Sakata la malipo ya korosho sehemu ya pili, Tandahimba kimenuka..!

wendawazimu kwelikweli. moja ya sababu za polisi kuwa na kawaida ya kukataa maandamano, ni baadhi ya wanaojivika waandamanaji kujiingiza katika unyang'anyi. wengi watapenda kujipitisha karibu na maduka yenye mali rahisi za kubebeka na kubomoa na kuzibeba

Yaani wizi tu unaoendelea.. Kifupi maandamano yalikuwa juzi na yalitambulika,lakini kwa kutopata majibu yaliyowaridhisha kutoka kwa DC,ndiyo wakapanga haya yaliyotokea leo..
 
Kufuatana na madai ya wakulima wa Korosho kukawia kulipwa,wananchi wameamua kufanya fujo za wizi na maandamano yasiyo halali,na kupora raia wengine...

Maduka yamefungwa,na huenda na risasi za moto zikawa zinatumika kwa kupigwa hewani..

More updates to follow..

Sasa wanakata miti na 'chain saw' inaangukia barabarani,ili magari yasipite..
Na wanataka kuanza kukata hadi nguzo za umeme....! Wanaona ngumu wanaamua kuzimwagia petroli,na kuchoma moto..

Magari na mabasi ya mikoani yameshindwa kufika mjini hapa.. Mf. Tandahimba Express..magogo makubwa kila mahali!

SASA WAANDAMANAJI HAO WANAVAMIA NYUMBA ZA MAASKARI POLISI,NA WANACHUKUA CHOCHOTE KINACHOBEBEKA.. MAPOLISI KARIBU WOTE WAMEIBIWA KWA LAZIMA,UWEPO,AU USIWEPO!



source: mimi mwenyewe

Wenzetu mmeamua! hakiyamguu, kama mpaka sasa no sign ya utulivu! giza likiingia na ubakaji utaripotiwa! hata mauaji si ajabu. umetoka wapi ujasiri huu wa misri. au maandamano yalianza baada ya swala ya ijumaa!!
 
Wenzetu mmeamua! hakiyamguu, kama mpaka sasa no sign ya utulivu! giza likiingia na ubakaji utaripotiwa! hata mauaji si ajabu. umetoka wapi ujasiri huu wa misri. au maandamano yalianza baada ya swala ya ijumaa!!

Nadhani kuna watu ambao ni vibaka tayari,au wenye tamaa ila wanangoja matukio kama haya ili watekeleze uhalifu..
 
kika huu ni udhaifu mkubwa sana kwa serikali ya bwan JK..... ikifika mahali serikali inatumia jeshi la polisi ili kuzima vuguvugu la wananchi kutafta haki yao basi ndio mwanzo wa kufanya na kupoteza mvuto katika jamii husika...... poleni wana tandahimba ila haki yenu ipo tu hata kama wakiichelewesha kwa mabomu
 
Hujui maana ya ghadhabu wewe!

Hiyo sio Ghadhabu ni upumbavu; hao ndio wanao gombana ndani ya nyumba na mkewe au mumewe afu unakimbilia kuvunja vyombo vyote au kuchoma nyumba moto"; Huwezi choma nguzo za umeme afu et wasema una ghadhabu la hasha, afu kesho watakuja kulalamika hawana umeme hiyo akili matope!!
 
Nawachukia sana wabunge wafuatao
1.Njau(Tandahimba)
2.mkuchika(Newala)
3.Hawa(mtwara vijijin)
Sijaona wakitetea maslai ya wapiga kura
 
Na Tandahimba huo mchezo wa magogo njiani haujaanza leo! Wasikate tu nguzo za umeme yakawa kama yale ya Newala sikumbuki mwaka.
 
Huu ndiyo mwisho wa kufikiria wa Kikwete na Pinda, kwamba watu wakiandamana kudai haki yao suluhisho ni mabomu ya machozi na risasi za polisi. Lakini na hao wananchi wana sababu gani ya kuwapora wenzao? Mgomvi wao ni serikali au wavuja jasho wenzao? Waandamanaji nao ni wendawazimu kama ndiyo hivyo!

mkuu, niko curious kidogo. kwenye mgomo wa madaktari uli-side na upande upi....wa ma-dr au pinda & co??
 
sema sehemu zinazoongozwa na ccm polisi hawawapi mabomu. hapo wamepiga mabomu yote yameisha. sasa hivi polisi watakuwa wanakamatwa kama kuku. Bunduki wanazo za kukabidhiana yaani walioko zamu ndo wana bunduki. wengine wote hamna kitu ndo maana wakakimbia.
 
Hiyo sio Ghadhabu ni upumbavu; hao ndio wanao gombana ndani ya nyumba na mkewe au mumewe afu unakimbilia kuvunja vyombo vyote au kuchoma nyumba moto"; Huwezi choma nguzo za umeme afu et wasema una ghadhabu la hasha, afu kesho watakuja kulalamika hawana umeme hiyo akili matope!!

Natafuta cha kukuambia, kwa kifupi action and reaction are equal ......., akili inabaki kuwa ile ile.
 
CCM wanatekeleza sera ya kilimo kwanza na mapinduzi ya kijani!!
 
nawachukia sana wabunge wafuatao
1.njau(tandahimba)
2.mkuchika(newala)
3.hawa(mtwara vijijin)
sijaona wakitetea maslai ya wapiga kura

kwani hao ni wabunge wa chama gani? Kumbe magamba! Umekoseaaaa! Mbona posho walizitetea sana? Walidai wao humgawia kila mwananchi wa jimboni kwake.
 
Kule mbeya Mr. Sugu Mbunge aliyechaguliwa na watu alienda kuwaomba wapigakura wake watulie kufuatia vurugu za maana dhidi ya serikali nao wakatulia, Unadhani mbunge wa huko akija wapigakura wake wataheshimu uwepo wake?

We, thubutu, wakati alimuibia kijana wa cuf kura? akienda watammaliza kwanza yeye. na sijui kama anafika jimboni tandahimba
 
Back
Top Bottom