Sakata la kuuzwa UDA: Kauli za Idd Simba, Masaburi, Kisena et al utata mtupu

IDD SIMBA MWIZI ndiye kafanya mpaka leo sukari iwe sh 2000 kwa kg kwa kuruhusu waingizaji wa 3 tuu wa sukari toka njee!huko yeye akijifanya kutoa kibali kwa jwtz kuingiza sukari kumbe ni dili lake
 
This is the same idi simba who was the champion of " wazawa "is now tarnished " if man can be so unjust to his fellow man whom can u trust ?" if this issue is right than he surely has let us down...he took ou venom against wahindis an now they are having the last laugh!
 
• Idadi ya watuhumiwa yaongezeka kila kukicha

na Salehe Mohamed, Dodoma


TUHUMA mpya za ufisadi zinazolizunguka Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), zimezidi kuongeza idadi ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaokabiliwa na kuhusishwa na tuhuma za ufisadi, Tanzania Daima Jumapili limebaini.
Ongezeko hilo la watuhumiwa wa ufisadi ambao takriban wote ni viongozi au makada wa chama hicho tawala, kunazidi kukiweka chama hicho katika hatua ngumu ya kuweza kujisafisha kutoka katika dimbwi la tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka, ubadhirifu wa fedha na mali ya umma na matendo mengine yenye mwelekeo wa uhujumu wa uchumi.

Kuibuka kwa tuhuma hizo mpya za ufisadi ndani ya Shirika la UDA zinazoyagusa majina mapya ya makada wa CCM kunakuja wakati chama hicho kikiwa katika hatua ya kipropaganda waliyoipa jina la kujivua gamba.

Hadi wakati tuhuma mpya za UDA zilipoibuka, majina ya makada wa CCM waliokuwa wakitajwa kuwa katika orodha rasmi ya magamba yanayopaswa kuvuliwa na ambayo yamekuwa yakipigiwa chapuo kubwa ndani ya vyombo vya habari yalikuwa ni matatu tu.

Majina ya makada hao ni lile la Mbunge wa Monduli na waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Mbunge wa Bariadi Magharibi ambaye pia ni mwanasheria mkuu wa zamani, Andrew Chenge na la mwisho ni la aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz.

Hata hivyo, idadi hiyo ilipungua na kubakiza majina mawili, baada ya Rostam kuamua kujiuzulu nafasi zake zote za kisiasa ndani ya chama hicho katika mazingira ambayo wadadisi wa mambo bado wanaendelea kufuatilia kiini chake.

Wakati CCM ikihangaika kutafakari namna ya kumalizana na makada wengine wawili waliobaki katika orodha hiyo, tuhuma mpya za ufisadi zinazogusa majina ya makada wake wapya zimeibuka na kuzusha mtafaruku mkubwa ndani ya chama hicho na pengine serikalini.

Miongoni mwa majina mapya ya kwanza kutajwa katika orodha hiyo mpya ya makada wanaotajwa katika tuhuma mpya za ufisadi unaoigusa UDA ni lile la aliyekuwa mwenyekiti wa bodi ya shirika hilo, Iddi Simba.

Mbali ya Simba, jina jingine la mwana CCM ambalo limetajwa ndani ya Bunge katika tuhuma mpya za ufisadi wa UDA ni lile la Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya.

Ukiwaacha makada hao wawili, mwingine anayetajwa katikati ya tuhuma hizo ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam anayetokana na CCM, Dk. Didas Masaburi, ambaye alikuwa ni mtu wa kwanza kuliibua sakata hilo wakati alipotangaza uamuzi wa kumuachisha kazi, Meneja wa UDA, Victor Milanzi.

Kutajwa kwa Masaburi katika sakata hilo la UDA ambalo mwenyewe anasema ndiye aliyeliibua na kulikemea, kumesababisha kuibuka kwa tuhuma nyingine mpya za ufisadi katika Jiji la Dar es Salaam zinazowagusa makada wengine wa CCM ambao pia ni wabunge wa jiji hilo.

