Sakata la DC anayejengewa nyumba na mwekezaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sakata la DC anayejengewa nyumba na mwekezaji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwikimbi, Feb 21, 2009.

 1. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #1
  Feb 21, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Waomba DC wao aondolewe

  2009-02-21 11:19:32
  Na Pendo Fundisha, Mbarali  Baadhi ya wakazi wa Kata za Chimala na Ubaruku, Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya, wameiomba serikali kumuondoa Mkuu wao wa Wilaya, Hawa Ngulume kwa madai kwamba ni kikwazo kwao cha kujiletea maendeleo.

  Wananchi hao wamedai kwamba, Mkuu huyo wa Wilaya, amekuwa akipeleka kwa viongozi wa juu yake taarifa zisizo sahihi na kuacha zinazowahusu wao kama zilivyowasilishwa kwake ili azifanyie kazi.

  Walitoa madai hayo juzi mbele ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma iliyokuwa mkoani Mbeya kutembelea Wilaya za Mbozi na Mbarali.

  Hata hivyo, wakati wananchi hao wakitoa madai hayo, Ngulume mwenyewe hakuwepo.

  Walidai kwamba, Mkuu huyo wa Wilaya, amekuwa akiwabeba wawekezaji na ambao ndio wanaojenga ofisi za CCM wilayani Mbarali.

  Lakini Nipashe ilipomtafuta Mkuu huyo wa Wilaya kwa njia ya simu na kuulizwa madai hayo, alisema hashangazwi na kauli ya baadhi ya wananchi hao.

  Aidha, alisema hana uhusiano na mwekezaji huyo na kwamba anachokifanya yeye, ni kusimamia sheria na kanuni zilizopo.

  Pia alisema mwekezaji huyo hajajenga ofisi yoyote ya CCM wala nyumba yake (Ngulume) kwa kuwa kwanza hana mpango wowote wa kuishi mkoani Mbeya.

  Kuhusu madai ya wananchi hao kupigwa, Ngulume alisema kama yupo mtu mwenye madai hayo, anaweza kuyafikisha madai yake kwa Mkuu wa Mkoa.

  Kwa mujibu wa wananchi hao, uongozi wa wilaya hiyo chini ya Ngulume, umekuwa ni tatizo na amekuwa anatumika na huwatumia wawekezaji kuwaangamiza na hata kuamrisha wananchi wapigwe viboko pale wanapopeleka malalamiko yao ya msingi.

  Waliieleza Kamati hiyo ya Bunge kuwa, matatizo yanasababishwa na mwekezaji wa shamba la mpunga Kapunga na yamekuwa yanachangiwa na Mkuu wa Wilaya huyo kwa kuonyesha upendeleo wa wazi kwa mwekezaji huku akiwasahau wananchi wake.

  Walidai kuwa, mwekezaji wa mashamba ya Kapunga, amekuwa akiwanyanyasa wananchi wanaolizunguka shamba hilo na imefikia hatua amevunja madaraja yote waliyotengeneza na hivyo kuwalazimu kuzunguka umbali mrefu wanapokwenda kwenye mashamba yao.

  Walisema na kama si amani iliyo ndani ya Watanzania, wangekuwa wamechukua uamuzi mwingine ambao ungekuwa mbaya kwa pande zote mbili kutokana na vituko wanavyofanyiwa na mwekezaji wa mashamba hayo.

  Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Kabwe Zitto, hakujibu chochote zaidi ya kueleza kwamba, ameyasikia malalamiko hayo.


  SOURCE: Nipashe
   
 2. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #2
  Feb 21, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Ni kweli kuwa mwekezaji anajenga nyumba ya katibu wa ccm wilaya ya mbarali na huyu mama anajifanya kuwa ndiye anayejenga jengo hili ili kujikomba ccm wasimtimue ukuu wa wilaya

  1966 mwalimu nyererre alitembelea mbarali wananchi wa kapunga wakamwomba awajengee miundo mbinu kwa ajili ya umwagiliaji,

  1976 serikali iliomba kutoka kwa wananchi wambarali hekta 5500 kwa ajili ya uendelezaji wa mradi huo.

