Waomba DC wao aondolewe
2009-02-21 11:19:32
Na Pendo Fundisha, Mbarali
Baadhi ya wakazi wa Kata za Chimala na Ubaruku, Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya, wameiomba serikali kumuondoa Mkuu wao wa Wilaya, Hawa Ngulume kwa madai kwamba ni kikwazo kwao cha kujiletea maendeleo.
Wananchi hao wamedai kwamba, Mkuu huyo wa Wilaya, amekuwa akipeleka kwa viongozi wa juu yake taarifa zisizo sahihi na kuacha zinazowahusu wao kama zilivyowasilishwa kwake ili azifanyie kazi.
Walitoa madai hayo juzi mbele ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma iliyokuwa mkoani Mbeya kutembelea Wilaya za Mbozi na Mbarali.
Hata hivyo, wakati wananchi hao wakitoa madai hayo, Ngulume mwenyewe hakuwepo.
Walidai kwamba, Mkuu huyo wa Wilaya, amekuwa akiwabeba wawekezaji na ambao ndio wanaojenga ofisi za CCM wilayani Mbarali.
Lakini Nipashe ilipomtafuta Mkuu huyo wa Wilaya kwa njia ya simu na kuulizwa madai hayo, alisema hashangazwi na kauli ya baadhi ya wananchi hao.
Aidha, alisema hana uhusiano na mwekezaji huyo na kwamba anachokifanya yeye, ni kusimamia sheria na kanuni zilizopo.
Pia alisema mwekezaji huyo hajajenga ofisi yoyote ya CCM wala nyumba yake (Ngulume) kwa kuwa kwanza hana mpango wowote wa kuishi mkoani Mbeya.
Kuhusu madai ya wananchi hao kupigwa, Ngulume alisema kama yupo mtu mwenye madai hayo, anaweza kuyafikisha madai yake kwa Mkuu wa Mkoa.
Kwa mujibu wa wananchi hao, uongozi wa wilaya hiyo chini ya Ngulume, umekuwa ni tatizo na amekuwa anatumika na huwatumia wawekezaji kuwaangamiza na hata kuamrisha wananchi wapigwe viboko pale wanapopeleka malalamiko yao ya msingi.
Waliieleza Kamati hiyo ya Bunge kuwa, matatizo yanasababishwa na mwekezaji wa shamba la mpunga Kapunga na yamekuwa yanachangiwa na Mkuu wa Wilaya huyo kwa kuonyesha upendeleo wa wazi kwa mwekezaji huku akiwasahau wananchi wake.
Walidai kuwa, mwekezaji wa mashamba ya Kapunga, amekuwa akiwanyanyasa wananchi wanaolizunguka shamba hilo na imefikia hatua amevunja madaraja yote waliyotengeneza na hivyo kuwalazimu kuzunguka umbali mrefu wanapokwenda kwenye mashamba yao.
Walisema na kama si amani iliyo ndani ya Watanzania, wangekuwa wamechukua uamuzi mwingine ambao ungekuwa mbaya kwa pande zote mbili kutokana na vituko wanavyofanyiwa na mwekezaji wa mashamba hayo.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Kabwe Zitto, hakujibu chochote zaidi ya kueleza kwamba, ameyasikia malalamiko hayo.
SOURCE: Nipashe