Sakata la Lissu "Handle with care"

Sakata la Lissu "Handle with care"

Hivi serikali nzima inashindwa akili na mtu mmoja?

Hapo ni man against man.

Mtu ndiye anayeongoza hoja za serikali na mtu ndiye anayeongoza hoja za wapinzani dhidi ya serikali.

Hakuna Aliyeshuka toka mbinguni. Wote ni wanadam na wote ni watanzania. Wote wanapata uongozi kupitia binadam wengine.
Jambo baya ni kuanzisha siasa zisizojali uhai na utu wa watu wengine.
Taifa halina raha ,watu wanaishi kwa huzuni na woga.
Hawa wanawawinda wengine kama swala na wengine nao wanaruka ruka huku na kule kutafuta pa kujificha nyuma ya wananchi.

Hawa wanatafuta huruma ya wananchi na hawa wanatafuta ulinzi na nguvu za silaha na majeshi.
Sheria na katiba zimewekwa pembeni.

Chadema kama Katiba inakiukwa nendeni Mahakamani. Kwa nini mnatumia nguvu zenu wenyewe wakati mahakama zipo.
Serikali inavunja katiba lakini Chadema nao wanavunja sheria na katiba kwa kuchukua sheria mikononi.
Tamko la polisi linaweza kupingwa mahakamani na sio maandamano na maneno ya kejeli au matamko.
 
Usighairi bado mapema mno hata mwaka hajamaliza.

Ila ukilinganisha imani ya wananchi kwa Magufuli na Kikwete kwa mwaka wa kwanza wa Utawala wao, ya Magufuli inaporomoka kwa kasi ya ajabu.
na umaarufu unapukutika kweli!
 
nami naunga mkono hoja . mkuu yeye ashughulikie ishu za msingi za taifa hili ambazo miaka mingi watanzania wamekuwa wakizililia na fisiemu wamekuwa wakiwanyonya watanzania wengi.Yaani kama kauli mbiu yake ya hapa kazi tu, basi atambue kuwa hakuna kazi yoyote ambayo huwa haikosi maneno, na mtu mvivu huwa anakatishwa tamaa na maneno ya watu na mwisho asifanye kazi kabisa,na kamwe jua halimsubiri mvivu.
Nashauri, wakati anaowahofia wakisema, asijali yeye aendelee na kazi, mwisho wa siku itafahamika, hakuchaguliwa na wananchi ili kupambambana na wapinzani, alichaguliwa kwa sela zake za kuondoa umasikini na kuleta usawa kwa watanzania... asipoteze muda na nguvu kwa kupambana na wapinzani, wapinzani aliwakuta na atawaacha, hata nyumbani kwake wapinzani wapo, wasimpotezee malengo yake na mwisho wa siku anakuja kukumbuka shuka wakati kumeshakucha...na pia mkuu, asisahau kuwa kelele za chura hazimzuii ng'ombe kunywa maji.....aendelee na sera yake ya kutumbua majipu na kukomesha mafisadi katika nchi hii, wapinzani awaaache kwani aliwakuta na atawaacha, wasipompinga hadharani watampinga chini kwa chini,yeye afanye kazi aliyowaahidi wananchi . Huwezi kuzuia maneneo ya watu, pinga maneno ya watu kwa kufanya kazi basi, na mwisho watakuheshimu na hata upinzani huo utaumaliza kwa kufanya kazi.
 
Wapinzani wanasema mikutano na maandamano ni haki yao kikatiba na kisheria. Sasa rais angetuambia yeye anazuia mikutano na maandamano ya vyama vya siasa kwa sheria ipi?
Hapo sasa! Na je CCm sio chama cha siasa? Kama ni chama cha siasa mbona majuzi kimefanya mkutano wake Dodoma? Mbona yeye anaendelea na mikutano yake ya hadhara na wanachama wake wanaonekana wamevaa rangi za chama cha siasa!

Nani haoni hayo manyanyaso kwa vyama vya siasa!
 
