Safari za E. Lowassa Mikoani: Anamwakilisha nani!?

Safari za E. Lowassa Mikoani: Anamwakilisha nani!?

Wana-JF,

Nimekuwa najaribu kufikiria jinsi Mbunge wa Monduli na Waziri aliyejihuzuru kwa kashfa ya Mradi tata wa Richmond, Bw. E. Lowassa anavyotemebelea mikoa na wilaya mbalimbali hapa Tanzania. Amekuwa akijihusisha na harambee na kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo hasa inayoendeshwa na makundi ya kidini.
Katika siku za hivi karibuni, EL amejikita hata katika kukutana na wazee wa jadi. Kwa hali ilivyo safari hizi zinatumia hela nyingi sana.

Lakini unaweza kunisaidia kutafakari kidogo!
1. Hizi kazi anazofanya anafanya kama nani, mfano ni mkutano wake wa Shinyanga ambao amesikika akitoa siri za Baraza la Mawairi katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria pia na mkutano na Chama cha Waendesha Boda Boda, Tabora. EL akiwa ameweka Jiwe La Msingi katika Kaburi la Mnyugumba; EL katika Tambiko
2. Nani anagharimia safari zake??? Ni chama tawala au serikali kuenzi utumishi wake wa Uwaziri Mkuu!
3. Nini hasa lengo lake kwa nchi yetu, kama hela anazotumia hazina chanzo kilichowazi?
4. Ni nani anayeanda mikutano hii ya kumkutanisha na wananchi? CCM! Serikali!

Naomba ufikiri kwa kina kabla hujajibu.

wewe inakuwashia nini kama mtu anapita huko na huko unachangia maendeleo ulitaka awe mchawi? achen mawazo ya kuku bana
 
lowasa ana mkondo mrefu amewashika matajiri na wafanya biashara wakubwa. kazi tunayo mungu atuepushe na janga hili
 
wewe inakuwashia nini kama mtu anapita huko na huko unachangia maendeleo ulitaka awe mchawi? achen mawazo ya kuku bana
Changia, sijui kama nimemtusi au kukataa anachofanya yeye. Elimika
 
Mkuu Micro E coli kumbe tutaona drama za kufa mtu kuelekea uteuzi wa mgombea urais kwa tiketi ya CCM.

mkuu familia ya Jk inamtaka Membe ilikulinda maslahi ya kina Liz kwenye biashara zao ambazo chanzo chake kinatia mashaka ndio maana hatutokubali Membe awe Rais kamwe.
 
hv watanzania,Huyu ndo mnategemea awe first lady kweli?anaye andika bila hata nukta,kweliiiiiiii dr nayeameingia choo cha kike kweli,

wewe ulisha wahi kiona hati ya fistlady wasasa acha ushamba bana.
 
Nakumbuka Josephine Mushumbusi alipokuwa anazunguka nchini kuimarisha kambi ya "mme" wake watu walihoji, lakini wengine wakawa wakali kupinga kuhojiwa huko.

Mpaka ikabidi Kamati Kuu ya Chadema iingilie kati kumpiga marufuku.

Wewe kiumbe rudi kwenye mada! Unakera unapo mwangia uchafu uzi wa mwenzio.
 
Nakumbuka Josephine Mushumbusi alipokuwa anazunguka nchini kuimarisha kambi ya "mme" wake watu walihoji, lakini wengine wakawa wakali kupinga kuhojiwa huko.

Mpaka ikabidi Kamati Kuu ya Chadema iingilie kati kumpiga marufuku.

njaa ni hatari sana , kumbe nawewe umenasa ? Mtamteteaje ulingoni mamvi ili mueleweke ?
 
jana nilianzisha uzi hapa jf,kwnn kila siku jf ni lowasa,lowasa,lowasa tu?cikupata majibu,hili jembe la kaskazn kwakweli limewashikw wapnzan wake pabaya,huyu mmasai hapigi kelele we utamtukan sana,wengn wamedirik kumuombea mabaya,jama ye anachanja mbuga,kwa taarif nikwamb tu hyu mzee dam ya yesu ndo inayo muongoza,

umeulizwa kwamba anazurura nchi nzima ( japo arusha mwisho wake ni monduli tu ! )anamwakilisha nani ? Familia yake , ccm au serikali ? Kama nani ? Hivi unawezaje kumhusisha fisadi aliyethibitishwa na bunge na damu takatifu ya yesu ? Ulaaniwe milele .
 
