shadow recruit
JF-Expert Member
- Dec 28, 2011
- 1,844
- 384
- Thread starter
- #141
Nikweli kabisa mkuu vita dhidi ya ufisadi ni ngumu sana, ila nakuomba upunguje jazba na ufuatilie sakata hili la iptl kwa umakini sana kama unataka kujua ukweli hata mimi kabla sijazama na kula nondo za kutosha nilipatwa na muhemko kama wewe mwanzo. Ufisadi kweli upo katika nchi yetu na mpaka sasa kesi nyingi tu zipo mahakamani bado na chunguzi nyingi tu zinafanyika. Lakini kwenye hili la iptl mkuu rest assured kwamba hakuna ufisadi hapa ni janjajanja za wafanyabiashara na unafki wa kisiasa tu huu. Hili ni skendo la kupikwa ili watu fulani wapakane matope. Alafu mkuu kwenye hili la nguvu ya umma, kama nikukipika kizazi chetu kwa suala la uzalendo sawa, watu wawe wazalendo kwa nchi yao, ili wapatikane viongozi ambao kweli watapigania umaskini wa watu wao. Ila naomba usiwe na fikra za nguvu ya umma inayofanana na ile ya Arabu Spring maana hapo nnamashaka kwamba kwa sisi na mazingira yetu na hulka na mikakati ya mabeberu tunaweza tusitoke salama na mkuu amani nikitu kikubwa sana hata kama unalala njaa leo.
Tukirudi kwa kafulila na CAG mkuu bado na kushauri uzame vizuri tu utagundua hila zao hawa jamaa, driving behind them pia utaiona, zama tu mkuu hata JF humu yameandikwa mengi tu yatakayo kujuza ukweli juu ya hawa vibaraka wanavyotumika.
mie nimejaribu kusoma soma jana hasa issue ya akaunti ya ESCROW nilichogundua ni uzushi wa kitoto hata darasa la pili anatosha kujua kuwa pesa ya Escrow haikuwa ya serikali tena kisheria maana serikali ilikua imeshawalipa wanahisa wa iptl kwa ajili ya mauzo ya umeme sasa kumbe kafulila anavyopambana kuwa escrow ina harufu ya ufisadi jamaa wamemdanganya sana, hata kama fedha za escrow zina ufisadi kwenye matumizi yao sisi kama tanzania haituhusu maana tumewalipa wao kwa kutuuzia umeme,habari ya matumizi ya hizo pesa si yetu hata kama wamehonga malaya