  1978 kupitia government gazzete wananchi walitoa eneo hilo

  1982? Mwalimu alipata msaada wa mabilioni ya fedha ndipo mradi huo ukatekelezwa kupitia kampuni ya kijapan ya kajima
  1987 mradi huo ulimazika1988 ukiwandiyo mradi mkubwa kabisa hapa nchini una uwezo wa kuzalisha at least 45% ya mahitaji ya mchele wa nchi nzima

  kinu cha kukoboa mpunga ni kikubwa barani afrika ukiacha kile kilichoko kando ya nile -misri,miundo mbinu ya mradi mzima ni zaidi ya 256bilioni!!

  2006, mtu aitwae mungai na mgasongwa waliuza mradi huu kwa mwekezaji kwa gharama ya tshs 2.5billioni tu, na kuwakejeli wananchi kuwa mwenye basi ameamua kuuza basi lake , kondakta analalamikia nini?

  Eneo la mradi lilikuwa hekta 5500 lakini serikali kupitia akina mungai imeuza hekta 7500 ikiwa ni pamoja na kijiji kizima

  mwekezaji hadi leo hajaweza kulima hat 25%, amebomoa madaraja miuondo mbinu ya asili iliyojengwa kwa nguvu za wananchi

  wananchi hawa wanapeleka kilio kwa dc, yeye anawatimua, anamukumbatia mwekezaji anayejenga jengo hilo la ccm na nyumba binafsi ya huyu mama

  huu ni ukoloni mpyaaaa
   
 3. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #3
  Feb 21, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  mbunge zitto kabwe ambaye ni member hapa jf atueleze zaidi kwa kuwa alikuwa mbarali na aliona mambo yote ikiwemo tuhuma dhidi ya dc huyu
   
 4. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Hivi ni kweli utumwa wa nchi Nyerere ameukomesha?
   
 5. t

  tk JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 270
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Loo! kama tarifa hizi ni za kweli hapa kuna tatizo kubwa. Tatizo la hawa wawekezaji, wakimshika tu kiongozi wa ngazi za juu basi mjue wananchi watanyimwa haki zao. Jamaa hawa kutoa mshiko au kujenga nyumba kama hivyo kwao ni kitu kidogo tu maana manufaa wanayopata ni makubwa.

  Hapa tunasubiri kuona makali ya Zitto.
   
 6. M

  MohamedSalum200 Member

  #6
  Feb 22, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  watanzania tushazoea kulalamika .kama inawezekana waende kwa jk wampe habari
   
 7. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Uongozi kazi ngumu sana...kama mwandishi angeandika chote au angemsikiliza na mama huyo nafikiri tungeweza ku measure vyema...hoja ya wananchi na mkuu wa wilaya..hapa na jadili one side of the story.....naweza sema bado hatujui wananchi wanalalamika tu..kwa kuwa hawataki kufanya wanalotakiwa kufanya...wanaangalia tatizo.Mwisho wa siku lao kibaya ni kibaya..na kizuri ni kibaya zaidi.
   
 8. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #8
  Feb 22, 2009
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Umesema yote.

  Hebu fikiria, serikali imekiomba kijiji Ardhi hekta 5500. Kijiji kupitia vikao vyake kikakubali. Serikali ikaanzisha shamba. Miaka minne baadae wakashindwa kuliandesha shamba.

  Baada ya miaka wakaliuza shamba lile Hekta 7370. Hivyo na kile kijiji ambacho kiliwakaribisha kikauzwa.

  Tumeamua kama Kamati. Serikali iwarudhishie pesa zao Ardhi ile irudi kwa wanakijiji. Kama nimekupa kitu, umeshindwa kuendesha, si unanirudishia?

  Safari yangu ya Mbarali ni experience of its own.
   
 9. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #9
  Feb 22, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Zito umenena,lakini ni nani wa kuhakikisha shamba linarudi kwa wanakijiji?
   
 10. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #10
  Feb 22, 2009
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  "Serikali" ndio nani bana, tunaongelea uwajibikaji wa kiumbe hai, huyu Mkuu wa Wilaya ambae anawaambia wananchi kwamba hana mpango wa kuishi Mbeya anyway! Usitumie maneno smokescreen, "serikali." Wananchi issue yao ni kurudishiwa kijiji chao na pia hawamtaki huyu DC. Unapoikosoa "serikali" wakati mhusika wa serikali tunae, unakua unasua sua kuhimiza uwajibikaji wa watu halisi ndani ya serikali. Yale yale uliyosema kwamba Richmonduli sio kosa la Lowassa ni kosa la "Serikali"! Acha woga siku hizi.

