Ufipa-Kinondoni
JF-Expert Member
- Jan 3, 2012
- 4,582
- 2,783
Wana-JF,
Nimekuwa najaribu kufikiria jinsi Mbunge wa Monduli na Waziri aliyejihuzuru kwa kashfa ya Mradi tata wa Richmond, Bw. E. Lowassa anavyotemebelea mikoa na wilaya mbalimbali hapa Tanzania. Amekuwa akijihusisha na harambee na kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo hasa inayoendeshwa na makundi ya kidini. Katika siku za hivi karibuni, EL amejikita hata katika kukutana na wazee wa jadi. Kwa hali ilivyo safari hizi zinatumia hela nyingi sana.
Lakini unaweza kunisaidia kutafakari kidogo!
1. Hizi kazi anazofanya anafanya kama nani, mfano ni mkutano wake wa Shinyanga ambao amesikika akitoa siri za Baraza la Mawairi katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria pia na mkutano na Chama cha Waendesha Boda Boda, Tabora. EL akiwa ameweka Jiwe La Msingi katika Kaburi la Mnyugumba; EL katika Tambiko
2. Nani anagharimia safari zake??? Ni chama tawala au serikali kuenzi utumishi wake wa Uwaziri Mkuu!
3. Nini hasa lengo lake kwa nchi yetu, kama hela anazotumia hazina chanzo kilichowazi?
4. Ni nani anayeanda mikutano hii ya kumkutanisha na wananchi? CCM! Serikali!
Naomba ufikiri kwa kina kabla hujajibu.