Sakata la Dc mstaafu kumpiga mkewe na kumtishia bastola lachukua sura mpya watoto wake washikiliwa na polisi Simanjiro

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
Sakata la Philomena Toima mke wa mkuu wa wilaya mstaafu nchini ,Peter Toima Kiroya limechukua sura mpya baada ya jeshi la polisi wilayani Simanjiro kuwashikilia watoto wake kwa sababu zisizojulikana mpaka sasa.

Watoto walioshikiliwa na polisi wilayani humo ni pamoja na Nahini Toima pamoja na Nosini Toima kwa sababu ambazo hazijulikani mpaka sasa.

Taarifa kutoka kwa mke wa kiongozi huyo mstaafu zinadai kwamba watoto wake walishikiliwa juzi usiku majira ya saa saba wakati walipofika hospitalini kumjulia hali.

Hatahivyo,hadi jana taarifa zimeeleza kuwa watoto hao waliachiawa kwa dhamana lakini wametakiwa kuripoti polisi kila siku na kuna taarifa wanahitajika katika makao makuu ya jeshi la polisi mkoani Manyara yaliyopo wilayani Babati.

Philomena alieleza kwamba polisi walifika hospitalini hapo na kisha kuwakamata watoto wake kwa madai kwamba baba yao amefungua mashtaka polisi kuwa wamemfanyia fujo.

“Polisi wapatao wanne walifika na gari wakapaki nje na kisha kuingia ndani hospitalini wakawakamata watoto ilikuwa majira ya saa saba usiku walikuj kunijulia hali “alisema Philomena

Alieleza kuwa hatua ya watoto wake kukamatwa ni mwendelezo wa vurugu na manyanyaso yanayofanywa na mme wake kwa kuwa wanaye wamekuwa wakipinga udhalilishaji unaofanywa na baba yao.

“Unajua hawa watoto siku zote wamekuwa upande wangu wanaumia ninavyonyanyaswa na mme wangu aliwatuhumu kwamba wao ndio waliwaita waandishi wa habari kunihoji hapa hospitalini “alieleza Philomena

Alieleza kuwa kwa sasa ameruhusiwa kutoka hospitalini na yuko nyumbani anauguza majeraha lakini amepata taarifa kuwa watoto wake wamepata dhamana na wanahitajika wilayani babati ambako ni makao makuu ya jeshi la polisi mkoani Manyara.

Kwa kipindi kirefu Toima na mkewe wamekuwa katika mgogoro wa ndoa huu chanzo kikubwa kikitajwa ni nyumba ndogo ambapo Philomena amekuwa akimtuhumu mmewe kutokuwa mwaminifu kwenye ndoa baada ya kuzaa na mwanamke aitwaye Scolla Mollel.

Mbali na tuhuma hizo Philomena amekuwa akimtuhumu mmewe kutumia mali za familia hovyo pamoja na kumjengea nyumba hawara yake pamoja kutumia hovyo fedha na rasilimali za taasisi waliyoianzisha miaka ya nyuma ambayo ni Eclat Foundation inayojikita kuhudumia masuala ya elimu hapa nchini.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Manyara alipotafutwa na waandishi wa habari ili kuzungumzia sakata hilo alisema kwamba yupo kikaoni atafutwe baadae na hata alipotafutwa baadae hakuweza kutoa ushirikiano kwani simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.

Mwisho.

Pichani chini ni Dc mstaafu Peter Toima akiwa na mkewe picha nyingine ni nyumba ndogo Scolla Mollel.

33FAC2BF-1005-49E7-91CD-E942C4472E20.jpeg


575EBDD8-8FF4-434E-A078-37BFE4A5F935.jpeg


D03C8257-4B0A-41D3-95B7-B475D10DA6D6.jpeg
 
Baba km mstaagu na wayoto tayari wakubwa, mama hana mpango tena na baba wanaume tulijue hili. Kuweni na biashara zenu uzeeni ndizo ziwe wake zenu
 
Kuna haja ya ugomvi si waige kwa hawa jamani watu wapige beche mambo yaishe
2741124_1618393507470.png
 
Uzuri wa mtu machoni kwa mtu. Unapiga mke kwa ajili ya nyumba ndogo plain kiasi hicho?
 
Huyo Dingi Usalama wa taifa huyo maana sio kwa mambo hayo yaani kapiga mwanamke yeye cha ajabu wanakamatwa wengine katkka mazingira ya kutatanisha
 
Emboreti na Lolikisale Patamu Sana....kuna ka SPISHI flani vile ka kimyakimya.....tembeya uwone Bandugu
 
Back
Top Bottom