   
 11. mwakatojofu

  mwakatojofu JF-Expert Member

  #11
  Feb 22, 2009
  Joined: Dec 17, 2008
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  'sina mpango wa kuishi mbeya anyway'. maneno yamekaa kinyodo nyodo. yamekaa kidharaudharau vilevile. mi naona hivyo. ni kama mbeya anakuona kuchafu vile.

  angeweza kujibu kwa kutumia maneno ambayo hayaleti picha ya nyodonyodo au dharaudharau. majibu ya kistaarabu hayanunuliwi. angeweza kusema - "ah, wala, hanijengei nyuma mimi. nina kiwanja mbezi dar es salaam sijaanza hata kujenga ningemwambia akanijengee kwenye hicho kiwanja kama angetaka kunijengea nyumba".

  huyu maza vipi? niliwahi kusoma kwenye gazeti kamlamba mtu kibao siku za nyuma kule kule mbarali. ndivyo viongoz wetu wanavyotakiwa kutujibu au kutuhandle tunapowauliza kitu? ndio utawala bora? ndio kasi mpya? ndio demokrasia? NO to all questions.

  mwikimbi kaandika kuwa 1966 mwalimu nyererre alitembelea mbarali wananchi wa kapunga wakamwomba awajengee miundo mbinu kwa ajili ya umwagiliaji na halafu 1976 serikali 'iliomba' kwa wananchi eneo kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo na wananchi walikubali.

  haionyeshi hapo juu wananchi walikuwa wanafaidikaje na mradi ule. na picha ninayopata ni kuwa 'waliombwa na kutoa bure hekari 5500'. na wakat wa kumuuzia mwekezaj wakachukuliwa hekari zingine 2000. walilipwa fidia? kama hapana huo ni uonevu.

  kwanza itakuwaje serikali iseme inaomba ardhi kubwa na kuanzisha mradi mkubwa kama huo bila kuwa na mpango wa kuwasaidia wananchi wa eneo husika kwa namna moja au ingine kupitia mradi huo?

  kwahiyo naamini wananchi wale walikuwa wanafaidika kwa namna moja au ingine na mradi ule. serikali isingeweza kuchukua ardhi kubwa kama ile na kuanzisha limradi kama lile bila kuwafikiria wananchi wake. ingekuwa kipindi cha bm au hiki ingewezekana. lakin si kipindi cha mwalimu.

  na sasa je, 'mwekezaji' alipokuwa anauziwa hilo limradi/mashamba aliambiwa jinsi mradi ulivyokuwa unawanufaisha wananchi wa eneo lile? na alikubaliana na hilo? au hilo halikuzingatiwa?

  nimalizie kwa kusema makelele ya watu yanayosikika ni kwasababu wanataka kulima na nasoma hapo juu kuwa 'mwekezaj' analima chini ya 25%. 75% inafanya nin wakat watu hawana pa kulima? na kama wanapo hapana miundombinu bora kama ya hayo mashamba? hii ni sawa na kumwaga chakula wakati jirani yako analia njaa.

  isingekuwa vibaya kuwaachia wanavijij wawe wanalima hiyo 75% ambayo halimi. kwanza mtu mwenyewe alipewa mashamba kwa bei ya bure
   
 12. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #12
  Feb 22, 2009
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  1. Serikali kupitia PSRC (sasa CHC) ndio waliobinafsisha shamba hili kwa kampuni binafsi. Sio DC anaebinafsisha. Hivyo serikali ndio inahusika na suala hili kupitia CHC na sio DC wa Mbarali.
  2. Wananchi kutaka DC wao aondoke halinihusu kwani mimi siteui DC. Mimi sijawa mamlaka wa uteuzi bado. Wenye mamlaka hayo ndio wanaohusika na Hawa Ngulume sio Mwenyekiti wa Kamati ya Mashirika ya Umma.
  3. Mwekezaji kajenga nyumba ya DC au ya Katibu wa CCM wilaya. Sio jipya hili kwangu na watu wengi humu JF. Hii ni moja ya ushahidi wa jinsi Taifa lilivyooza kwa ufisadi. Ulitaka niseme nini - we mwekezaji usijenge nyumba ya Katibu wa CCM!

