Naweza nikakubaliana nawe somehow kuwa hakuna kiongozi yeyote wa kisiasa, whether anatoka chama tawala au upinzani, ambaye atakuwa 100% perfect.
Hilo limeandikwa hata katika vitabu vyetu vitukufu vya dini kuwa, ambaye pekee yuko 100% perfect, ni Mwenyezi Mungu, aliyeumba dunia na sayari zote, pamoja na kutuumba sisi binadamu.
Ila tofauti yake ni kuwa watawala wetu walio wengi, ambao ndiyo wanapata 'michongo' na dili nyingi za kifisadi za mabilioni ya pesa, viongozi wa opposition parties, hawana hizo fursa.
Ndiyo maana sisi raia wa kawaida walala hoi, tunapaswa kupiga kelele kwa nguvu zote, kuwa kwa nini watawala wetu wanakosa huruma hata kidogo, kwa kufikiria wagonjwa maelfu wanaolazwa mahospitalini, ambao wengi wao wanakufa kwa malaria, kwa kukosekana tu vidonge vya 'mseto' wakati watawala wetu,wao wanaogelea kwenye 'mabwawa' ya utajiri wa mabilioni ya shilingi waliyoyapata kwa njia za ufisadi?!