Sakata la Lissu "Handle with care"

Sakata la Lissu "Handle with care"

Huwa wanamuita Mbowe kwa kebehi kuwa ni DJ, lakini ukweli ni kuwa kama ni DJ basi ni wa ukweli kwani kila muziki anaouweka Ccm wanaucheza na serikali wananengua mpaka basi.

Kamusi iko wazi kuhusu neno Dikteta jee wanashindwa kulisoma na kujua tafsiri yake kuwa sio matusi?

DJ Mbowe shusha CD za kutosha kwa mtindo wa bandika bandua wacheze mpaka nyonga zifyatuke.

Leo ni Lissu, kesho CD nyingine, hivyo hivyo hadi sept1 hapo ndio unashusha remix
Dj ameweka CD ya makirikiri sasa hivi Mwigulu Nchemba na vijana wake majasho yanawatoka wanasakata makirikiri pale uwanja wa taifa
 
Huwa wanamuita Mbowe kwa kebehi kuwa ni DJ, lakini ukweli ni kuwa kama ni DJ basi ni wa ukweli kwani kila muziki anaouweka Ccm wanaucheza na serikali wananengua mpaka basi.

Kamusi iko wazi kuhusu neno Dikteta jee wanashindwa kulisoma na kujua tafsiri yake kuwa sio matusi?

DJ Mbowe shusha CD za kutosha kwa mtindo wa bandika bandua wacheze mpaka nyonga zifyatuke.

Leo ni Lissu, kesho CD nyingine, hivyo hivyo hadi sept1 hapo ndio unashusha remix
 
Kuna kitu kinaitwa Presidential Decree.
Huko tulishatoka zamani sana,sasa tunaongozwa na katiba!Kipindi hicho Rais akisema jambo ndio linakuwa sheria hata angesema kuanzia leo kigoma inakuwa sehemu ya burundi,ndio inakuwa hivyo!Si sasa ambapo tuna muongozo wa uongozaji serikali!
 
Nimesikia et kamanda wa police Singida anadai wanawasiliana na TCRA et wamfungie Lissu kwny mitandao ya kijamii.
Kisa aliwezaje kutuma jumbe huko baada ya kukamatwa.VITUKO
 
Watawala wanachoshindwa kukifahamu ni kwamba kuna watu ambao wamejitoa kafara kwa alili ya kuwatetea wananchi na wako tayari kwa lolote,wako tayari hata kukatwa kichwa ilimradi wahakikishe adhima yao inatimia.

Watu wenyewe ni kama hawa wa aina ya Lissu ambao huwezi ukawanyamazisha kwa kuwakamata na kuwafunga gerezani na hata kama utatumia mabavu yako kwa kuwafunga bado wataendelea kupiga kerere hukohuko gerezani.

Na usipotumia akili jinsi ya kudili na watu wa aina hii utaishia kuwapaisha bure kwa kuwa ulishindwa namna ya kuchukuliana,kama siyo kuwapaisha utajikuta unawakata vichwa.

Ukifiri kuwa ndiiyo njia kumaliza tatizo kumbe ndiyo unazalisha tatizo lingine,kwa kuwa unapomkata Lissu kichwa ndiyo wanazaliwa akina Lissu wengine maelfu na maelu na huku jela inakusubiri kwa kuwa hakuna atakayekubaliana na wewe umkate mwenzako kichwa kwa kuwa mmetofautiana naye kimtazomo.

Na kwa kuwa wewe ni mbabe unayemiliki vyombo vya dola basi unahaki ya kujifanyia chochote unachotaka na huku watu wakikuchekea na kukupigia makofi pwaa,pwaa kama mazuzu vile.

Makaburu wa Afrika ya kusini waliwaua wapinzani wao na kumfunga Mandela wakiamini kuwa hiyo ndo njia sahihi ya kuwanyamazisha wapinzani wao haki ya kudai haki yao.

Mwisho wake waliishia kubana makalio yao na kupiga saluti mamilioni na mamilioni kwa mtu waliye mnyanyasa na kumdhihaki huku wakiimba tata Madiba Nelson Mandela.
Tatizo kubwa la watawala wetu ni kuishi zama za akina Nyerere, Kenyata sr, Idd Amini nyakati ambazo viongozi walikuwa miungu watu.

Leo ni tofauti kabisa na wanavyodhani, uelewa wa watu umeongezeka na ule woga wa vitisho vya serikali umepungua.

Watu kama Lissu, Seif, Lema, Sugu, marehemu Mtikila si watu wa kutishia kuwakamata.

Kuliko kuendelea kuvimbiana serikali ingetumia busara zaidi kuliko nguvu ku handle issue kama hizi.
 
Sasa unadhani serikali haijui...mtu akishakua na serikali sio mwenzako, CCM ni Chama dola..
 
Tumeshuhudia siku za hivi karibuni polisi imekuwa ikihangaika na matamshi ya Mbunge wa Singida Mashariki Mh. Tundu Lissu kuwa rais Magufuli ni "dikteta uchwara".

Hebu tujiulize nini hasa lengo la hili sakata kwa pande zote zinazovutana.

Haiwezekani mtu unakamatwa/shitakiwa kwa kosa fulani halafu unarudi kutenda kosa lilelile tena nje tu ya jengo la mahakama.

Binafsi naona ni kama kuna mtego fulani kwa chama tawala utakaohitimishwa September 1, chini ya Operation UKUTA.

Nafikiri nia hasa ya Chadema ni ama Lissu afungwe au awekwe ndani ipatikane sababu ya kufanikisha operation hiyo.

Lengo lingine nafikiri ni kukiweka chama kwenye headline kwa muda mrefu na kufifisha ziara za mtukufu rais zinazoendelea. Kumbuka kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Mh. Mbowe alisema wanauwezo wa kufanya siasa ndani na nje ya bunge.

Lengo lingine "nafikiri" ni mkakati wa kumuandaa mtu atakayeaminiwa na kuonewa huruma na jamii (Mandela style) ili labda baadaye aje kugombea cheo kikubwa ndani au nje ya chama.

Lengo lingine nafikiri ni kuionyesha dunia na watanzania kwa ujumla kuwa serikali ya Magufuli ni ya kidikteta inayovunja katiba yake ili kuthibitisha maneno ambayo yamekuwa yakisemwa na chama hicho.

Serikali ijue Chadema ni chama kikubwa kina uzoefu mkubwa kina wanasiasa wazoefu na wakongwe, hivyo kina mikakati yake na mbinu mbalimbali za kujiimarisha. Hivyo, serikali isilichukulie sakata la Lissu kama jambo dogo, should handle this issue with care.

Kumbuka moto huanza na cheche moja baadaye husambaa na kuunguza msitu mzima.

Haya ni mawazo yangu binafsi.
1.Jpm ana pambana na waliotokana na utawala wa Jk
2. LISSU ANAPAMBANA NA JPM
 
Sijui karogwa na nani mwanzo hata mi nilifikiria kumpa kura yangu 2020 ila sasa mmh, nishaghairi
Usighairi bado mapema mno hata mwaka hajamaliza.

Ila ukilinganisha imani ya wananchi kwa Magufuli na Kikwete kwa mwaka wa kwanza wa Utawala wao, ya Magufuli inaporomoka kwa kasi ya ajabu.
 
Hivi serikali inatumia kiasi gani kufukuzana na huyu jamaa???..
 
Back
Top Bottom