Sakata la malipo ya korosho sehemu ya pili, Tandahimba kimenuka..!

Hivi maana yake ni nini?
Ni mfumo ambao Serikali kupitia vyama vya ushirika hukusanya mazao ya wakulima
kwa lazima (Utake usitake) na kuyauza huko mnadani kwa bei ambayo mkulima haijui
na kisha hukaa na kujadili mkulima alipwe kiasi gani.
 
Kwa taarifa nilizonazo kutoka kwa askari ambaye si msemaji
wa jeshi la polisi ni kwamba kuna askari wameongezwa kutoka
Lindi lengo ikiwa ni kuimarisha mapambano na wananchi.

Nataka nitoe ufafanuzi kidogo wa kilichokuwa kinatokea
maana nashukuru Mungu nimeshaondoka eneo la Tukio na sasa
niko Dar, nimeingia saa 9 usiku huu.

Kwa taarifa nilizonazo mpaka sasa ni kuwa nyumba nyingi ambazo
zinavamiwa ni zile ambazo wanaishi Polisi, wafanyakazi wa TANECU,
na wale wanaofahamikawazi kuwa ni wafurukutwa wa CCM.
Polisi wanavamiwa kwa sababu ambazo nafikiri ni KISASI kwani
wakati wa uchaguzi Polisi waliwapigawatu na kupiga mabomu ya
machozi mitaani wakati hakukuwa na vurugu yoyote, Hii ilitokana
na kutangaza matokeo ya ubunge ambayo wenyewe walijua wazi
kuwa ni batili.

Nyumba yangu pia ni miongoni mwa nyumba zilizovunjwa kwani
nilipangisha askari Polisi, Sisikitiki kwa lolote kwani hakuna sauti
nzuri zaidi kwa serikali zaidi ya hiyo. ALUTA CONTINUA
.

Pole sana mkuu, hizo ndiyo gharama za kudai uhuru mpya, ALUTA CONTNUA.
 
ni mfumo ambao serikali kupitia vyama vya ushirika hukusanya mazao ya wakulima
kwa lazima (utake usitake)
na kuyauza huko mnadani kwa bei ambayo mkulima haijui
na kisha hukaa na kujadili mkulima alipwe kiasi gani.

hiki ni kitu kibaya sana kiuchumi......ni mfumo wa kijamaa wakati nchi iko katika soko huria
 
Acha uzushi, wanaoshambuliwa kwa kiasi kikubwa ni askari ingawa kuna wanaotumia mwanya
huo kufanya mambo yao. Rafiki yangu ni mmakonde lakini nyumba yake imevunjwa pia kwa sababu
amepangisha askari. Acha kutumiwa na kupotosha wewe hakuna tatizo la ukabila kule!

hakuna nyumba ya mmakonde iliyovunjwa. Kama una uhakika itaje. Mtu aliyevunjiwa nyumba kwa kupangisha askari anatokea kilwa. By the way, wewe kwa akili yako unaona ni poa tu kuvunja nyumba ya mtu kwa sababu tu amepangisha askari? Pathetic!
 
utaratibu wa kusuburi serikali ifanye ama kutimiza ahadi kwa tanzania utaratibu huu umrshashindwa serikali setu si sikivu tena ni waongo wakubwa, wamekuwa wanaendesha mambo ya muhimu kwa taratibu bila shida yoyote bila shinikizo mambo hayatabadilika.
chen ten jana niliona jinsi wakulima wanavyolalamika.na vurugu walizofanya.
kwa kweli serikali ijirekebishe vinginevyo yenyewe ndio inayosababisha vurugu.
 
hakuna nyumba ya mmakonde iliyovunjwa. Kama una uhakika itaje. Mtu aliyevunjiwa nyumba kwa kupangisha askari anatokea kilwa. By the way, wewe kwa akili yako unaona ni poa tu kuvunja nyumba ya mtu kwa sababu tu amepangisha askari? Pathetic!
Sitaitaja hiyo nyumba abadani kwa sababu nimeuona mtego uliopo hapa
ambao ni wa KIINTELEJENSIA zaidi. Siungi mkono kuvunja nyumba za watu
kwa sababu ya kupangisha askari lakini najua kunako vita mengi hutokea.
I think it is a cost of freedom.
 
Tarehe 11-04-2012 chama cha wananchi (cuf) kiliitisha maandamano makubwa ya wakulima kuishinikiza serikali kulipa malipo hayo ambayo wakulima wameendelea kusubiri kwa takribani miezi mitano sasa! Mkuu wa wilaya aliwajibu kwa kejeli na dharau waandamanaji hao kwamba yeye hajui chochote kuhusiana na korosho wala si wajibu wake kulishughulikia tatizo hilo, kwa hasira wananchi wameziba bara bara ya mtwara/newala na zile za vijijini pia ktk baadhi ya vijiji wamefunga shule za msingi na sekondari.
SOURCE_PRIDE FM

Hii hatari
 
Back
Top Bottom