leta inflation kwa sababu ni hela halali sio ya madawa ya kulevya!
Shilingi ilitelemka zaidi ya fluctuations za kawaida?

1624505891300.png

1624505925542.png

1624505979411.png

Ukiangalia record hiyo; kipindi chochote kulipokuwa na hela nyingi mitaani, thaamani ya shilingi ila ilishuka kwa asiliia kubwa sana. Wakati wa magufuli, exchange rate ilipanda kwa asilimia 8.8, wakati miaka mitano ya mwisho ya Kikwete ilipanda kwa asilimia 60, na miaka mitano ya kwanza ya Kikwete ilipanda kwa asilimia 14.5
 
Ni kweli mnachosema kukiwa na hela nyingi mtaani italeta hiyo hali, lakini serikali ikiwa makini na monetary and fiscal policies zake hiyo hali haitatokea. Kwani ukimwongeza mtu mshahara ndiyo lazima hela ziwe nyingi mtaani? Serikali tu icheze vizuri na policies zake. Ila huyo mbunge mpuuzi sana. Watumishi wa umma tumenyimwa increment miaka sita sasa yeye anasema mishahara na posho ni midogo! Si aache ubunge aingie mtaani!!!
point yako ni kweli kwa kiasi fulani ila ni vigumu kuwa na monetary policy inayocontrol inflation huku kukiwa na circulation kubwa bila kuongeza interest rates. Ukishaongeza interest rates unaanza kukwamisha uchumi ambayo ndio mwanzo wa downfall ya currency yako.
 
Kitakachoshusha thamani ya shilingi siyo hiyo miradi bali wingi wa shilingi zatakazokuwa kwenye mzunguko bila kuwa proportional na mwenendo wa uchumi. Wabunge akishaanza kujipangia kuwa wapewe pesa nyingi, viongozi wa serikali nao wakaanza hizo zinazoitwa semina endekezi zenye per diem kubwa kubwa ambazo zinaishia kwenye mzunguko, ndipo hapo thamani ya shilingi itakapoanza kuporomoka.
Ikiwa Tz kuna tatizo sugu la ajira na kujiajiri hawa watu hata wakijilipa kiasi kikubwa na per diem zikiwepo siyo kwamba itakua ni miongoni mwa watu wachache wenye ajira na hii in turn itacompensate kwa ambao hawana ajira?

Ni sawa na kusema waajiriwe watu wengi zaidi ya sasa ila mshahara uwe wa kawaida au waajiriwe wachache halafu mshahara uwe kufuru.
 
Tunaohoji hadi Kuwashangaa Wabunge kudai nyongeza ya Mshahara tumeshajiuliza Swali ni lini Mshahara umewahi Kumtosha Mwanadamu?

Kuna Shirika moja la Ndege ( hapa hapa EAC Kwetu ) Marubani wake kila Mwezi wanalipwa USD 8000 ( Hela ambayo ukiichenji kwa Shilingi yetu inazidi hata ya Wabunge ) huku Posho zao kila wakiruka ( wakipaa ) ni USD 200 lakini bado walitishia Kugoma ili waongezewe.

Huko nyuma nami GENTAMYCINE nilikuwa ni Muumini wa 'Kukurupuka Kudemka' hasa Kushangaa Wabunge wakitaka Kuongezeka Mishahara yao ili nilivyokaa Siku moja na Mbunge fulani na akanichambulia jinsi Pesa zao zinavyotumika na kuishia kwa Kuwasaidia Wananchi ambao 24/7 huwapelekea Shida zao mbalimbali kiukweli wakidai hiyo nyongeza ni halali ( haki ) yao.

Tatizo Kubwa nililoligundua humu Mtandaoni ( Mitandaoni ) ni kwamba kumekuwa na 'Kautamaduni' ambako naona kana Ushamba na Upumbavu mwingi ambapo Watu tumekuwa 'tunahemka' kwa Hisia zetu tu za Itikadi ya Vyama vyetu vya Kisiasa pamoja na Chuki kwa Bunge lenye Wabunge wengi wa CCM na Serikali yake pia ila hatutaki Kujishughulisha kutumia Akili zaidi ya Kutafakari na Kuchambua jambo.

Nimalizie tu kwa Kuwauliza je, nyie mnaopinga Wabunge Kuongezewa Mshahara au hata Watu wa Kada zingine Kupandishiwa Mishahara nyie mngekuwa ndiyo Wabunge au Watu hao mngekuja humu Mitandaoni na Kukataa kuwa isipandishwe?

Ifike muda tupunguze Nongwa na Wivu.
 
point yako ni kweli kwa kiasi fulani ila ni vigumu kuwa na monetary policy inayocontrol inflation huku kukiwa na circulation kubwa bila kuongeza interest rates. Ukishaongeza interest rates unaanza kukwamisha uchumi ambayo ndio mwanzo wa downfall ya currency yako.
Point yangu ni kuwa kupitia tight monetary policy hali ya kuwa na circulation kubwa haitakuwepo. Mi muda mrefu watumishi wa serikali hawajaongezwa mishahara lakini bei za bidhaa zimekuwa zinapanda. Watu wakipewa imcrements zao sidhani kama circulation ya pesa itakuwa kubwa. Tukumbuke kipindi cha Raisi Mwinyi, Mkapa na Kikwete.

