Dr Slaa, Zitto watofautiana na viongozi wenzao
Wakati gazeti la Majira Novemba 8 na Mwanachi Novemba 9 yakiandika habari kwamba Mbowe amefanya kikao kisicho rasmi Dodoma na kuamua kuwafukuza uanachama Kafulila, Danda na Shida Salum kutokana na kuwa kambi ya Zitto; naibu katibu mkuu wa CHADEMA Zitto Kabwe amekanusha kuwepo kwa kikao kilichofanya maamuzi hayo.
Akichangia katika Mtandao wa Jamii Forums Zitto amesema: Nadhani mnakuwa emotional sana. Mimi siamini kuwa kuna mpago wowote wa kumfukuza mtu yeyote uanachama wa CHADEMA kwani kaiba yetu ipo wazi kuhusu taratibu za kufukuza uanachama. Nadhani kuna watu ni waoga ndani ya chama kuhusu nafasi zao na kwamba watafukuzwa kwa kuwa walikuwa wakiniunga mkono kufanya mabadiliko ya uongozi. Lakini pia kuna uwezekano mkubwa mjadala huu umeletwa ili kuficha mjadala wa CCM wa umeendelea kwa wiki nzima na pia kuonyesha kuwa hata CHADEMA wanagombana.
Chama kipo shwari na viongozi hawana ugomvi. Pia David Kafulila wala Shida Salum hawawezi kuwa wasaliti wa chama hata kidogo. Nimewahi kusema humu ndani kuwa kule Kigoma CHADEMA ni movement - anayetaka kuvuruga CHADEMA hatatoka salama hata kidogo.
Mwenyekiti Mbowe ni mzoefu wa siasa na hawezi kufanya haya ambayo yameandikwa katika magazeti.
Ninawaomba mtulie kwani CHADEMA ipo imara kabisa na hakuna ugomvi wowote na wala hakuna atakayefukuzwa!
Kauli hiyo ya Zitto akwenda tofauti kabisa na kauli zilizotolewa na Maafisa wenzake David Kafulila- Afisa Habari na Danda Juju Martin-Afisa wa Bunge wa chama hicho.
Gazeti la Majira lilimnukuu Bwana Kafulila akisema kwamba habari hizo amezisoma kwenye vyombo vya habari na kwamba kama kuna kikao ambacho Mbowe amekifanya Dodoma basi kitakuwa ni kikao cha geto. Kwa upande wake gazeti la Mwananchi lilimnukuu Kafulila akieleza amesikia taarifa kuwa amejadiliwa Dodoma na kufukuzwa uanachama na anasubiri barua rasmi. Kwa upande wake Bwana Danda alinukuliwa na Mwanachi ameeleza kwamba anaamini taarifa za kuwa amefukuzwa uanachama kwa kuwa anajua kuwa Mbowe alikuwa na kikao kisicho rasmi Dodoma.
Hata hivyo, Katibu Mkuu- Dr Slaa na gazeti la leo la Mwananchi na vyombo vingine akifafanua kwamba hakuna kikao kilichokaa kufukuza mwanachama yoyote kwa sababu taratibu za kikatiba za CHADEMA yanapokuja masuala makubwa kama hayo zinajulikana. Ameeleza kuwa Dodoma palifanyika retreat ya chama iliyoitishwa na viongozi wakuu wa chama kwa ajili ya kutafakari mikakati ya CHADEMA kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2010. Ameeleza kuwa ni kawaida kwa chama hicho kuitisha vikao hivyo kila mwaka ambavyo hufuatiwa na vikao vya sekretariati na kamati kuu. Dr Slaa ameeleza kuwa kikao hicho kilitishwa na Mwenyekiti kikihusisha viongozi wakuu- Makamu Mwenyekiti Arfi Said na yeye. Ameeleza kuwa Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe hakuhudhuria kutokana na kuwa safarini kikazi. Ameendelea kufafanua kuwa Wakurugenzi wa chama waliakwa katika kikao hicho. Katika kikao hicho maafisa wa chama hawakualikwa. Kafulila ni Afisa habari ambaye mkurugenzi wake ni Erasto Tumbo ambaye alihudhuria. Mkurugenzi wa Bunge ni John Mrema, ambaye afisa wake Danda Juju ni mmoja wa waliolalamikia kikao hicho. Wakurugenzi wengine waliohudhuria ni pamoja na Benson Kigaila, John Mnyika na Antoni Komu. Kikao hicho kilihusisha pia wabunge wote wa CHADEMA waliokuwepo Dodoma wakati huo wakiwemo Ndesamburo, Charles Mwera, Susan Lyimo na Grace Kiwelu. Wabunge Halima Mdee, Lucy Owenya na Ana Komu ambao wametajwa na magazeti yote mawili kuwa walihudhuria kikao hicho Dodoma hawakuwepo Dodoma wala kuhudhuria kikao hicho kutokana na kuwa safari nje ya nchi. Dr Slaa ameeleza kuwa katika kikao hicho hakujajadiliwa wala kutajwa jina la Mama Zitto, wala kafulila wala Danda Juju, sembuse kufukuzwa uanachama. Kauli ya Dr Slaa imeendana na kauli ambayo Zitto kabwe kwenye mtandao wa Jamii Forums akieleza kwamba hakuna suala hilo la mwanachama kufukuzwa uanachama.