  Kuhani, wakati mwingine uwe 'objective'
   
 13. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #13
  Feb 22, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Waliofuata baada yake wameurudisha chini ya kivuli cha uwekezaji.
   
 14. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #14
  Feb 22, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  ..inawezekana hana habari? Hata hivyo hili ni suala la uwajibikaji, kwa hiyo kwa collective governance ilitakiwa liwe linafahamika katika ngazi ya wilaya na mkoa, nadhani wananchi walitoa maoni yao kwa kamati baada ya kutoshughulikiwa katika ngazi zinazohusika. Na viongozi wetu wameshajityuni kufanya kazi baada ya maandamano ya wananchi. nadhani wanasubiri jamaa wagome na watie kufuli ofisi za mkuu wa wilaya, hapo ndipo utaona reaction ya serikali. .....inachosha sasa :confused:
   
 15. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #15
  Feb 22, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,968
  Likes Received: 222
  Trophy Points: 160
  Ni kweli kuna haja ya kupata ukweli.Haya mashamba kabla ya kubinafsishwa si wananchi walikuwa wanakodishwa kulima.serikali ilipata nini hata kodi hakuna aliyelipa isipokuwa bado waliitaka serikali iwaimarishie miundo mbinu.Tatizo la watanzania tunapenda vya bure sana.hivi kama kweli wananchi wananyanyaswa hivi serikali ya mkoa haina habari.Kinachieleweka huko barari ni matatizo yafuatayo.1 wananchi hakuridhia mashamba ya kapunga kupewa muwekezaji.2.wananchi hawakutaka kuhama kwenye bonde la ihefu.Ssasa walimkataa DC dololo kwa madai hayohayo.sasa wanamkataa mama huyu kwa madai hayohayo hivi nchi watanzania wanafikiria amaisha ni mzaha ndo maana majirani zetu wanatupita kwa maendeleo ya mtu mmojammoja na kiinchi.Kama wananchi wa maeneo ya kapunga wangekuwa serious wanganzisha kampuni.Na kuomba seriali iwasaidie kupata mikopo ili kuendesha mashamba hayo kisasa naamini wangepewa mashamba hayo na hata kama serikali ingelikataa wangekuwa na haki kuiomba mahakama kuzuia uuzaji wa mashamba hayo.Nimesikia kuwa diwani mmja na mbunge ndio chanzo cha chokochoko sijui kama madai hayo ni kweli.Ni vyema walioko huko wakatufahamisha vizuri
   
 16. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #16
  Feb 22, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  ni vema ukaongea na zito au mtu aliyeko mbarali akakuambia hali halisi, mashamba yaliyobinafsishwa ni mawili, mbarali rice farms, miundo mbinu yake ilijengwa na wachina, hili halina tatizo kubwa mwekezaji anafanya angalua kilichompeleka pale, wananchi wanalalamika kuhusu kapunga rice, mwekezaji anafanya ubabaishaji mtupu, wananchi hawana pa kulima, 75% ya eneo lile ni pori, amevamia hektari 2200 na ushee hazikuwepo kwenye mradi lakini umwamba wa mungai na ngasongwa ulitumika kuuza kijiji cha watu, sasa wakilima kwenye kijiji chao wanakamatwa wanaswekwa ndani kwa msaada wa dc, wanapojiuliza kulikoni dc hawatetei wanashindwa kujua kulikoni sasa inapofika mahali kama hapo inabidi wajiulize maswali mengi na hapo ndo linapozuka kuwa mwekezaji anajenga nyumba ya katibu wa ccm mbarali na huku dc akijigamba kwa uongozi wa juu kuwa yeye ndo anajenga kumarisha ccm mbarali
   
 17. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #17
  Feb 23, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,968
  Likes Received: 222
  Trophy Points: 160
  kama uamuzi ni huo naona busara imetumika wanastahili kulipwa na kurudishiwa ardhi yao.
   