Hahaa! #TeamLowasa

Naona unajiandAa kuwa Afisa Habari wa Ikulu.

Mkuu na Mimi usinisahau kwenye Ufalme wenu, Maana na Mimi namuunga mkono huyu Lwaiganani hasa kwenye sera yake ya ELIMU KWANZA.

Mkuu 2015 nitakuwa naitwa Kibanga OLE Ampiga Mklolone.
Pasco
Mkuu Kibanga, very unfortunately, mimi sio Team EL!, hivyo sitegemei chochote! "ole wao wawategemeao binadamu!".
 
mimi nadhani ndugu lowasa amechanganyikiwa ! Unajua zile kashfa zilizompata zimesambaa worldwide , hana pa kujificha ! Wala hana hata anayemwakilisha , hivi hamad rashid akiitisha mkutano utasema anawakilisha cuf , adc au serikali ya umoja wa kitaifa ? Siasa siyo ajira mzee lowasa , pumzika , utapararaizi bure ! Huko tunakoenda ndiyo unaelekea kuumbuka zaidi , maadam mwakyembe yuko hai tusubiri makubwa zaidi .
 
mkuu usilalamike,ndo hali yenyew,mlichelew kumvua gamba na kambi yen ya kina membe,
 
mkuu,
kama issue ni urais, kwani anatumia hela ya nani katika mizunguko hiyo? Kwani ameteuliwa na chama chake kugombea au ni mgombea binafsi?

mkuu,unataka kuthibitisha kuwa nawe ni mmoja kati ya wale wa LUMUMBA?
 
umeulizwa kwamba anazurura nchi nzima ( japo arusha mwisho wake ni monduli tu ! )anamwakilisha nani ? Familia yake , ccm au serikali ? Kama nani ? Hivi unawezaje kumhusisha fisadi aliyethibitishwa na bunge na damu takatifu ya yesu ? Ulaaniwe milele .
peleka unafiki wako huko na hao wanaokutuma,umeena ww ndo unamjua yesu tu peke yako mchawi mkubwa ww,na ulaaniwe na ww na kizazi chenu chote asibakie hata panya,unajidai mlokole kumbe umekali ushirikina tu,
 
acha uongo.kijana jifunze kutulia na fanyia utafiti wa kina unayosema.

kumbuka Dr Slaa alipokuwa akiomba kura 2010 nilizunguka nae nchi nzima,nilisimama jukwaani na kuhaidi kuwatumikia, utakuha na matusi hapa na maswali, ngoja nikujibu.
kipindi cha uchaguzi Dr aliitaji uwepi wangu kuliko wakati wowote,ndiyo wakati aliitaji maombi,malezi ya mfumo wa chakula,kutiwa moyo nazaidi ni kipindi alipata shida ya mkono hivyo ili kwenda na mda uwrpi wangu ulikuwa wa msingi.

kamati kuu ya chadema haiwezi na haijawahi kuingilia kazi zangu.toa ushahidi,unless unamuongelea Josephine mwingine.

kwa taarifa,nimeingia usiku wa jana nilikuwa Geita,kahama na nzega.
sifanyi haya kwa kutafuta ama kuimarisha kambi,hatulilii Ikulu wala hatuitafuti Ikulu tunatimiza ahadi ya kuzidi kuwaelimisha wananchi hata kama hatukuingia Ikuku.ahadi ni deni,nawiwa kufanya hivyo kwakuwa niliwaahidi akina mama.
tembelea tovuti yangu,nimekuwa mwanaharakati wa maendeleo kabla sijakutana na Dr.