Aliyeibua majina mapya ya makada hao wa CCM ni Masaburi mwenyewe ambaye alikuwa akijibu tuhuma za ufisadi wa UDA ambazo zimelizonga jina lake ndani ya Bunge kwa siku kadhaa sasa.

Masaburi ambaye alikuwa akizungumza na waandishi wa habari Arusha, alisema baadhi ya wabunge wa Dar es Salaam ambao walikuwapo tangu Bunge lililopita wanamhusisha katika ufisadi wa UDA kama mbinu ya kukwepa kubambwa katika tuhuma za namna hiyo hiyo zinazoelekea kuwagusa wao.

Akitoa mifano, Masaburi alisema kumekuwa na tuhuma za ufisadi zinazogusa soko la wafanyabiashara ndogogo lililopo maeneo ya Ilala, maarufu kwa jina la Machinga Complex, ambalo mwenyekiti wake wa bodi alikuwa ni Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan ‘Zungu’.

Kutokana na hali hiyo, meya huyo wa Jiji la Dar es Salaam, alieleza kutoshangazwa na tuhuma zinazoelekezwa kwake na wabunge wa Dar es Salaam hususan wale wa CCM.

Mbali ya hilo, Masaburi alilitaja jina la Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu kuwa aliloliweka katika orodha ya kuchunguzwa kutokana na kuwapo kwa tuhuma nyingi za ufisadi katika Shirika la Uchumi na Maendeleo Dar es Salaam (DDC).

Kwa mujibu wa Masaburi, kutokana na ukweli kwamba, Mtemvu yuko katika bodi ya DDC na Zungu katika Machinga Complex, ambazo ameshatangaza kuelekeza harakati zake za kusafisha ufisadi, hakushangazwa na kitendo cha wabunge hao wawili wa Dar es Salaam kuungana na wenzao wengine kumshambulia na kumtuhumu kwa ufisadi wa UDA ilhali wakijua fika kwamba hausiki kwa namna yoyote.

Madai hayo ya Masaburi yanakuja wakati kukiwa na taarifa kwamba katika kikao cha wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam kilichokaa mjini Dodoma hivi karibuni kujadili suala la UDA, mbunge mmoja wa CCM aliwajia juu wenzake kwa kubeba hoja za wapinzani katika suala hilo.

Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kwamba mbunge huyo (jina tunalo) aliwashambulia wabunge wenzake akiwahusisha katika tuhuma kadha wa kadhaa za ufisadi.

Mtoa habari zetu anaeleza kwamba mbunge huyo wa CCM alifikia hatua ya kuwaeleza wabunge wenzake kwamba wakati wakishabikia masuala ya UDA wao wenyewe walikuwa katika vitanzi vya kupoteza nyadhifa zao, iwapo tuhuma zao zitafikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Uchunguzi wa Tanzania Daima Jumapili umebaini kwamba tuhuma za ufisadi zinazoendelea kukichafua chama hicho zimesababisha kuibuka kwa hasira miongoni mwa wabunge wa chama hicho wa maeneo ya nje ya Dar es Salaam.

Baadhi ya wabunge wa CCM waliozungumza na gazeti hili kwa masharti ya majina yao kutoandikwa waliweka bayana msimamo wao kuwa wamechoshwa na vitisho wanavyovipata kutoka kwa viongozi wao wa chama na hivi sasa wapo tayari kujiengua ndani ya chama hicho na kujiunga na upinzani.

Walibainisha kuwa tabia ya kufumbia macho vitendo vya ubadhirifu wa mali za umma ndiyo unaokifanya chama hicho kupoteza imani kwa wananchi ambao kadiri siku zinavyokwenda ndivyo wanatumbukia kwenye lindi la umasikini.

Walisema mchawi wa CCM si vyama vya upinzani ila ni watendaji wa serikali na vigogo wa chama hicho ambao wameamua kugawana rasilimali za taifa kwa masilahi yao.