 18. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #18
  Feb 23, 2009
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ndio, nilitegemea useme huko huko wilayani kwamba hiyo conflict of interest is unacceptable.

  Mwakilishi wetu wa chama mbadala, mmoja wa watu wachache, wachache mno, next to Dr. W. Slaa na wengine wawili watatu wanaobena matumaini ya watu wa Tanzania unasema kwamba Taifa limeshaoza unataka niseme nini? Unatamka hivyo kweli, au ni ulimi umeteleza?

  Tena shukuru hawajasikia, sali Mtume na ufunge siku mbili uombee wananchi wa Kigoma Kaskazini wasisikie umetamka hadharani kwamba "...Sio jipya hili kwangu... ushahidi wa jinsi Taifa lilivyooza kwa ufisadi. Ulitaka niseme nini..."

  Mbunge kazi yako ni kusimamia serikali, that entails calling for, and demanding, responsibility for any and all official improprieties you know of, sio kurekebisha uozo peke yake (kuagiza kurudishwa shamba) bali hata kuhimiza uwajibikaji wa wanaosababisha uozo ( kukemea Mkuu wa Wilaya kujengewa nyumba na wawekezaji ).

  Sio kutamka hadharani bila soni "Taifa limeoza ufisadi...unataka nifanyeje..."

  Tema mate chini!

   
  Last edited: Feb 23, 2009
 19. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #19
  Feb 23, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Kuhani,

  Tanzania bado tuna standards za chini sana, hatuna "zero tolerance" kwenye mambo ya rushwa na mengine muhimu yanayohusu maendeleo yetu.

  Hata wabunge machachari kama kina Zitto wanakuwa wanasuasua, huko bungeni kuna politics kibao na ma coalitions kwa hiyo na wao wanakuwa wanauma na kupuliza, hawataki ku "step on people's toes" they play it safe, compromising principles for security. Hatuna "Profiles in Courage" types, at least not in the spotlight.

  Those who compromise principles for (false) security will end up with neither.

  Zitto tulitegemea uonyeshe njia kwa cheche za kizazi kipya, majibu yako hapa yanakufanya uonekane kama ushachoka.
   
 20. Companero

  Companero Platinum Member

  #20
  Feb 23, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  "Kwa hiyo, nimwombe Waziri Mkuu kwamba, wakae tena waangalie kwa sababu hakuna kipato kingine Wilayani Mbarali. Ukizungumza kwamba, kuna chakula safari hii Mbeya, Mbarali uitoe kwa sababu haina mvua, inategemea kilimo cha umwagiliaji na tangu mwaka 1992 baada ya NAFCO kushindwa kulima. Wakulima wamekuwa wakikodi mle ndani ya mashamba, kwa zaidi ya miaka kumi sasa…Kwa sababu NAFCO ilipokuwepo hata wananchi wenyewe walikuwa wanaajiriwa mle ndani, hawakuweza kumudu maisha yao ya kila siku. Lakini baada ya kuambiwa sasa mtakodi yale mashamba na wamekuwa wakilipa shilingi 25,000 kwa hekta moja, vipato vimeongezeka. Mheshimiwa Waziri Mkuu ulifika miaka ya 1980, uliona sasa ni tofauti kabisa. Hali ya Mbarali watu walivyoendelea, walivyobadilika, mashule tumejenga kwa kutumia kipato cha kilimo cha mpunga si kitu kingine na kwa mfano tu ulio rahisi, katika hekta moja ya shamba, mkulima akilima pale anapata magunia 40 na akiuza anapata karibu shilingi milioni 1.8, ukitoa gharama inabaki shilingi 1,200,000 kwa hekta moja. Sasa kwa mwaka mzima kwa hekta hizo 7,000 ambazo ziko kwenye shamba moja, kuna shilingi bilioni nane ambazo zinazalishwa pale kwenye ile Wilaya na hizo pesa zinabaki ndani wa Wilaya ya Mbarali. Sasa leo akipewa mtu mmoja, sielewi unamfanyaje huyu mwananchi aweze kumudu maisha yake ya kila siku, unampa wapi eneo lingine la kulima akitoka mle ndani ya mashamba?" - Estherina Julio Kilasi, Mbunge wa Mbarali akitoa Hoja Bungeni 27 Juni 2006
   
Loading...