nikitu kilicho ndani yangu wala sijifunzi.fanya utafiti.nilianza kuwatumikia wananchi toka nikuwa binti mdogo,sijaanza sasa;utumushi is my spirit,sasa kazi yangu imetanuka tu.sijawahi kutafuta uongozi popote.nenda kimara baruti mtaa nilioishi hapo nyuma watakwambia.

nenda mitaa ya Afrika sana watakwambia my spirit.nilifanya kwa moyo sikutamani hata ubalozi.
Naamini katika kutumia akili na nguvu alizonipa Mungu katika kufanya jambo na malipo yanayotoka juu.Leadership is given hivyo siyo jambo la kufukuzia.

sijawahi na sitegemei kutumua pesa ya chama,nafanya kazi kwa mikono yangu.stop kunifananisha na yeyote.nitabaki kuwa watofauti kwakuwa the purpose of God in me will never be the same .........

Josephine

Josephine,

Ni kweli wewe hujawahi kugombea uongozi. Sababu ya kutokugombea ilikuwa ni kukosa kwako kujiamini na ulikuwa unaamini mpaka upate mtu wa kukukingia kifua ndio ugombee. Sasa hivi umeshapata mtu wa kukukingia kifua na tutakuona unagombea uongozi very soon. Post hii naitunza kama ushahidi.

Ni kweli kuwa Kamati Kuu ya Chadema ilikudhibiti ulipanza kufuja pesa za chama kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kulipwa sh. milioni 10 kwa kazi unayoiita ya kujitolea. Bila kamati kuu kuwa macho ungesababisha hasara kubwa zaidi.

Siku hizi umekuja na gear nyingine ya IGEHETE na imeshafaamika jinsi unavyotumia jina la Chadema katika kujipatia pesa kwenye NGO yako ya magumashi ya IGEHETE.

Dr. Slaa zamani alikuwa mtu focused, ila sasa hivi umeshamdiverge towards uroho wa pesa na madaraka.
 
mkuu,unataka kuthibitisha kuwa nawe ni mmoja kati ya wale wa LUMUMBA?
Haaaaaaaah! Haya kaka, mimi nimejikita katika kutafuta uhalali wa yeye kubeba mzigo kama huo na kutaka kujua anafanya kwa maslahi ya nani. Hoja yangu pia iko wazi kwa anayetaka ajadili moja kwa moja.
 
Wana-JF,

Nimekuwa najaribu kufikiria jinsi Mbunge wa Monduli na Waziri aliyejihuzuru kwa kashfa ya Mradi tata wa Richmond, Bw. E. Lowassa anavyotemebelea mikoa na wilaya mbalimbali hapa Tanzania. Amekuwa akijihusisha na harambee na kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo hasa inayoendeshwa na makundi ya kidini.
Katika siku za hivi karibuni, EL amejikita hata katika kukutana na wazee wa jadi. Kwa hali ilivyo safari hizi zinatumia hela nyingi sana.

Lakini unaweza kunisaidia kutafakari kidogo!
1. Hizi kazi anazofanya anafanya kama nani, mfano ni mkutano wake wa Shinyanga ambao amesikika akitoa siri za Baraza la Mawairi katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria pia na mkutano na Chama cha Waendesha Boda Boda, Tabora. EL akiwa ameweka Jiwe La Msingi katika Kaburi la Mnyugumba; EL katika Tambiko
2. Nani anagharimia safari zake??? Ni chama tawala au serikali kuenzi utumishi wake wa Uwaziri Mkuu!
3. Nini hasa lengo lake kwa nchi yetu, kama hela anazotumia hazina chanzo kilichowazi?
4. Ni nani anayeanda mikutano hii ya kumkutanisha na wananchi? CCM! Serikali!

Naomba ufikiri kwa kina kabla hujajibu.

Mzee wa watu anatumia gharama yake kusaidia wengine ila yuko strategic sana..mind you hakuna mtu ambaye anainvest pasipo lipa..na huwa anaingia kule ambako wengi hawatarajii kama alivyoenda kwenye ngome ya mzee wa E.A community na kuweka jiwe la msingi! ha ha mwacheni avute kasi...
 
Back
Top Bottom