Sakata la Lissu "Handle with care"

Sakata la Lissu "Handle with care"

Kwetu kuna methali inayosema, baadhi ya matukio ni nzi katoka kwenye kinyesi.ikimaanisha kuwa nyuma ya pazia kuna jambo kubwa zaidi linapangiliwa.Siasa hizi za kujengeana fitina ni za kitambo,na kwa bahati mbaya,kutokana na upofu wa kutaka madaraka hawa wapanga mikakati hawasemi mema yanayofanywa na Serikali.watu wote wenye mapenzi mema na nchi yetu, tunaona jitihada KUBWA NA YA DHATI inayofanywa na JPM, hakuna masika yasiyokuwa na umbu.hiyo ndo fact.
 
Watanzania wengi tumeishamchagua rais.
Mkuu kwani kura zimeshahakikiwa na WAtanzania wengi hadi useme watanzania Wengi wamemchagua? Kumbuka Tume si huru imechaguliwa na mwenye nchi kama Shamba la Bwana Kheri
 
Haya maoni niliyatoa mwaka jana Aug.5.
Lengo lingine "nafikiri" ni mkakati wa kumuandaa mtu atakayeaminiwa na kuonewa huruma na jamii (Mandela style) ili labda baadaye aje kugombea cheo kikubwa ndani au nje ya chama.

Haya ni mawazo yangu binafsi.
 
Tumeshuhudia siku za hivi karibuni polisi imekuwa ikihangaika na matamshi ya Mbunge wa Singida Mashariki Mh. Tundu Lissu kuwa rais Magufuli ni "dikteta uchwara".

Hebu tujiulize nini hasa lengo la hili sakata kwa pande zote zinazovutana.

Haiwezekani mtu unakamatwa/shitakiwa kwa kosa fulani halafu unarudi kutenda kosa lilelile tena nje tu ya jengo la mahakama.

Binafsi naona ni kama kuna mtego fulani kwa chama tawala utakaohitimishwa September 1, chini ya Operation UKUTA.

Nafikiri nia hasa ya Chadema ni ama Lissu afungwe au awekwe ndani ipatikane sababu ya kufanikisha operation hiyo.

Lengo lingine nafikiri ni kukiweka chama kwenye headline kwa muda mrefu na kufifisha ziara za mtukufu rais zinazoendelea. Kumbuka kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Mh. Mbowe alisema wanauwezo wa kufanya siasa ndani na nje ya bunge.

Lengo lingine "nafikiri" ni mkakati wa kumuandaa mtu atakayeaminiwa na kuonewa huruma na jamii (Mandela style) ili labda baadaye aje kugombea cheo kikubwa ndani au nje ya chama.

Lengo lingine nafikiri ni kuionyesha dunia na watanzania kwa ujumla kuwa serikali ya Magufuli ni ya kidikteta inayovunja katiba yake ili kuthibitisha maneno ambayo yamekuwa yakisemwa na chama hicho.

Serikali ijue Chadema ni chama kikubwa kina uzoefu mkubwa kina wanasiasa wazoefu na wakongwe, hivyo kina mikakati yake na mbinu mbalimbali za kujiimarisha. Hivyo, serikali isilichukulie sakata la Lissu kama jambo dogo, should handle this issue with care.

Kumbuka moto huanza na cheche moja baadaye husambaa na kuunguza msitu mzima.

Haya ni mawazo yangu binafsi.
Mawazo haya bado yanaishi, bado namuona Lissu kama icon fulani itakayokuja kuleta mabadiliko nchini.
 
Back
Top Bottom