Walimbebesha lawama Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, kuwa ndiye mwenye kukwamisha kuchukuliwa hatua kwa baadhi ya vigogo wa chama hicho kwa madai ya kutaka sheria zifuatwe na wengine kuwasamehe kwa vigezo anavyovijua mwenyewe.

Mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka, alisema tatizo kubwa linalowakabili wabunge wa chama hicho ni kujipendekeza kwa viongozi wa serikali pamoja na kutofahamu kile kinachopingwa na wabunge wenzao wasiotaka rasilimali za umma zitumike kwa upendeleo au ubadhirifu.

Alisema baadhi ya wabunge wamekuwa wakimuona yeye ni kikwazo na anayetoa kauli za ubaguzi wa kimaeneo mara kwa mara anapopinga ugawaji wa rasilimali lakini hawataki kuchunguza kwa undani kile anachokisema.

“Hatuwezi kukiimarisha chama na serikali kama tutaendelea kuwa waoga kwa viongozi wetu na watu wanaotumia rasilimali za taifa kwa faida ya kikundi fulani au eneo fulani,” alisema.

Sendeka alisema ni lazima wabunge watambue kuwa masilahi ya taifa ndiyo yanapaswa kupewa kipaumbele halafu ndio yafuatie ya chama kilichotoa ridhaa kwa mbunge husika kuwania wadhifa wake.

Mbunge wa Tabora Mjini (CCM), Ismail Aden Rage, wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Uchukuzi alisema kuwa tatizo kubwa la serikali ya CCM ni kuvumilia makada wake wanaoshiriki kwenye ubadhirifu badala ya kuwachukulia hatua ikiwemo kufilisi mali zao.

Deo Filikunjombe, Mbunge wa Ludewa (CCM) anasema umefika wakati kwa serikali ya chama hicho kutoa adhabu kali kwa makada wake na watendaji wa serikali wanaobainika kushiriki katika ubadhirifu ikiwezekana wanyongwe.

Mbunge huyo alisema CCM inajimaliza kwa kutumia muda na nguvu nyingi za kupambana na CHADEMA inayoratibu maandamano ya kupinga ugumu wa maisha badala ya nguvu hizo kuzielekeza kuboresha maisha ya wananchi pamoja na kupambana na mafisadi.

Mbunge wa Kahama, James Lembeli (CCM), anasema watu walioingia mikataba mibovu inayolifilisi taifa bado wapo bungeni, chamani na serikalini badala ya kuwepo magerezani.

Lembeli alisema hakuna sababu ya Rais Kikwete na serikali ya chama hicho kujali sheria katika kuwaadhibu vigogo wanaotafuna rasilimali za taifa na kusababisha maisha magumu kwa wananchi.

Wakati wabunge hao wakiona hatari ya chama chao kuanguka kwa sababu ya kuwalinda wabadhirifu, Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) (Uchumi na Fedha Taifa) Mwingulu Nchemba, anahofia chama chao kupinduliwa na CHADEMA inayofanya maandamano ya kupinga ugumu wa maisha na upandaji wa gharama za bidhaa mbalimbali.

Juzi Nchemba, alivitaka vyombo vya dola kuingilia kati maandamano yanayofanywa na CHADEMA kwa madai kuwa yanalenga kufanya mapinduzi ya serikali iliyopo madarakani.


 
Na Nassor Abdallah

WAKATI Meya wa jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi, akimtuhumu Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu kuuza shamba linalomilikiwa na Shirika la Maendeleo Dar es Salaam (DDC), lililopo Ruvu, Meneja wa shirika hilo, Cyprian Mbuya, ameibuka na kusema shamba hilo halijauzwa na wala hakuna mpango kama huo kama anavyodai Masaburi.


Mbuya alibainisha hayo jana alipozungumza na Tanzania Daima kwa lengo la kutaka kujua ukweli kuhusu tuhuma hizo zilizotolewa kwake na Meya Masaburi alipozungumza na waandishi wa habari mjini Arusha alipokuwa akijibu shutuma za ufisadi katika uuzwaji wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) na kutakiwa kujiuzulu.