By tyhe way who is mtukufu? Nafikiri mleta mada ana mawazo mtindio
 
nami naunga mkono hoja . mkuu yeye ashughulikie ishu za msingi za taifa hili ambazo miaka mingi watanzania wamekuwa wakizililia na fisiemu wamekuwa wakiwanyonya watanzania wengi.Yaani kama kauli mbiu yake ya hapa kazi tu, basi atambue kuwa hakuna kazi yoyote ambayo huwa haikosi maneno, na mtu mvivu huwa anakatishwa tamaa na maneno ya watu na mwisho asifanye kazi kabisa,na kamwe jua halimsubiri mvivu.
Nashauri, wakati anaowahofia wakisema, asijali yeye aendelee na kazi, mwisho wa siku itafahamika, hakuchaguliwa na wananchi ili kupambambana na wapinzani, alichaguliwa kwa sela zake za kuondoa umasikini na kuleta usawa kwa watanzania... asipoteze muda na nguvu kwa kupambana na wapinzani, wapinzani aliwakuta na atawaacha, hata nyumbani kwake wapinzani wapo, wasimpotezee malengo yake na mwisho wa siku anakuja kukumbuka shuka wakati kumeshakucha...na pia mkuu, asisahau kuwa kelele za chura hazimzuii ng'ombe kunywa maji.....aendelee na sera yake ya kutumbua majipu na kukomesha mafisadi katika nchi hii, wapinzani awaaache kwani aliwakuta na atawaacha, wasipompinga hadharani watampinga chini kwa chini,yeye afanye kazi aliyowaahidi wananchi . Huwezi kuzuia maneneo ya watu, pinga maneno ya watu kwa kufanya kazi basi, na mwisho watakuheshimu na hata upinzani huo utaumaliza kwa kufanya kazi.

Big up umesema vema, na pia wapinzania sio maadui wa maendeleo yetu bali ufisadi, elimu duni hasa kwa watendaji na upindishaji haki.
 
Sasa unadhani serikali haijui...mtu akishakua na serikali sio mwenzako, CCM ni Chama dola..
Lini mawazo ya kizamani yatawatoka akilini? Bado hamjui kuwa hii ni dunia nyingine?
Muulize Kenyatta akuambie jinsi ambavyo ni amiri jeshi mkuu Kenya lakini kule Uholanzi alikuwa ana kaa na kusimama kwa heshima kizimbani.
 
Dah neno mtukufu huwa linanipa ukakasi hasa likitumiwa vibaya!!hata Mungu hapendi.
 
Wapinzani wanasema mikutano na maandamano ni haki yao kikatiba na kisheria. Sasa rais angetuambia yeye anazuia mikutano na maandamano ya vyama vya siasa kwa sheria ipi?
Hakuna sharia hapa yeye anataka maendeleo.
 
Ukitegemea jua kuja kukausha nguo zak utapotea buree,,,,,,,,acha upepo uje uzikaushe,,,mwenye akil kanielew
 
Hlo jina la Dikteta Uchwara akiendelea kulikataa niiteni mimi basiiii maana mwenye nalo kalikataa aisee
 
Wapo smart hao hakina Lissu.Wamejipanga.
Ni vita ya miguvu dhidi ya maarifa.
 
Wapinzani wanasema mikutano na maandamano ni haki yao kikatiba na kisheria. Sasa rais angetuambia yeye anazuia mikutano na maandamano ya vyama vya siasa kwa sheria ipi?
"Tukisema mamlaka ya Rais kuzuia shughuri za kisiasa hayapo kikatiba, CCM wenzetu watatupiga mawe maana wote wanasifu na kuabudu tu wakiamini ni MTUKUFU, na tukisema mamlaka ya upinzani yapo kikatiba kufanya siasa, wananchi watatuuliza sasa mbona nyie CCM hamsidiki...."

Two Lumumbaz in a room discussing the ongoing issue....
 
Back
Top Bottom