Kipindi cha Kikwete Mishahara yetu ilikuwa inapanda na increment tunapata lakini hakukuwa na inflation kubwa!!! Mwinyi yes hali ilikuwa mbaya sana. Ben akaja akarekebisha mambo. Kikwete aliendeliza ukiacha matatizo naye aliyosababisha lakini hali haikuwa mbaya. Ila ni kweli hela serikali iwe makini sana kusiwe na hela nyingi mtaani. Kubana sana kuna repercussions mbaya kwa uchumi wa nchi na watu pia.
 
point yako ni kweli kwa kiasi fulani ila ni vigumu kuwa na monetary policy inayocontrol inflation huku kukiwa na circulation kubwa bila kuongeza interest rates. Ukishaongeza interest rates unaanza kukwamisha uchumi ambayo ndio mwanzo wa downfall ya currency yako.
Hata kama riba ni affordable?

Kwa Tz naona shida yetu ni kubwa kwakua hatufanyi exportation kwa kiwango cha kuzidi importation.
 
Kama kweli mshahara wa mbunge ni 3.8m badi kweli ni mdogo
Wamajiwekea 3.8M kwenye salary slip ili kukwepa makato ya kodi.

Kwenye hiyo 3.8M wamejiwekea miposho posho na allowance kibao isiyo na makato yoyote mpaka kitu inaenda mpaka 12M kwa mwezi.

Kubwa kuliko yote ni wao kupewa mafao ya zaidi ya Tsh 250M ndani ya miaka 5 tu bila yao kuchangia chochote kwenye mfuko.
 
Tunaohoji hadi Kuwashangaa Wabunge kudai nyongeza ya Mshahara tumeshajiuliza Swali ni lini Mshahara umewahi Kumtosha Mwanadamu?

Kuna Shirika moja la Ndege ( hapa hapa EAC Kwetu ) Marubani wake kila Mwezi wanalipwa USD 8000 ( Hela ambayo ukiichenji kwa Shilingi yetu inazidi hata ya Wabunge ) huku Posho zao kila wakiruka ( wakipaa ) ni USD 200 lakini bado walitishia Kugoma ili waongezewe.

Huko nyuma nami GENTAMYCINE nilikuwa ni Muumini wa 'Kukurupuka Kudemka' hasa Kushangaa Wabunge wakitaka Kuongezeka Mishahara yao ili nilivyokaa Siku moja na Mbunge fulani na akanichambulia jinsi Pesa zao zinavyotumika na kuishia kwa Kuwasaidia Wananchi ambao 24/7 huwapelekea Shida zao mbalimbali kiukweli wakidai hiyo nyongeza ni halali ( haki ) yao.

Tatizo Kubwa nililoligundua humu Mtandaoni ( Mitandaoni ) ni kwamba kumekuwa na 'Kautamaduni' ambako naona kana Ushamba na Upumbavu mwingi ambapo Watu tumekuwa 'tunahemka' kwa Hisia zetu tu za Itikadi ya Vyama vyetu vya Kisiasa pamoja na Chuki kwa Bunge lenye Wabunge wengi wa CCM na Serikali yake pia ila hatutaki Kujishughulisha kutumia Akili zaidi ya Kutafakari na Kuchambua jambo.

Nimalizie tu kwa Kuwauliza je, nyie mnaopinga Wabunge Kuongezewa Mshahara au hata Watu wa Kada zingine Kupandishiwa Mishahara nyie mngekuwa ndiyo Wabunge au Watu hao mngekuja humu Mitandaoni na Kukataa kuwa isipandishwe?

Ifike muda tupunguze Nongwa na Wivu.
Mimi bado naamini mbunge analipwa pesa nyingi pasipo na ulazima.

Kusaidia wananchi kipesa siyo takwa la kisheria, ni utashi wa mhusika. Kama amekuchambulia na matumizi makubwa kaonyesha ni kusaidia wananchi kifedha hiyo ni juu yake. Tunavyojua ni wabunge wachache waliwahi kutoa/ wanatoa pesa zao mfukoni kuhudumia miradi Mo Dewj akiwa kinara, wengine wengi husubiri pesa ya serikali.

Leo hii wafanyakazi wa kada za msingi kabisa wanalipwa hela ya kawaida tu, kada ya elimu na afya zikiongoza kulipwa pesa kidogo kulinganisha na umuhimu wao sasa mbunge anaingia mule anasubiri kupiga makofi na kumsikiliza Ndugai halafu ana posho ya ya zaidi ya 300K per kikao.

Bora huyo rubani atasema anaweza kufa akiwa kazini maana hata kusinzia haitakiwi. Wabunge hadi kulala wanalala.
 
Back
Top Bottom