Kwa mujibu wa Mbuya hata ikitokea ikaamuliwa kuuzwa kwa shamba hilo, lazima sheria zifuatwe ikiwemo saini ya Waziri Mkuu.


"Jamani haya mambo hayaendi kienyeji tu kama wanavyofikiria, yana mlolongo mrefu, wala wasijidanganye kuwa watu wawili wanaweza kukaa na kuuza mali ya umma isipokuwa kwa kushirikisha mamlaka zote husika," alisema.



Naye aliyewahi kuwa Ofisa Tarafa wa Ruvu ambaye kwa sasa amehamishiwa mjini Bagamoyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Madeni, alisema akiwa Ofisa Tarafa wa Ruvu kulikuwa na malalamiko yaliyopelekwa na wabunge wa jiji la
Dar es Salaam kuhusu kutaka shamba hilo.



Madeni alisema shamba hilo lilidaiwa kumegwa wakati wa kutenganisha wilaya ya Kisarawe na Kibaha na kusema kuwa itakuwa ajabu kwa sasa mali ambayo walikuwa wakiidai, Mwenyekiti wa Bodi ya DDC, ambaye ni Mtemvu kuiuza.



Hata hivyo, ofisa huyo alisema hayuko tayari kuzungumzia sana kwa kuwa kwa sasa yeye anatumikia wilaya ya Bagamoyo.



Akijibu shutuma hizo hivi karibuni, Dk. Masaburi aliwatusi wabunge wa jiji la Dar es Salaam na kusema kuwa wanafikiri kwa kutumia "makalio" badala ya kichwa.



Alisema anashangazwa na tuhuma zinazoelekezwa kwake kwamba anahusisha na uuzaji wa hisa na mali za shirika la UDA, wakati yeye ndiye aliyeibua ubadhirifu huo.



Dk. Masaburi alikwenda mbali zaidi na kusema kuwa anakusudia kuendeleza kazi hiyo katika mashirika mengine na miradi mingine ya maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam.



Baadhi ya maeneo hayo ni Shirika la Maendeleo Dar es Salaam (DDC) na Machinga Complex.



"Baada ya kuibua ufisadi UDA sasa nimepanga nihamie shirika la DDC ambako Mtemvu ni mwenyekiti wa bodi; shirika ambalo nalo kuna ufisadi mkubwa umefanyika ikiwemo kuuza mashamba ya shirika hilo na baadhi ya nyumba," alinukuliwa Masaburi.



Kutokana na kauli hiyo ya Masaburi, wabunge hao wameapa kumfikisha kwenye vyombo vya sheria meya huyo kwa kuwadhalilisha.



Mmoja wa wabunge waliolengwa na matusi hayo ni Mtemvu ambaye alisema hatua hiyo wataitolea ufafanuzi zaidi kesho watakapokutana na waandishi wa habari.



 

SAAFI SANA..!

naam pamefika pazuri maana ukiwaona hawa jamaa wakishirikiana na wenzao wa CDM ujue wameshikana mikono wakati wakila sahani moja...,
so hapa walipoanzia mbona pataleta habari njema za aina yake kwa yale yote yaliyojificha ndani ya mafaili yenye neno SIRI...?

hii ndiyo nafasi pekee ya kuumbuana wakati kila m2 anataka kujisafisha mbele ya Umma.
 
Hawa watu wananichekesha sana tena sana,kuna thread ipo hewan hapa nimeuliza MASABURI,ZUNGU NA ABASI MTEMVU,nimuamin nani????na kwanini sasa kwanin wanavuana nguo kias hiki????
 
Viongozi wengi wa Umma wanaotokana na CCM ni opportunists. Wakikwaruzana ujue ni kwa maslahi yao na kamwe si kwa maslahi ya wananchi.

