Jamani sisi tulioko huku mikoani tunaomba Live Press Conference mtuwekee tujue kinachoendelea tafadhali!
Mawani yangu yameposuka, hebu mtu asome hapo kwenye bold!
Tundu Lissu amefanya Press muda mfupi uliopita. Anasema
1. Anafungua kesi Mahakama kuu kuiomba iiamuru Mahakama ya Kisutu kuendelea kusikiliza kesi ya awali iliyofutwa na DPP katika kesi inayomhusu Lwakatare kwani DPP amevuka mipaka yake inayomruhusu kufuta kesi na isitoshe kesi aliyofungua ni ile ile hivyo Mahakama iamuru shauri la awali liendelee.
2. Kuhusu video iliyoonyeshwa kwenye mitandao Lissu anasema kuna mashaka makubwa sana kuhusiana na video ile na kisheria kesi hiyo ikifika mahakamani haitachukua hata nusu saa ataibuka mshindi.
Lissu anasema
- Hakuna mtu anayepanga mauaji katika hadhara mahali ambapo watu wanapitapita kama inavyoonekana kwenye video ile.
-Lwakatare kama alirekodiwa basi lazima ielezwe je ilikuwa ni kwa hiari yake kama si hivyo ni makosa
-Issa Michuzi Mpiga picha wa Rais alikuwa akipongezana na watu wa Ikulu wenzake kuwa TISS (Usalama wa Taifa) wamefanya kazi nzuri kwa kurekodi ile video. Kisheria usalama wa taifa hawatakiwi wala hawaruhusiwi kurekodi au kuvifanyia ushushu vyama vya siasa kwa maslahi ya Chama tawala.
-Ludovick baada ya kukutana na Rwakatale tarehe 28Dec saa 5 muda mfupi baadae yaani saa 5:59 alimpigia simu Mwigulu Nchemba kwa kutumia namba ya simu ya Mwigulu ambayo ameiandikisha kwenye kumbukumbu na vitabu vya Bunge Lissu anadai wana rekodi ya mazungumzo yao.
-Siku iliyofuata tarehe 29Dec akiwa kwenye kipindi cha Tuongee asubuhi cha Star TV alidai ana mkanda wa video unaowaonyesha CHADEMA wakipanga mauaji.
-Pia amedai itabidi waambiwe video hiyo imerekodiwa studio gani, maneno gani yameondolewa na yapi yameongezwa.
Anamalizia kwa kusema walianza kwa kusema CHADEMA ni chama cha familia wakashindwa, wakasema ni chama cha wachaga wakashindwa, wakesema ni chama cha wakatoliki wakashindwa, wakasema ni chama cha wakristo wakashindwa, wakasema ni chama cha ukanda wakashindwa leo wanasema ni chama cha kigaidi WATASHINDWA. Press nzima itakuwa www.chadema.tv muda mfupi ujao
Nyongeza: kuhusu video amesema tayari kuna ushahidi wa kimawasiliano baina ya Mwigulu Nchemba ya tarehe 28.12.2012 wakiwasiliana na Ludovick saa 5:55 asubuhi , na Lwakatare amesema kuwa yeye alikutana na Ludovick kuanzia saa tano asubuhi tarehe 28.
hapo vipi, unaweza kuona bila miwani!?Mawani yangu yameposuka, hebu mtu asome hapo kwenye bold!
tundu lissu siku ile alijidhalilisha sana pale mahakamani mpaka akachekwa na umati wa watu!!!
How? alisema nini? na unahisi umati ulicheka kwasababu gani? umati ulimcheka Lisu au ulichekeshwa kwa jambo lingine? ZeMarcopolo ni miongoni mwa watu wachache sana nisiowaelewa kabisa hapa Jamvini!!!!
Mbona wanasheria hawasemi ile video ni fake?
Kama ule mkanda nk genuine basi huo ni ugaidi.
Maelezo aliyotoa Lwakatare polisi kuhusu maneno yaliyoko kwenye video alisema kuwa yeye anakumbuka siku ya tarehe 28, alikuwa nyumbani kwake na Ludovick ndio alienda kwake , ila picha ya video ni ya kwake , sura ni ya kwake ila baadhi ya maneno yaliyoko sio ya kwake na ameandika hivyo , kwa hiyo kuhusu ukweli wa mkanda majibu ya kina yanatakiwa kutoka polisi , Mwigulu na Denis ndio wanajua nini kipo kwenye mkanda . Hivyo picha limeanza kuonekana , na kwa taarifa zaidi ni kuwa polisi wana video yenye dakika 27.06 na maneno yanatofautiana sana na yaliyoko kwenye You tube iliyowekwa kwenye mitandao .
Pia amedai itabidi waambiwe video hiyo imerekodiwa studio gani, maneno gani yameondolewa na yapi yameongezwa.
Naona kidogokidogo chadema wanaanza kumtema Ludovick.
Vilevile kidogokidogo wananza kukubali kuwa video ya Lwakatare sio fake.
Dr. Slaa amejidhalilisha sana kumtetea Lwakatare kabla hajajua nini kinaendelea.
Pasco aliwapa ushauri wa thamani kubwa sana wa kumkana Lwakatare mkaukataa, sasa muda wa kufanya hivyo umeshapita. La Lwakatare ni la chadema, hamuwezi kujitenga nae...
Stay tuned...
sina imani kama kweli kwa hali ya Tz mahakamani ni sehemu ya kupatia haki kwa mwenendo wa mambo sasa yanavyokwenda kisiasa, yani kila kitu ni siasa
huu muda wa kubabikiziana mi-kesi isiyo na manufaa kwa taifa tungeutumia kutengeneza mitaala ya elimu ambayo hatuna tangu uhuru - eti UGAIDI, hivi mnacheza na UGAIDI nyie? hiyo kidnapping mnaita ugaid? police wa tanzania wanaseza kupeleleza UGAIDI?
nafikiri Tanzania mnautaka UGAIDI mtaupata, kama mlivyouomba udini na ukabila.
Nia ya hawa watu ni kutafuta wakubwa wa chama cha CHADEMA ili ionekane ndio waliomtuma Lwakatare apange njama za uharifu huo!!! Wamesahau kuwa CHADEMA kuna wanasheria wa kuchunguza na kutoa utetezi ulio halali badala ya viini macho!!! CCM imeishiwa sera wakalale kazi yao imekwisha!!!Baada ya mabishano ya kisheria, juzi mahakamani , hakimu alisema angetoa hukumu juu ya kama mashitaka ni sahihi kwa mujibu wa sheria ama laa, ila jana asubuhi badala ya kusubiria hukumu ya awali juu ya uhalali wa mashitaka hayo hawakusubiri hukumu badala yake walipeleka hati ya kufuta kesi na baada ya dakika tano walimkamata na kumfungulia mashitaka yale yale , ila kilichobadilika. Ni namba ya file ya kesi tuu , ila mashitaka ni yaleyeale mpaka nukta ya mashitaka.
Lengo lilikuwa ni kuizuia mahakama isitoe uamuzi ndio maana waliamua kufuta kesi na kuifungua hiyo hiyo,