Katika hatua nyingine Zitto ametofautiana na msaidizi wake wa karibu Omar Ilyas kuhusiana na kuendeleza mijadala yenye kujenga makundi ndani ya chama baada ya uchaguzi wa chama hicho kumalizika. Msimamo huo wa Omar Ilyas ambao umeonekana kuendeleza malumbano aliutoa kwenye mtandao wa Jamii Forums kama ifuatavyo:Now I understand kwanini MWAFRIKA alikuwa akilazimisha kuwa mimi nasema kama msemaji wa Zitto. Mwanzoni nilidhani ni upofu wa kudhani kila mtu hana akili ya kusema ama kuwa na msimamo wake mwenyewe kumbe ugali ulikuwa unaandaliwa kuni?
Wakati haya yakifanyika kama ni kweli ushauri wangu ni kuwa mtambue kuwa Shida Salum alihchaguli kwa kura zaidi ya asilimia 70 kuingia kamati kuu/baraza kuu na pia Kafulila alipata kura nyingi kuliko wagombea wote ndani ya baraza la vijana hivyo hapo mjiandae kupambana na pengine zaidi ya nusu ya wanachama wa CHADEMA.
Hapo sijamuongelea Zitto ambaye wote mnamjua uwezo wake, ubishi wake, umaarufu wake, uthabiti wake na pia ni kiongozi anayejua mapungufu yenu mengi tu na kama sio wote. Na bila ya kusahau wale wote walio na tofauti na uongozi wenu mara baada ya Chacha Wangwe na wengineo kutokea ambao Zitto alifanya kazi ya ziada kupunguza wengi wao wasipige kura za maruhani wakati ule. Kamwe huwezi ukafanya haya yanayosemwa hapa bila ya kuwa na nia mbaya na Zitto. Na hakuna anayeweza kukubali vinginevyo.
Mwenzenu baada ya yale yaliyopita hivi mujuzi hapa jamiiforum,nilikuwa nimeshaanza kufanya mikakati ya kuwakutanisha ninyi na Zitto haraka iwezekanavyo ili muongee mjue na kutambua hasa sababu zinazowafanya muwe kama mlivyo sasa. Sasa kama mmefika huko mnapoelekea then nitakachoweza kufanya ni kuwatakia safari njema ninyi wajuvi na asanteni sana kwa mnayotundea sisi watanzania wenye matumaini yasiyokwisha ya kuona Tanzania yenye demokrasia makini na yenye uwezo wa kujenga taifa lenye ustawi wa wote na imara zaidi...
Katika hali ambayo inaonyesha kuweka mkazo katika kulinda chama na kuachana na siasa za makundi, Zitto alitofautiana naye katika mtazamo wake hapo huu na kusema Omar, haya malumbano hayana tija yeyote kwa Taifa letu. Sisi tunapita tu na hizi Asasi tulizoanzisha zitadumu. Tutoe fursa kwa Taifa kupumua. Sitisha malumbano haya na huyu Mwafrika. Tafadhali nakusihi ndugu yangu.