Kutokana na yanayoendelea kuna kila sababu ya kuamini kuwa Mtemvu na Masaburi wana mgogoro wa kimaslahi (conflicts of interest).

Huenda kuna mahali wamezidiana kete sasa kila mmoja anataka kutumia nafasi yake kumkomoa mwenzie.

Mtemvu ana advantage ya ubunge, na uenyekiti wa wabunge wa Dar (ambao wanajumuisha vyama vyote vyenye wabunge Dar)

Hii inamsaidia kuonekana decent. Lakini ukweli ukijulikana huenda tukazungumza mengine.
 
Siku chache baada ya meya wa jiji la dar Dr.Masaburi kuwajia juu wabunge wa dar na kuwatuhumu kuwa ni sehemu ya ufisadi wa UDA,leo mbunge wa Temeke abbas mtemvu na Zungu wa ilala wamempa siku saba masaburi kuthibitisha tuhuma zake kabla hawajampeleka mahakamani.Pia gazeti lililoripoti limetakiwa kuwasafisha wabunge hao kwenye ukurasa wa mbele kwa kutoa habari hiyo bila kupata taarifa za upande wa pili.
Source.Channel ten.
 
Sakata la ufisadi katika Shirika la Usafirishaji (UDA) na jengo la Machinga Complex, limezidi kuchukua sura mpya baada ya Mbunge wa Ilala (CCM), Mussa Azzan Zungu, kusisitiza kuwa Meya wa Jiji, Dk. Didas Masaburi hawezi kujinasua na tope la ufisadi wa kuliuza shirika hilo hivyo anapaswa kuwajibika. Mbunge huyo jana aliahidi kuweka mambo hadharani kuelezea ufisadi ndani ya UDA na namna alivyoshikiri kwenye kuingiza wafanyabiashara kwenye jengo la Machinga Complex, akiwa Mwenyekiti wa Bodi.

Akizungumza na NIPASHE jana, Zungu alisema Dk. Masaburi anatapatapa baada ya dhambi zake katika uuzaji wa UDA kuwekwa hadharani hivyo anachofanya ni kuwahadaa Watanzania. “Anajitahidi kwa nguvu zote kuhamisha hoja, hoja iliyopo ni kwanini UDA iuzwe kiholela, lakini yeye anahangaika na Machinga Complex kujaribu kuzima hoja ambayo anajua itamuunguza mwishowe…Machinga Complex anatoa shutuma za jumla jumla hasemi ufisadi gani uliofanyika, sisi tuna nyaraka za ufisadi wake na yeye kama anazo aonyeshe,” alisema Zungu.

Alisema ujenzi wa jengo hilo la wafanyabiashara ulitokana na mkataba halali wa Jiji na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) hivyo alisema Dk. Masaburi inawezekana hajui anachosema au anajaribu kuzima hoja ya ufisadi wake. Zungu alikiri kuwa aliwahi kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Machinga Complex, lakini kazi ya bodi hiyo ilikuwa kuingiza wafanyabiashara tu na haihusiki na mkataba wowote.

“Bodi yangu haikuwa na nguvu ya kisheria kama ilivyo bodi ya sasa, sisi tulipewa jukumu la kuingiza wafanyabiashara, tukawaingiza na kuondoka zetu, zabuni zote walitoa Jiji sisi hatukuhusika kabisa na suala la zabuni sasa huo ufisadi anaozungumza mbona hauweki wazi kama sio kutapatapa?” alihoji.
“Mwambieni aweke wazi tuhuma zetu, asiseme juu juu tu, yeye amevunja bodi ya UDA na anauza shirika bila idhini yoyote huo ushahidi tunao mbona yeye hasemi ufisadi wetu pale Machinga ni upi?” alisisitiza.

Zungu alisema alipopewa jukumu la kuwa mwenyekiti wa bodi alikuta tayari jengo limeshajengwa hivyo hakuhusika na manunuzi yoyote.
Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Azan, alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwani wabunge wa Mkoa wa Dar es salaam wana viongozi wao.
“Mtafute Abbas Mtemvu ndo mwenyekiti wetu au John Mnyika ambaye ni katibu, hawa ndio wana mamlaka ya kuzungumza kwa kuwa ndio viongozi wetu,” alisema.

Kwa upande wake, Dk. Masaburi alisema ataendelea kuchunguza mikataba yote mibovu ambayo wabunge wa Dar es Salaam walishiriki na kwamba hataogopa. Alisema wanachofanya wabunge hao hivi sasa wakiongozwa na Zungu na Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu ni kujaribu kumtisha, lakini alisisitiza kuwa atafanya uchunguzi huo yeye binafsi na hatatishika kamwe. Alisema mikataba atakayoichunguza ni ule wa Machinga Complex, Shirika la Maendeleo Dar es Salaam (DDC) na uuzwaji wa mashamba ya Jiji huko Mpiji Majohe na Ruvu.

Mwenyekiti wa wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mbunge wa Temeke,(CCM), Abbas Mtemvu, hakupatikana kuzungumzia sakata hilo kwa kuwa simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa. Hivi karibuni, wabunge wa Dar es Salaam, wakiongozwa na Mtemvu waliitaka serikali kuagizwa kusitishwa mara moja mkataba batili uliofanyika awali na maamuzi haramu yaliyofanyika kwa kukabidhi hisa, mali na uendeshaji wa UDA kwa kampuni ya Simon Group Limited. Walitaka hilo lifanyike ili katika kipindi cha uchunguzi masuala yote ya kampuni hiyo yaratibiwe na bodi huru itakayoundwa na kusimamiwa na Shirika Hodhi la Mali za Mashirika ya Umma (CHC) kwa mujibu wa sheria zinazohusika.

:: IPPMEDIA
 
Hii sinema nzuri, waache wang'atane tu, sisi tutafuta damu. Watasema kila kitu mwaka huu.
 
Kumtaka Mayor athibitishe au kuomba msamaha hapo sawa, lakini hii habari kuwa Gazeti liliandika nalo liombe msamaha kwa kutopata maoni yao wao Mtemvu na Zungu sio sahihi. Gazeti lime-report alilosema Mayor. In other words, newspapers are 'newsmakers' they are 'newsreporters'. Unless wametunga hii habari, vinginevyo Mtemvu na Zungu wanatakiwa wafuatilie channzo - yaani newsmaker.
 
Nitashangaa kama DCI atafanya uchunguzi wa sakata hili bila kuwasweka ndani wahusika ili kuisaidia Polisi.
 
Mpango mzima wa kuwaibia Watanzania katika mradi huu wa uuzaji wa Uda Umebumburuka na hivyo ni vyema kwa hili wakanyanyua mikono kama ishara ya kusalimu amri. Tungewapa muda wa kusalimisha mapato haya yaliyolipwa serikalini kama tulivyofanya wakati wa sakata la EPA. Mzee akikaidi kuzisalimisha basi hatua zifaazo zichukuliwe. Tusiendelee kumhukumu ila tumpe nafasi aturudishie kwani tumemkamata kama tunavyofanya mitaani petu tunapomkamata kibaka. Hapa mzee kazidiwa. Consultancy fees 250 million? Huna haya? Umeuza kitu gani au ni ushauri wa aina gani wa kibiashara huo. Rates za consultance fees nazo zitengenezewe utaratibukuna hatari ya kwenda hovyo kama huyu mzee.
 
Hivi huyu Idd Simba anadhani watanzania ni wajinga saaaaaana?

Ukitaka kumprove kuwa he is right, subiri uone nini kitafanyika. Unaweza ukaona uozo wazi kabisa lakini hakuna hatua inayochukuliwa. Huo unaweza kuita nini??
 
Nataka tuzungumzie uhusiano wa Idd Simba na Taifa letu leo hii:

Idd Simba ni fisadi na mhujumu mkubwa wa Taifa la Tanzania. Soma hii biashara ya Idd kwa deals zake Tanzania. Kitu kibaya sana nimegundua hata JF kuna support za kuzuia wananchi wasi-post thread za watu kama Idd Simba na kuna watu JF work hard on behalf of Rostam and Idd Simba kuhusu ufisadi wake na kwa taarifa tunaweza kufikisha kwa wananchi bila kutumia JF sio hapa pekee ndio forum zitafika kwa wananchi.

Kwa kifupi, soma uhuni wa Idd juu ya deals na hii kampuni ya Agrisol. Ukifuatilia kazi za Serengeti Advisers utaona jinsi gani kikwete na mkapa wanavyomtumia Idd Simba kama mhuni wa policies na deals Tanzania. Chukua muda kidogo usome kazi ya Serengeti Advisers Tanzania kutoka dodoma mpaka Ikulu.


U.S. firm, AgriSol Energy LLC, and its joint venture partner in Tanzania will invest more than $100 million over the next 10 years to develop a large-scale commercial farming project in the east African country, a company director said on Tuesday.AgriSol, led by well-known Iowa farming and ethanol executive Bruce Rastetter, has joined with Serengeti Advisers, a Tanzanian investments and consulting firm, to invest in crop and poultry production in western Tanzania.
"Our initial project in Lugufu involves approximately 10,000 hectares -- a tiny percentage of the overall available land in Tanzania -- but large enough to have a meaningful impact on the country's agricultural industry," Bertram Eyakuze, one of AgriSol Tanzania's directors, said in an e-mailed response to questions submitted by Reuters.
"We project that it will cost in excess of $100 million over the next ten years to develop Lugufu fully," Eyakuze said, adding the focus would initially be on the growth of maize and soy, which would in part be used to produce feed for livestock and cooking oil.
Poultry production would also be a focus of the project, to eventually wean Tanzania off importing chicken from Brazil and other countries.
"Tanzania has 43 million hectares of arable land, of which only about 10 million hectares, or 23 percent, is currently being farmed, leaving more than 30 million hectares available to produce food for the people of Tanzania and eventually the rest of Africa," Eyakuze said.
He said investors would look into expanding farming activities once the Lugufu project was completed.
AFRICAN LAND-GRAB DENIALS
Tanzanian prime minister Mizengo Pinda said in June the country would offer over 1.6 million hectares of land for lease to investors to set up large-scale projects.
Companies have already injected about 1 trillion shillings in free trade zones since 2007 and exported goods worth 525 billion shillings in the same period, Pinda said at the time.
AgriSol denied allegations it was among wealthy U.S. and European investors accumulating large swathes of African agricultural lands in deals that have little accountability and give them greater control over food supply for the world's poor.
A report by Oakland Institute, a think tank in California, said in June some U.S. public universities, pension and hedge funds and speculators were among those in on the land rush, eyeing returns of 20 to as much as 40 percent.
"Some recent news accounts and reports have inaccurately portrayed our intentions ... Our project is about partnering with world-class agricultural experts and putting Tanzanian farmland to its best and fullest use," Iddi Simba, a director at Serengeti Advisers, said in an open letter to the public posted on AgriSol's website last month.
"(Tanzanian) government made AgriSol aware of three tracts of land in western Tanzania that were previously used as camps for refugees, but were, at the time, either closed or being closed. The decision to close these camps was made well before AgriSol became involved and was based on a model program agreed to with the United Nations."
Eyakuze said Agrisol's farms in Tanzania would generate thousands of jobs and improve food security in the country.

US firm to invest in $100 mln Tanzania farms JV

http://www.undp.org/legalempowermen...- MKURABITA-CONFERENCE-PROCEEDINGS-VOL.II.pdf

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...c-debate-on-land-grabbing-in-tanzania-14.html

About Us | Serengeti Advisers


Iddi, Rostam, Mengi Kapuya, Chenge, kikwete, mkapa wanatofauti gani?
 
Back
Top Bottom